@Furqanbot

@Furqanbot


قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُهُ بَيَاتًا أَوْ نَهَارًا مَّاذَا يَسْتَعْجِلُ مِنْهُ الْمُجْرِمُونَ﴿٥٠﴾

50. Sema: “Mnaonaje ikikufikieni adhabu Yake usiku au mchana, sehemu ipi wanaihimiza wakhalifu?”

 

 

 

أَثُمَّ إِذَا مَا وَقَعَ آمَنتُم بِهِ ۚ آلْآنَ وَقَدْ كُنتُم بِهِ تَسْتَعْجِلُونَ﴿٥١﴾

51. Kisha tena itakapotokea ndio mtaiamini? “Je, sasa tena? Na ilhali mlikuwa mnaihimiza?”

 

 

 

ثُمَّ قِيلَ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا ذُوقُوا عَذَابَ الْخُلْدِ هَلْ تُجْزَوْنَ إِلَّا بِمَا كُنتُمْتَكْسِبُونَ﴿٥٢﴾

52. Kisha wataambiwa wale waliodhulumu: “Onjeni adhabu yenye kudumu. Kwani je, mtalipwa isipokuwa kwa yale ambayo mliyokuwa mkiyachuma?”

 

 

 

وَيَسْتَنبِئُونَكَ أَحَقٌّ هُوَ ۖ قُلْ إِي وَرَبِّي إِنَّهُ لَحَقٌّ ۖ وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ﴿٥٣﴾

53. Na wanakuuliza: “Je, hiyo (adhabu na Qiyaamah) ni kweli?” Sema: “Ndio! Naapa kwa Rabb wangu! Hakika hiyo bila shaka ni kweli! Nanyi si wenye kuweza kukwepa.”

 

 

 

وَلَوْ أَنَّ لِكُلِّ نَفْسٍ ظَلَمَتْ مَا فِي الْأَرْضِ لَافْتَدَتْ بِهِ ۗ وَأَسَرُّوا النَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُا الْعَذَابَ ۖ وَقُضِيَ بَيْنَهُم بِالْقِسْطِ ۚ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿٥٤﴾

54. Na kama ingelikuwa kila nafsi iliyodhulumu, inamiliki yote yaliyomo katika ardhi, bila shaka ingeliyatolea fidia kwayo. Na wataficha (au watadhihirisha) majuto watakapoona adhabu. Na itahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatodhulumiwa. 

 

 

 

أَلَا إِنَّ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗأَلَا إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٥٥﴾

55. Tanabahi! Hakika ni vya Allaah vilivyomo katika mbingu na ardhi. Tanabahi! Hakika ahadi ya Allaah ni kweli, lakini wengi wao hawajui.

 

 

 

هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴿٥٦﴾

56. Yeye Ndiye Anayehuisha na Anayefisha, na Kwake mtarejeshwa.

 

 

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَتْكُم مَّوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَشِفَاءٌ لِّمَا فِي الصُّدُورِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ﴿٥٧﴾

57. Enyi watu! Kwa yakini yamekujieni mawaidha kutoka kwa Rabb wenu, na shifaa ya yale yaliyomo vifuani, na mwongozo na rahmah kwa Waumini.

 

 

 

قُلْ بِفَضْلِ اللَّـهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ مِّمَّايَجْمَعُونَ﴿٥٨﴾

58. Sema: “Kwa fadhila za Allaah na kwa rahmah Yake basi kwa hayo wafurahi.” Hayo ni khayr kuliko wanayoyakusanya.

 

 

 

قُلْ أَرَأَيْتُم مَّا أَنزَلَ اللَّـهُ لَكُم مِّن رِّزْقٍ فَجَعَلْتُم مِّنْهُ حَرَامًا وَحَلَالًا قُلْ آللَّـهُ أَذِنَ لَكُمْ ۖ أَمْ عَلَى اللَّـهِ تَفْتَرُونَ﴿٥٩﴾

59. Sema: “Mnaonaje zile riziki Alizokuteremshieni Allaah, kisha mkazifanya katika hizo ni haramu na halali.” Sema: “Je, Allaah Amekupeni idhini au mnamtungia (uongo) Allaah?”

 

 

 

وَمَا ظَنُّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَشْكُرُونَ﴿٦٠﴾

60. Na nini dhana ya wale wanaomtungia Allaah uongo Siku ya Qiyaamah? Hakika Allaah bila shaka Ana fadhila (nyingi) juu ya watu, lakini wengi wao hawashukuru.

 

 

 

وَمَا تَكُونُ فِي شَأْنٍ وَمَا تَتْلُو مِنْهُ مِن قُرْآنٍ وَلَا تَعْمَلُونَ مِنْ عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيْكُمْ شُهُودًا إِذْ تُفِيضُونَ فِيهِ ۚوَمَا يَعْزُبُ عَن رَّبِّكَ مِن مِّثْقَالِ ذَرَّةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ وَلَا أَصْغَرَ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْبَرَ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ﴿٦١﴾

61. Na hushughuliki katika jambo lolote, na wala husomi humo katika Qur-aan, na wala hamtendi ‘amali yoyote isipokuwa Tunakuwa Mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo. Na hakifichiki kwa Rabb wako hata cha uzito wa chembe (au sisimizi) katika ardhi wala mbinguni na wala kidogo kuliko hicho na wala kikubwa zaidi ya hicho isipokuwa kimo katika Kitabu kilicho bayana.

 

 

 

أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْوَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿٦٢﴾

62. Tanabahi! Hakika vipenzi wa Allaah hawana khofu juu yao, na wala hawatohuzunika.

 

 

 

الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ﴿٦٣﴾

63. Ambao wameamini na wakawa wana taqwa.

 

 

 

لَهُمُ الْبُشْرَىٰ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۚ لَا تَبْدِيلَ لِكَلِمَاتِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٦٤﴾

64. Watapata bishara katika uhai wa dunia na wa Aakhirah. Hakuna mabadiliko katika Maneno ya Allaah. Huko ndiko kufuzu adhimu.

 

 

 

وَلَا يَحْزُنكَ قَوْلُهُمْ ۘ إِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا ۚ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ﴿٦٥﴾

65. Na wala isikuhuzunishe kauli yao. Hakika taadhima zote ni za Allaah Pekee. Yeye Ndiye Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

أَلَا إِنَّ لِلَّـهِ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ ۗ وَمَا يَتَّبِعُ الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ شُرَكَاءَ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ﴿٦٦﴾

66. Tanabahi kwamba ni wa Allaah wote waliomo mbinguni na waliomo ardhini. Na hawafuati wale ambao wanawaomba pasi na Allaah kuwa ni washirika (Wake). Hawafuati isipokuwa dhana, nao hawana isipokuwa wanabuni uongo.

 

 

 

هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ وَالنَّهَارَ مُبْصِرًا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ﴿٦٧﴾

67. Yeye Ndiye Aliyekufanyieni usiku ili mpate utulivu humo, na mchana kwa ajili ya kuonea. Hakika katika hayo ni Aayaat (ishara, hoja, dalili) kwa watu wanaosikia (wakazingatia).

 

 

 

قَالُوا اتَّخَذَ اللَّـهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۖ هُوَ الْغَنِيُّ ۖ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ إِنْ عِندَكُم مِّن سُلْطَانٍ بِهَـٰذَا ۚأَتَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ مَا لَاتَعْلَمُونَ﴿٦٨﴾

68. Wanasema: “Allaah Amejifanyia mwana!” Utakasifu ni Wake! Yeye Ni Mkwasi Ni Vyake vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Hamna nyinyi dalili kwa hayo. Je, mnasema juu ya Allaah msiyoyajua?

 

 

 

قُلْ إِنَّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ﴿٦٩﴾

69. Sema: “Hakika wale wanaomtungia uongo Allaah hawatofaulu.”

 

 

 

مَتَاعٌ فِي الدُّنْيَا ثُمَّ إِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ ثُمَّ نُذِيقُهُمُ الْعَذَابَ الشَّدِيدَ بِمَا كَانُوايَكْفُرُونَ﴿٧٠﴾

70. Starehe ya muda katika dunia, kisha Kwetu ndio marejeo yao, kisha Tutawaonjesha adhabu kali kwa yale waliyokuwa wakiyakufuru.

 

 

 

وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ نُوحٍ إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ إِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكُم مَّقَامِي وَتَذْكِيرِي بِآيَاتِ اللَّـهِ فَعَلَى اللَّـهِ تَوَكَّلْتُ فَأَجْمِعُوا أَمْرَكُمْ وَشُرَكَاءَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُنْ أَمْرُكُمْ عَلَيْكُمْ غُمَّةً ثُمَّ اقْضُوا إِلَيَّ وَلَا تُنظِرُونِ﴿٧١﴾

71. Na wasomee khabari ya Nuwh, alipoiambia kaumu yake: “Enyi kaumu yangu! Ikiwa kukaa kwangu na kukumbusha kwangu Aayaat (ishara, hoja) za Allaah kumekuwa ni mashaka juu yenu basi kwa Allaah natawakali. Hivyo pangeni jambo lenu na washirika wenu (mnidhuru), kisha jambo lenu lisifichike kwenu; kisha mpitishe kwangu wala msinipe muhula.”

 

 

 

فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَمَا سَأَلْتُكُم مِّنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُسْلِمِينَ﴿٧٢﴾

72. “Lakini mkikengeuka, basi sijakuombeni ujira wowote. Sitaki ujira isipokuwa kwa Allaah na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu.”

 

 

 

فَكَذَّبُوهُ فَنَجَّيْنَاهُ وَمَن مَّعَهُ فِي الْفُلْكِ وَجَعَلْنَاهُمْ خَلَائِفَ وَأَغْرَقْنَا الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُنذَرِينَ﴿٧٣﴾

73. Lakini walimkadhibisha; Tukamuokoa (Nuwh) pamoja na waliokuwa naye katika jahazi, na Tukawafanya wao ndio waliobakia na Tukawagharikisha wale waliokadhibisha Aayaat (ishara) Zetu. Basi tazama vipi ilikuwa khatima ya walioonywa.

 

 

 

ثُمَّ بَعَثْنَا مِن بَعْدِهِ رُسُلًا إِلَىٰ قَوْمِهِمْ فَجَاءُوهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا بِمَا كَذَّبُوا بِهِ مِن قَبْلُ ۚ كَذَٰلِكَ نَطْبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِ الْمُعْتَدِينَ﴿٧٤﴾

74. Kisha Tukapeleka baada yake, Rusuli kwa kaumu zao, wakawajia kwa hoja bayana; lakini hawakuwa wenye kuyaamini yale waliyoyakadhibisha zamani. Hivyo ndivyo Tunavyopiga chapa juu ya nyoyo za wenye kutaadi.

 

 

 

ثُمَّ بَعَثْنَا مِن بَعْدِهِم مُّوسَىٰ وَهَارُونَ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ بِآيَاتِنَا فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْمًا مُّجْرِمِينَ﴿٧٥﴾

75. Kisha baada ya hao, Tukamtuma Muwsaa na Haaruwn kwa Fir’awn na wakuu wake kwa Aayaat (miujiza, ishara) Zetu walitakabari na wakawa watu wakhalifu.

 

 

 

فَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا إِنَّ هَـٰذَا لَسِحْرٌ مُّبِينٌ﴿٧٦﴾

76. Ilipowajia haki kutoka Kwetu, walisema: “Hii bila shaka ni sihiri bayana.”

 

 

 

قَالَ مُوسَىٰ أَتَقُولُونَ لِلْحَقِّ لَمَّا جَاءَكُمْ ۖ أَسِحْرٌ هَـٰذَا وَلَا يُفْلِحُالسَّاحِرُونَ﴿٧٧﴾

77. Muwsaa akasema: “Je, mnasema kuhusu haki ilipokujeni? Hii ni sihiri? Na wachawi hawafaulu.”

 

 

 

قَالُوا أَجِئْتَنَا لِتَلْفِتَنَا عَمَّا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا وَتَكُونَ لَكُمَا الْكِبْرِيَاءُ فِي الْأَرْضِ وَمَا نَحْنُ لَكُمَا بِمُؤْمِنِينَ﴿٧٨﴾

78. Wakasema: “Je, umetujia ili utugeuze kutokana na yale tuliyowakuta nayo baba zetu, na ili muwe na ukubwa na uadhama katika ardhi? Na sisi hatutawaamini nyinyi.”

 

 

 

وَقَالَ فِرْعَوْنُ ائْتُونِي بِكُلِّ سَاحِرٍ عَلِيمٍ﴿٧٩﴾

79. Na Fir’awn akasema: “Nileteeni kila mchawi mjuzi.”

 

 

 

فَلَمَّا جَاءَ السَّحَرَةُ قَالَ لَهُم مُّوسَىٰ أَلْقُوا مَا أَنتُم مُّلْقُونَ﴿٨٠﴾

80. Basi walipokuja wachawi, Muwsaa akawaambia: “Tupeni mnavyotaka kuvitupa.”

 

 

 

فَلَمَّا أَلْقَوْا قَالَ مُوسَىٰ مَا جِئْتُم بِهِ السِّحْرُ ۖ إِنَّ اللَّـهَ سَيُبْطِلُهُ ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُصْلِحُ عَمَلَ الْمُفْسِدِينَ﴿٨١﴾

81. Basi walipotupa, Muwsaa alisema: “Mliyokuja nayo ni sihiri. Hakika Allaah Atayabatilisha. Hakika Allaah Hatengenezi ‘amali za mafisadi.”

 

 

 

وَيُحِقُّ اللَّـهُ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ وَلَوْ كَرِهَالْمُجْرِمُونَ﴿٨٢﴾

82. “Na Allaah Atathibitisha haki kwa maneno Yake; japokuwa watakirihika wakhalifu.”

 

 

 

فَمَا آمَنَ لِمُوسَىٰ إِلَّا ذُرِّيَّةٌ مِّن قَوْمِهِ عَلَىٰ خَوْفٍ مِّن فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِمْ أَن يَفْتِنَهُمْ ۚ وَإِنَّ فِرْعَوْنَ لَعَالٍ فِي الْأَرْضِ وَإِنَّهُ لَمِنَ الْمُسْرِفِينَ﴿٨٣﴾

83. Basi hawakumwamini Muwsaa isipokuwa dhuriya katika kaumu yake kwa sababu ya kumkhofu Fir’awn na wakuu wao wasiwatese. Na hakika Fir’awn ni jeuri katika ardhi, na hakika yeye bila shaka ni miongoni mwa wapindukao mipaka.

 

 

 

وَقَالَ مُوسَىٰ يَا قَوْمِ إِن كُنتُمْ آمَنتُم بِاللَّـهِ فَعَلَيْهِ تَوَكَّلُوا إِن كُنتُممُّسْلِمِينَ﴿٨٤﴾

84. Na Muwsaa akasema: “Enyi kaumu yangu! Ikiwa mmemwamini Allaah; basi Kwake mtawakali, mkiwa ni Waislamu.”

 

 

 

فَقَالُوا عَلَى اللَّـهِ تَوَكَّلْنَا رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ﴿٨٥﴾

85. Wakasema: “Tumetawakali kwa Allaah. Ee Rabb wetu! Usitujaalie kuwa ni mtihani kwa watu madhalimu.”

 

 

 

وَنَجِّنَا بِرَحْمَتِكَ مِنَ الْقَوْمِالْكَافِرِينَ﴿٨٦﴾

86. “Na Tuokoe kwa rahmah Yako dhidi ya watu makafiri.”

 

 

 

وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ وَأَخِيهِ أَن تَبَوَّآ لِقَوْمِكُمَا بِمِصْرَ بُيُوتًا وَاجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ قِبْلَةً وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ ۗ وَبَشِّرِالْمُؤْمِنِينَ﴿٨٧﴾

87. Na Tukamfunulia Wahy Muwsaa na kaka yake kwamba: “Watengenezeeni watu wenu katika mji nyumba na zifanyeni nyumba zenu sehemu za ‘ibaadah na simamisheni Swalaah. Na wabashirie Waumini.”

 

 

 

وَقَالَ مُوسَىٰ رَبَّنَا إِنَّكَ آتَيْتَ فِرْعَوْنَ وَمَلَأَهُ زِينَةً وَأَمْوَالًا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا رَبَّنَا لِيُضِلُّوا عَن سَبِيلِكَ ۖ رَبَّنَا اطْمِسْ عَلَىٰ أَمْوَالِهِمْ وَاشْدُدْ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُوا حَتَّىٰ يَرَوُا الْعَذَابَ الْأَلِيمَ﴿٨٨﴾

88. Na Muwsaa akasema: “Ee Rabb Wetu! Hakika Wewe Umempa Fir’awn na wakuu wake mapambo na mali katika uhai wa dunia. Ee Rabb wetu, ili wapoteze (watu) njia Yako. Rabb wetu! Ziangamize mali zao na fanya nyoyo zao ziwe ngumu kwani hawatoamini mpaka waone adhabu iumizayo.”

 

 

 

قَالَ قَدْ أُجِيبَت دَّعْوَتُكُمَا فَاسْتَقِيمَا وَلَا تَتَّبِعَانِّ سَبِيلَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ﴿٨٩﴾

89. (Allaah) Akasema: “Imekwishaitikiwa du’aa yenu nyinyi wawili, basi lingamaneni sawasawa na wala msifuate njia ya wale ambao hawajui.”

 

 

 

وَجَاوَزْنَا بِبَنِي إِسْرَائِيلَ الْبَحْرَ فَأَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ وَجُنُودُهُ بَغْيًا وَعَدْوًا ۖ حَتَّىٰ إِذَا أَدْرَكَهُ الْغَرَقُ قَالَ آمَنتُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا الَّذِي آمَنَتْ بِهِ بَنُو إِسْرَائِيلَ وَأَنَا مِنَ الْمُسْلِمِينَ﴿٩٠﴾

90. Na Tukawavukisha wana wa Israaiyl bahari, basi Fir’awn akawafuata na jeshi lake kwa ukandamizaji na uadui; mpaka ilipomfikia (Fir’awn) gharka akasema: “Nimeamini kwamba hapana mwabudiwa wa haki, isipokuwa Yule waliyemwamini wana wa Israaiyl, na mimi ni miongoni mwa Waislamu.”

 

 

 

آلْآنَ وَقَدْ عَصَيْتَ قَبْلُ وَكُنتَ مِنَالْمُفْسِدِينَ﴿٩١﴾

91. “Sasa (ndio unaamini) na ihali umeasi kabla, na ulikuwa miongoni mwa mafisadi!?”

 

 

 

فَالْيَوْمَ نُنَجِّيكَ بِبَدَنِكَ لِتَكُونَ لِمَنْ خَلْفَكَ آيَةً ۚ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ عَنْ آيَاتِنَا لَغَافِلُونَ﴿٩٢﴾

92. Basi leo Tunakuokoa kwa (kuuweka) mwili wako ili uwe Aayah (zingatio, ishara) kwa watakaokuja nyuma yako. Na hakika watu wengi wameghafilika na Aayaat Zetu.  

 

 

 

وَلَقَدْ بَوَّأْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ مُبَوَّأَ صِدْقٍ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ فَمَا اخْتَلَفُوا حَتَّىٰ جَاءَهُمُ الْعِلْمُ ۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِي بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ﴿٩٣﴾

93. Na kwa yakini Tuliwapa makazi wana wa Israaiyl; makazi mazuri, na Tukawaruzuku katika vizuri; na hawakukhitilafiana mpaka ilipowajia elimu. Hakika Rabb wako Atahukumu baina yao Siku ya Qiyaamah katika yale yote waliyokuwa wakikhitilafiana.

 

 

 

فَإِن كُنتَ فِي شَكٍّ مِّمَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ فَاسْأَلِ الَّذِينَ يَقْرَءُونَ الْكِتَابَ مِن قَبْلِكَ ۚ لَقَدْ جَاءَكَ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ﴿٩٤﴾

94. Na ukiwa una shaka (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika yale Tuliyokuteremshia, basi waulize wale wanaosoma Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekujia haki kutoka kwa Rabb wako, basi usijekuwa miongoni mwa wanaoshuku.

 

 

 

وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ فَتَكُونَ مِنَ الْخَاسِرِينَ﴿٩٥﴾

95. Wala usijekuwa miongoni mwa wale waliokadhibisha Aayaat za Allaah ukawa miongoni mwa waliokhasirika.

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ حَقَّتْ عَلَيْهِمْ كَلِمَتُ رَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ﴿٩٦﴾

96. Hakika wale ambao neno la (ghadhabu la) Rabb wako limethibiti juu yao, hawataamini.

 

 

 

وَلَوْ جَاءَتْهُمْ كُلُّ آيَةٍ حَتَّىٰ يَرَوُاالْعَذَابَ الْأَلِيمَ﴿٩٧﴾

97. Japokuwa itawajia kila Aayah (mawaidha, dalili) mpaka waone adhabu iumizayo.

 

 

 

فَلَوْلَا كَانَتْ قَرْيَةٌ آمَنَتْ فَنَفَعَهَا إِيمَانُهَا إِلَّا قَوْمَ يُونُسَ لَمَّا آمَنُوا كَشَفْنَا عَنْهُمْ عَذَابَ الْخِزْيِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَمَتَّعْنَاهُمْ إِلَىٰ حِينٍ﴿٩٨﴾

98. Basi kwa nini usiweko mji mmoja ukaamini na iymaan yake ikawafaa - (haukutokea) isipokuwa kaumu ya Yuwnus. Walipoamini, Tuliwaondoshea adhabu ya hizaya duniani, na Tukawasterehesha mpaka muda maalumu.

 

 

 

وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ لَآمَنَ مَن فِي الْأَرْضِ كُلُّهُمْ جَمِيعًا ۚ أَفَأَنتَ تُكْرِهُ النَّاسَ حَتَّىٰ يَكُونُوا مُؤْمِنِينَ﴿٩٩﴾

99. Na kama Angetaka Rabb wako, basi wangeliamini wote pamoja walioko katika ardhi. Je, basi wewe (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) utashurutisha watu mpaka wawe Waumini?

 

 

 

وَمَا كَانَ لِنَفْسٍ أَن تُؤْمِنَ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَيَجْعَلُ الرِّجْسَ عَلَى الَّذِينَ لَا يَعْقِلُونَ﴿١٠٠﴾

100. Na hakuna nafsi yoyote iamini isipokuwa kwa idhini ya Allaah. Naye Hujaalia adhabu (na upotofu) kwa wale ambao wasiotia akilini.

 

 

 

قُلِ انظُرُوا مَاذَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَمَا تُغْنِي الْآيَاتُ وَالنُّذُرُ عَن قَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ﴿١٠١﴾

101. Sema: “Tazameni nini yaliyoko mbinguni na ardhini.” Lakini Aayaat (ishara, dalili) zote na maonyo haiwafai kitu watu wasioamini.

 

 

 

فَهَلْ يَنتَظِرُونَ إِلَّا مِثْلَ أَيَّامِ الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلِهِمْ ۚ قُلْ فَانتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُنتَظِرِينَ﴿١٠٢﴾

102. Je, wanangojea jingine (la maangamizi) isipokuwa mfano wa siku za wale waliopita kabla yao? Sema: “Basi ngojeeni, hakika mimi ni pamoja nanyi miongoni mwa wanaongojea.”

 

 

 

ثُمَّ نُنَجِّي رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا ۚ كَذَٰلِكَ حَقًّا عَلَيْنَا نُنجِ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٠٣﴾

103. Kisha Tunawaokoa Rusuli Wetu na wale walioamini. Hivyo ndivyo haki Kwetu kuwaokoa Waumini.

 

 

 

قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِن كُنتُمْ فِي شَكٍّ مِّن دِينِي فَلَا أَعْبُدُ الَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِنْ أَعْبُدُ اللَّـهَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُمْ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٠٤﴾

104. Sema: (Ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) “Enyi watu! Ikiwa mna shaka kutokana na Dini yangu, basi mimi siabudu ambavyo mnaviabudu badala ya Allaah; lakini namwabudu Allaah Ambaye Anakufisheni. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waumini.”

 

 

 

وَأَنْ أَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١٠٥﴾

105.  Na kwamba elekeza uso wako kwa Dini haniyfaa (Tawhiyd ya Allaah), na wala usijekuwa miongoni mwa washirikina.

 

 

 

وَلَا تَدْعُ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَ ۖ فَإِن فَعَلْتَ فَإِنَّكَ إِذًا مِّنَ الظَّالِمِينَ﴿١٠٦﴾

106. Na wala usiombe badala ya Allaah visivyokufaa wala visivyokudhuru. Na ukifanya, basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu.

 

 

 

وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يُرِدْكَ بِخَيْرٍ فَلَا رَادَّ لِفَضْلِهِ ۚ يُصِيبُ بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚ وَهُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿١٠٧﴾

107. Na Allaah Akikugusisha dhara, basi hakuna wa kuiondosha isipokuwa Yeye. Na Akikutakia khayr, basi hakuna wa kurudisha fadhila Zake, Anasababisha kumfikia kwayo (fadhila Yake) Amtakaye katika waja Wake. Naye ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 

 

قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُمُ الْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَنِ اهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِي لِنَفْسِهِ ۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيْهَا ۖوَمَا أَنَا عَلَيْكُم بِوَكِيلٍ﴿١٠٨﴾

108. Sema: “Enyi watu! Kwa yakini imekujieni haki kutoka kwa Rabb wenu. Basi atakayeongoka, hakika anaongoka kwa faida ya nafsi yake. Na atakayepotoka, hakika anapotoka kwa hasara ya nafsi yake. Nami si mdhamini wenu.”

 

 

 

وَاتَّبِعْ مَا يُوحَىٰ إِلَيْكَ وَاصْبِرْ حَتَّىٰ يَحْكُمَ اللَّـهُ ۚ وَهُوَ خَيْرُالْحَاكِمِينَ﴿١٠٩﴾

109. Na fuata (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) yale ulofunuliwa Wahy na subiri mpaka Allaah Ahukumu. Naye ni Mbora wa wanaohukumu.

 

 

 

 

[1] Faida: Maana ya Istawaa: Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah. Na rejea tanbihi kwa faida bayana: (2: 29).




Report Page