009 - At-Tawbah

009 - At-Tawbah

التَّوْبَة

At-Tawbah: 9

 

 

 

بَرَاءَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ إِلَى الَّذِينَ عَاهَدتُّم مِّنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١﴾

1. Kujitoa katika dhima (kunatangazwa) kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake kwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa washirikina.

 

 

 

فَسِيحُوا فِي الْأَرْضِ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ غَيْرُ مُعْجِزِي اللَّـهِ ۙ وَأَنَّ اللَّـهَ مُخْزِي الْكَافِرِينَ﴿٢﴾

2. Basi tembeeni katika ardhi miezi minne; na jueni kwamba nyinyi hamuwezi kushinda kumwepuka Allaah na kwamba Allaah ni Mwenye kuwahizi makafiri.

 

 

 

وَأَذَانٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ إِلَى النَّاسِ يَوْمَ الْحَجِّ الْأَكْبَرِ أَنَّ اللَّـهَ بَرِيءٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ ۙ وَرَسُولُهُ ۚ فَإِن تُبْتُمْ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ غَيْرُ مُعْجِزِي اللَّـهِ ۗ وَبَشِّرِ الَّذِينَ كَفَرُوا بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣﴾

3. Na ni tangazo kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake kwa watu siku ya Hajj kubwa, kwamba Allaah Hana dhima na washirikina na Rasuli Wake (pia hana dhima). Basi mkitubu, hiyo ni khayr kwenu; na mkikengeuka, basi jueni kwamba nyinyi hamuwezi kushinda kumwepuka Allaah. Na wabashirie wale waliokufuru kwa adhabu iumizayo. 

 

 

 

إِلَّا الَّذِينَ عَاهَدتُّم مِّنَ الْمُشْرِكِينَ ثُمَّ لَمْ يَنقُصُوكُمْ شَيْئًا وَلَمْ يُظَاهِرُوا عَلَيْكُمْ أَحَدًا فَأَتِمُّوا إِلَيْهِمْ عَهْدَهُمْ إِلَىٰ مُدَّتِهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ﴿٤﴾

4. Isipokuwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa washirikina, kisha hawakukupunguzieni chochote na wala hawakumsaidia yeyote dhidi yenu, basi watimizieni ahadi yao mpaka muda wao (umalizike). Hakika Allaah Anapenda wenye taqwa.

 

 

 

فَإِذَا انسَلَخَ الْأَشْهُرُ الْحُرُمُ فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ وَخُذُوهُمْ وَاحْصُرُوهُمْ وَاقْعُدُوا لَهُمْ كُلَّ مَرْصَدٍ ۚ فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٥﴾

5. Itapomalizika miezi mitukufu, basi waueni washirikina popote muwakutapo, na wachukueni (mateka) na wahusuruni, na wakalieni katika kila sehemu ya uvamizi. Lakini wakitubu, na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah, basi iacheni njia yao (huru). Hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 

 

وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ أَبْلِغْهُ مَأْمَنَهُ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْلَمُونَ﴿٦﴾

6. Na ikiwa mmoja wa washirikina akikuomba umlinde, basi mlinde mpaka asikie Maneno ya Allaah (Qur-aan), kisha mfikishe mahali pake pa amani. Hivyo kwa kuwa wao ni watu wasiojua.

 

 

 

كَيْفَ يَكُونُ لِلْمُشْرِكِينَ عَهْدٌ عِندَ اللَّـهِ وَعِندَ رَسُولِهِ إِلَّا الَّذِينَ عَاهَدتُّمْ عِندَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۖ فَمَا اسْتَقَامُوا لَكُمْ فَاسْتَقِيمُوا لَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ﴿٧﴾

7. Vipi iweko ahadi na washirikina mbele ya Allaah na mbele ya Rasuli Wake isipokuwa wale mlioahidiana mbele ya Al-Masjidil-Al-Haraam. Basi wakikunyookeeni (kwa uzuri), nanyi wanyookeeni. Hakika Allaah Anapenda wenye taqwa.

 

 

 

كَيْفَ وَإِن يَظْهَرُوا عَلَيْكُمْ لَا يَرْقُبُوا فِيكُمْ إِلًّا وَلَا ذِمَّةً ۚ يُرْضُونَكُم بِأَفْوَاهِهِمْ وَتَأْبَىٰ قُلُوبُهُمْ وَأَكْثَرُهُمْ فَاسِقُونَ﴿٨﴾

8. Vipi (mtashikamana na mkataba) hali wakikushindeni hawachungi kwenu udugu wa damu wala ahadi ya himaya? Wanakuridhisheni kwa midomo yao, na hali nyoyo zao zinakataa; na wengi wao ni mafasiki.

 

 

 

اشْتَرَوْا بِآيَاتِ اللَّـهِ ثَمَنًا قَلِيلًا فَصَدُّوا عَن سَبِيلِهِ ۚ إِنَّهُمْ سَاءَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩﴾

9. Wamebadili Aayaat za Allaah kwa thamani ndogo, na wakazuilia njia Yake. Hakika ni maovu waliyokuwa wakitenda.

 

 

 

لَا يَرْقُبُونَ فِي مُؤْمِنٍ إِلًّا وَلَا ذِمَّةً ۚوَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُعْتَدُونَ﴿١٠﴾

10. Hawachungi kwa Muumini udugu wa damu wala ahadi ya himaya. Na hao ndio wenye kutaadi.

 

 

 

فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ ۗ وَنُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ﴿١١﴾

11. Wakitubu, na wakasimamisha Swalaah, na wakatoa Zakaah; basi ni ndugu zenu katika Dini. Na Tunafasili waziwazi Aayaat kwa watu wanaojua.

 

 

 

وَإِن نَّكَثُوا أَيْمَانَهُم مِّن بَعْدِ عَهْدِهِمْ وَطَعَنُوا فِي دِينِكُمْ فَقَاتِلُوا أَئِمَّةَ الْكُفْرِ ۙ إِنَّهُمْ لَا أَيْمَانَ لَهُمْ لَعَلَّهُمْ يَنتَهُونَ﴿١٢﴾

12. Na wakivunja viapo vyao baada ya ahadi yao, na wakatukana Dini yenu, basi wapigeni vita viongozi wa ukafiri. Hakika viapo vyao havina maana. (Piganeni nao) ili wapate kukoma.

 

 

 

أَلَا تُقَاتِلُونَ قَوْمًا نَّكَثُوا أَيْمَانَهُمْ وَهَمُّوا بِإِخْرَاجِ الرَّسُولِ وَهُم بَدَءُوكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ ۚ أَتَخْشَوْنَهُمْ ۚ فَاللَّـهُ أَحَقُّ أَن تَخْشَوْهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿١٣﴾

13. Je, hamtopigana na watu waliovunja viapo vyao, na wakafanya hima kumtoa Rasuli, nao ndio waliokuanzeni mara ya kwanza? Je, mnawaogopa? Basi Allaah Anastahiki zaidi mumwogope ikiwa nyinyi ni Waumini.

 

 

 

قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللَّـهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُّؤْمِنِينَ﴿١٤﴾

14. Piganeni nao, Allaah Atawaadhibu kwa mikono yenu, na Atawahizi na Atakunusuruni dhidi yao, na Atapozesha vifua vya Waumini.  

 

 

 

وَيُذْهِبْ غَيْظَ قُلُوبِهِمْ ۗ وَيَتُوبُ اللَّـهُ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿١٥﴾

15. Na Ataondosha ghaidhi za nyoyo zao (Waumini); na Allaah Anapokea tawbah kwa Amtakaye, na Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

 

أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تُتْرَكُوا وَلَمَّا يَعْلَمِ اللَّـهُ الَّذِينَ جَاهَدُوا مِنكُمْ وَلَمْ يَتَّخِذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَا رَسُولِهِ وَلَا الْمُؤْمِنِينَ وَلِيجَةً ۚ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴿١٦﴾

16. Je, mmedhani kuwa mtaachwa na hali Allaah Hakuwadhihirisha wale waliofanya jihaad miongoni mwenu; na hawakufanya rafiki mwandani isipokuwa Allaah na Rasuli Wake na Waumini (wenzao)? Na Allaah ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika kwa yale myatendayo.

 

 

 

مَا كَانَ لِلْمُشْرِكِينَ أَن يَعْمُرُوا مَسَاجِدَ اللَّـهِ شَاهِدِينَ عَلَىٰ أَنفُسِهِم بِالْكُفْرِ ۚأُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ وَفِي النَّارِ هُمْ خَالِدُونَ﴿١٧﴾

17. Haiwi kwa washirikina kuamirisha Misikiti ya Allaah hali wanajishuhudia nafsi zao kwa ukafiri. Hao zimeporomoka ‘amali zao na katika moto wao ni wenye kudumu.

 

 

 

إِنَّمَا يَعْمُرُ مَسَاجِدَ اللَّـهِ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى الزَّكَاةَ وَلَمْ يَخْشَ إِلَّا اللَّـهَ ۖ فَعَسَىٰ أُولَـٰئِكَ أَن يَكُونُوا مِنَ الْمُهْتَدِينَ﴿١٨﴾

18. Hakika wanaoamirisha Misikiti ya Allaah ni wale wanaomwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah na hawamkhofu (yeyote) isipokuwa Allaah. Basi asaa hao wakawa miongoni mwa walioongoka.

 

 

 

أَجَعَلْتُمْ سِقَايَةَ الْحَاجِّ وَعِمَارَةَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ كَمَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَجَاهَدَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚلَا يَسْتَوُونَ عِندَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿١٩﴾

19. Je, mmefanya kunywesha maji Hujaji na kuamirisha Al-Masjid Al-Haraam kama sawasawa na (‘amali za) anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na akafanya jihaad katika njia ya Allaah? (Hapana!) Hawawi sawa mbele ya Allaah. Na Allaah Haongoi watu madhalimu.

 

 

 

الَّذِينَ آمَنُوا وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ أَعْظَمُ دَرَجَةً عِندَ اللَّـهِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَائِزُونَ﴿٢٠﴾

20. Wale walioamini na wakahajiri na wakafanya jihaad katika njia ya Allaah kwa mali zao na nafsi zao; wana daraja kuu kwa Allaah. Na hao ndio waliofuzu.

 

 

 

يُبَشِّرُهُمْ رَبُّهُم بِرَحْمَةٍ مِّنْهُ وَرِضْوَانٍ وَجَنَّاتٍ لَّهُمْ فِيهَا نَعِيمٌ مُّقِيمٌ﴿٢١﴾

21. Rabb wao Anawabashiria kwa rahmah kutoka Kwake na radhi na Jannaat, watapata humo neema zenye kudumu.

 

 

 

خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عِندَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ﴿٢٢﴾

22. Ni wenye kudumu humo abadi. Hakika Allaah Kwake kuna ujira adhimu.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا آبَاءَكُمْ وَإِخْوَانَكُمْ أَوْلِيَاءَ إِنِ اسْتَحَبُّوا الْكُفْرَ عَلَى الْإِيمَانِ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿٢٣﴾

23. Enyi walioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu marafiki wandani ikiwa wanapendelea ukafiri badala ya iymaan. Na yeyote miongoni mwenu atakayewafanya marafiki wandani basi hao ndio madhalimu.

 

 

 

قُلْ إِن كَانَ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَاؤُكُمْ وَإِخْوَانُكُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ وَعَشِيرَتُكُمْ وَأَمْوَالٌ اقْتَرَفْتُمُوهَا وَتِجَارَةٌ تَخْشَوْنَ كَسَادَهَا وَمَسَاكِنُ تَرْضَوْنَهَا أَحَبَّ إِلَيْكُم مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَجِهَادٍ فِي سَبِيلِهِ فَتَرَبَّصُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّـهُ بِأَمْرِهِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ﴿٢٤﴾

24. Sema: “Ikiwa baba zenu na watoto wenu na ndugu zenu na wake (au waume) zenu na jamaa zenu na mali mliyoichuma na biashara mnayoikhofia kuharibika kwake, na majumba mnayoridhika nayo, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Allaah na Rasuli Wake na kufanya jihaad katika njia Yake; basi ngojeeni mpaka Allaah Alete Amri Yake (ya adhabu). Na Allaah Haongoi watu mafasiki.

 

 

 

لَقَدْ نَصَرَكُمُ اللَّـهُ فِي مَوَاطِنَ كَثِيرَةٍ ۙوَيَوْمَ حُنَيْنٍ ۙ إِذْ أَعْجَبَتْكُمْ كَثْرَتُكُمْ فَلَمْ تُغْنِ عَنكُمْ شَيْئًا وَضَاقَتْ عَلَيْكُمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ ثُمَّ وَلَّيْتُم مُّدْبِرِينَ﴿٢٥﴾

25. Kwa yakini Amekunusuruni Allaah katika maeneo mengi, na Siku ya (vita vya) Hunayn (pia); ulipokupendezeni wingi wenu (kwa kujigamba), lakini haukukufaeni chochote; na ardhi ikawa dhiki juu yenu juu ya upana wake, kisha mkageuka na kurudi nyuma kukimbia.

 

 

 

ثُمَّ أَنزَلَ اللَّـهُ سَكِينَتَهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ وَعَلَى الْمُؤْمِنِينَ وَأَنزَلَ جُنُودًا لَّمْ تَرَوْهَا وَعَذَّبَ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْكَافِرِينَ﴿٢٦﴾

26. Kisha Allaah Akateremsha utulivu Wake kwa Rasuli Wake na kwa Waumini, na Akateremsha majeshi (ya Malaika) msiyoyaona; na Akawaadhibu wale waliokufuru. Na hivyo ndio jazaa ya makafiri.

 

 

 

ثُمَّ يَتُوبُ اللَّـهُ مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٢٧﴾

27. Kisha Allaah Anapokea tawbah baada ya hapo kwa Amtakaye. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ فَلَا يَقْرَبُوا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ بَعْدَ عَامِهِمْ هَـٰذَا ۚ وَإِنْ خِفْتُمْ عَيْلَةً فَسَوْفَ يُغْنِيكُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ إِن شَاءَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿٢٨﴾

28. Enyi walioamini! Hakika washirikiana ni najisi, basi wasikaribie Al-Masjid Al-Haraam baada ya mwaka wao huu. Na mkikhofu umasikini basi Allaah Atakutajirisheni kutokana na fadhila Zake Akitaka. Hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

 

قَاتِلُوا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَلَا يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَلَا يَدِينُونَ دِينَ الْحَقِّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حَتَّىٰ يُعْطُوا الْجِزْيَةَ عَن يَدٍ وَهُمْ صَاغِرُونَ﴿٢٩﴾

29. Piganeni na wale wasiomwamini Allaah na wala Siku ya Mwisho, na wala hawaharamishi Aliyoyaharamisha Allaah na Rasuli Wake, na wala hawafuati Dini ya haki miongoni mwa wale waliopewa Kitabu, (piganeni nao) mpaka watoe jizyah (kodi) kwa khiyari, wakiwa hali ya kurudi chini kutii.

 

 

 

وَقَالَتِ الْيَهُودُ عُزَيْرٌ ابْنُ اللَّـهِ وَقَالَتِ النَّصَارَى الْمَسِيحُ ابْنُ اللَّـهِ ۖ ذَٰلِكَ قَوْلُهُم بِأَفْوَاهِهِمْ ۖ يُضَاهِئُونَ قَوْلَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَبْلُ ۚ قَاتَلَهُمُ اللَّـهُ ۚأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ﴿٣٠﴾

30. Na Mayahudi wanasema: “‘Uzayr ni mwana wa Allaah”; na Manaswara wanasema: “Al-Masiyh (‘Iysaa) ni mwana wa Allaah.” Hiyo ni kauli yao kwa midomo yao. Wanaiga kauli ya wale waliokufuru kabla. Allaah Awaangamize! Basi namna gani wanavyoghilibiwa?

 

 

 

اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا إِلَـٰهًا وَاحِدًا ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٣١﴾

31. Wamewafanya Wanachuoni Marabai wao wa dini na Wamonakiwao kuwa ni miola badala ya Allaah, na (pia) Al-Masiyh mwana wa Maryam na hali hawakuamrishwa isipokuwa kumwabudu Ilaah Mmoja Pekee. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Utakasifu ni Wake kutokana na yale yote wanayomshirkisha nayo.  

 

 

 

يُرِيدُونَ أَن يُطْفِئُوا نُورَ اللَّـهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّـهُ إِلَّا أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ﴿٣٢﴾

32. Wanataka kuzima nuru ya Allaah kwa midomo yao; lakini Allaah Anakataa isipokuwa Atimize nuru Yake, japo watakirihika makafiri.

 

 

 

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴿٣٣﴾

33. Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote, japo watakirihika washirikina.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ كَثِيرًا مِّنَ الْأَحْبَارِ وَالرُّهْبَانِ لَيَأْكُلُونَ أَمْوَالَ النَّاسِ بِالْبَاطِلِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۗ وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣٤﴾

34. Enyi walioamini! Hakika wengi katika Wanachuoni Marabai wa dini (zao) na Wamonaki wanakula mali za watu kwa batili, na wanazuia njia ya Allaah. Na wale wanaorundika dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika njia ya Allaah, basi wabashirie adhabu iumizayo. 

 

 

 

يَوْمَ يُحْمَىٰ عَلَيْهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكْوَىٰ بِهَا جِبَاهُهُمْ وَجُنُوبُهُمْ وَظُهُورُهُمْ ۖ هَـٰذَا مَا كَنَزْتُمْ لِأَنفُسِكُمْ فَذُوقُوا مَا كُنتُمْ تَكْنِزُونَ﴿٣٥﴾

35. Siku zitakapopashwa katika Jahannam, na kwazo vikachomwa moto vipaji vyao, na mbavu zao, na migongo yao (wakiambiwa): “Haya ndiyo mliyoyarundika kwa ajili ya nafsi zenu. Basi onjeni yale mliyokuwa mkiyarundika.”

 

 

 

إِنَّ عِدَّةَ الشُّهُورِ عِندَ اللَّـهِ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِي كِتَابِ اللَّـهِ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ۚذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ ۚ فَلَا تَظْلِمُوا فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ ۚ وَقَاتِلُوا الْمُشْرِكِينَ كَافَّةً كَمَا يُقَاتِلُونَكُمْ كَافَّةً ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ﴿٣٦﴾

36. Hakika idadi ya miezi mbele ya Allaah ni kumi na mbili katika hukmu ya makadirio ya Allaah, (tangu) siku Aliyoumba mbingu na ardhi. Kati ya hiyo iko minne mitukufu. Hivyo ndiyo Dini iliyo nyoofu. Basi msijidhulumu humo nafsi zenu, na piganeni vita na washirikina wote kama wao wanavyokupigeni vita nyote. Na jueni kwamba Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa.

 

 

 

إِنَّمَا النَّسِيءُ زِيَادَةٌ فِي الْكُفْرِ ۖ يُضَلُّ بِهِ الَّذِينَ كَفَرُوا يُحِلُّونَهُ عَامًا وَيُحَرِّمُونَهُ عَامًا لِّيُوَاطِئُوا عِدَّةَ مَا حَرَّمَ اللَّـهُ فَيُحِلُّوا مَا حَرَّمَ اللَّـهُ ۚ زُيِّنَ لَهُمْ سُوءُ أَعْمَالِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ﴿٣٧﴾

37. Hakika kuakhirisha (au kuizuia miezi mitukufu) ni kuzidi katika kufuru. Hupotezwa kwayo wale waliokufuru, wanauhalalisha mwaka na wanauharamisha mwaka (mwingine) ili kuusawazisha na idadi ya (miezi) Aliyoitukuza Allaah. Basi huhalalisha Alivyoviharamisha Allaah. Wamepambiwa uovu wa ‘amali zao. Na Allaah Haongoi watu makafiri.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انفِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ ۚ أَرَضِيتُم بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ ۚ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ﴿٣٨﴾

38. Enyi walioamini! Mna nini mnapoambiwa tokeni mwende (jihaad) katika njia ya Allaah, mnajitia uzito katika ardhi. Je, mmeridhika na uhai wa dunia kwa ya Aakhirah? Basi starehe za uhai wa dunia kulinganisha na Aakhirah ni chache.

 

 

 

إِلَّا تَنفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَيَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئًا ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٣٩﴾

39. Msipotoka kwenda Atakuadhibuni adhabu iumizayo, na Atabadilisha watu wasiokuwa nyinyi, na wala hamtomdhuru chochote. Na Allaah juu ya kila kitu ni Muweza.

 

 

 

إِلَّا تَنصُرُوهُ فَقَدْ نَصَرَهُ اللَّـهُ إِذْ أَخْرَجَهُ الَّذِينَ كَفَرُوا ثَانِيَ اثْنَيْنِ إِذْ هُمَا فِي الْغَارِ إِذْ يَقُولُ لِصَاحِبِهِ لَا تَحْزَنْ إِنَّ اللَّـهَ مَعَنَا ۖ فَأَنزَلَ اللَّـهُ سَكِينَتَهُ عَلَيْهِ وَأَيَّدَهُ بِجُنُودٍ لَّمْ تَرَوْهَا وَجَعَلَ كَلِمَةَ الَّذِينَ كَفَرُوا السُّفْلَىٰ ۗوَكَلِمَةُ اللَّـهِ هِيَ الْعُلْيَا ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿٤٠﴾

40. Msipomnusuru (Rasuli), basi Allaah Amekwishamnusuru, pale walipomtoa (Makkah) wale waliokufuru akiwa wa pili katika wawili; walipokuwa katika pango, alipomwambia swahibu yake: “Usihuzunike, hakika Allaah Yu Pamoja nasi.” Basi Allaah Akamteremshia utulivu Wake, na Akamsaidia kwa majeshi msiyoyaona, na Akajaalia neno la waliokufuru kuwa chini. Na Neno la Allaah kuwa ndilo lililo juu. Na Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

 

انفِرُوا خِفَافًا وَثِقَالًا وَجَاهِدُوا بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿٤١﴾

41. Tokeni mwende mkiwa wepesi na mkiwa wazito, na fanyeni jihaad kwa mali zenu na nafsi zenu katika njia ya Allaah. Hivyo ni khayr kwenu mkiwa mnajua.

 

 

 

لَوْ كَانَ عَرَضًا قَرِيبًا وَسَفَرًا قَاصِدًا لَّاتَّبَعُوكَ وَلَـٰكِن بَعُدَتْ عَلَيْهِمُ الشُّقَّةُ ۚوَسَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَوِ اسْتَطَعْنَا لَخَرَجْنَا مَعَكُمْ يُهْلِكُونَ أَنفُسَهُمْ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ﴿٤٢﴾

42. Kama ingelikuwa pato la karibu na safari nyepesi ya karibu, basi (wanafiki) wangelikufuata; lakini imekuwa ni ya masafa ya mbali kwao na ina mashaka. Na watakuapia kwa Jina la Allaah: “Lau tungeliweza, bila shaka tungelitoka pamoja nanyi.” Wanaangamiza nafsi zao na Allaah Anajua kwamba wao bila shaka ni waongo.

 

 

 

عَفَا اللَّـهُ عَنكَ لِمَ أَذِنتَ لَهُمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكَ الَّذِينَ صَدَقُوا وَتَعْلَمَ الْكَاذِبِينَ﴿٤٣﴾

43. Allaah Akusamehe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), kwanini umewapa ruhusa? (Usingelifanya hivyo) Mpaka wakubainikie wale waliosadikishana uwajue waliokadhibisha.

 

 

 

لَا يَسْتَأْذِنُكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ أَن يُجَاهِدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالْمُتَّقِينَ﴿٤٤﴾

44. Hawakuombi ruhusa wale waliomwamini Allaah na Siku ya Mwisho wasifanye jihaad kwa mali zao na nafsi zao. Na Allaah ni Mjuzi kwa wenye taqwa.

 

 

 

إِنَّمَا يَسْتَأْذِنُكَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَارْتَابَتْ قُلُوبُهُمْ فَهُمْ فِي رَيْبِهِمْ يَتَرَدَّدُونَ﴿٤٥﴾

45. Hakika wanaokuomba ruhusa ni wale ambao hawamwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na nyoyo zao zina shaka, basi wao katika shaka zao wanasitasita.

 

 

 

وَلَوْ أَرَادُوا الْخُرُوجَ لَأَعَدُّوا لَهُ عُدَّةً وَلَـٰكِن كَرِهَ اللَّـهُ انبِعَاثَهُمْ فَثَبَّطَهُمْ وَقِيلَ اقْعُدُوا مَعَ الْقَاعِدِينَ﴿٤٦﴾

46. Na ingelikuwa wametaka kutoka, bila shaka wangeliandaa maandalizi yake, lakini Allaah Amekirihika kutoka kwao, basi Akawazuia na ikasemwa: “Kaeni pamoja na wanaokaa.”

 

 

 

لَوْ خَرَجُوا فِيكُم مَّا زَادُوكُمْ إِلَّا خَبَالًا وَلَأَوْضَعُوا خِلَالَكُمْ يَبْغُونَكُمُ الْفِتْنَةَ وَفِيكُمْ سَمَّاعُونَ لَهُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ﴿٤٧﴾

47. Lau wangelitoka nanyi, wasingelikuzidishieni isipokuwa machafuko (vurugu, rabsha) na wangeliharakia huku na huku baina yenu kukutakieni fitnah; na miongoni mwenu wako wanaowasikiliza kwa makini. Na Allaah ni Mjuzi kwa madhalimu.

 

 

 

لَقَدِ ابْتَغَوُا الْفِتْنَةَ مِن قَبْلُ وَقَلَّبُوا لَكَ الْأُمُورَ حَتَّىٰ جَاءَ الْحَقُّ وَظَهَرَ أَمْرُ اللَّـهِ وَهُمْ كَارِهُونَ﴿٤٨﴾

48. Walikwishataka kabla kukuleteeni fitnah, na wakakupindulia mambo mpaka ikaja haki na ikadhihirika amri ya Allaah; nao ni wenye kukirihika.

 

 

 

وَمِنْهُم مَّن يَقُولُ ائْذَن لِّي وَلَا تَفْتِنِّي ۚأَلَا فِي الْفِتْنَةِ سَقَطُوا ۗ وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمُحِيطَةٌ بِالْكَافِرِينَ﴿٤٩﴾

49. Na miongoni mwao yuko anayesema: “Niruhusu na wala usinifitini.” Tanabahi! Wamekwishaanguka katika fitnah. Na hakika Jahannam umewazunguka makafiri.

 

 

 

إِن تُصِبْكَ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ ۖ وَإِن تُصِبْكَ مُصِيبَةٌ يَقُولُوا قَدْ أَخَذْنَا أَمْرَنَا مِن قَبْلُ وَيَتَوَلَّوا وَّهُمْ فَرِحُونَ﴿٥٠﴾

50. Linapokusibu zuri lolote lile linawachukiza. Na unapokusibu msiba wowote ule, wanasema: “Tumechukua tahadhari jambo letu tokea mwanzo,” na wanageuka kwenda zao na huku wanafurahia.

Endelea Kusoma Kwa Kugusa Hapa 👈



Report Page