026 - Ash-Shu'araa
الشُّعَرآءAsh-Shu’araa: 26
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
طسم ﴿١﴾
1. Twaa Siyn Miym.
تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿٢﴾
2. Hizo ni Aayaat za Kitabu kilicho bayana.
لَعَلَّكَ بَاخِعٌ نَّفْسَكَ أَلَّا يَكُونُوا مُؤْمِنِينَ﴿٣﴾
3. Huenda utaiangamiza nafsi yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa sikitiko kwamba hawawi wenye kuamini.
إِن نَّشَأْ نُنَزِّلْ عَلَيْهِم مِّنَ السَّمَاءِ آيَةً فَظَلَّتْ أَعْنَاقُهُمْ لَهَا خَاضِعِينَ ﴿٤﴾
4. Tungetaka Tungewateremshia kutoka mbinguni Aayah, (muujiza, ishara) kisha zingebakia shingo zao zenye kuinyenyekea.
وَمَا يَأْتِيهِم مِّن ذِكْرٍ مِّنَ الرَّحْمَـٰنِ مُحْدَثٍ إِلَّا كَانُوا عَنْهُ مُعْرِضِينَ ﴿٥﴾
5. Na hauwafikii ukumbusho wowote ule mpya kutoka kwa Ar-Rahmaan isipokuwa walikuwa ni wenye kuupuuza.
فَقَدْ كَذَّبُوا فَسَيَأْتِيهِمْ أَنبَاءُ مَا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٦﴾
6. Basi kwa yakini wamekadhibisha, basi itawafikia khabari ya yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.
أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَى الْأَرْضِ كَمْ أَنبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍ كَرِيمٍ ﴿٧﴾
7. Je, hawaioni ardhi, mimea mingapi Tumeiotesha humo ya kila aina nzuri?
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٨﴾
8. Hakika katika hayo pana Aayah (ishara, zingatio n.k.), lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿٩﴾
9. Na hakika Rabb wako bila shaka Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kurehemu.
وَإِذْ نَادَىٰ رَبُّكَ مُوسَىٰ أَنِ ائْتِ الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿١٠﴾
10. Na Rabb wako Alipomwita Muwsaa kwamba: “Nenda kwa watu madhalimu.”
قَوْمَ فِرْعَوْنَ ۚ أَلَا يَتَّقُونَ ﴿١١﴾
11. “Watu wa Fir’awn; je, hawamchi Allaah?”
قَالَ رَبِّ إِنِّي أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ﴿١٢﴾
12. (Muwsaa) Akasema: “Rabb wangu! Hakika mimi nakhofu wasije kunikadhibisha.”
وَيَضِيقُ صَدْرِي وَلَا يَنطَلِقُ لِسَانِي فَأَرْسِلْ إِلَىٰ هَارُونَ ﴿١٣﴾
13. “Na kinadhikika kifua changu, na wala ulimi wangu haukunjuki vizuri basi mtume Haaruwn.”
وَلَهُمْ عَلَيَّ ذَنبٌ فَأَخَافُ أَن يَقْتُلُونِ﴿١٤﴾
14. “Nao wana (madai ya) dhambi juu yangu, basi nakhofu wasiniue.”
قَالَ كَلَّا ۖ فَاذْهَبَا بِآيَاتِنَا ۖ إِنَّا مَعَكُم مُّسْتَمِعُونَ ﴿١٥﴾
15. (Allaah) Akasema: “Hapana! Nendeni kwa Aayaat (ishara, dalili) Zetu, hakika Sisi Tuko pamoja nanyi Wenye kusikiliza.”
فَأْتِيَا فِرْعَوْنَ فَقُولَا إِنَّا رَسُولُ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦﴾
16. “Basi mfikieni Fir’awn, na mseme: “Hakika sisi ni Rasuli wa Rabb wa walimwengu.”
أَنْ أَرْسِلْ مَعَنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿١٧﴾
17. “Waachilie wana wa Israaiyl waondoke pamoja nasi.”
قَالَ أَلَمْ نُرَبِّكَ فِينَا وَلِيدًا وَلَبِثْتَ فِينَا مِنْ عُمُرِكَ سِنِينَ ﴿١٨﴾
18. (Fira’wn) Akasema: “Je, hatukukulea kwetu ulipokuwa mtoto, na ukaishi kwetu miaka mingi ya umri wako.
وَفَعَلْتَ فَعْلَتَكَ الَّتِي فَعَلْتَ وَأَنتَ مِنَ الْكَافِرِينَ ﴿١٩﴾
19. “Na ukafanya kitendo chako ambacho ulikifanya nawe ni miongoni mwa wasio na shukurani.”
قَالَ فَعَلْتُهَا إِذًا وَأَنَا مِنَ الضَّالِّينَ﴿٢٠﴾
20. (Muwsaa) Akasema: “Nilikifanya hapo wakati nilikuwa miongoni mwa waliokosea.
فَفَرَرْتُ مِنكُمْ لَمَّا خِفْتُكُمْ فَوَهَبَ لِي رَبِّي حُكْمًا وَجَعَلَنِي مِنَ الْمُرْسَلِينَ﴿٢١﴾
21. “Nikakukimbieni nilipokukhofuni, na Rabb wangu Akanitunukia hikmah na Akanijalia ni miongoni mwa Rusuli.
وَتِلْكَ نِعْمَةٌ تَمُنُّهَا عَلَيَّ أَنْ عَبَّدتَّ بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿٢٢﴾
22. “Na hiyo ni neema unayonisimbulia, kwamba umewatia utumwani wana wa Israaiyl.”
قَالَ فِرْعَوْنُ وَمَا رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٢٣﴾
23. Fir’awn Akasema: “Na ni nani kwani Rabb wa walimwengu?”
قَالَ رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ ﴿٢٤﴾
24. (Muwsaa) Akasema: “Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake mkiwa ni wenye yakini.”
قَالَ لِمَنْ حَوْلَهُ أَلَا تَسْتَمِعُونَ ﴿٢٥﴾
25. (Fir’awn) Akawaambia waliomzunguka: “Je, hamsikilizi kwa makini?”
قَالَ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ ﴿٢٦﴾
26. (Muwsaa) Akasema: “Rabb wenu na Rabb wa baba zenu wa awali.”
قَالَ إِنَّ رَسُولَكُمُ الَّذِي أُرْسِلَ إِلَيْكُمْ لَمَجْنُونٌ ﴿٢٧﴾
27. (Fir’awn) Akasema: “Hakika Rasuli wenu ambaye ametumwa kwenu bila shaka ni majununi.”
قَالَ رَبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٢٨﴾
28. (Muwsaa) Akasema: “Rabb wa Mashariki na Magharibi na vilivyo baina yake, mkiwa nyinyi ni wenye kutia akilini.”
قَالَ لَئِنِ اتَّخَذْتَ إِلَـٰهًا غَيْرِي لَأَجْعَلَنَّكَ مِنَ الْمَسْجُونِينَ ﴿٢٩﴾
29. (Fir’wan) Akasema: “Ukichagua mwabudiwa mwengine badala yangu, nitakufanya miongoni mwa wafungwao gerezani.”
قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكَ بِشَيْءٍ مُّبِينٍ ﴿٣٠﴾
30. (Muwsaa) Akasema: “Je, hata kama nikikujia na kitu bayana?”
قَالَ فَأْتِ بِهِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ﴿٣١﴾
31. (Fir’wan) Akasema: “Kilete ukiwa wewe ni miongoni mwa wakweli.”
فَأَلْقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعْبَانٌ مُّبِينٌ﴿٣٢﴾
32. (Muwsaa) Akatupa fimbo yake, tahamaki hiyo ikawa joka kubwa bayana.
وَنَزَعَ يَدَهُ فَإِذَا هِيَ بَيْضَاءُ لِلنَّاظِرِينَ﴿٣٣﴾
33. Na akavuta mkono wake; tahamaki huo ukawa mweupe kwa watazamao.
قَالَ لِلْمَلَإِ حَوْلَهُ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ عَلِيمٌ﴿٣٤﴾
34. (Fir’awn) Akawaambia wakuu waliomzunguka: “Hakika huyu bila shaka ni mchawi mjuzi.
يُرِيدُ أَن يُخْرِجَكُم مِّنْ أَرْضِكُم بِسِحْرِهِ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ ﴿٣٥﴾
35. “Anataka kukutoeni kutoka ardhini mwenu kwa sihiri yake; basi mnaamrisha nini?”
قَالُوا أَرْجِهْ وَأَخَاهُ وَابْعَثْ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ ﴿٣٦﴾
36. Wakasema: “Muakhirishe kidogo na kaka yake, na tuma katika miji wakusanyao wachawi.”
يَأْتُوكَ بِكُلِّ سَحَّارٍ عَلِيمٍ ﴿٣٧﴾
37. “Watakujia na kila mchawi mjuzi.”
فَجُمِعَ السَّحَرَةُ لِمِيقَاتِ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ﴿٣٨﴾
38. Basi wakakusanywa wachawi katika mahali na wakati siku maalumu.
وَقِيلَ لِلنَّاسِ هَلْ أَنتُم مُّجْتَمِعُونَ﴿٣٩﴾
39. Na wakaambiwa watu: “Je, mmekwishakusanyika?
لَعَلَّنَا نَتَّبِعُ السَّحَرَةَ إِن كَانُوا هُمُ الْغَالِبِينَ ﴿٤٠﴾
40. “Ili tuwafuate wachawi, wakiwa wao ndio watakaoshinda.”
فَلَمَّا جَاءَ السَّحَرَةُ قَالُوا لِفِرْعَوْنَ أَئِنَّ لَنَا لَأَجْرًا إِن كُنَّا نَحْنُ الْغَالِبِينَ ﴿٤١﴾
41. Basi walipokuja wachawi walimwambia Fir’awn: “Je, tutapata ujira wowote ikiwa sisi tutakuwa wenye kushinda?”
قَالَ نَعَمْ وَإِنَّكُمْ إِذًا لَّمِنَ الْمُقَرَّبِينَ﴿٤٢﴾
42. (Fir’awn) Akasema: “Naam! Na bila shaka nyinyi hapo mtakuwa miongoni mwa waliokurubishwa (kwangu).”
قَالَ لَهُم مُّوسَىٰ أَلْقُوا مَا أَنتُم مُّلْقُونَ﴿٤٣﴾
43. Muwsaa akawambia: “Tupeni vile mnavyotupa.”
فَأَلْقَوْا حِبَالَهُمْ وَعِصِيَّهُمْ وَقَالُوا بِعِزَّةِ فِرْعَوْنَ إِنَّا لَنَحْنُ الْغَالِبُونَ ﴿٤٤﴾
44. Wakatupa kamba zao na fimbo zao; na wakasema: “Kwa utukufu wa Fir’awn! Hakika sisi ni wenye kushinda.”
فَأَلْقَىٰ مُوسَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ تَلْقَفُ مَا يَأْفِكُونَ ﴿٤٥﴾
45. Basi Muwsaa akatupa fimbo yake, tahamaki inameza vyote walivyovizua.
فَأُلْقِيَ السَّحَرَةُ سَاجِدِينَ ﴿٤٦﴾
46. Basi wale wachawi wakaanguka wakisujudu.
قَالُوا آمَنَّا بِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٤٧﴾
47. Wakasema: “Tumemwamini Rabb wa walimwengu.
رَبِّ مُوسَىٰ وَهَارُونَ ﴿٤٨﴾
48. “Rabb wa Muwsaa na Haaruwn.”
قَالَ آمَنتُمْ لَهُ قَبْلَ أَنْ آذَنَ لَكُمْ ۖ إِنَّهُ لَكَبِيرُكُمُ الَّذِي عَلَّمَكُمُ السِّحْرَ فَلَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ۚ لَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَافٍ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٤٩﴾
49. (Fira’wn) Akasema: “Je, mmemwamini kabla sijakupeni idhini? Hakika bila shaka kubwa lenu ndiye amekufunzeni sihiri. Basi mtakuja kujua. Nitakukatenikateni mikono yenu na miguu yenu kinyume (kulia kwa kushoto), kisha nitakusulubuni nyote.”
قَالُوا لَا ضَيْرَ ۖ إِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ﴿٥٠﴾
50. Wakasema: “Hakuna dhara yoyote! Hakika sisi tunarudi kwa Rabb wetu.
إِنَّا نَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لَنَا رَبُّنَا خَطَايَانَا أَن كُنَّا أَوَّلَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٥١﴾
51. “Hakika sisi tunatumai kwamba Rabb wetu Atatughufuria madhambi yetu kwa vile tumekuwa wa kwanza wenye kuamini.”
وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنْ أَسْرِ بِعِبَادِي إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ ﴿٥٢﴾
52. Na Tukamfunulia Wahy Muwsaa kwamba: “Safiri usiku pamoja na waja Wangu, hakika nyinyi ni wenye kufuatwa.”
فَأَرْسَلَ فِرْعَوْنُ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ﴿٥٣﴾
53. Basi Fir’awn akawatuma wakusanyao wachawi katika miji.
إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ لَشِرْذِمَةٌ قَلِيلُونَ ﴿٥٤﴾
54. (Akisema): “Hakika hawa ni kikosi kidhaifu kidogo, wachache.”
وَإِنَّهُمْ لَنَا لَغَائِظُونَ ﴿٥٥﴾
55. “Na hakika wao wanatughadhibisha.
وَإِنَّا لَجَمِيعٌ حَاذِرُونَ ﴿٥٦﴾
56. “Na hakika sisi, bila shaka ni jamii wenye kuchukua hadhari mno.”
فَأَخْرَجْنَاهُم مِّن جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ ﴿٥٧﴾
57. Basi Tukawatoa katika mabustani na chemchemu.
وَكُنُوزٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ ﴿٥٨﴾
58. Na mahazina na vyeo vya heshima.
كَذَٰلِكَ وَأَوْرَثْنَاهَا بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿٥٩﴾
59. Hivyo ndivyo (Tulivyofanya); na Tukayarithisha hayo wana wa Israaiyl.
فَأَتْبَعُوهُم مُّشْرِقِينَ ﴿٦٠﴾
60. Basi wakawafuata walipopambazukiwa.
فَلَمَّا تَرَاءَى الْجَمْعَانِ قَالَ أَصْحَابُ مُوسَىٰ إِنَّا لَمُدْرَكُونَ ﴿٦١﴾
61. Yalipoonana makundi mawili, wakasema watu wa Muwsaa: “Hakika sisi bila shaka tutadirikiwa kukamatwa.”
قَالَ كَلَّا ۖ إِنَّ مَعِيَ رَبِّي سَيَهْدِينِ﴿٦٢﴾
62. (Muwsaa) akasema: “Hapana! Hakika Rabb wangu Yu pamoja nami Ataniongoza.”
فَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنِ اضْرِب بِّعَصَاكَ الْبَحْرَ ۖ فَانفَلَقَ فَكَانَ كُلُّ فِرْقٍ كَالطَّوْدِ الْعَظِيمِ ﴿٦٣﴾
63. Tukamfunulia Wahy Muwsaa kwamba: “Piga kwa fimbo yako bahari.” Basi ikatengana ikawa kila sehemu kama jabali kubwa mno.
وَأَزْلَفْنَا ثَمَّ الْآخَرِينَ ﴿٦٤﴾
64. Na Tukawaleta karibu hapo wengine.
وَأَنجَيْنَا مُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُ أَجْمَعِينَ﴿٦٥﴾
65. Tukamuokoa Muwsaa na walio pamoja naye wote.
ثُمَّ أَغْرَقْنَا الْآخَرِينَ ﴿٦٦﴾
66. Kisha Tukawagharikisha wengine.
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٦٧﴾
67. Hakika katika hayo pana Aayah (ishara, zingatio n.k.), lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿٦٨﴾
68. Na hakika Rabb wako bila shaka Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kurehemu.
وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ إِبْرَاهِيمَ ﴿٦٩﴾
69. Na wasomee (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) khabari za Ibraahiym.
إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ مَا تَعْبُدُونَ﴿٧٠﴾
70. Alipomwambia baba yake na watu wake: “Mnaabudu nini?”
قَالُوا نَعْبُدُ أَصْنَامًا فَنَظَلُّ لَهَا عَاكِفِينَ﴿٧١﴾
71. Wakasema: “Tunaabudu masanamu, na tutaendelea kuyakalia kwa kuyaabudu.”
قَالَ هَلْ يَسْمَعُونَكُمْ إِذْ تَدْعُونَ ﴿٧٢﴾
72. Akasema: “Je, yanakusikieni mnapoyaomba?”
أَوْ يَنفَعُونَكُمْ أَوْ يَضُرُّونَ ﴿٧٣﴾
73. “Au yanakunufaisheni au yanakudhuruni?”
قَالُوا بَلْ وَجَدْنَا آبَاءَنَا كَذَٰلِكَ يَفْعَلُونَ﴿٧٤﴾
74. Wakasema: “Tumewakuta baba zetu wakifanya hivyo.”
قَالَ أَفَرَأَيْتُم مَّا كُنتُمْ تَعْبُدُونَ ﴿٧٥﴾
75. Akasema: “Je, mnaona hivyo mlivyokuwa mkiviabudu?
أَنتُمْ وَآبَاؤُكُمُ الْأَقْدَمُونَ ﴿٧٦﴾
76. “Nyinyi na baba zenu waliotangulia?
فَإِنَّهُمْ عَدُوٌّ لِّي إِلَّا رَبَّ الْعَالَمِينَ ﴿٧٧﴾
77. “Basi hakika hao ni adui zangu isipokuwa Rabb wa walimwengu.
الَّذِي خَلَقَنِي فَهُوَ يَهْدِينِ ﴿٧٨﴾
78. “Ambaye Ameniumba, Naye Ananiongoza.”
وَالَّذِي هُوَ يُطْعِمُنِي وَيَسْقِينِ ﴿٧٩﴾
79. “Na Ambaye Ndiye Anayenilisha na Ananinywesha.
وَإِذَا مَرِضْتُ فَهُوَ يَشْفِينِ ﴿٨٠﴾
80. “Na ninapokuwa mgonjwa, basi Yeye Ananiponyesha.
وَالَّذِي يُمِيتُنِي ثُمَّ يُحْيِينِ ﴿٨١﴾
81. “Na Ambaye Atanifisha kisha Atanihuisha.
وَالَّذِي أَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لِي خَطِيئَتِي يَوْمَ الدِّينِ ﴿٨٢﴾
82. “Na Ambaye natumai Atanighufuria makosa yangu Siku ya Malipo.
رَبِّ هَبْ لِي حُكْمًا وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ ﴿٨٣﴾
83. “Rabb wangu! Nitunukie hikmah; elimu ya Dini na Unikutanishe na Swalihina.
وَاجْعَل لِّي لِسَانَ صِدْقٍ فِي الْآخِرِينَ﴿٨٤﴾
84. “Na Nijaalie kusifika kwa heshima kwa vizazi watakaokuja baadaye.
وَاجْعَلْنِي مِن وَرَثَةِ جَنَّةِ النَّعِيمِ ﴿٨٥﴾
85. “Na Nijaalie miongoni mwa warithi wa Jannah ya neema.
وَاغْفِرْ لِأَبِي إِنَّهُ كَانَ مِنَ الضَّالِّينَ﴿٨٦﴾
86. “Na Mghufurie baba yangu, hakika yeye amekuwa miongoni mwa waliopotea.
وَلَا تُخْزِنِي يَوْمَ يُبْعَثُونَ ﴿٨٧﴾
87. “Na wala Usinihizi Siku watakayofufuliwa.
يَوْمَ لَا يَنفَعُ مَالٌ وَلَا بَنُونَ ﴿٨٨﴾
88. “Siku hayatofaa mali wa watoto.
إِلَّا مَنْ أَتَى اللَّـهَ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ ﴿٨٩﴾
89. “Isipokuwa yule atakayemfikia Allaah na moyo uliosalimika.
وَأُزْلِفَتِ الْجَنَّةُ لِلْمُتَّقِينَ ﴿٩٠﴾
90. Na itakurubishwa Jannah kwa wenye taqwa.
وَبُرِّزَتِ الْجَحِيمُ لِلْغَاوِينَ ﴿٩١﴾
91. Na utadhihirishwa moto uwakao vikali mno kwa wapotofu.
وَقِيلَ لَهُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ تَعْبُدُونَ﴿٩٢﴾
92. Na wataambiwa: “Wako wapi wale mliokuwa mkiwaabudu?”
مِن دُونِ اللَّـهِ هَلْ يَنصُرُونَكُمْ أَوْ يَنتَصِرُونَ ﴿٩٣﴾
93. “Badala ya Allaah. Je, wataweza kukunusuruni au kujinusuru wenyewe?”
فَكُبْكِبُوا فِيهَا هُمْ وَالْغَاوُونَ ﴿٩٤﴾
94. Watapinduliwa gubigubi humo wao na wapotofu.
وَجُنُودُ إِبْلِيسَ أَجْمَعُونَ ﴿٩٥﴾
95. Na majeshi ya Ibliys yote.
قَالُوا وَهُمْ فِيهَا يَخْتَصِمُونَ ﴿٩٦﴾
96. Watasema na huku wao wanakhasimiana humo.
تَاللَّـهِ إِن كُنَّا لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٩٧﴾
97. “Wa-Allaahi! Hakika tulikuwa bila shaka katika upotofu bayana.”
إِذْ نُسَوِّيكُم بِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٩٨﴾
98. “Tulipokusawazisheni na Rabb wa walimwengu.
وَمَا أَضَلَّنَا إِلَّا الْمُجْرِمُونَ ﴿٩٩﴾
99. “Na hakuna aliyetupoteza isipokuwa wakhalifu.