010 - Yuwnus
يُونُس
Yuwnus: 10
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْحَكِيمِ﴿١﴾
1. Alif Laam Raa. Hizo ni Aayaat za Kitabu chenye hikmah.
أَكَانَ لِلنَّاسِ عَجَبًا أَنْ أَوْحَيْنَا إِلَىٰ رَجُلٍ مِّنْهُمْ أَنْ أَنذِرِ النَّاسَ وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا أَنَّ لَهُمْ قَدَمَ صِدْقٍ عِندَ رَبِّهِمْ ۗ قَالَ الْكَافِرُونَ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ مُّبِينٌ﴿٢﴾
2. Je, imekuwa ni ajabu kwa watu kwamba Tumemfunulia Wahy mtu miongoni mwao kwamba: “Waonye watu na wabashirie wale walioamini kwamba watapata cheo kitukufu mbele ya Rabb wao.” Makafiri wakasema: “Hakika huyu bila shaka ni mchawi bayana.”
إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۖ مَا مِن شَفِيعٍ إِلَّا مِن بَعْدِ إِذْنِهِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿٣﴾
3. Hakika Rabb wenu ni Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Akawa juu (Istawaa[1]) ya ‘Arsh. Anaendesha mambo yote. Hakuna mwombezi yeyote ila baada ya idhini Yake. Huyu Ndiye Allaah Rabb Wenu, basi mwabuduni. Je, hamkumbuki?
إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا ۖ وَعْدَ اللَّـهِ حَقًّا ۚإِنَّهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ لِيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ بِالْقِسْطِ ۚ وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ﴿٤﴾
4. Kwake ni marejeo yenu nyote. Ni ahadi ya Allaah ya kweli. Hakika Yeye Anaanzisha uumbaji, kisha Anaurejesha ili Awalipe kwa uadilifu wale walioamini na wakatenda mema. Na wale waliokufuru watapata kinywaji cha maji ya kuchemka, na adhabu iumizayo kwa yale waliyokuwa wakikufuru.
هُوَ الَّذِي جَعَلَ الشَّمْسَ ضِيَاءً وَالْقَمَرَ نُورًا وَقَدَّرَهُ مَنَازِلَ لِتَعْلَمُوا عَدَدَ السِّنِينَ وَالْحِسَابَ ۚ مَا خَلَقَ اللَّـهُ ذَٰلِكَ إِلَّا بِالْحَقِّ ۚ يُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ﴿٥﴾
5. Yeye Ndiye Aliyejaalia jua kuwa ni mwanga na mwezi kuwa ni nuru; na Akaukadiria vituo ili mjue idadi ya miaka na hesabu. Allaah Hakuumba hivyo ila kwa haki. Anafasili waziwazi Aayaat kwa watu wanaojua.
إِنَّ فِي اخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَمَا خَلَقَ اللَّـهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَّقُونَ﴿٦﴾
6. Hakika katika mabadiliko ya mfuatano ya usiku na mchana na Alivyoviumba Allaah katika mbingu na ardhi, bila shaka ni Aayaat (ishara, hoja) kwa watu walio na taqwa.
إِنَّ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا وَرَضُوا بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَاطْمَأَنُّوا بِهَا وَالَّذِينَ هُمْ عَنْ آيَاتِنَا غَافِلُونَ﴿٧﴾
7. Hakika wale wasiotaraji kukutana Nasi, na wakaridhika na uhai wa dunia na wakakinaika nayo, na wale ambao wanaghafilika na Aayaat Zetu.
أولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمُ النَّارُ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٨﴾
8. Hao makazi yao ni moto, kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ يَهْدِيهِمْ رَبُّهُم بِإِيمَانِهِمْ ۖتَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ﴿٩﴾
9. Hakika wale walioamini na wakatenda mema, Rabb wao Atawaongoza kwa iymaan zao. Zitapita chini yao mito katika Jannaat za neema.
دَعْوَاهُمْ فِيهَا سُبْحَانَكَ اللَّـهُمَّ وَتَحِيَّتُهُمْ فِيهَا سَلَامٌ ۚ وَآخِرُ دَعْوَاهُمْ أَنِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿١٠﴾
10. Wito wao humo ni: “Utakasifu ni Wako ee Allaah.” Na maamkizi yao humo ni “Salaamun!” Na wito wao wa mwisho ni “AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah), Rabb wa walimwengu.”
وَلَوْ يُعَجِّلُ اللَّـهُ لِلنَّاسِ الشَّرَّ اسْتِعْجَالَهُم بِالْخَيْرِ لَقُضِيَ إِلَيْهِمْ أَجَلُهُمْ ۖ فَنَذَرُ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ﴿١١﴾
11. Na lau Allaah Angeliwaharakizia watu shari kama wanavyojihimizia khayr, bila shaka wangehukumiwa muda wao (wa kuangamizwa). Basi Tunawaacha wale wasiotarajia kukutana Nasi katika upindukaji mipaka ya kuasi kwao, wakitangatanga kwa upofu.
وَإِذَا مَسَّ الْإِنسَانَ الضُّرُّ دَعَانَا لِجَنبِهِ أَوْ قَاعِدًا أَوْ قَائِمًا فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُ ضُرَّهُ مَرَّ كَأَن لَّمْ يَدْعُنَا إِلَىٰ ضُرٍّ مَّسَّهُ ۚكَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْمُسْرِفِينَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٢﴾
12. Na inapomgusa insani dhara hutuomba anapolala ubavu, au anapokaa au kusimama. Tunapomuondolea dhara, hupita kama kwamba hakutuomba dhara iliyomgusa. Hivyo ndivyo walivyopambiwa wapindukao mipaka yale waliyokuwa wakiyatenda.
وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا الْقُرُونَ مِن قَبْلِكُمْ لَمَّا ظَلَمُوا ۙ وَجَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ وَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْقَوْمَ الْمُجْرِمِينَ﴿١٣﴾
13. Na kwa yakini Tuliangamiza karne nyingi kabla yenu walipodhulumu, na wakawajia Rusuli wao kwa hoja bayana, na hawakuwa wa kuamini. Hivyo ndivyo Tunavyowalipa watu wakhalifu.
ثُمَّ جَعَلْنَاكُمْ خَلَائِفَ فِي الْأَرْضِ مِن بَعْدِهِمْ لِنَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ﴿١٤﴾
14. Kisha Tukakufanyeni warithi katika ardhi baada yao, ili Tutazame vipi mtatenda.
وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ ۙ قَالَ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا ائْتِ بِقُرْآنٍ غَيْرِ هَـٰذَا أَوْ بَدِّلْهُ ۚ قُلْ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أُبَدِّلَهُ مِن تِلْقَاءِ نَفْسِي ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ ۖ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ﴿١٥﴾
15. Na wanaposomewa Aayaat Zetu bayana, wale wasiotaraji kukutana Nasi husema: “Lete Qur-aan isiyokuwa hii au ibadilishe.” Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hainipasii mimi kuibadilisha kwa khiyari ya nafsi yangu. Mimi sifuati ila tu yale nilofunuliwa Wahy. Hakika mimi nakhofu nikimuasi Rabb wangu, adhabu ya siku adhimu.”
قُل لَّوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا تَلَوْتُهُ عَلَيْكُمْ وَلَا أَدْرَاكُم بِهِ ۖ فَقَدْ لَبِثْتُ فِيكُمْ عُمُرًا مِّن قَبْلِهِ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ﴿١٦﴾
16. Sema: “Kama Angetaka Allaah nisingelikusomeeni (hii Qur-aan) na wala Asingelikujulisheni nayo. Kwani nimekwishaishi nanyi umri wote kabla yake. Je, basi hamtii akilini?”
فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْمُجْرِمُونَ﴿١٧﴾
17. Basi nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemtungia Allaah uongo au amekadhibisha Aayaat Zake? Hakika wakhalifu hawatofaulu.
وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ ۚ قُلْ أَتُنَبِّئُونَ اللَّـهَ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ ۚسُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿١٨﴾
18. Na wanaabudu pasi na Allaah ambavyo haviwadhuru wala haviwanufaishi na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.” Sema: “Je, mnamjulisha Allaah kwa yale Asiyoyajua katika mbingu na ardhini?” Utakasifu ni Wake na Ametukuka kwa ‘Uluwa kwa yale yote wanayomshirikisha.
وَمَا كَانَ النَّاسُ إِلَّا أُمَّةً وَاحِدَةً فَاخْتَلَفُوا ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ فِيمَا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ﴿١٩﴾
19. Na wala watu hawakuwa ila ni ummah mmoja kisha wakakhitilafiana. Na kama si neno lililotangulia kutoka kwa Rabb wako; bila shaka ingehukumiwa baina yao katika yale waliyokuwa kwayo wakikhitilafiana.
وَيَقُولُونَ لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِّن رَّبِّهِ ۖفَقُلْ إِنَّمَا الْغَيْبُ لِلَّـهِ فَانتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُنتَظِرِينَ﴿٢٠﴾
20. Na wanasema: “Kwanini haikuteremshwa juu yake Aayah (ishara, dalili) kutoka kwa Rabb wake?” Basi sema: “Hakika ya ghayb ni ya Allaah Pekee. Basi ngojeeni; hakika mimi niko pamoja nanyi miongoni mwa wanaongojea.”
وَإِذَا أَذَقْنَا النَّاسَ رَحْمَةً مِّن بَعْدِ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُمْ إِذَا لَهُم مَّكْرٌ فِي آيَاتِنَا ۚقُلِ اللَّـهُ أَسْرَعُ مَكْرًا ۚ إِنَّ رُسُلَنَا يَكْتُبُونَ مَا تَمْكُرُونَ﴿٢١﴾
21. Na Tunapowaonjesha watu rahmah baada ya dhara iliyowagusa; tahamaki wanafanyia hila katika Aayaat (ishara) Zetu. Sema: “Allaah ni Mwepesi zaidi wa kuvurumisha hila.” Hakika Wajumbe wetu wanaandika yale mnayofanya hila.
هُوَ الَّذِي يُسَيِّرُكُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۖحَتَّىٰ إِذَا كُنتُمْ فِي الْفُلْكِ وَجَرَيْنَ بِهِم بِرِيحٍ طَيِّبَةٍ وَفَرِحُوا بِهَا جَاءَتْهَا رِيحٌ عَاصِفٌ وَجَاءَهُمُ الْمَوْجُ مِن كُلِّ مَكَانٍ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ أُحِيطَ بِهِمْ ۙ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ لَئِنْ أَنجَيْتَنَا مِنْ هَـٰذِهِ لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ﴿٢٢﴾
22. Yeye Ndiye Anayekuendesheni katika bara na bahari. Mpaka mnapokuwa katika majahazi na yanakwenda nao kwa upepo mzuri, na wakafurahia; mara ukawajia upepo wa dhoruba, na yakawajia mawimbi kutoka kila upande, na wakayakinisha kwamba wameshazungukwa. Hapo humwomba Allaah wenye kumtakasia Yeye Dini (wakisema): “Ukituokoa katika haya, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.”
فَلَمَّا أَنجَاهُمْ إِذَا هُمْ يَبْغُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۗ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّمَا بَغْيُكُمْ عَلَىٰ أَنفُسِكُم ۖ مَّتَاعَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ ثُمَّ إِلَيْنَا مَرْجِعُكُمْ فَنُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٢٣﴾
23. Lakini Anapowaokoa, tahamaki wao wanafanya baghi (uasi) katika ardhi bila ya haki. Enyi watu! Hakika baghi yenu ni dhidi ya nafsi zenu. Ni starehe ya uhai wa dunia. Kisha Kwetu marejeo yenu; Tutakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
إِنَّمَا مَثَلُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ مِمَّا يَأْكُلُ النَّاسُ وَالْأَنْعَامُ حَتَّىٰ إِذَا أَخَذَتِ الْأَرْضُ زُخْرُفَهَا وَازَّيَّنَتْ وَظَنَّ أَهْلُهَا أَنَّهُمْ قَادِرُونَ عَلَيْهَا أَتَاهَا أَمْرُنَا لَيْلًا أَوْ نَهَارًا فَجَعَلْنَاهَا حَصِيدًا كَأَن لَّمْ تَغْنَ بِالْأَمْسِ ۚ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿٢٤﴾
24. Hakika mfano wa uhai wa dunia ni kama maji Tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, kisha yakachanganyika nayo mimea ya ardhi katika wanayoila watu na wanyama, mpaka ardhi ilipokamilisha uzuri wake na ikapambika na wakayakinisha watu wake kwamba wanao uwezo juu yake (kuivuna); tahamaki amri Yetu ikaijia usiku au mchana, Tukaifanya kama iliyofekwa kama kwamba haikusitawi jana. Hivyo ndivyo Tunavyofasili waziwazi Aayaat (ishara, hoja) kwa watu wanaotafakari.
وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَىٰ دَارِ السَّلَامِ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٢٥﴾
25. Na Allaah Anaitia katika Daar As-Salaam (Nyumba ya amani) na Anamwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.
لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ ۖ وَلَا يَرْهَقُ وُجُوهَهُمْ قَتَرٌ وَلَا ذِلَّةٌ ۚ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿٢٦﴾
26. Kwa wale waliofanya ihsaanwatapata (jazaa) nzuri kabisa na ziada (kumuona Allaah Jannah). Na wala vumbi halitowafunika nyuso zao na wala udhalilifu. Hao ni watu wa Jannah. Wao humo ni wenye kudumu.
وَالَّذِينَ كَسَبُوا السَّيِّئَاتِ جَزَاءُ سَيِّئَةٍ بِمِثْلِهَا وَتَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۖ مَّا لَهُم مِّنَ اللَّـهِ مِنْ عَاصِمٍ ۖ كَأَنَّمَا أُغْشِيَتْ وُجُوهُهُمْ قِطَعًا مِّنَ اللَّيْلِ مُظْلِمًا ۚ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿٢٧﴾
27. Na wale waliochuma maovu, jazaa ya uovu ni mfano wake vile vile, na udhalilifu utawafunika. Hawatopata atakayewaepusha na (adhabu ya) Allaah. Zitakuwa nyuso zao kamakwamba zimefunikwa na vipande vya usiku wenye giza kubwa. Hao ni watu wa motoni, wao humo ni wenye kudumu.
وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا مَكَانَكُمْ أَنتُمْ وَشُرَكَاؤُكُمْ ۚ فَزَيَّلْنَا بَيْنَهُمْ ۖ وَقَالَ شُرَكَاؤُهُم مَّا كُنتُمْ إِيَّانَا تَعْبُدُونَ﴿٢٨﴾
28. Na Siku Tutakayowakusanya wote, kisha Tutawaambia wale walioshirikisha: “(Bakieni) mahali penu nyinyi na washirika wenu.” Kisha Tutawatenganisha baina yao. Na washirika wao watasema: “Hamkuwa mkituabudu sisi.”
فَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ إِن كُنَّا عَنْ عِبَادَتِكُمْ لَغَافِلِينَ﴿٢٩﴾
29. “Basi Allaah Anatosheleza kuwa Mwenye kushuhudia yote baina yetu na baina yenu kwamba sisi tulikuwa hatuna khabari na ‘ibaadah zenu.”
هُنَالِكَ تَبْلُو كُلُّ نَفْسٍ مَّا أَسْلَفَتْ ۚوَرُدُّوا إِلَى اللَّـهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ ۖ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ﴿٣٠﴾
30. Huko (Qiyaamah) kila nafsi itatiwa mtihanini kwa iliyoyatanguliza. Na watarudishwa kwa Allaah, Mola wao wa haki. Na yatawapotea yale yote waliyokuwa wakiyatunga.
قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أَمَّن يَمْلِكُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَمَن يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۚفَسَيَقُولُونَ اللَّـهُ ۚ فَقُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ﴿٣١﴾
31. Sema: “Nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini. Au nani anayemiliki kusikia na kuona; na nani anayemtoa aliye hai kutoka mfu, na anayemtoa mfu kutoka aliye uhai; na nani anayeendesha mambo (yote)?” Watasema: “Ni Allaah”; basi sema: “Je, basi hamuwi na taqwa?”
فَذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمُ الْحَقُّ ۖ فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ﴿٣٢﴾
32. Basi Huyo Ndiye Allaah, Rabb wenu wa haki. Na kuna nini baada ya haki ila upotofu? Basi wapi mnageuzwa?
كَذَٰلِكَ حَقَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ عَلَى الَّذِينَ فَسَقُوا أَنَّهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ﴿٣٣﴾
33. Hivyo ndivyo Neno la Rabb wako lilivyothibiti juu ya wale waliofanya ufasiki kwamba hawatoamini.
قُلْ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ۚ قُلِ اللَّـهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ﴿٣٤﴾
34. Sema: “Je, yuko kati ya washirika wenu anayeanzisha uumbaji kisha anaurudisha?” Sema: “Allaah Anaanzisha uumbaji kisha Anaurudisha. Basi vipi mnaghilibiwa?
قُلْ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ ۚ قُلِ اللَّـهُ يَهْدِي لِلْحَقِّ ۗ أَفَمَن يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ أَحَقُّ أَن يُتَّبَعَ أَمَّن لَّا يَهِدِّي إِلَّا أَن يُهْدَىٰ ۖ فَمَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ﴿٣٥﴾
35. Sema: “Je, yuko kati ya washirika wenu anayeongoza kwenye haki?” Sema: “Allaah Anaongoza kwenye haki. Je, basi anayeongoza kwenye haki anastahiki zaidi kufuatwa au ambaye asiyeongoza isipokuwa tu yeye aongozwe? Basi mna nini, mnavyohukumu?”
وَمَا يَتَّبِعُ أَكْثَرُهُمْ إِلَّا ظَنًّا ۚ إِنَّ الظَّنَّ لَا يُغْنِي مِنَ الْحَقِّ شَيْئًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِمَا يَفْعَلُونَ﴿٣٦﴾
36. Na wengi wao hawafuati ila dhana tu. Hakika dhana haifai kitu chochote mbele ya haki. Hakika Allaah ni Mjuzi kwa yale yote wayatendayo.
وَمَا كَانَ هَـٰذَا الْقُرْآنُ أَن يُفْتَرَىٰ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِن تَصْدِيقَ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَتَفْصِيلَ الْكِتَابِ لَا رَيْبَ فِيهِ مِن رَّبِّ الْعَالَمِينَ﴿٣٧﴾
37. Na haiwezekani hii Qur-aan kuwa imetungwa pasi na Allaah, lakini inasadikisha yale yaliyokuja kabla yake na ni tafsili ya Kitabu ambayo haina shaka ndani yake imetoka kwa Rabb wa walimwengu.
أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّثْلِهِ وَادْعُوا مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٣٨﴾
38. Je, wanasema (Qur-aan) ameitunga (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)? Sema: “Hebu basi leteni Suwrah ya mfano wake, na waiteni mnaoweza pasi na Allaah mkiwa ni wakweli.”
بَلْ كَذَّبُوا بِمَا لَمْ يُحِيطُوا بِعِلْمِهِ وَلَمَّا يَأْتِهِمْ تَأْوِيلُهُ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الظَّالِمِينَ﴿٣٩﴾
39. Bali wamekadhibisha yale wasiyoyaelewa vyema elimu yake, na wala uhakika wake halisi haujawafikia. Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale wa kabla yao. Basi tazama vipi ilikuwa khatima ya madhalimu.
وَمِنْهُم مَّن يُؤْمِنُ بِهِ وَمِنْهُم مَّن لَّا يُؤْمِنُ بِهِ ۚ وَرَبُّكَ أَعْلَمُ بِالْمُفْسِدِينَ﴿٤٠﴾
40. Na miongoni mwao wako wanaoiamini, na miongoni mwao wako wasioiamini. Na Rabb wako Anawajua zaidi mafisadi.
وَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل لِّي عَمَلِي وَلَكُمْ عَمَلُكُمْ ۖ أَنتُم بَرِيئُونَ مِمَّا أَعْمَلُ وَأَنَا بَرِيءٌ مِّمَّا تَعْمَلُونَ﴿٤١﴾
41. Na wakikukadhibisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi sema: “Mimi nina ‘amali zangu, nanyi mna ‘amali zenu. Nyinyi hamna dhima na yale niyatendayo, na wala mimi sina dhima na yale myatendayo.”
وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُونَ إِلَيْكَ ۚ أَفَأَنتَ تُسْمِعُ الصُّمَّ وَلَوْ كَانُوا لَا يَعْقِلُونَ﴿٤٢﴾
42. Na miongoni mwao ambao wanaokusikiliza. Je, kwani wewe unasikilizisha viziwi japokuwa hawatii akilini?
وَمِنْهُم مَّن يَنظُرُ إِلَيْكَ ۚ أَفَأَنتَ تَهْدِي الْعُمْيَ وَلَوْ كَانُوا لَا يُبْصِرُونَ﴿٤٣﴾
43. Na miongoni mwao ambao wanaokutazama. Je, kwani wewe unaongoza kipofu japokuwa hawaoni?
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ النَّاسَ شَيْئًا وَلَـٰكِنَّ النَّاسَ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ﴿٤٤﴾
44. Hakika Allaah Hadhulumu watu chochote, lakini watu wenyewe ni wenye kudhulumu nafsi zao.
وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ كَأَن لَّمْ يَلْبَثُوا إِلَّا سَاعَةً مِّنَ النَّهَارِ يَتَعَارَفُونَ بَيْنَهُمْ ۚ قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِلِقَاءِ اللَّـهِ وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ﴿٤٥﴾
45. Na Siku Atakayowakusanya (wataona) kama kwamba hawakuishi isipokuwa saa moja ya mchana, watatambuana. Kwa yakini wamekhasirika wale waliokadhibisha kukutana na Allaah, na hawakuwa wenye kuongoka.
وَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعْضَ الَّذِي نَعِدُهُمْ أَوْ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ ثُمَّ اللَّـهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ﴿٤٦﴾
46. Na kama Tutakuonyesha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) baadhi ya yale Tunayowaahidi (ya adhabu) au Tukikufisha, basi Kwetu ni marejeo yao; kisha Allaah ni Mwenye kushuhudia yote juu ya yale wanayoyatenda.
وَلِكُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولٌ ۖ فَإِذَا جَاءَ رَسُولُهُمْ قُضِيَ بَيْنَهُم بِالْقِسْطِ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿٤٧﴾
47. Na kila ummah kuna Rasuli. Basi anapokuja Rasuli wao inahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatodhulumiwa.
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٤٨﴾
48. Na wanasema: “Lini (itafika) hiyo ahadi mkiwa ni wakweli?”
قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي ضَرًّا وَلَا نَفْعًا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۗ لِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ ۚ إِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ فَلَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ﴿٤٩﴾
49. Sema: “Siimilikii nafsi yangu dhara wala manufaa isipokuwa Aliyotaka Allaah. Kwa kila Ummah una muda maalumu. Utakapofika muda wao, basi hawatoweza kuakhirisha saa moja wala hawatoweza kutanguliza.”