Juzuu Ya 3 Tilkar-Rusulu
Juzuu ya 03
Juzuu Ya 3 Tilkar-Rusulu
Juzuu: 3
تِلْكَ الرُّسُلُ
تِلْكَ الرُّسُلُ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۘ مِّنْهُم مَّن كَلَّمَ اللَّـهُ ۖ وَرَفَعَ بَعْضَهُمْ دَرَجَاتٍ ۚ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ ۗ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا اقْتَتَلَ الَّذِينَ مِن بَعْدِهِم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ وَلَـٰكِنِ اخْتَلَفُوا فَمِنْهُم مَّنْ آمَنَ وَمِنْهُم مَّن كَفَرَ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا اقْتَتَلُوا وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ ﴿٢٥٣﴾
253. Hao ni Mitume, Tumewafadhilisha baadhi yao juu ya baadhi. Miongoni mwao (yuko) aliyesemeshwa na Allaah, na Akawapandisha baadhi yao vyeo. Na Tukampa ‘Iysaa mwana wa Maryam hoja bayana na Tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu. Na lau Angelitaka Allaah wasingelipigana wale ambao (walikuja) baada yao, baada ya kuwajia hoja bayana. Lakini walikhitalifiana, basi miongoni mwao (kuna) walioamini na miongoni mwao waliokufuru. Na lau Angelitaka Allaah wasingelipigana lakini Allaah Anafanya Ayatakayo. يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِمَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا بَيْعٌ فِيهِ وَلَا خُلَّةٌ وَلَا شَفَاعَةٌ ۗ وَالْكَافِرُونَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٢٥٤﴾
254. Enyi mlioamini! Toeni katika Tulivyokuruzukuni kabla haijafika Siku (ambayo) hakutakuweko biashara (kuuza na kununua) humo wala urafiki wala uombezi. Na makafiri wao ndio madhalimu. اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾
255. Allaah, laa ilaaha illaa Huwa (hapana mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye), Al-Hayyul-Qayyuwm (Aliyehai daima, Msimamia kila jambo milele, Mwenye Kusimama kwa Nafsi Yake na dhati Yake milele). Haumchukuwi usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai (anayeombea) mbele Yake bila ya idhini Yake. Anajua yaliyo mbele yao (viumbe) na yaliyo nyuma yao. Wala hawadiriki kitu chochote kile katika Elimu Yake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy Yake (Kiti Chake) mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Al-‘Aliyyul-‘Adhwiym(Yuko Juu ya vyote, Mwenye Uluwa – Mwenye Taadhima). لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ ۖ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ ۚ فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٥٦﴾
256. Hapana kulazimisha katika (kuingia) Dini, kwani imekwishabainika kati ya Uongofu na upotofu. Basi atakayemkanusha twaaghuwt (miungu ya uongo) na akamwamini Allaah kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika, na Allaah ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye Kusikia yote daima – Mjuzi wa yote daima). اللَّـهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُم مِّنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ ۗ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٥٧﴾
257. Allaah ni Walii wa wale ambao wameamini, Anawatoa kutoka katika dhwulumaat (vizani) kuwaingiza katika Nuwr (mwanga). Na wale ambao wamekufuru mawalii wao ni twaaghuwt (miungu ya uongo) huwatoa kutoka katika Nuwr na kuwaingiza katika dhwulumaat. Hao ni watu wa Motoni wao humo watadumu milele. أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِي حَاجَّ إِبْرَاهِيمَ فِي رَبِّهِ أَنْ آتَاهُ اللَّـهُ الْمُلْكَ إِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّيَ الَّذِي يُحْيِي وَيُمِيتُ قَالَ أَنَا أُحْيِي وَأُمِيتُ ۖ قَالَ إِبْرَاهِيمُ فَإِنَّ اللَّـهَ يَأْتِي بِالشَّمْسِ مِنَ الْمَشْرِقِ فَأْتِ بِهَا مِنَ الْمَغْرِبِ فَبُهِتَ الَّذِي كَفَرَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٢٥٨﴾
258. Je, hukumuona (hukumzingatia) yule ambaye alimuhoji Ibraahiym kuhusu Mola wake kwa vile Allaah Alimpa ufalme; aliposema Ibraahiym: “Mola wangu ni Ambaye Anahuisha na Anafisha.” Akasema: “Mimi pia nahuisha na nafisha.” Ibraahiym akasema: “Hakika Allaah Analileta (Analichomozesha) jua kutoka Mashariki basi wewe lilete kutoka Magharibi.” Akapigwa na butwaa (akafedheheka) yule aliyekufuru. Na Allaah Haongoi watu madhalimu.أَوْ كَالَّذِي مَرَّ عَلَىٰ قَرْيَةٍ وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا قَالَ أَنَّىٰ يُحْيِي هَـٰذِهِ اللَّـهُ بَعْدَ مَوْتِهَا ۖ فَأَمَاتَهُ اللَّـهُ مِائَةَ عَامٍ ثُمَّ بَعَثَهُ ۖ قَالَ كَمْ لَبِثْتَ ۖ قَالَ لَبِثْتُ يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ ۖ قَالَ بَل لَّبِثْتَ مِائَةَ عَامٍ فَانظُرْ إِلَىٰ طَعَامِكَ وَشَرَابِكَ لَمْ يَتَسَنَّهْ ۖ وَانظُرْ إِلَىٰ حِمَارِكَ وَلِنَجْعَلَكَ آيَةً لِّلنَّاسِ ۖ وَانظُرْ إِلَى الْعِظَامِ كَيْفَ نُنشِزُهَا ثُمَّ نَكْسُوهَا لَحْمًا ۚ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ قَالَ أَعْلَمُ أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٥٩﴾
259. Au (hukuzingatia mfano wa) kama yule aliyepita katika kijiji nacho ni kilichoporomoka kabisa juu ya mapaa yake (kuwa gofu); akasema (kwa mshangao): “Vipi Allaah Atahuisha hiki (kijiji) baada ya kufa kwake?” Basi Allaah Alimfisha miaka mia; kisha Akamfufua. Akasema: (kwa kumuuliza) “Umekaa muda gani?” Akasema: “Nimekaa siku (moja) au sehemu ya siku”. (Allaah) Akasema: “Bali umekaa miaka mia; basi kitazame chakula chako na kinywaji chako hakikuharibika. Na mtazame punda wako; na Tutakufanya (uwe) ishara kwa watu. Na itazame mifupa (ya punda) jinsi Tunavyoinyanyua, kisha Tunaivisha nyama”. Basi ilipombainikia alisema: “Najua kwamba hakika Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr(Muweza wa yote daima).”
وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ أَرِنِي كَيْفَ تُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۖ قَالَ أَوَلَمْ تُؤْمِن ۖ قَالَ بَلَىٰ وَلَـٰكِن لِّيَطْمَئِنَّ قَلْبِي ۖ قَالَ فَخُذْ أَرْبَعَةً مِّنَ الطَّيْرِ فَصُرْهُنَّ إِلَيْكَ ثُمَّ اجْعَلْ عَلَىٰ كُلِّ جَبَلٍ مِّنْهُنَّ جُزْءًا ثُمَّ ادْعُهُنَّ يَأْتِينَكَ سَعْيًا ۚ وَاعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٦٠﴾
260. Na (taja) aliposema Ibraahiym: “Mola wangu nionyeshe vipi Unahuisha wafu?” Akasema (Allaah): “Je kwani huamini?” Akasema: “La! (Naamini) lakini (kwayo) moyo wangu upate kutulia.” Akasema (Allaah): “Basi chukua ndege wanne wazoeshe kwako, (wachinje) kisha weke juu ya kila jabali katika hao (ndege uliowachinja) sehemu yao; kisha waite watakujia mbio (wakiwa wameumbika upya nawe huku unawaona wanavyojiunga viungo vyao kila mmoja); na elewa kwamba hakika Allaah ni ‘Aziyzun-Hakiym(Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika daima – Mwenye Hikmah wa yote daima). مَّثَلُ الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنبَتَتْ سَبْعَ سَنَابِلَ فِي كُلِّ سُنبُلَةٍ مِّائَةُ حَبَّةٍ ۗ وَاللَّـهُ يُضَاعِفُ لِمَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦١﴾
261. Mfano wa wale ambao wanatoa mali zao katika njia ya Allaah ni kama mfano wa punje moja (ya mbegu) iliyotoa mashuke saba, katika kila shuke kuna punje mia. Na Allaah Humzidishia Amtakaye; na Allaah ni Waasi’un-‘Aliym(Mwenye Wasaa, Mkunjufu – Mjuzi wa yote daima). الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ثُمَّ لَا يُتْبِعُونَ مَا أَنفَقُوا مَنًّا وَلَا أَذًى ۙ لَّهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٢٦٢﴾
262. Wale ambao wanatoa mali zao katika njia ya Allaah kisha hawafuatishii kwa waliyoyatoa masimbulizi wala udhia watapa ujira wao kwa Mola wao, na wala hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika. قَوْلٌ مَّعْرُوفٌ وَمَغْفِرَةٌ خَيْرٌ مِّن صَدَقَةٍ يَتْبَعُهَا أَذًى ۗ وَاللَّـهُ غَنِيٌّ حَلِيمٌ ﴿٢٦٣﴾
263. Kauli njema na msamaha ni bora kuliko swadaqah inayoifuata udhia. Na Allaah ni Ghaniyyun-Haliym(Mkwasi, Hahitaji lolote – Mpole wa kuwavumilia waja). يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُم بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ كَالَّذِي يُنفِقُ مَالَهُ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ صَفْوَانٍ عَلَيْهِ تُرَابٌ فَأَصَابَهُ وَابِلٌ فَتَرَكَهُ صَلْدًا ۖ لَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِّمَّا كَسَبُوا ۗوَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٢٦٤﴾
264. Enyi mlioamini! Msibatilishe swadaqah zenu kwa masimbulizi na udhia kama yule ambaye anatoa mali yake kwa riyaa-a (kujionyesha) kwa watu, wala hamwamini Allaah na Siku ya Aakhirah. Basi mfano wake ni kama jabali juu yake pana udongo, kisha likapigwa hilo jabali na mvua kubwa ikaliacha tupu. Hawatakuwa na uwezo juu ya lolote katika waliyoyachuma. Na Allaah Haongoi watu makafiri. وَمَثَلُ الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ وَتَثْبِيتًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ كَمَثَلِ جَنَّةٍ بِرَبْوَةٍ أَصَابَهَا وَابِلٌ فَآتَتْ أُكُلَهَا ضِعْفَيْنِ فَإِن لَّمْ يُصِبْهَا وَابِلٌ فَطَلٌّ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٦٥﴾
265. Na mfano wa wale ambao wanatoa mali zao kutafuta mardhwaat (radhi) ya Allaah na kujithibitisha nafsi zao ni kama mfano wa bustani iliyoko pahala paliponyanyuka; ikafikiwa hiyo bustani na mvua kubwa, ikatoa mazao yake maradufu, na hata kama haikufikiwa na mvua kubwa basi mvua ndogo (huitosheleza kutoa mazao). Na Allaah kwa muyatendayo ni Baswiyr (Mwenye Kuona yote daima). أَيَوَدُّ أَحَدُكُمْ أَن تَكُونَ لَهُ جَنَّةٌ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَابٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ لَهُ فِيهَا مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ وَأَصَابَهُ الْكِبَرُ وَلَهُ ذُرِّيَّةٌ ضُعَفَاءُ فَأَصَابَهَا إِعْصَارٌ فِيهِ نَارٌ فَاحْتَرَقَتْ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢٦٦﴾
266. Je! Anapenda mmoja wenu kuwa na (kumiliki) bustani ya mitende na mizabibu ipitayo chini yake mito; anayo humo kila aina ya matunda; ukamfikia uzee, naye ana kizazi dhaifu; kisha ikapigwa hiyo bustani na kimbunga cha moto kikaiteketeza? Hivyo ndivyo Allaah Anavyobainisha Aayah Zake (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) kwenu mpate kutafakari. يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ الْأَرْضِ ۖ وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ وَلَسْتُم بِآخِذِيهِ إِلَّا أَن تُغْمِضُوا فِيهِ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ ﴿٢٦٧﴾
267. Enyi mlioamini! Toeni katika twayyibaat (halaal, vizuri) mlivyochuma na katika ambayo Tumekutoleeni kutoka katika ardhi. Na wala msikusudie vibaya kutoka humo mkavitoa na hali nyinyi (wenyewe) si wenye kuvichukuwa isipokuwa kuvifumbia macho. Na jueni kwamba hakika Allaah ni Ghaniyyun-Hamiyd(Mkwasi, Hahitaji lolote – Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa na Kushukuriwa kwa yote daima). الشَّيْطَانُ يَعِدُكُمُ الْفَقْرَ وَيَأْمُرُكُم بِالْفَحْشَاءِ ۖ وَاللَّـهُ يَعِدُكُم مَّغْفِرَةً مِّنْهُ وَفَضْلًا ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦٨﴾
268. Shaytwaan anakutishieni ufukara na anakuamrisheni al-fahshaa (ubakhili, zinaa, kufru, shirki, madhambi n.k.), na Allaah Anakuahidini Maghfirah kutoka Kwake na fadhila. Na Allaah ni Waasi’un-‘Aliym (Mwenye Wasaa, Mkunjufu – Mjuzi wa yote daima).يُؤْتِي الْحِكْمَةَ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُؤْتَ الْحِكْمَةَ فَقَدْ أُوتِيَ خَيْرًا كَثِيرًا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٢٦٩﴾
269. Humpa Hikmah Amtakaye. Na anayepewa hikmah basi kwa yakini huwa amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki (na kuwaidhika) isipokuwa wenye akili. وَمَا أَنفَقْتُم مِّن نَّفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُم مِّن نَّذْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُهُ ۗ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ ﴿٢٧٠﴾
270. Na chochote mtoacho katika matumizi au mkiwekacho nadhiri katika nadhiri, basi Allaah Anakijua. Na madhalimu hawana wa kuwanusuru. إِن تُبْدُوا الصَّدَقَاتِ فَنِعِمَّا هِيَ ۖ وَإِن تُخْفُوهَا وَتُؤْتُوهَا الْفُقَرَاءَ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۚ وَيُكَفِّرُ عَنكُم مِّن سَيِّئَاتِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٢٧١﴾
271. Mkidhihirisha swadaqah basi ni vizuri hivyo, na mkizificha na kuwapa mafakiri, basi hilo ni kheri kwenu. Na Atakufutieni katika maovu yenu. Na Allaah kwa myatendayo ni Khabiyr (Mjuzi wa undani na ukina wa mambo). لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَاهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَلِأَنفُسِكُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُونَ إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ اللَّـهِ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٢﴾
271. Si juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uongofu wao, lakini Allaah Humhidi Amtakaye. Na mtoacho chochote katika kheri basi ni kwa ajili ya nafsi zenu. Na hamtoi ila kutaka Wajhi wa Allaah. Na chochote mtoacho katika kheri mtalipwa kamilifu nanyi hamtodhulumiwa. لِلْفُقَرَاءِ الَّذِينَ أُحْصِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ ضَرْبًا فِي الْأَرْضِ يَحْسَبُهُمُ الْجَاهِلُ أَغْنِيَاءَ مِنَ التَّعَفُّفِ تَعْرِفُهُم بِسِيمَاهُمْ لَا يَسْأَلُونَ النَّاسَ إِلْحَافًا ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٢٧٣﴾
273. (Swadaqah ni) Kwa ajili ya mafakiri ambao wamezuilika katika njia ya Allaah hawawezi kwenda huku na kule katika ardhi; asiyewajua huwadhania kuwa ni matajiri kutokana na staha, unawatambua kwa alama zao, hawaombi watu kwa ung’ang’anizi. Na chochote mtoacho katika kheri basi Allaah kwacho ni ‘Aliym (Mjuzi wa yote daima). الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ سِرًّا وَعَلَانِيَةً فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٢٧٤﴾
273. Wale ambao wanatoa mali zao usiku na mchana, kwa siri na kwa dhahiri; watapata ujira wao kwa Mola wao, na wala hakuna khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika.الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا إِنَّمَا الْبَيْعُ مِثْلُ الرِّبَا ۗ وَأَحَلَّ اللَّـهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا ۚفَمَن جَاءَهُ مَوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّهِ فَانتَهَىٰ فَلَهُ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَمَنْ عَادَ فَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٧٥﴾
275. Wale ambao wanakula ribaa hawasimami (Siku ya Qiyaamah) ila kama anavyosimama yule aliyezugwa na shaytwaan kwa kuguswa. Hivyo kwa sababu wao wamesema: “Hakika biashara (kuuza na kununua) ni kama ribaa.” Na Allaah Amehalalisha biashara na Ameharamisha ribaa. Basi atakayefikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake akakoma (kula ribaa); basi ni yake yale yaliyopita, na hukumu yake iko kwa Allaah. Na atakayerudia (ribaa) basi hao ni watu wa Motoni humo wao humo watadumu milele. يَمْحَقُ اللَّـهُ الرِّبَا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ ﴿٢٧٦﴾
276. Allaah Huifuta (baraka mali ya) ribaa na Huzibariki swadaqah. Na Allaah Hapendi kila kafiri apapiae madhambi. إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٢٧٧﴾
277. Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah; watapata ujira kutoka kwa Mola wao na wala hakuna khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika.يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٢٧٨﴾
278. Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na acheni yaliyobakia katika ribaa ikiwa nyinyi ni Waumini (wa kweli). فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٩﴾
279. Na msipofanya basi tangazeni vita kutoka kwa Allaah na Mtume Wake. Na mkitubu basi mtapata rasilmali zenu msidhulumu na wala msidhulumiwe. وَإِن كَانَ ذُو عُسْرَةٍ فَنَظِرَةٌ إِلَىٰ مَيْسَرَةٍ ۚ وَأَن تَصَدَّقُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٨٠﴾
280. Na ikiwa (mdaiwa) ni mwenye hali ngumu, basi (mdai) angoje muda wa kufarijika (anayemdai). Na mkifanya (deni mnalodai) swadaqah basi ni kheri kwenu mkiwa mnajua. وَاتَّقُوا يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ إِلَى اللَّـهِ ۖ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٢٨١﴾
280. Na iogopeni Siku mtayorejeshwa humo kwa Allaah, kisha kila nafsi italipwa kamilifu iliyoyachuma nao hawatodhulumiwa.يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا تَدَايَنتُم بِدَيْنٍ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى فَاكْتُبُوهُ ۚ وَلْيَكْتُب بَّيْنَكُمْ كَاتِبٌ بِالْعَدْلِ ۚ وَلَا يَأْبَ كَاتِبٌ أَن يَكْتُبَ كَمَا عَلَّمَهُ اللَّـهُ ۚ فَلْيَكْتُبْ وَلْيُمْلِلِ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ وَلْيَتَّقِ اللَّـهَ رَبَّهُ وَلَا يَبْخَسْ مِنْهُ شَيْئًا ۚ فَإِن كَانَ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ سَفِيهًا أَوْ ضَعِيفًا أَوْ لَا يَسْتَطِيعُ أَن يُمِلَّ هُوَ فَلْيُمْلِلْ وَلِيُّهُ بِالْعَدْلِ ۚ وَاسْتَشْهِدُوا شَهِيدَيْنِ مِن رِّجَالِكُمْ ۖ فَإِن لَّمْ يَكُونَا رَجُلَيْنِ فَرَجُلٌ وَامْرَأَتَانِ مِمَّن تَرْضَوْنَ مِنَ الشُّهَدَاءِ أَن تَضِلَّ إِحْدَاهُمَا فَتُذَكِّرَ إِحْدَاهُمَا الْأُخْرَىٰ ۚ وَلَا يَأْبَ الشُّهَدَاءُ إِذَا مَا دُعُوا ۚ وَلَا تَسْأَمُوا أَن تَكْتُبُوهُ صَغِيرًا أَوْ كَبِيرًا إِلَىٰ أَجَلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ أَقْسَطُ عِندَ اللَّـهِ وَأَقْوَمُ لِلشَّهَادَةِ وَأَدْنَىٰ أَلَّا تَرْتَابُوا ۖإِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً حَاضِرَةً تُدِيرُونَهَا بَيْنَكُمْ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَلَّا تَكْتُبُوهَا ۗ وَأَشْهِدُوا إِذَا تَبَايَعْتُمْ ۚ وَلَا يُضَارَّ كَاتِبٌ وَلَا شَهِيدٌ ۚ وَإِن تَفْعَلُوا فَإِنَّهُ فُسُوقٌ بِكُمْ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ وَيُعَلِّمُكُمُ اللَّـهُ ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٨٢﴾
282. Enyi mlioamini! Mtakapokopeshana deni kwa muda maalumu basi liandikeni. Na aandike baina yenu mwandishi kwa uadilifu. Na wala asikatae mwandishi kuandika kama Allaah Alivyomfunza. Basi aandike na atamke (maneno yanayoandikwa) yule ambaye ana haki (mdai) na amuogope Allaah Mola Wake, na wala asipunguze humo kitu chochote. Basi ikiwa yule ambaye ana haki amepumbaa (hajakomaa kiakili) au dhaifu (mnyonge), au hawezi kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe walii (msimamizi) wake kwa uadilifu. Na mshuhudishe mashahidi wawili wanaume miongoni mwenu. Na ikiwa hakuna wanaume wawili, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili katika wale mnaowaridhia miongoni mwa mashahidi, ili kama mmoja wao akipotea, basi mmoja wao atamkumbusha mwengine. Na mashahidi wasikatae watapoitwa. Na wala msichukie kuliandika (deni likiwa) dogo au kubwa mpaka muda wake. Hivyo kwenu ndiyo aqswatw (uadilifu upasavyo) mbele ya Allaah na ndio imara (unyoofu) zaidi kwa ushahidi; na ni karibu zaidi ili msiwe na shaka; isipokuwa itakapokuwa biashara taslimu (mkono-kwa-mkono) mnayoiendesha baina yenu, basi si dhambi kwenu msipoiandika. Na shuhudisheni mnapouziana. Na wala asidhuriwe mwandishi wala shahidi; na mkifanya basi hakika huo ni ufasiki kwenu. Na mcheni Allaah, na Allaah Anakufunzeni, na Allaah kwa kila kitu ni ‘Aliym (Mjuzi wa yote daima). وَإِن كُنتُمْ عَلَىٰ سَفَرٍ وَلَمْ تَجِدُوا كَاتِبًا فَرِهَانٌ مَّقْبُوضَةٌ ۖ فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ الَّذِي اؤْتُمِنَ أَمَانَتَهُ وَلْيَتَّقِ اللَّـهَ رَبَّهُ ۗ وَلَا تَكْتُمُوا الشَّهَادَةَ ۚوَمَن يَكْتُمْهَا فَإِنَّهُ آثِمٌ قَلْبُهُ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ ﴿٢٨٣﴾
283. Na mkiwa safarini na hamkumpata mwandishi, basi (mdai) akabidhiwe rahani. Na ikiwa mmoja wenu amewekewa amana na mwengine, basi airudishe yule ambaye ameaminiwa amana ya mwenzake; na amuogope Allaah Mola wake; na wala msifiche ushahidi; na mwenye kuuficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Allaah kwa mnayoyatenda ni ‘Aliym (Mjuzi wa yote daima).لِّلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَإِن تُبْدُوا مَا فِي أَنفُسِكُمْ أَوْ تُخْفُوهُ يُحَاسِبْكُم بِهِ اللَّـهُ ۖ فَيَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٨٤﴾
284. Ni vya Allaah pekee vyote viliomo mbinguni na viliomo ardhini. Na mkidhihirisha yale yaliyomo ndani ya nafsi zenu au mkiyaficha; basi Allaah Atakuhesabuni kwayo. Humghufuria Amtakaye na Humuadhibu Amtakaye. Na Allaah kwa kila kitu ni Qadiyr (Muweza wa yote daima).آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ ۚ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴿٢٨٥﴾
285. Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake na Waumini (pia wameamini). Wote wamemwamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Mitume Wake. (Nao husema): “Hatutafautishi baina ya yeyote kati ya Mitume Wake”. Na wakasema: “Tumesikia na tumetii, tunakuomba Maghfirah Mola wetu na Kwako ni marejeo (ya mwisho).” لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ ۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ ۖ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۚ أَنتَ مَوْلَانَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٢٨٦﴾
286. Allaah Hakalifishi nafsi yo yote ila kwa kadiri ya uwezo wake. Itapata iliyoyachuma, na ni dhidi yake iliyojichumia. “Mola wetu Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Usitubebeshe mzigo kama Ulivyoubebesha juu ya wale ambao waliokuwa kabla yetu. Mola wetu Usitutwike tusiyoyaweza, na Tusamehe, na Tughufurie na Turehemu, Wewe ni Mawlaa wetu, basi Tunusuru dhidi ya watu makafiri. سُورَةُ آل عِمْران
Aal-‘Imraan: 3
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الم ﴿١﴾
1. Alif Laam Miym. اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ﴿٢﴾
2. Allaah, laa ilaaha illaa Huwa (hapana mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye), Al-Hayyul-Qayyuwm(Aliyehai daima, Msimamia kila jambo milele – Mwenye Kusimama kwa Nafsi Yake na Dhati Yake milele). نَزَّلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَأَنزَلَ التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ﴿٣﴾
3. Amekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu kwa haki kinachosadikisha yaliyo baina yake (yaliyo kabla yake) na Akateremsha Tawraat na Injiyl. مِن قَبْلُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَأَنزَلَ الْفُرْقَانَ ۗ إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٤﴾
4. Kabla, ni Hudan (Uongofu) kwa watu na Akateremsha Al-Furqaan. Hakika wale ambao wamezikanusha Aayah za Allaah (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) watapata adhabu kali. Na Allaah ni ‘Aziyz (Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika daima) Mwenye kulipiza. إِنَّ اللَّـهَ لَا يَخْفَىٰ عَلَيْهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ ﴿٥﴾
5. Hakika Allaah Hakifichiki Kwake chochote katika ardhi wala katika mbingu. هُوَ الَّذِي يُصَوِّرُكُمْ فِي الْأَرْحَامِ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٦﴾
6. Yeye Ndiye Aliyekutieni sura katika matumbo ya uzazi vile Atakavyo. Laa ilaaha illaa Huwa (hapana mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye), Al-‘Aziyzul-Hakiym(Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika daima – Mwenye Hikmah wa yote daima). هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ ۖ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ ۗ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّـهُ ۗ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٧﴾
7. Yeye Ndiye Aliyeteremsha kwako Kitabu humo mna Aayah Muhkam (zilizo wazi maana yake, hazihitaji Aayah zingine kuzifasiri) hizo ndio msingi wa Kitabu, na nyinginezo ni mutashaabih (haziko wazi maana yake, zinahitaji Aayah za Muhkam kuzifasiri). Basi wale ambao katika nyoyo zao mna upotovu, hufuata zile zilizoshabihiana kutafuta fitnah na kutafuta tafsiri zake; na hakuna ajuae tafsiri zake isipokuwa Allaah. Na Ar-Raasikhuwna (wenye msingi madhubuti) katika elimu husema: “Tumeziamini, zote ni kutoka kwa Mola wetu.” Na hawakumbuki ila wenye akili.رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ ﴿٨﴾
8. “Mola wetu, usizipotoe nyoyo zetu baada ya kuwa Umeshatuhidi na Tutunukie kutoka kwako Rahmah. Hakika Wewe ni Al-Wahhaab (Mwingi wa Kutunuku, Mpaji wa yote).”رَبَّنَا إِنَّكَ جَامِعُ النَّاسِ لِيَوْمٍ لَّا رَيْبَ فِيهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُخْلِفُ الْمِيعَادَ ﴿٩﴾
9. “Mola wetu! Hakika Wewe ni Mkusanyaji watu Siku isiyo na shaka ndani yake. Hakika Allaah Havunji miadi.” إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَن تُغْنِيَ عَنْهُمْ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُم مِّنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۖوَأُولَـٰئِكَ هُمْ وَقُودُ النَّارِ ﴿١٠﴾
10. Hakika wale ambao wamekufuru hazitowafaa kitu mali zao na wala watoto wao mbele ya Allaah, na hao ndio kuni za moto. كَدَأْبِ آلِ فِرْعَوْنَ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا فَأَخَذَهُمُ اللَّـهُ بِذُنُوبِهِمْۗ وَاللَّـهُ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿١١﴾
11. Kama mwendo wa watu wa Fir’awn na wale ambao wa kabla yao. Wamekadhibisha Aayah Zetu (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) basi Allaah Aliwachukua kwa madhambi yao, na Allaah ni Shadiydul-‘Iqaab (Mkali wa kuadhibu).