JUZUU

JUZUU


 قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا سَتُغْلَبُونَ وَتُحْشَرُونَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ ۚ وَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴿١٢

 

12. Sema (kuwaambia) waliokufuru: “Karibuni mtashindwa na mtakusanywa katika (moto wa) Jahannam, na ni pabaya mno mahala pa kupumzika.”  قَدْ كَانَ لَكُمْ آيَةٌ فِي فِئَتَيْنِ الْتَقَتَا ۖ فِئَةٌ تُقَاتِلُ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَأُخْرَىٰ كَافِرَةٌ يَرَوْنَهُم مِّثْلَيْهِمْ رَأْيَ الْعَيْنِ ۚ وَاللَّـهُ يُؤَيِّدُ بِنَصْرِهِ مَن يَشَاءُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّأُولِي الْأَبْصَارِ ﴿١٣﴾

 

13. Kwa hakika ilikuwa ni Aayah kwenu (Ishara, dalili, miujiza, mazingatio) katika makundi mawili; yalipokutana. Kundi linapigana katika njia ya Allaah na jingine kafiri, linawaona wao (Waislamu) mara mbili yao kwa uoni wa jicho. Na Allaah Humsaidia kwa nusura Yake Amtakaye. Hakika katika hayo ni zingatio kwa wenye macho. زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ الشَّهَوَاتِ مِنَ النِّسَاءِ وَالْبَنِينَ وَالْقَنَاطِيرِ الْمُقَنطَرَةِ مِنَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ وَالْخَيْلِ الْمُسَوَّمَةِ وَالْأَنْعَامِ وَالْحَرْثِ ۗ ذَٰلِكَ مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الْمَآبِ ﴿١٤﴾

 

14. Watu wamepambiwa kupenda matamanio (miongoni mwake) wanawake, na watoto, na mirundi ya mali iliyorundikwa ya dhahabu na fedha na farasi wenye chapa (ya aina bora) na wanyama wa mifugo na mashamba. Hayo ni burudisho (liwazo) la maisha ya dunia, na Allaah Kwake kuna marejeo mazuri. قُلْ أَؤُنَبِّئُكُم بِخَيْرٍ مِّن ذَٰلِكُمْ ۚ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَأَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ وَرِضْوَانٌ مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ ﴿١٥﴾

 

15. Sema: “Je, nikujulisheni yaliyo bora kuliko hayo? Kwa wale waliokuwa na taqwa kwa Mola wao (watapata) mabustani yapitayo mito chini yake, watadumu humo (Peponi) milele na wake waliotakasika na radhi kutoka kwa Allaah. Na Allaah ni Baswiyr (Mwenye Kuona yote daima) kwa waja Wake.الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا إِنَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴿١٦﴾

 

16. Wale wasemao: “Mola wetu hakika sisi tumeamini, basi Tughufurie madhambi yetu na Tukinge na adhabu ya Moto.” الصَّابِرِينَ وَالصَّادِقِينَ وَالْقَانِتِينَ وَالْمُنفِقِينَ وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ ﴿١٧﴾

 

17. Wenye kusubiri na wasemao kweli, na watiifu, na watoaji (mali zao fiy sabiyli- Allaah) na waombao maghfirah kabla ya Alfajiri.شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٨﴾

 

18. Allaah Ameshuhudia kwamba laa ilaaha illaa Huwa(hapana mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye); na Malaika, na wenye elimu (wote wameshuhudia kwamba Yeye) ni Mwenye Kusimamisha uadilifu. Laa ilaaha illaa HuwaAl-‘Aziyzul-Hakiym(Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika Daima – Mwenye Hikmah wa yote daima).  إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ ۗ وَمَا اخْتَلَفَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِآيَاتِ اللَّـهِ فَإِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿١٩﴾

 

19. Hakika Dini mbele ya Allaah ni Uislamu. Na hawakukhitilafiana waliopewa Kitabu ila baada ya kuwajia elimu (ikawa) ni chuki baina yao. Na atakayekanusha Aayah za Allaah; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) basi hakika Allaah ni Sariy’ul-Hisaab (Mwepesi wa kuhesabu). فَإِنْ حَاجُّوكَ فَقُلْ أَسْلَمْتُ وَجْهِيَ لِلَّـهِ وَمَنِ اتَّبَعَنِ ۗ وَقُل لِّلَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْأُمِّيِّينَ أَأَسْلَمْتُمْ ۚ فَإِنْ أَسْلَمُوا فَقَدِ اهْتَدَوا ۖ وَّإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ ﴿٢٠﴾

 

20. Na wakikuhoji, basi sema: “Nimesalimisha uso wangu kwa Allaah na yeyote atakayenifuata.” Na waambie waliopewa Kitabu na Al-Ummiyyuwn(wasiojua kusoma na kuandika): “Je mmesilimu?” Wakisilimu basi wameongoka, na wakikengeuka basi hakika juu yako ni kubalighisha. Na Allaah ni Baswiyr(Mwenye Kuona yote daima) kwa waja Wake.إِنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَيَقْتُلُونَ الَّذِينَ يَأْمُرُونَ بِالْقِسْطِ مِنَ النَّاسِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٢١﴾

 

21. Hakika waliokanusha Aayah za Allaah; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) na wakaua Manabii bila ya haki, na wakaua wale wanaoamrisha haki miongoni mwa watu, basi wabashirie adhabu iumizayo.أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٢٢﴾

 

22. Hao ni wale ambao ‘amali zao zimeharibika katika dunia na Aakhirah na hawatopata yeyote mwenye kunusuru. أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُدْعَوْنَ إِلَىٰ كِتَابِ اللَّـهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ يَتَوَلَّىٰ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ وَهُم مُّعْرِضُونَ ﴿٢٣﴾

 

23. Je, hukuona (hukuzingatia ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wale waliopewa sehemu katika Kitabu wanaitwa katika Kitabu cha Allaah ili kiwahukumu baina yao; kisha kundi miongoni mwao linageuka na huku wanapuuza.  ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لَن تَمَسَّنَا النَّارُ إِلَّا أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ ۖ وَغَرَّهُمْ فِي دِينِهِم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٢٤﴾

 

24. Hivyo ni kwa sababu wamesema: “Hautatugusa moto isipokuwa siku za kuhesabika.” Na yakawadanganya katika dini yao yale waliyokuwa wakiyazua. فَكَيْفَ إِذَا جَمَعْنَاهُمْ لِيَوْمٍ لَّا رَيْبَ فِيهِ وَوُفِّيَتْ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٢٥﴾

 

25. Basi itakuwa vipi Tutakapowakusanya katika Siku ambayo haina shaka ndani yake, na kila nafsi italipwa kikamilifu yale iliyochuma; nao hawatodhulumiwa. قُلِ اللَّـهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَن تَشَاءُ وَتَنزِعُ الْمُلْكَ مِمَّن تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَاءُ ۖ بِيَدِكَ الْخَيْرُ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٦﴾

 

26. Sema: “Ee Allaah Mfalme Uliyemiliki ufalme wote, Unampa ufalme Umtakaye, na Unamuondoshea ufalme Umtakaye, na Unamtukuza Umtakaye, na Unamdhalilisha Umtakaye, Kheri imo Mikononi Mwako. Hakika Wewe ni Qadiyr (Muweza daima) wa kila kitu. تُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَتُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ ۖ وَتُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَتُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ ۖ وَتَرْزُقُ مَن تَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٢٧﴾

 

27. Unauingiza usiku katika mchana na Unauingiza mchana katika usiku; na Unamtoa aliyehai kutoka aliye maiti na Unamtoa aliye maiti kutoka aliye hai na Unamruzuku Umtakaye bila ya hesabu. لَّا يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَلَيْسَ مِنَ اللَّـهِ فِي شَيْءٍ إِلَّا أَن تَتَّقُوا مِنْهُمْ تُقَاةً ۗ وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ ۗوَإِلَى اللَّـهِ الْمَصِيرُ ﴿٢٨﴾

 

28. Waumini hawawachukui makafiri kuwa wapenzi wao badala ya Waumini. Na atakayefanya hivyo, basi hatokua na chochote mbele ya Allaah. Isipokuwa mkiwa mnajilinda (kwayo) na shari (zao). Na Allaah Anakutahadharisheni Nafsi Yake. Na Kwa Allaah ni marejeo (ya mwisho). قُلْ إِن تُخْفُوا مَا فِي صُدُورِكُمْ أَوْ تُبْدُوهُ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ ۗ وَيَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٩﴾

 

29. Sema: “Mkificha yale yaliyomo katika vifua vyenu au mkiyafichua, Allaah Anayajua. Na Anajua yale yaliyomo katika mbingu na yale yaliyomo katika ardhi. Na Allaah ni ni Qadiyr (Muweza daima) wa kila kitu.” يَوْمَ تَجِدُ كُلُّ نَفْسٍ مَّا عَمِلَتْ مِنْ خَيْرٍ مُّحْضَرًا وَمَا عَمِلَتْ مِن سُوءٍ تَوَدُّ لَوْ أَنَّ بَيْنَهَا وَبَيْنَهُ أَمَدًا بَعِيدًا ۗ وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ ۗ وَاللَّـهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ ﴿٣٠﴾

 

30. Siku itayokuta kila nafsi yale iliyoyatenda katika kheri yamehudhurishwa, na yale iliyoyatenda katika maovu, itatamani nafsi lau kama ingelikuwa baina yake na baina ya maovu masafa ya mbali. Na Anakutahadharisheni Allaah Nafsi Yake na Allaah ni Rauwf (Mwenye Huruma mno) kwa waja. قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗوَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾

 

31. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa Kughufiria – Mwenye Kurehemu).قُلْ أَطِيعُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْكَافِرِينَ ﴿٣٢﴾

 

32. Sema: “Mtiini Allaah na Mtume, lakini mkikengeuka basi hakika Allaah Hapendi makafiri.”إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ آدَمَ وَنُوحًا وَآلَ إِبْرَاهِيمَ وَآلَ عِمْرَانَ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٣٣﴾

 

33. Hakika Allaah Amemteua Aadam na Nuwh na ukoo wa Ibraahiym na ukoo wa ‘Imraan juu ya Al-‘Aalamiyna (walimwengu). ذُرِّيَّةً بَعْضُهَا مِن بَعْضٍ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٣٤﴾

 

34. Vizazi wao kwa wao, na Allaah ni Samiy’un-‘Aliym(Mwenye Kusikia yote daima – Mjuzi wa yote daima).  إِذْ قَالَتِ امْرَأَتُ عِمْرَانَ رَبِّ إِنِّي نَذَرْتُ لَكَ مَا فِي بَطْنِي مُحَرَّرًا فَتَقَبَّلْ مِنِّي ۖ إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٣٥﴾

 

35. (Tajaee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Aliposema mke wa ‘Imraan: “Mola wangu hakika mimi nimeweka nadhiri Kwako kilichomo katika tumbo langu kuwa ni wakfu, basi nitakabalie. Hakika wewe ni As-Samiy’ul-‘Aliym(Mwenye Kusikia yote daima – Mjuzi wa yote daima). فَلَمَّا وَضَعَتْهَا قَالَتْ رَبِّ إِنِّي وَضَعْتُهَا أُنثَىٰ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا وَضَعَتْ وَلَيْسَ الذَّكَرُ كَالْأُنثَىٰ ۖ وَإِنِّي سَمَّيْتُهَا مَرْيَمَ وَإِنِّي أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ ﴿٣٦﴾

 

36. Basi alipomzaa akasema: “Mola wangu hakika mimi nimezaa mwanamke,” na Allaah Anajua alichokizaa. “Na mwanamme si kama mwanamke. Nami nimemwita Mayram nami namkinga Kwako na kizazi chake kutokana na shaytwaan aliyelaaniwa (aliyewekwa mbali na Rahmah ya Allaah). فَتَقَبَّلَهَا رَبُّهَا بِقَبُولٍ حَسَنٍ وَأَنبَتَهَا نَبَاتًا حَسَنًا وَكَفَّلَهَا زَكَرِيَّا ۖ كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيْهَا زَكَرِيَّا الْمِحْرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزْقًا ۖ قَالَ يَا مَرْيَمُ أَنَّىٰ لَكِ هَـٰذَا ۖ قَالَتْ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ ۖ إِنَّ اللَّـهَ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٣٧﴾

 

37. Basi Mola wake Akampokea kwa kabuli njema na Akamkuza mkuzo mzuri na Akamfanya Zakariyyah kuwa mlezi wake. Kila Zakariyyah alipoingia katika chumba chake cha kuswali, alikuta iko kwake riziki (chakula) Akasema: “Ee Maryam! Umepata wapi hivi? ”Akasema: “Hivi ni kutoka kwa Allaah. Hakika Allaah Anamruzuku Amtakaye bila ya hesabu.” هُنَالِكَ دَعَا زَكَرِيَّا رَبَّهُ ۖ قَالَ رَبِّ هَبْ لِي مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً ۖ إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاءِ ﴿٣٨﴾

 

38. Hapo hapo Zakariyyah akamwomba Mola wake, akasema: “Mola wangu Nitunukie kutoka Kwako kizazi chema hakika Wewe ni Samiy’u (Mwenye Kusikia) du’aa yangu.”فَنَادَتْهُ الْمَلَائِكَةُ وَهُوَ قَائِمٌ يُصَلِّي فِي الْمِحْرَابِ أَنَّ اللَّـهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحْيَىٰ مُصَدِّقًا بِكَلِمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَسَيِّدًا وَحَصُورًا وَنَبِيًّا مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٣٩﴾

 

39. Basi mara Malaika akamwita (Zakariyyah) naye akiwa amesimama anaswali katika chumba cha kuswalia kwamba: “Hakika Allaah Anakubashiria Yahyaa mwenye kusadikisha neno kutoka kwa Allaah na ni bwana na mtawa na Nabii miongoni mwa Asw-Swaalihiyn (waja wema.”) قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَقَدْ بَلَغَنِيَ الْكِبَرُ وَامْرَأَتِي عَاقِرٌ ۖ قَالَ كَذَٰلِكَ اللَّـهُ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ ﴿٤٠﴾

 

40. (Zakariyyah) Akasema: “Nitapataje mwana na hali uzee umeshanifikia na mke wangu ni tasa?!” Akasema: “Hivyo ndivyo Allaah Anafanya Atakavyo”قَالَ رَبِّ اجْعَل لِّي آيَةً ۖ قَالَ آيَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ النَّاسَ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ إِلَّا رَمْزًا ۗوَاذْكُر رَّبَّكَ كَثِيرًا وَسَبِّحْ بِالْعَشِيِّ وَالْإِبْكَارِ ﴿٤١﴾

 

41. (Zakariyyah) Akasema: “Mola wangu niwekee ishara (nipate kutambua kuwa mke wangu ameshika mimba)” Akasema: Ishara yako ni kwamba hutowasemesha watu siku tatu ila kwa kuashiria tu. Na mdhukuru Mola wako kwa wingi na Msabbih(Mtakase) jioni na asubuhi.”وَإِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَاكِ وَطَهَّرَكِ وَاصْطَفَاكِ عَلَىٰ نِسَاءِ الْعَالَمِينَ ﴿٤٢

 

42. Na (Taja) aliposema Malaika: “Ee Maryam! Hakika Allaah Amekuteua na Amekutwaharisha na Amekuteua (Amekufadhilisha) juu ya wanawake wa Al-‘Aalamiyna (walimwengu).” يَا مَرْيَمُ اقْنُتِي لِرَبِّكِ وَاسْجُدِي وَارْكَعِي مَعَ الرَّاكِعِينَ ﴿٤٣﴾

 

43. “Ee Maryam! Kuwa mtiifu kwa Mola wako, na sujudu, na rukuu pamoja na wanaorukuu (katika Swalaah).” ذَٰلِكَ مِنْ أَنبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهِ إِلَيْكَ ۚ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يُلْقُونَ أَقْلَامَهُمْ أَيُّهُمْ يَكْفُلُ مَرْيَمَ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يَخْتَصِمُونَ ﴿٤٤﴾

 

44. Hizo ni khabari za ghayb Tunakufunulia kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na hukuwa pamoja nao walipotupa kalamu zao, nani kati yao amlee Maryam. Na hukuwa pamoja nao walipokhasimiana. إِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللَّـهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٍ مِّنْهُ اسْمُهُ الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ وَجِيهًا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ ﴿٤٥﴾

 

45. (Taja) Aliposema Malaika: “Ee Maryam! Hakika Allaah Anakubashiria neno kutoka Kwake jina lake ni al-Masiyhu ‘Iysaa mwana wa Maryam, mwenye taadhima katika dunia na Aakhirah na ni miongoni mwa waliokurubishwa (kwa Allaah).وَيُكَلِّمُ النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلًا وَمِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٤٦﴾

 

46. Na Atawasemesha watu katika utoto wake na utu uzima wake na ni miongoni mwa Asw-Swaalihiyn(waja wema.) قَالَتْ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي وَلَدٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ ۖ قَالَ كَذَٰلِكِ اللَّـهُ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ إِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٤٧﴾

 

47. Akasema Maryam: “Itakuwaje nipate mtoto na hali hakunigusa (hakuniingilia) mtu?” Akasema (Malaika Jibiriyl): “Hivyo ndivyo Allaah Huumba Akitakacho. Anapokidhia jambo basi hapana ila huliambia: ‘Kun’(Kuwa) nalo huwa.” وَيُعَلِّمُهُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَالتَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ﴿٤٨﴾

 

48. “Na Atamfunza Kitabu na Hikmah na Tawraat na Injiyl.”  وَرَسُولًا إِلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنِّي قَدْ جِئْتُكُم بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ أَنِّي أَخْلُقُ لَكُم مِّنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ فَأَنفُخُ فِيهِ فَيَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۖ وَأُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ وَأُحْيِي الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۖ وَأُنَبِّئُكُم بِمَا تَأْكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِي بُيُوتِكُمْ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٤٩﴾

 

49. “Na ni Mtume kwa wana wa Israaiyl (akisema), Hakika mimi nimekujieni na Aayah (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza) kutoka kwa Mola wenu, kwamba nakuumbieni kutokana na udongo kama umbo la ndege, kisha napuliza humo basi huwa ndege kwa Idhini ya Allaah. Na naponyesha vipofu na wenye mbalanga na nahuisha wafu kwa Idhini ya Allaah. Na nakujulisheni mtakavyokula na mtakavyoweka akiba majumbani mwenu. Hakika katika hayo bila shaka kuna Aayah (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) kwenu mkiwa Waumini (wa kweli).” وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَلِأُحِلَّ لَكُم بَعْضَ الَّذِي حُرِّمَ عَلَيْكُمْ ۚوَجِئْتُكُم بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿٥٠﴾

 

50. “Na mwenye kusadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat na ili nikuhalalishieni baadhi ya yale yaliyoharamishwa kwenu. Na nimekujieni na Aayah (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza.) kutoka kwa Mola wenu. Basi mcheni Allaah na nitiini.”  إِنَّ اللَّـهَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۗ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ ﴿٥١﴾

 

51. “Hakika Allaah ni Mola wangu na Mola wenu basi mwabuduni. Hii ndio Swiraatwil-Mustaqiym (njia iliyonyooka).” فَلَمَّا أَحَسَّ عِيسَىٰ مِنْهُمُ الْكُفْرَ قَالَ مَنْ أَنصَارِي إِلَى اللَّـهِ ۖ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ اللَّـهِ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَاشْهَدْ بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٥٢﴾

 

52. Basi alipohisi ‘Iysaa kutoka kwao ukafiri; alisema: “Nani Answaar (wasaidizi) wangu kwa (ajili ya) Allaah? Wakasema al-Hawaariyyuwn (Wanafunzi wa Nabii ‘Iysaa): “Sisi Answaar wa Allaah. Tumemwamini Allaah na shuhudia kwamba sisi ni Waislamu.” رَبَّنَا آمَنَّا بِمَا أَنزَلْتَ وَاتَّبَعْنَا الرَّسُولَ فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ ﴿٥٣﴾

 

53. “Mola wetu, tumeamini Uliyoyateremsha na tumemfuata Mtume, basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia. وَمَكَرُوا وَمَكَرَ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ ﴿٥٤﴾

 

54. Na wakapanga njama, lakini Allaah Akapanga (kuwalipiza) njama. Na Allaah ni Mbora wa kurudisha njama za wenye kupanga njama.إِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَىٰ إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ وَمُطَهِّرُكَ مِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا وَجَاعِلُ الَّذِينَ اتَّبَعُوكَ فَوْقَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۖ ثُمَّ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأَحْكُمُ بَيْنَكُمْ فِيمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿٥٥﴾

 

55. (Taja) Aliposema Allaah: “Ee ‘Iysaa, hakika Mimi ni Mwenye kukuchukua na Mwenye kukupandisha Kwangu na Mwenye kukutwahirisha kutokana na wale waliokufuru na Nitawafanya wale waliokufuata (wakajisilimisha kwa Allaah Pekee) kuwa juu ya wale waliokufuru mpaka Siku ya Qiyaamah, kisha Kwangu ndio marejeo yenu Nitahukumu baina yenu katika yale mliyokuwa kwayo mkikhitilafiana.”فَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَأُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٥٦﴾

56. Basi wale ambao wamekufuru, Nitawaadhibu adhabu kali katika dunia na Aakhirah, na hawatopata yeyote mwenye kunusuru.وَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُوَفِّيهِمْ أُجُورَهُمْ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ ﴿٥٧﴾

 

57. Ama wale waliomini na wakatenda mema, basi Atawalipa kikamilifu ujira wao. Na Allaah Hapendi madhalimu. ذَٰلِكَ نَتْلُوهُ عَلَيْكَ مِنَ الْآيَاتِ وَالذِّكْرِ الْحَكِيمِ ﴿٥٨﴾

 

58. Hizo Tunakusomea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika Aayah na dhikr (ukumbusho) wenye hikmah.إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِندَ اللَّـهِ كَمَثَلِ آدَمَ ۖ خَلَقَهُ مِن تُرَابٍ ثُمَّ قَالَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٥٩﴾

59. Hakika mfano wa ‘Iysaa kwa Allaah ni kama mfano wa Aadam. Amemuumba kutokana na udongo kisha Akamwambia: ‘Kun’ (Kuwa) basi akawa.الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُن مِّنَ الْمُمْتَرِينَ ﴿٦٠﴾

 

60. Haki kutoka kwa Mola wako, basi usiwe miongoni mwa wanaotia shaka. فَمَنْ حَاجَّكَ فِيهِ مِن بَعْدِ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ فَقُلْ تَعَالَوْا نَدْعُ أَبْنَاءَنَا وَأَبْنَاءَكُمْ وَنِسَاءَنَا وَنِسَاءَكُمْ وَأَنفُسَنَا وَأَنفُسَكُمْ ثُمَّ نَبْتَهِلْ فَنَجْعَل لَّعْنَتَ اللَّـهِ عَلَى الْكَاذِبِينَ ﴿٦١﴾

 

61. Basi yeyote atakayekuhoji kwayo baada ya kukujia elimu, basi sema: “Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsi zetu, na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu, tuifanye laana ya Allaah iwe juu ya waongo (kati yetu). إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْقَصَصُ الْحَقُّ ۚ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٦٢﴾

 

62. Hakika haya ni masimulizi ya haki. Na hakuna ilaaha (Allaah: mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki) isipokuwa Allaah. Na hakika Allaah Yeye Ndiye  Al-‘Aziyzul-Hakiym(Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika daima – Mwenye Hikmah wa yote daima).  فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِالْمُفْسِدِينَ ﴿٦٣﴾

 

63. Wakikengeuka, basi hakika Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi wa yote daima) wa mafisadi. قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٦٤﴾

 

64. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaabi! (Mayahudi na Manaswaara) Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu, kwamba tusiabudu isipokuwa Allaah Pekee, na wala tusimshirkishe na chochote, na wala tusichukue baadhi yetu sisi kwa sisi waungu badala ya Allaah.” Wakikengeuka; basi semeni: “Shuhudieni kwamba sisi ni Waislamu.” يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تُحَاجُّونَ فِي إِبْرَاهِيمَ وَمَا أُنزِلَتِ التَّوْرَاةُ وَالْإِنجِيلُ إِلَّا مِن بَعْدِهِ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٦٥﴾

 

65. Enyi Ahlal-Kitaabi!(Mayahudi na Manaswaara) Kwanini mnahojiana kuhusu Ibraahiym na hali haikuteremshwa Tawraat na Injiyl isipokuwa baada yake? Je, hamtii akilini?هَا أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ حَاجَجْتُمْ فِيمَا لَكُم بِهِ عِلْمٌ فَلِمَ تُحَاجُّونَ فِيمَا لَيْسَ لَكُم بِهِ عِلْمٌ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٦٦﴾

 

66. Ha! (Angalieni) nyinyi ndio hawa mliohojiana katika yale ambayo mnayo elimu nayo, basi kwa nini (sasa) mnahojiana katika yale msiyokuwa na elimu nayo? Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui. مَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَـٰكِن كَانَ حَنِيفًا مُّسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٦٧﴾

 

67. Hakuwa Ibraahiym Yahudi wala Naswara; lakini alikuwa haniyfaa, (aliyejiengua na dini potofu akaelemea Dini ya haki); Muislamu; na hakuwa miongoni mwa washirikna. إِنَّ أَوْلَى النَّاسِ بِإِبْرَاهِيمَ لَلَّذِينَ اتَّبَعُوهُ وَهَـٰذَا النَّبِيُّ وَالَّذِينَ آمَنُوا ۗ وَاللَّـهُ وَلِيُّ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٦٨﴾

 

68. Hakika watu waliokaribu zaidi kwa Ibraahiym ni wale ambao waliomfuata (wakajisilimisha kwa Allaah) na huyu Nabii (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na wale walioamini. Na Allaah ni Walii wa Waumini. وَدَّت طَّائِفَةٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يُضِلُّونَكُمْ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿٦٩﴾

 

69. Linatamani kundi katika Ahlil-Kitaabi (Mayahudi na Manaswaara) kama wangelikupotezeni. Na hawapotezi ila nafsi zao na hawahisi. يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَأَنتُمْ تَشْهَدُونَ ﴿٧٠﴾

 

70. Enyi Ahlal-Kitaabi! (Mayahudi na Manaswaara) Kwanini mnakanusha Ayaah Allaah (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza) na hali nyinyi mnashuhudia? يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَلْبِسُونَ الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُونَ الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٧١﴾

 

71. Enyi Ahlal-Kitaabi! (Mayahudi na Manaswaara) Kwanini mnachanganya haki na batili na mnaficha haki na hali nyinyi mnajua? وَقَالَت طَّائِفَةٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ آمِنُوا بِالَّذِي أُنزِلَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَجْهَ النَّهَارِ وَاكْفُرُوا آخِرَهُ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿٧٢﴾

 

72. Na kundi miongoni mwa Ahlil-Kitaabi (Mayahudi na Manaswaara) likasema (kuambiana): “Aminini yale ambayo yameteremshwa kwa wale walioamini mwanzo wa mchana na kanusheni mwisho wake, wapate kurejea (waache dini yao).”وَلَا تُؤْمِنُوا إِلَّا لِمَن تَبِعَ دِينَكُمْ قُلْ إِنَّ الْهُدَىٰ هُدَى اللَّـهِ أَن يُؤْتَىٰ أَحَدٌ مِّثْلَ مَا أُوتِيتُمْ أَوْ يُحَاجُّوكُمْ عِندَ رَبِّكُمْ ۗ قُلْ إِنَّ الْفَضْلَ بِيَدِ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٧٣﴾

 

73. “Na wala msimwamini isipokuwa yule anayefuata dini yenu”. Sema (Ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika Al-Hudaa (Uongofu) ni Huda-Allaahi(Uongofu wa Allaah) (mnakhofu) kwamba atapewa mmoja (elimu) mfano wa yale mlivyopewa nyinyi au (kisha) wakuhojini mbele ya Allaah.” Sema: “Hakika Fadhila zi Mkononi mwa Allaah; Humpa Amtakaye. Na Allaah ni Waasi’un-‘Aliym (Mwenye Wasaa, Mkunjufu – Mjuzi wa yote daima). يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٧٤﴾

 

74. Humchagua kwa Rahmah Yake Amtakaye; na Allaah ni Mwenye Fadhila kubwa.وَمِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مَنْ إِن تَأْمَنْهُ بِقِنطَارٍ يُؤَدِّهِ إِلَيْكَ وَمِنْهُم مَّنْ إِن تَأْمَنْهُ بِدِينَارٍ لَّا يُؤَدِّهِ إِلَيْكَ إِلَّا مَا دُمْتَ عَلَيْهِ قَائِمًا ۗ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لَيْسَ عَلَيْنَا فِي الْأُمِّيِّينَ سَبِيلٌ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٥﴾

 

75. Na katika Ahlil-Kitaab (Mayahudi na Manaswaara) yuko ambaye ukimpa amana ya mrundi (wa mali) atakurejeshea, na katika wao yuko ambaye ukimpa amana ya dinari moja (tu) hatoirudisha kwako isipokuwa utakapodumisha kumsimamia (kumdai). Hilo ni kwa sababu wao wamesema: “Hakuna juu yetu lawama kwa ummiyyiyn (wasiojua kusoma na kuandika)” na wanamsingizia uongo Allaah, na wao wanajua.بَلَىٰ مَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ وَاتَّقَىٰ فَإِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ ﴿٧٦﴾

 

76. Bali sivyo! Atakayetimiza ahadi yake akawa na taqwa, basi hakika Allaah Anapenda Al-Muttaqiyn(wamchao Allaah). إِنَّ الَّذِينَ يَشْتَرُونَ بِعَهْدِ اللَّـهِ وَأَيْمَانِهِمْ ثَمَنًا قَلِيلًا أُولَـٰئِكَ لَا خَلَاقَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّـهُ وَلَا يَنظُرُ إِلَيْهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٧﴾

 

77. Hakika wale ambao wanauza Ahadi ya Allaah na viapo vyao kwa thamani ndogo; hao hawana sehemu yoyote katika Aakhirah na wala Allaah Hatowasemesha na wala Hatowatazama Siku Ya Qiyaamah na wala Hatowatakasa na watapata adhabu iumizayo. وَإِنَّ مِنْهُمْ لَفَرِيقًا يَلْوُونَ أَلْسِنَتَهُم بِالْكِتَابِ لِتَحْسَبُوهُ مِنَ الْكِتَابِ وَمَا هُوَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَقُولُونَ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَمَا هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٨﴾

 

78. Na hakika miongoni mwao kuna kundi wanaopinda ndimi zao kwa (kusoma) Kitabu ili mdhanie kuwa hayo ni yanayotoka katika Kitabu, na hali hayo si yenye kutoka katika Kitabu, na wanasema: “Hayo ni kutoka kwa Allaah”; na hali hayo si kutoka kwa Allaah na wanamsingizia uongo Allaah na wao wanajua. مَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُؤْتِيَهُ اللَّـهُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ثُمَّ يَقُولَ لِلنَّاسِ كُونُوا عِبَادًا لِّي مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِن كُونُوا رَبَّانِيِّينَ بِمَا كُنتُمْ تُعَلِّمُونَ الْكِتَابَ وَبِمَا كُنتُمْ تَدْرُسُونَ ﴿٧٩﴾

 

79. Haiwi (mustahili) kwa mtu kwamba Allaah amempa Kitabu na Hikmah na Unabii (Utume) kisha awaambie watu: “Kuweni wenye kuniabudu mimi badala ya Allaah” Bali (yeye atawaambia): “Kuweni rabbaaniyyiyn (waja wanaoabudu) kwa yale mliyokuwa mkiyafundisha (ya) Kitabu na kwa yale mliyokuwa mkiyasoma.”وَلَا يَأْمُرَكُمْ أَن تَتَّخِذُوا الْمَلَائِكَةَ وَالنَّبِيِّينَ أَرْبَابًا ۗ أَيَأْمُرُكُم بِالْكُفْرِ بَعْدَ إِذْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿٨٠﴾

 

80. Na wala hakuamuruni kuwachukua Malaika na Manabii kuwafanya miungu. Je anakuamrisheni ukafiri baada ya nyinyi kuwa Waislamu? وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ النَّبِيِّينَ لَمَا آتَيْتُكُم مِّن كِتَابٍ وَحِكْمَةٍ ثُمَّ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مُّصَدِّقٌ لِّمَا مَعَكُمْ لَتُؤْمِنُنَّ بِهِ وَلَتَنصُرُنَّهُ ۚ قَالَ أَأَقْرَرْتُمْ وَأَخَذْتُمْ عَلَىٰ ذَٰلِكُمْ إِصْرِي ۖ قَالُوا أَقْرَرْنَا ۚ قَالَ فَاشْهَدُوا وَأَنَا مَعَكُم مِّنَ الشَّاهِدِينَ ﴿٨١﴾

 

81. Na (kumbukeni enyi watu wa Kitabu) Alipochukua Allaah fungamano kwa Manabii (akawaambia) “Kwa niliyokupeni kutoka Kitabu na Hikmah, kisha akakujieni Mtume mwenye kusadikisha yaliyo pamoja nanyi; (akawaambia) ni juu yenu kumwamini na kumnusuru.” Akasema (Allaah): “Je, mmekiri na mmekubali kuchukua juu ya hayo Agizo Langu?” Wakasema: “Tumekiri”. Akasema (Allaah): “Basi shuhudieni na Mimi Niko pamoja nanyi katika wenye kushuhudia.”فَمَن تَوَلَّىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿٨٢﴾

82. Basi atakayekengeuka baada ya hayo, basi hao ni mafasiki.أَفَغَيْرَ دِينِ اللَّـهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ ﴿٨٣﴾

 

83. Je, wanataka dini isiyokuwa ya Allaah, na hali Kwake amesilimu kila aliye katika mbingu na katika ardhi kwa akipenda asipende na Kwake watarejeshwa. قُلْ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ عَلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَالنَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿٨٤﴾

 

84. Sema: “Tumemwamini Allaah, na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym, na Ismaa’iyl na Is-haaq, na Ya’quwb na al-Asbaatw (vizazi) na yale aliyopewa Muwsaa na ‘Iysaa na Manabii kutoka kwa Mola wao, hatutofautishi baina ya mmoja yeyote miongoni mwao, nasi ni Kwake tumejisalimisha. وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٨٥﴾

 

85. Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake; naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika. كَيْفَ يَهْدِي اللَّـهُ قَوْمًا كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ وَشَهِدُوا أَنَّ الرَّسُولَ حَقٌّ وَجَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٦﴾

 

86. Vipi Allaah Atawahidi watu waliokufuru baada ya kuamini kwao na wakashuhudia kwamba Mtume ni haki na ikawajia hoja bayana? Na Allaah Hawahidi watu madhalimu. أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُمْ أَنَّ عَلَيْهِمْ لَعْنَةَ اللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ﴿٨٧﴾

 

87. Hao jazaa yao ni kwamba juu yao ipo laana ya Allaah na ya Malaika na watu wote. خَالِدِينَ فِيهَا لَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ ﴿٨٨﴾

 

88. Watadumu humo milele hawatopunguziwa adhabu wala hawatopewa muda wa kuakhirishwa adhabu. إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٨٩﴾

 

89. Isipokuwa wale waliotubu baada ya hayo na wakatengenea, basi hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa Kughufiria- Mwenye Kurehemu).إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ ثُمَّ ازْدَادُوا كُفْرًا لَّن تُقْبَلَ تَوْبَتُهُمْ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الضَّالُّونَ ﴿٩٠﴾

90. Hakika wale waliokufuru baada ya kuamini kwao kisha wakazidi kukufuru; haitokubaliwa tawbah yao, na hao ndio waliopotoka. إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يُقْبَلَ مِنْ أَحَدِهِم مِّلْءُ الْأَرْضِ ذَهَبًا وَلَوِ افْتَدَىٰ بِهِ ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٩١﴾

91. Hakika wale waliokufuru na wakafa nao wakiwa makafiri, basi haitakubaliwa kutoka kwa mmoja wao (fidia ya) dhahabu ya kujaza dunia nzima lau wakitaka kujikombolea nayo. Hao watapata adhabu iumizayo na hawatopata mwenye kuwanusuru.

Report Page