012 - Yuwsuf
يُوسُفْYuwsuf: 12
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿١﴾
1. Alif Laam Raa. Hizo ni Aayaat za Kitabu kinachobainisha.
إِنَّا أَنزَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ﴿٢﴾
2. Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan kwa (lugha ya) Kiarabu ili muifahamu.
نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ بِمَا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ هَـٰذَا الْقُرْآنَ وَإِن كُنتَ مِن قَبْلِهِ لَمِنَ الْغَافِلِينَ ﴿٣﴾
3. Sisi Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) simulizi nzuri kabisa katika Tuliyokufunulia Wahy hii Qur-aan. Na japokuwa kabla yake ulikuwa miongoni mwa wasiojua.
إِذْ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ إِنِّي رَأَيْتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوْكَبًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ رَأَيْتُهُمْ لِي سَاجِدِينَ ﴿٤﴾
4. Pale Yuwsuf alipomwambia baba yake: “Ee baba yangu! Hakika mimi nimeona (ndotoni) nyota kumi na moja na jua na mwezi; nimeziona zikinisujudia.”
قَالَ يَا بُنَيَّ لَا تَقْصُصْ رُؤْيَاكَ عَلَىٰ إِخْوَتِكَ فَيَكِيدُوا لَكَ كَيْدًا ۖ إِنَّ الشَّيْطَانَ لِلْإِنسَانِ عَدُوٌّ مُّبِينٌ﴿٥﴾
5. Akasema: “Ee mwanangu! Usisimulie ndoto yako kwa kaka zako watakupangia njama. Hakika shaytwaan kwa insani ni adui bayana.”
وَكَذَٰلِكَ يَجْتَبِيكَ رَبُّكَ وَيُعَلِّمُكَ مِن تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ وَيُتِمُّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَعَلَىٰ آلِ يَعْقُوبَ كَمَا أَتَمَّهَا عَلَىٰ أَبَوَيْكَ مِن قَبْلُ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿٦﴾
6. Na hivyo ndivyo Atakuteua Rabb wako na Atakufunza tafsiri za hadithi (za ndoto na matukio) na Atakutimizia neema Yake juu yako, na juu ya kizazi cha Ya’quwb, kama Alivyoitimiza kabla juu ya baba zako; Ibraahiym na Is-haaq. Hakika Rabb wako ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.
لَّقَدْ كَانَ فِي يُوسُفَ وَإِخْوَتِهِ آيَاتٌ لِّلسَّائِلِينَ﴿٧﴾
7. Kwa yakini zilikuwepo katika (kisa cha) Yuwsuf na kaka zake Aayaat (ishara, dalili, zingatio) kwa waulizao.
إِذْ قَالُوا لَيُوسُفُ وَأَخُوهُ أَحَبُّ إِلَىٰ أَبِينَا مِنَّا وَنَحْنُ عُصْبَةٌ إِنَّ أَبَانَا لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٨﴾
8. Pale waliposema: “Bila shaka Yuwsuf na ndugu yake (Bin-yaamiyn) ni vipenzi zaidi kwa baba yetu kuliko sisi, na hali sisi ni kikundi chenye nguvu, hakika baba yetu yumo katika kosa bayana.”
اقْتُلُوا يُوسُفَ أَوِ اطْرَحُوهُ أَرْضًا يَخْلُ لَكُمْ وَجْهُ أَبِيكُمْ وَتَكُونُوا مِن بَعْدِهِ قَوْمًا صَالِحِينَ﴿٩﴾
9. “Muueni Yuwsuf, au mtupilieni mbali katika nchi ya mbali ili uso wa baba yenu ukuelekeeni nyinyi na muwe baada ya hapo Swalihina.”
قَالَ قَائِلٌ مِّنْهُمْ لَا تَقْتُلُوا يُوسُفَ وَأَلْقُوهُ فِي غَيَابَتِ الْجُبِّ يَلْتَقِطْهُ بَعْضُ السَّيَّارَةِ إِن كُنتُمْ فَاعِلِينَ﴿١٠﴾
10. Akasema msemaji miongoni wao: “Msimuue Yuwsuf, bali mtupeni katika kisima kirefu watamwokota baadhi ya misafara, ikiwa nyinyi ni wenye (kuazimia) kufanya.”
قَالُوا يَا أَبَانَا مَا لَكَ لَا تَأْمَنَّا عَلَىٰ يُوسُفَ وَإِنَّا لَهُ لَنَاصِحُونَ﴿١١﴾
11. Wakasema: “Ee baba yetu! Una nini, hutuamini juu ya Yuwsuf, na hakika sisi kwake ni wenye kumnasihi?”
أَرْسِلْهُ مَعَنَا غَدًا يَرْتَعْ وَيَلْعَبْ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ﴿١٢﴾
12. “Mpeleke pamoja nasi kesho, ale atakacho na acheze na sisi tutamhifadhi.”
قَالَ إِنِّي لَيَحْزُنُنِي أَن تَذْهَبُوا بِهِ وَأَخَافُ أَن يَأْكُلَهُ الذِّئْبُ وَأَنتُمْ عَنْهُ غَافِلُونَ﴿١٣﴾
13. Akasema: “Hakika mimi inanihuzunisha kwamba nyinyi mwende naye, na nakhofu asije kuliwa na mbwa mwitu; nanyi muwe mmeghafilika naye.”
قَالُوا لَئِنْ أَكَلَهُ الذِّئْبُ وَنَحْنُ عُصْبَةٌ إِنَّا إِذًا لَّخَاسِرُونَ﴿١٤﴾
14. Wakasema: “Ikiwa mbwa mwitu atamla na hali sisi ni kikundi chenye nguvu; hakika sisi hapo bila shaka tutakuwa wenye kukhasirika.”
فَلَمَّا ذَهَبُوا بِهِ وَأَجْمَعُوا أَن يَجْعَلُوهُ فِي غَيَابَتِ الْجُبِّ ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِ لَتُنَبِّئَنَّهُم بِأَمْرِهِمْ هَـٰذَا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ﴿١٥﴾
15. Basi walipokwenda naye, na wakakubaliana wamtie katika kisima kirefu. Tukamtia ilhamu (Yuwsuf) kwamba bila shaka utakuja kuwajulisha jambo lao hili; na hali wao hawahisi.
وَجَاءُوا أَبَاهُمْ عِشَاءً يَبْكُونَ﴿١٦﴾
16. Wakaja kwa baba yao usiku wakilia.
قَالُوا يَا أَبَانَا إِنَّا ذَهَبْنَا نَسْتَبِقُ وَتَرَكْنَا يُوسُفَ عِندَ مَتَاعِنَا فَأَكَلَهُ الذِّئْبُ ۖ وَمَا أَنتَ بِمُؤْمِنٍ لَّنَا وَلَوْ كُنَّا صَادِقِينَ﴿١٧﴾
17. Wakasema: “Ee baba yetu! Hakika sisi tulikwenda tukishindana mbio na tulimwacha Yuwsuf kwenye vitu vyetu; basi mbwa mwitu akamla. Nawe hutotuamini japo tukiwa ni wakweli.”
وَجَاءُوا عَلَىٰ قَمِيصِهِ بِدَمٍ كَذِبٍ ۚ قَالَ بَلْ سَوَّلَتْ لَكُمْ أَنفُسُكُمْ أَمْرًا ۖ فَصَبْرٌ جَمِيلٌ ۖ وَاللَّـهُ الْمُسْتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ﴿١٨﴾
18. Wakaja na shati lake likiwa na damu ya uongo. (Baba yao) Akasema: “Bali zimekushawishini nafsi zenu jambo. Basi subira njema, na Allaah ni Mwenye kuombwa msaada juu ya mnayoyavumisha.”
وَجَاءَتْ سَيَّارَةٌ فَأَرْسَلُوا وَارِدَهُمْ فَأَدْلَىٰ دَلْوَهُ ۖ قَالَ يَا بُشْرَىٰ هَـٰذَا غُلَامٌۚ وَأَسَرُّوهُ بِضَاعَةً ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِمَا يَعْمَلُونَ﴿١٩﴾
19. Ukaja msafara wakamtuma mtekaji maji wao, naye akatumbukiza ndoo yake. Akasema: “Ee bishara njema! Huyu ni ghulamu!” na wakamficha kuwa ni bidhaa. Na Allaah ni Mjuzi kwa yale wanayoyatenda.
وَشَرَوْهُ بِثَمَنٍ بَخْسٍ دَرَاهِمَ مَعْدُودَةٍ وَكَانُوا فِيهِ مِنَ الزَّاهِدِينَ﴿٢٠﴾
20. Wakamuuza kwa thamani pungufu ya dirham za kuhesabika; na walikuwa ni wenye kuridhika na kidogo.
وَقَالَ الَّذِي اشْتَرَاهُ مِن مِّصْرَ لِامْرَأَتِهِ أَكْرِمِي مَثْوَاهُ عَسَىٰ أَن يَنفَعَنَا أَوْ نَتَّخِذَهُ وَلَدًا ۚ وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي الْأَرْضِ وَلِنُعَلِّمَهُ مِن تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ ۚ وَاللَّـهُ غَالِبٌ عَلَىٰ أَمْرِهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿٢١﴾
21. Na yule aliyemnunua huko Misri alimwamrisha mke wake: “Mkirimu makazi yake, asaa akatufaa au tutamchukua kama ni mwanetu.” Na hivyo ndivyo Tulivyommakinisha Yuwsuf katika ardhi na ili Tumfunze tafsiri za masimulizi (ya ndoto na matukio). Na Allaah ni Mwenye kushinda juu ya jambo Lake, lakini watu wengi hawajui.
وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا ۚوَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ﴿٢٢﴾
22. Na (Yuwsuf) alipobaleghe kufikia umri wa kupevuka, Tulimpa hikma na elimu. Na hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsaan.
وَرَاوَدَتْهُ الَّتِي هُوَ فِي بَيْتِهَا عَن نَّفْسِهِ وَغَلَّقَتِ الْأَبْوَابَ وَقَالَتْ هَيْتَ لَكَ ۚ قَالَ مَعَاذَ اللَّـهِ ۖ إِنَّهُ رَبِّي أَحْسَنَ مَثْوَايَ ۖ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ﴿٢٣﴾
23. Na yule mwanamke ambaye yeye (Yuwsuf) alikuwa katika nyumba yake alimtongoza kinyume na nafsi yake; na akafunga milango, na akasema: “Haya njoo!” (Yuwsuf) Akasema: “Najikinga kwa Allaah! Hakika yeye bwana wangu amenifanyia makazi mazuri. Hakika madhalimu hawafaulu.”
وَلَقَدْ هَمَّتْ بِهِ ۖ وَهَمَّ بِهَا لَوْلَا أَن رَّأَىٰ بُرْهَانَ رَبِّهِ ۚ كَذَٰلِكَ لِنَصْرِفَ عَنْهُ السُّوءَ وَالْفَحْشَاءَ ۚ إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُخْلَصِينَ﴿٢٤﴾
24. Na kwa yakini alimtamani (Yuwsuf) na (Yuwsuf) angelimtamani lau kwamba asingeliona buruhani kutoka kwa Rabb wake. Hivyo ndivyo Tunavyomwepusha na uovu na machafu. Hakika yeye ni miongoni mwa waja Wetu waliokhitariwa kwa ikhlaasw zao.
وَاسْتَبَقَا الْبَابَ وَقَدَّتْ قَمِيصَهُ مِن دُبُرٍ وَأَلْفَيَا سَيِّدَهَا لَدَى الْبَابِ ۚ قَالَتْ مَا جَزَاءُ مَنْ أَرَادَ بِأَهْلِكَ سُوءًا إِلَّا أَن يُسْجَنَ أَوْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٢٥﴾
25. Wakakimbilia mlangoni wote wawili na akairarua kanzu yake (Yuwsuf) kwa nyuma, na wakamkuta bwana wake mlangoni. (Mke wa ‘Aziyz) Akasema: “Hakuna jazaa ya anayemtakia uovu ahli wako isipokuwa kufungwa jela au adhabu iumizayo.”
قَالَ هِيَ رَاوَدَتْنِي عَن نَّفْسِي ۚ وَشَهِدَ شَاهِدٌ مِّنْ أَهْلِهَا إِن كَانَ قَمِيصُهُ قُدَّ مِن قُبُلٍ فَصَدَقَتْ وَهُوَ مِنَ الْكَاذِبِينَ﴿٢٦﴾
26. (Yuwsuf) Akasema: “Yeye ndiye aliyenitongoza kinyume na nafsi yangu.” Na akashuhudia shahidi miongoni mwa ahli zake (akasema): “Ikiwa kanzu yake imechanwa mbele, basi mwanamke amesema kweli; naye (Yuwsuf) ni miongoni mwa waongo.”
وَإِن كَانَ قَمِيصُهُ قُدَّ مِن دُبُرٍ فَكَذَبَتْ وَهُوَ مِنَ الصَّادِقِينَ﴿٢٧﴾
27. “Na ikiwa kanzu yake imechanwa nyuma, basi mwanamke amesema uongo; naye (Yuwsuf) ni miongoni mwa wakweli.”
فَلَمَّا رَأَىٰ قَمِيصَهُ قُدَّ مِن دُبُرٍ قَالَ إِنَّهُ مِن كَيْدِكُنَّ ۖ إِنَّ كَيْدَكُنَّ عَظِيمٌ﴿٢٨﴾
28. Basi (mumewe) alipoona kanzu yake imechanwa nyuma; alisema: “Hakika hii ni katika vitimbi vyenu wanawake. Hakika vitimbi vyenu wanawake ni vikubwa mno.”
يُوسُفُ أَعْرِضْ عَنْ هَـٰذَا ۚ وَاسْتَغْفِرِي لِذَنبِكِ ۖ إِنَّكِ كُنتِ مِنَ الْخَاطِئِينَ﴿٢٩﴾
29. “Yuwsuf yaachilie mbali haya. Na mwanamke omba maghfirah kwa ajili ya dhambi yako. Hakika wewe ulikuwa miongoni mwa wenye hatia.”
وَقَالَ نِسْوَةٌ فِي الْمَدِينَةِ امْرَأَتُ الْعَزِيزِ تُرَاوِدُ فَتَاهَا عَن نَّفْسِهِ ۖ قَدْ شَغَفَهَا حُبًّا ۖ إِنَّا لَنَرَاهَا فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٣٠﴾
30. Na wanawake katika mji ule wakasema: “Mke wa ‘Aziyz anataka kumtongoza kijana wake kinyume na nafsi yake. Kwa yakini amemuathiri kwa mapenzi. Hakika sisi tunamuona yumo katika upotofu bayana.”
فَلَمَّا سَمِعَتْ بِمَكْرِهِنَّ أَرْسَلَتْ إِلَيْهِنَّ وَأَعْتَدَتْ لَهُنَّ مُتَّكَأً وَآتَتْ كُلَّ وَاحِدَةٍ مِّنْهُنَّ سِكِّينًا وَقَالَتِ اخْرُجْ عَلَيْهِنَّ ۖفَلَمَّا رَأَيْنَهُ أَكْبَرْنَهُ وَقَطَّعْنَ أَيْدِيَهُنَّ وَقُلْنَ حَاشَ لِلَّـهِ مَا هَـٰذَا بَشَرًا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا مَلَكٌ كَرِيمٌ﴿٣١﴾
31. Basi (mke wa ‘Aziyz) aliposikia kuhusu hila zao, aliwaita na akawaandalia hafla na akampa kila mmoja wao kisu. Kisha akasema: “Tokeza mbele yao.” Basi walipomuona (Yuwsuf) walimpa haiba na utukuzo, wakajikatakata mikono yao, na wakasema: “Utakasifu ni wa Allaah (au Allaah Asijaalie)! Huyu si mtu! Hakuwa huyu ila ni Malaika mtukufu.”
قَالَتْ فَذَٰلِكُنَّ الَّذِي لُمْتُنَّنِي فِيهِ ۖ وَلَقَدْ رَاوَدتُّهُ عَن نَّفْسِهِ فَاسْتَعْصَمَ ۖ وَلَئِن لَّمْ يَفْعَلْ مَا آمُرُهُ لَيُسْجَنَنَّ وَلَيَكُونًا مِّنَ الصَّاغِرِينَ﴿٣٢﴾
32. Akasema: “Basi huyo ndiye mliyekuwa mkinilaumia. Na kwa yakini nilimtamani kinyume na nafsi yake, akajilinda. Na kama hatofanya ninalomuamrisha, basi bila shaka atafungwa jela, na bila shaka atakuwa miongoni mwa waliodhalilishwa.”
قَالَ رَبِّ السِّجْنُ أَحَبُّ إِلَيَّ مِمَّا يَدْعُونَنِي إِلَيْهِ ۖ وَإِلَّا تَصْرِفْ عَنِّي كَيْدَهُنَّ أَصْبُ إِلَيْهِنَّ وَأَكُن مِّنَ الْجَاهِلِينَ﴿٣٣﴾
33. (Yuwsuf) Akasema: “Ee Rabb wangu! Nastahabu zaidi jela kuliko yale wanayoniitia. Na Usiponiepusha na vitimbi vyao nitaelemea kwao na nitakuwa miongoni mwa majahili.”
فَاسْتَجَابَ لَهُ رَبُّهُ فَصَرَفَ عَنْهُ كَيْدَهُنَّ ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ﴿٣٤﴾
34. Basi Rabb wake Akamuitikia; Akamuepusha na vitimbi vyao. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.
ثُمَّ بَدَا لَهُم مِّن بَعْدِ مَا رَأَوُا الْآيَاتِ لَيَسْجُنُنَّهُ حَتَّى حِينٍ﴿٣٥﴾
35. Kisha ikawadhihirikia baada ya kuona Aayaat (dalili) kuwa wamfunge jela kwa muda kidogo.
وَدَخَلَ مَعَهُ السِّجْنَ فَتَيَانِ ۖ قَالَ أَحَدُهُمَا إِنِّي أَرَانِي أَعْصِرُ خَمْرًا ۖوَقَالَ الْآخَرُ إِنِّي أَرَانِي أَحْ مِلُ فَوْقَ رَأْسِي خُبْزًا تَأْكُلُ الطَّيْرُ مِنْهُ ۖ نَبِّئْنَا بِتَأْوِيلِهِ ۖ إِنَّا نَرَاكَ مِنَ الْمُحْسِنِينَ﴿٣٦﴾
36. Wakaingia pamoja naye jela vijana wawili. Mmoja wao akasema: “Hakika mimi najiona ndotoni kuwa nakamua mvinyo.” Na mwengine akasema: “Hakika mimi najiona ndotoni nabeba juu ya kichwa changu mikate wanaila ndege humo. Tujulishe tafsiri yake, hakika sisi tunakuona ni miongoni mwa wafanyao ihsaan.”
قَالَ لَا يَأْتِيكُمَا طَعَامٌ تُرْزَقَانِهِ إِلَّا نَبَّأْتُكُمَا بِتَأْوِيلِهِ قَبْلَ أَن يَأْتِيَكُمَا ۚذَٰلِكُمَا مِمَّا عَلَّمَنِي رَبِّي ۚ إِنِّي تَرَكْتُ مِلَّةَ قَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ﴿٣٧﴾
37. (Yuwsuf) Akasema: “Hakitokufikieni chakula chochote mtakachoruzukiwa isipokuwa nitakujulisheni tafsiri yake kabla hakijakufikieni. Haya ni katika Aliyonifunza Rabb wangu. Hakika mimi nimeacha mila ya watu wasiomwamini Allaah na wao ni wenye kuikanusha Aakhirah.”
وَاتَّبَعْتُ مِلَّةَ آبَائِي إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۚ مَا كَانَ لَنَا أَن نُّشْرِكَ بِاللَّـهِ مِن شَيْءٍ ۚ ذَٰلِكَ مِن فَضْلِ اللَّـهِ عَلَيْنَا وَعَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ﴿٣٨﴾
38. “Na nimefuata mila ya baba zangu; Ibraahiym, na Is-haaq na Ya’quwb. Haikutupasa kumshirikisha Allaah na kitu chochote. Hiyo ni katika fadhila za Allaah juu yetu na juu ya watu, lakini watu wengi hawashukuru.”
يَا صَاحِبَيِ السِّجْنِ أَأَرْبَابٌ مُّتَفَرِّقُونَ خَيْرٌ أَمِ اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ﴿٣٩﴾
39. “Enyi masahibu wangu wawili wa jela. Je, miola wengi wanaofarakana ni bora au Allaah Mmoja Pekee, Mwenye kudhibiti na kudhalilisha, Asiyepingika?”
مَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِهِ إِلَّا أَسْمَاءً سَمَّيْتُمُوهَا أَنتُمْ وَآبَاؤُكُم مَّا أَنزَلَ اللَّـهُ بِهَا مِن سُلْطَانٍ ۚ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّـهِ ۚ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿٤٠﴾
40. “Hamuabudu pasi Naye (Allaah) isipokuwa majina tu mmeyaita nyinyi na baba zenu, Hakuyateremshia Allaah kwayo mamlaka yoyote. Hakuna hukumu isipokuwa ya Allaah. Ameamrisha kwamba msiabudu isipokuwa Yeye Pekee. Hiyo ndio Dini iliyonyooka, lakini watu wengi hawajui.”
يَا صَاحِبَيِ السِّجْنِ أَمَّا أَحَدُكُمَا فَيَسْقِي رَبَّهُ خَمْرًا ۖ وَأَمَّا الْآخَرُ فَيُصْلَبُ فَتَأْكُلُ الطَّيْرُ مِن رَّأْسِهِ ۚقُضِيَ الْأَمْرُ الَّذِي فِيهِ تَسْتَفْتِيَانِ﴿٤١﴾
41. “Enyi masahibu wangu wawili wa jela! Ama mmoja wenu atamnywesha bwana wake mvinyo. Na ama mwengine atasulubiwa, na ndege watakula kutoka kichwani mwake. Imeshahukumiwa jambo ambalo mkiliulizia.”
وَقَالَ لِلَّذِي ظَنَّ أَنَّهُ نَاجٍ مِّنْهُمَا اذْكُرْنِي عِندَ رَبِّكَ فَأَنسَاهُ الشَّيْطَانُ ذِكْرَ رَبِّهِ فَلَبِثَ فِي السِّجْنِ بِضْعَ سِنِينَ﴿٤٢﴾
42. (Yuwsuf) Akasema kumwambia yule aliyejua kuwa ataokoka miongoni mwa wale wawili: “Nikumbuke mbele ya bwana wako.” Lakini shaytwaan alimsahaulisha kumkumbuka kwa bwana wake. Basi akabakia jela miaka kadhaa.
وَقَالَ الْمَلِكُ إِنِّي أَرَىٰ سَبْعَ بَقَرَاتٍ سِمَانٍ يَأْكُلُهُنَّ سَبْعٌ عِجَافٌ وَسَبْعَ سُنبُلَاتٍ خُضْرٍ وَأُخَرَ يَابِسَاتٍ ۖ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ أَفْتُونِي فِي رُؤْيَايَ إِن كُنتُمْ لِلرُّؤْيَا تَعْبُرُونَ﴿٤٣﴾
43. (Kisha) Na mfalme akasema: “Hakika mimi naona ndotoni ng’ombe saba wanene wanaliwa na ng’ombe saba waliokonda, na mashuke saba ya kijani na mengineyo (saba) yabisi. Enyi wakuu! Nifutuni kuhusu ndoto yangu, mkiwa ni wenye kuagua ndoto.”
قَالُوا أَضْغَاثُ أَحْلَامٍ ۖ وَمَا نَحْنُ بِتَأْوِيلِ الْأَحْلَامِ بِعَالِمِينَ﴿٤٤﴾
44. Wakasema: “Mkorogano wa ndoto! Nasi si wenye kujua kufasiri ndoto.”
وَقَالَ الَّذِي نَجَا مِنْهُمَا وَادَّكَرَ بَعْدَ أُمَّةٍ أَنَا أُنَبِّئُكُم بِتَأْوِيلِهِ فَأَرْسِلُونِ﴿٤٥﴾
45. Akasema yule aliyeokoka kati ya wale wawili na akakumbuka baada ya muda: “Mimi nitakujulisheni kuhusu tafsiri yake. Basi, nitumeni.”
يُوسُفُ أَيُّهَا الصِّدِّيقُ أَفْتِنَا فِي سَبْعِ بَقَرَاتٍ سِمَانٍ يَأْكُلُهُنَّ سَبْعٌ عِجَافٌ وَسَبْعِ سُنبُلَاتٍ خُضْرٍ وَأُخَرَ يَابِسَاتٍ لَّعَلِّي أَرْجِعُ إِلَى النَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَعْلَمُونَ﴿٤٦﴾
46. “Yuwsuf! Ee mkweli! Tufutu (ndoto ya) ng’ombe saba wanene wanaliwa na ng’ombe saba waliokonda, na mashuke saba ya kijani na mengineyo (saba) yabisi; ili nirejee kwa watu ili wapate kujua.”
قَالَ تَزْرَعُونَ سَبْعَ سِنِينَ دَأَبًا فَمَا حَصَدتُّمْ فَذَرُوهُ فِي سُنبُلِهِ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّا تَأْكُلُونَ﴿٤٧﴾
47. Akasema: “Mtalima miaka saba mfululizo bila kusita. Mtakachokivuna kiacheni katika mashuke yake isipokuwa kichache mtakachokula.”
ثُمَّ يَأْتِي مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ سَبْعٌ شِدَادٌ يَأْكُلْنَ مَا قَدَّمْتُمْ لَهُنَّ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّا تُحْصِنُونَ﴿٤٨﴾
48. “Kisha itakuja baada ya hapo (miaka) saba ya shida itakayokula vile mlivyovitanguliza kuviweka kwa ajili yao isipokuwa kidogo katika vile mtakavyoweka akiba.”
ثُمَّ يَأْتِي مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ عَامٌ فِيهِ يُغَاثُ النَّاسُ وَفِيهِ يَعْصِرُونَ﴿٤٩﴾
49. “Kisha utakuja baada ya hapo mwaka humo watu watasaidiwa kwa kunyweshewa mvua na humo watakamua (vya kukamuliwa).”
وَقَالَ الْمَلِكُ ائْتُونِي بِهِ ۖ فَلَمَّا جَاءَهُ الرَّسُولُ قَالَ ارْجِعْ إِلَىٰ رَبِّكَ فَاسْأَلْهُ مَا بَالُ النِّسْوَةِ اللَّاتِي قَطَّعْنَ أَيْدِيَهُنَّ ۚإِنَّ رَبِّي بِكَيْدِهِنَّ عَلِيمٌ﴿٥٠﴾
50. Mfalme akasema: “Nileteeni (Yuwsuf).” Basi (Yuwsuf) alipojiwa na mjumbe alisema: “Rejea kwa bwana wako umuulize nini mkasa wa wanawake waliojikata mikono yao. Hakika Rabb wangu kwa vitimbi vyao ni Mjuzi.”