@furqanbot
قُل لَّن يُصِيبَنَا إِلَّا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَنَا هُوَ مَوْلَانَا ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ﴿٥١﴾
51. Sema: “Halitusibu (lolote) isipokuwa lile Alilotukidhia Allaah. Yeye ni Maulaa wetu.” Basi kwa Allaah watawakali Waumini.
قُلْ هَلْ تَرَبَّصُونَ بِنَا إِلَّا إِحْدَى الْحُسْنَيَيْنِ ۖ وَنَحْنُ نَتَرَبَّصُ بِكُمْ أَن يُصِيبَكُمُ اللَّـهُ بِعَذَابٍ مِّنْ عِندِهِ أَوْ بِأَيْدِينَا ۖ فَتَرَبَّصُوا إِنَّا مَعَكُم مُّتَرَبِّصُونَ﴿٥٢﴾
52. Sema: “Je, mnalo la kungojea kututazamia isipokuwa mojawapo ya mazuri mawili? Na sisi tunangojea kukutazamieni kwamba Allaah Atakusibuni kwa adhabu kutoka Kwake au kutokana na mikono yetu. Basi ngojeeni, nasi tuko pamoja nanyi tunangojea.”
قُلْ أَنفِقُوا طَوْعًا أَوْ كَرْهًا لَّن يُتَقَبَّلَ مِنكُمْ ۖ إِنَّكُمْ كُنتُمْ قَوْمًا فَاسِقِينَ﴿٥٣﴾
53. Sema: “Toeni (mali) kwa khiari au kutokupenda haitokubaliwa kwenu. Hakika nyinyi mmekuwa ni watu mafasiki.”
وَمَا مَنَعَهُمْ أَن تُقْبَلَ مِنْهُمْ نَفَقَاتُهُمْ إِلَّا أَنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّـهِ وَبِرَسُولِهِ وَلَا يَأْتُونَ الصَّلَاةَ إِلَّا وَهُمْ كُسَالَىٰ وَلَا يُنفِقُونَ إِلَّا وَهُمْ كَارِهُونَ﴿٥٤﴾
54. Na haikuwazuilia ikubaliwe kwao michango yao isipokuwa kwa kuwa wao walimkufuru Allaah na Rasuli Wake, na wala hawafiki katika Swalaah isipokuwa wao huwa katika hali ya uvivu, na wala hawatoi isipokuwa wakiwa wamekirihika.
فَلَا تُعْجِبْكَ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُمْ ۚإِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُعَذِّبَهُم بِهَا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَتَزْهَقَ أَنفُسُهُمْ وَهُمْ كَافِرُونَ﴿٥٥﴾
55. Basi zisikupendezee mali zao na wala watoto wao. Hakika Allaah Anataka kuwaadhibu kwayo katika uhai wa dunia, na zitokelee mbali nafsi zao na huku wao wakiwa makafiri.
وَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ إِنَّهُمْ لَمِنكُمْ وَمَا هُم مِّنكُمْ وَلَـٰكِنَّهُمْ قَوْمٌ يَفْرَقُونَ﴿٥٦﴾
56. Na wanaapa kwa Jina la Allaah kwamba wao ni miongoni mwenu. Na wala wao si katika nyinyi, lakini wao (wanafiki) ni watu wanaoogopa mno.
لَوْ يَجِدُونَ مَلْجَأً أَوْ مَغَارَاتٍ أَوْ مُدَّخَلًا لَّوَلَّوْا إِلَيْهِ وَهُمْ يَجْمَحُونَ﴿٥٧﴾
57. Lau wangelipata mahali pa kukimbilia, au mapango, au mahali pa kuingilia (na kujificha), wangeliyaelekea nao huku wanakimbilia haraka.
وَمِنْهُم مَّن يَلْمِزُكَ فِي الصَّدَقَاتِ فَإِنْ أُعْطُوا مِنْهَا رَضُوا وَإِن لَّمْ يُعْطَوْا مِنْهَا إِذَا هُمْ يَسْخَطُونَ﴿٥٨﴾
58. Na miongoni mwao wako wanaokufedhehesha kwa kushutumu katika (ugawaji wa) Swadaqah. Wakipewa humo wanaridhika, na wasipopewa humo tahamaki wao wanaghadhibika.
وَلَوْ أَنَّهُمْ رَضُوا مَا آتَاهُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّـهُ سَيُؤْتِينَا اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ وَرَسُولُهُ إِنَّا إِلَى اللَّـهِ رَاغِبُونَ﴿٥٩﴾
59. Na lau wangeliridhiya yale Aliyowapa Allaah na Rasuli Wake, na wakasema: “Anatutosheleza Allaah, karibuni Allaah Atatupa katika fadhila Zake na Rasuli Wake (pia); hakika sisi kwa Allaah tuna raghba.”
إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۖ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗوَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿٦٠﴾
60. Hakika Zakaah ni kwa ajili ya mafakiri na masikini na wanaozitumikia, na wanaotiwa nguvu nyoyo zao (katika Uislamu) na kuwakomboa mateka, na wenye deni na katika njia ya Allaah na msafiri (aliyeharibikiwa). Ni faradhi itokayo kwa Allaah. Na Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.
وَمِنْهُمُ الَّذِينَ يُؤْذُونَ النَّبِيَّ وَيَقُولُونَ هُوَ أُذُنٌ ۚ قُلْ أُذُنُ خَيْرٍ لَّكُمْ يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَيُؤْمِنُ لِلْمُؤْمِنِينَ وَرَحْمَةٌ لِّلَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ ۚ وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ رَسُولَ اللَّـهِ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٦١﴾
61. Na miongoni mwao wako wale wanaomuudhi Nabiy, na wanasema: “Yeye ni mtegaji sikio tu.” Sema: “Sikio la khayr kwenu anamwamini Allaah na anawaamini Waumini, na ni rahmah kwa wale walioamini miongoni mwenu.” Na wale wanaomuudhi Rasuli wa Allaah watapata adhabu iumizayo.
يَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَكُمْ لِيُرْضُوكُمْ وَاللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَحَقُّ أَن يُرْضُوهُ إِن كَانُوا مُؤْمِنِينَ﴿٦٢﴾
62. Wanakuapieni kwa Jina la Allaah ili wakuridhisheni, hali ya kuwa Allaah na Rasuli Wake ndio wanaostahiki zaidi kuridhishwa lau kama wao ni Waumini.
أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّهُ مَن يُحَادِدِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَأَنَّ لَهُ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدًا فِيهَاۚ ذَٰلِكَ الْخِزْيُ الْعَظِيمُ﴿٦٣﴾
63. Je, hawajui kwamba yeyote mwenye kumpinga Allaah na Rasuli Wake basi hakika atapata Jahannam ni mwenye kudumu humo. Hiyo ni hizaaya kuu.
يَحْذَرُ الْمُنَافِقُونَ أَن تُنَزَّلَ عَلَيْهِمْ سُورَةٌ تُنَبِّئُهُم بِمَا فِي قُلُوبِهِمْ ۚ قُلِ اسْتَهْزِئُوا إِنَّ اللَّـهَ مُخْرِجٌ مَّا تَحْذَرُونَ﴿٦٤﴾
64. Wanafiki wanatahadhari isije kuteremshwa Suwrah itakayowajulisha yaliyomo nyoyoni mwao. Sema: “Fanyeni istihzai; hakika Allaah Atayatoa yale mnayotahadhari nayo.”
وَلَئِن سَأَلْتَهُمْ لَيَقُولُنَّ إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلْعَبُ ۚ قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ﴿٦٥﴾
65. Na ukiwauliza, bila shaka watasema: “Hakika tulikuwa tunaporoja na tunacheza.” Sema: “Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayaat Zake na Rasuli Wake?”
لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ ۚإِن نَّعْفُ عَن طَائِفَةٍ مِّنكُمْ نُعَذِّبْ طَائِفَةً بِأَنَّهُمْ كَانُوا مُجْرِمِينَ﴿٦٦﴾
66. Msitoe udhuru. Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu. Tukilisamehe kundi miongoni mwenu, Tutaliadhibu kundi (jingine), kwa kuwa wao walikuwa wakhalifu.
الْمُنَافِقُونَ وَالْمُنَافِقَاتُ بَعْضُهُم مِّن بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمُنكَرِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمَعْرُوفِ وَيَقْبِضُونَ أَيْدِيَهُمْ ۚ نَسُوا اللَّـهَ فَنَسِيَهُمْ ۗ إِنَّ الْمُنَافِقِينَ هُمُ الْفَاسِقُونَ﴿٦٧﴾
67. Wanafiki wanaume na wanafiki wanawake wenyewe kwa wenyewe, wanaamrisha munkari na wanakataza mema na hufumba mikono yao; wamemsahau Allaah, basi Naye Amewasahau. Hakika wanafiki wao ndio mafasiki.
وَعَدَ اللَّـهُ الْمُنَافِقِينَ وَالْمُنَافِقَاتِ وَالْكُفَّارَ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ هِيَ حَسْبُهُمْ ۚ وَلَعَنَهُمُ اللَّـهُ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّقِيمٌ﴿٦٨﴾
68. Allaah Amewaahidi wanafiki wanaume na wanafiki wanawake na makafiri moto wa Jahannam, ni wenye kudumu humo; unawatosheleza Na Allaah Amewalaani, na watapata adhabu ya kudumu.
كَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ كَانُوا أَشَدَّ مِنكُمْ قُوَّةً وَأَكْثَرَ أَمْوَالًا وَأَوْلَادًا فَاسْتَمْتَعُوا بِخَلَاقِهِمْ فَاسْتَمْتَعْتُم بِخَلَاقِكُمْ كَمَا اسْتَمْتَعَ الَّذِينَ مِن قَبْلِكُم بِخَلَاقِهِمْ وَخُضْتُمْ كَالَّذِي خَاضُوا ۚ أُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖوَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ﴿٦٩﴾
69. Ni kama wale wa kabla yenu, walikuwa wana nguvu zaidi kuliko nyinyi, na wana mali na watoto wengi zaidi. Basi walistarehe kwa fungu lao nanyi mnastarehe kwa fungu lenu, kama walivyostarehe kwa fungu lao wale wa kabla yenu; na mkatumbukia katika ubatilifu na ukanushaji kama walivyotumbukia. Hao zimeporomoka ‘amali zao duniani na Aakhirah. Na hao ndio waliokhasirika.
أَلَمْ يَأْتِهِمْ نَبَأُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ قَوْمِ نُوحٍ وَعَادٍ وَثَمُودَ وَقَوْمِ إِبْرَاهِيمَ وَأَصْحَابِ مَدْيَنَ وَالْمُؤْتَفِكَاتِ ۚ أَتَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ ۖ فَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ﴿٧٠﴾
70. Je, haikuwafikia khabari ya wale wa kabla yao; kaumu ya Nuwh, na ‘Aad na Thamuwd, na kaumu ya Ibraahiym, na watu ya Madyan, na miji iliyopinduliwa juu chini? Rusuli wao waliwafikia kwa hoja bayana. Na Allaah Hakuwa Mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao wenyewe.
وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَيُطِيعُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚأُولَـٰئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ اللَّـهُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿٧١﴾
71. Na Waumini wanaume na Waumini wanawake ni marafiki wandani wao kwa wao, wanaamrisha mema na wanakataza munkari na wanasimamisha Swalaah na wanatoa Zakaah na wanamtii Allaah na Rasuli Wake. Hao Allaah Atawarehemu. Hakika Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.
وَعَدَ اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ۚ وَرِضْوَانٌ مِّنَ اللَّـهِ أَكْبَرُ ۚذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٧٢﴾
72. Allaah Amewaahidi Waumini wanaume na Waumini wanawake Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo na makazi mazuri katika Jannaat za kudumu milele. Na radhi kutoka kwa Allaah ndio kubwa zaidi. Huko ndiko kufuzu adhimu.
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ جَاهِدِ الْكُفَّارَ وَالْمُنَافِقِينَ وَاغْلُظْ عَلَيْهِمْ ۚ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖوَبِئْسَ الْمَصِيرُ﴿٧٣﴾
73. Ee Nabiy! Fanya jihaad dhidi ya makafiri na wanafiki na kuwa mkali kwao. Na makazi yao ni Jahannam, na ubaya ulioje mahali pa kuishia.
يَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ مَا قَالُوا وَلَقَدْ قَالُوا كَلِمَةَ الْكُفْرِ وَكَفَرُوا بَعْدَ إِسْلَامِهِمْ وَهَمُّوا بِمَا لَمْ يَنَالُوا ۚ وَمَا نَقَمُوا إِلَّا أَنْ أَغْنَاهُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ مِن فَضْلِهِ ۚ فَإِن يَتُوبُوا يَكُ خَيْرًا لَّهُمْ ۖ وَإِن يَتَوَلَّوْا يُعَذِّبْهُمُ اللَّـهُ عَذَابًا أَلِيمًا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ وَمَا لَهُمْ فِي الْأَرْضِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ﴿٧٤﴾
74. Wanaapa kwa Jina la Allaah kuwa hawakusema na hali wamekwishasema neno la kufuru, na wakakufuru baada ya kusilimu kwao. Na wakaazimia yale ambayo hawakuweza kuyafikia. Na hawakuchukia isipokuwa kwa kuwa Allaah na Rasuli Wake Amewatajirisha kwa fadhila Zake. Basi wakitubia, itakuwa ni khayr kwao. Na wakikengeuka, Allaah Atawaadhibu adhabu iumizayo duniani na Aakhirah. Na hawatopata katika ardhi mlinzi yeyote wala mwenye kunusuru.
وَمِنْهُم مَّنْ عَاهَدَ اللَّـهَ لَئِنْ آتَانَا مِن فَضْلِهِ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ الصَّالِحِينَ﴿٧٥﴾
75. Na miongoni mwao wako waliomuahidi Allaah (kuwa): “Akitupa katika fadhila Zake, bila shaka tutatoa Swadaqah, na bila shaka tutakuwa miongoni mwa Swalihina.”
فَلَمَّا آتَاهُم مِّن فَضْلِهِ بَخِلُوا بِهِ وَتَوَلَّوا وَّهُم مُّعْرِضُونَ﴿٧٦﴾
76. Alipowapa katika fadhila Zake; walizifanyia ubakhili, na wakakengeuka huku wakipuuza.
فَأَعْقَبَهُمْ نِفَاقًا فِي قُلُوبِهِمْ إِلَىٰ يَوْمِ يَلْقَوْنَهُ بِمَا أَخْلَفُوا اللَّـهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ﴿٧٧﴾
77. Basi Akawapatilizia unafiki katika nyoyo zao mpaka Siku watakayokutana Naye kwa vile walivyomkhalifu kwao Allaah kwa waliyomuahidi, na kwa yale waliyokuwa wakikadhibisha.
أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُمْ وَأَنَّ اللَّـهَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ﴿٧٨﴾
78. Je, hawajui kwamba Allaah Anajua siri zao na minong’ono yao; na kwamba Allaah ni Mjuzi wa ghayb.
الَّذِينَ يَلْمِزُونَ الْمُطَّوِّعِينَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ فِي الصَّدَقَاتِ وَالَّذِينَ لَا يَجِدُونَ إِلَّا جُهْدَهُمْ فَيَسْخَرُونَ مِنْهُمْۙ سَخِرَ اللَّـهُ مِنْهُمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٧٩﴾
79. Wale wanaowafedhehesha kwa kushutumu wenye kujitolea kwa khiari katika kutoa Swadaqah miongoni mwa Waumini, na wale wasiopata (cha kutoa) isipokuwa juhudi zao, wanawafanyia dhihaka, Allaah Analipiza dhihaka zao na watapata adhabu iumizayo.
اسْتَغْفِرْ لَهُمْ أَوْ لَا تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ إِن تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ سَبْعِينَ مَرَّةً فَلَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَهُمْ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ﴿٨٠﴾
80. Waombee maghfirah (ee, Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), au usiwaombee maghfirah, hata ukiwaombea maghfirah mara sabini, Allaah Hatowaghufuria. Hivyo kwa kuwa wao wamemkufuru Allaah na Rasuli Wake. Na Allaah Haongoi watu mafasiki.
فَرِحَ الْمُخَلَّفُونَ بِمَقْعَدِهِمْ خِلَافَ رَسُولِ اللَّـهِ وَكَرِهُوا أَن يُجَاهِدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَقَالُوا لَا تَنفِرُوا فِي الْحَرِّ ۗ قُلْ نَارُ جَهَنَّمَ أَشَدُّ حَرًّا ۚ لَّوْ كَانُوا يَفْقَهُونَ﴿٨١﴾
81. Waliobaki nyuma walifurahi kwa kule kukaa kwao (wasiende vitani) baada ya Rasuli wa Allaah (kutoka); na walikirihika kufanya jihaad kwa mali zao na nafsi zao katika njia ya Allaah; na wakasema: “Msitoke kwenda katika joto.” Sema: “Moto wa Jahannam ni mkali zaidi lau wangelifahamu.”
فَلْيَضْحَكُوا قَلِيلًا وَلْيَبْكُوا كَثِيرًا جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٨٢﴾
82. Basi na wacheke kidogo (duniani), na watalia sana (Aakhirah); jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.
فَإِن رَّجَعَكَ اللَّـهُ إِلَىٰ طَائِفَةٍ مِّنْهُمْ فَاسْتَأْذَنُوكَ لِلْخُرُوجِ فَقُل لَّن تَخْرُجُوا مَعِيَ أَبَدًا وَلَن تُقَاتِلُوا مَعِيَ عَدُوًّا ۖإِنَّكُمْ رَضِيتُم بِالْقُعُودِ أَوَّلَ مَرَّةٍ فَاقْعُدُوا مَعَ الْخَالِفِينَ﴿٨٣﴾
83. Basi Allaah Akikurejesha kwa kundi miongoni mwao na wakakutaka idhini ya kutoka; sema: “Hamtotoka pamoja nami abadani, na wala hamtopigana na maadui pamoja nami. Hakika nyinyi mliridhika kukaa (majumbani) mara ya kwanza; basi kaeni pamoja na wanaobakia nyuma.
وَلَا تُصَلِّ عَلَىٰ أَحَدٍ مِّنْهُم مَّاتَ أَبَدًا وَلَا تَقُمْ عَلَىٰ قَبْرِهِ ۖ إِنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَمَاتُوا وَهُمْ فَاسِقُونَ﴿٨٤﴾
84. Na wala usimswalie yeyote abadani miongoni mwao akifa; na wala usisimame kaburini kwake. Hakika wao wamemkufuru Allaah na Rasuli Wake, na wakafa hali wao ni mafasiki.
وَلَا تُعْجِبْكَ أَمْوَالُهُمْ وَأَوْلَادُهُمْ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُعَذِّبَهُم بِهَا فِي الدُّنْيَا وَتَزْهَقَ أَنفُسُهُمْ وَهُمْ كَافِرُونَ﴿٨٥﴾
85. Na wala isikupendezee mali zao na watoto wao. Hakika Allaah Anataka Awaadhibu kwayo duniani, na zitokelee mbali nafsi zao na huku wao wakiwa ni makafiri.
وَإِذَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ أَنْ آمِنُوا بِاللَّـهِ وَجَاهِدُوا مَعَ رَسُولِهِ اسْتَأْذَنَكَ أُولُو الطَّوْلِ مِنْهُمْ وَقَالُوا ذَرْنَا نَكُن مَّعَ الْقَاعِدِينَ﴿٨٦﴾
86. Na inapoteremshwa Suwrah kwamba “Muaminini Allaah, na fanyeni jihaad pamoja na Rasuli Wake,” wanakuomba idhini wale (wanafiki) wenye utajiri miongoni mwao, na husema: “Tuache tuwe pamoja na wanaokaa (majumbani).”
رَضُوا بِأَن يَكُونُوا مَعَ الْخَوَالِفِ وَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَفْقَهُونَ﴿٨٧﴾
87. Wameridhika kuwa pamoja na waliokaa nyuma, na zikapigwa chapa nyoyo zao, basi wao hawafahamu.
لَـٰكِنِ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ جَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ ۚ وَأُولَـٰئِكَ لَهُمُ الْخَيْرَاتُ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿٨٨﴾
88. Lakini Rasuli na wale walioamini pamoja naye, walifanya jihaad kwa mali zao na nafsi zao. Na hao watapata khayr nyingi. Na hao ndio wenye kufaulu.
أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٨٩﴾
89. Allaah Amewaandalia Jannaatzipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo. Huko ndiko kufuzu adhimu.
وَجَاءَ الْمُعَذِّرُونَ مِنَ الْأَعْرَابِ لِيُؤْذَنَ لَهُمْ وَقَعَدَ الَّذِينَ كَذَبُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚسَيُصِيبُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٩٠﴾
90. Na wakaja wenye nyudhuru katika Mabedui ili waruhusiwe (wasiende vitani), na wakakaa (majumbani) wale waliomkadhibisha Allaah na Rasuli Wake. Itawasibu wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo.
لَّيْسَ عَلَى الضُّعَفَاءِ وَلَا عَلَى الْمَرْضَىٰ وَلَا عَلَى الَّذِينَ لَا يَجِدُونَ مَا يُنفِقُونَ حَرَجٌ إِذَا نَصَحُوا لِلَّـهِ وَرَسُولِهِ ۚ مَا عَلَى الْمُحْسِنِينَ مِن سَبِيلٍ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٩١﴾
91. Hapana lawama juu ya wale walio dhaifu na wala juu ya walio wagonjwa, na wala juu ya wale wasiopata cha kutoa (katika jihaad), madamu wakimsafia niyyah Allaah na Rasuli Wake. Hapana njia ya kuwalaumu wafanyao ihsaan. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.
وَلَا عَلَى الَّذِينَ إِذَا مَا أَتَوْكَ لِتَحْمِلَهُمْ قُلْتَ لَا أَجِدُ مَا أَحْمِلُكُمْ عَلَيْهِ تَوَلَّوا وَّأَعْيُنُهُمْ تَفِيضُ مِنَ الدَّمْعِ حَزَنًا أَلَّا يَجِدُوا مَا يُنفِقُونَ﴿٩٢﴾
92. Na wala (hakuna lawama) juu ya wale ambao wanapokujia ili uwapatie kipando; Ukasema: “Sina cha kukupandisheni.” Wamegeuka nyuma na huku macho yao yanamiminika machozi kwa huzuni ya kukosa kupata cha kutoa mchango.
إِنَّمَا السَّبِيلُ عَلَى الَّذِينَ يَسْتَأْذِنُونَكَ وَهُمْ أَغْنِيَاءُ ۚ رَضُوا بِأَن يَكُونُوا مَعَ الْخَوَالِفِ وَطَبَعَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٩٣﴾
93. Hakika (ipo) sababu ya kulaumu kwa wale wanaokuomba idhini na hali wao ni matajiri. Wameridhia kuwa pamoja na waliobakia nyuma; na Allaah Akapiga chapa juu ya nyoyo zao, basi wao hawajui.
يَعْتَذِرُونَ إِلَيْكُمْ إِذَا رَجَعْتُمْ إِلَيْهِمْ ۚقُل لَّا تَعْتَذِرُوا لَن نُّؤْمِنَ لَكُمْ قَدْ نَبَّأَنَا اللَّـهُ مِنْ أَخْبَارِكُمْ ۚ وَسَيَرَى اللَّـهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٩٤﴾
94. Watakutoleeni udhuru mtakaporejea kwao. Sema: “Msitoe udhuru, hatutokuaminini! Allaah Amekwishatujulisha khabari zenu. Na hivi karibuni Allaah na Rasuli Wake wataona ‘amali zenu. Kisha mtarudishwa kwa Mjuzi wa ghayb na dhahiri, Atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.”
سَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَكُمْ إِذَا انقَلَبْتُمْ إِلَيْهِمْ لِتُعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ فَأَعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ إِنَّهُمْ رِجْسٌ ۖ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٩٥﴾
95. Watakuapieni kwa Allaah, mtakaporudi kwao ili muwapuuze. Basi wapuuzeni; hakika wao ni najsi, na makazi yao ni Jahannam. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.
يَحْلِفُونَ لَكُمْ لِتَرْضَوْا عَنْهُمْ ۖ فَإِن تَرْضَوْا عَنْهُمْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يَرْضَىٰ عَنِ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ﴿٩٦﴾
96. Watakuapieni ili muwaridhie. Mkiwaridhia, basi hakika Allaah Haridhii watu mafasiki.
الْأَعْرَابُ أَشَدُّ كُفْرًا وَنِفَاقًا وَأَجْدَرُ أَلَّا يَعْلَمُوا حُدُودَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿٩٧﴾
97. Mabedui wamezidi zaidi kufuru na unafiki, na wameelekea zaidi kwamba wasijue mipaka ya (shariy’ah) Alizoteremsha Allaah juu ya Rasuli Wake. Na Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.
وَمِنَ الْأَعْرَابِ مَن يَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ مَغْرَمًا وَيَتَرَبَّصُ بِكُمُ الدَّوَائِرَ ۚ عَلَيْهِمْ دَائِرَةُ السَّوْءِ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿٩٨﴾
98. Na katika Mabedui, wako wanaochukulia yale wanayoyatoa kuwa ni gharama tupu, na wanakungojeleeni migeuko ya misiba. Misiba mibaya itawafika wao. Na Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.
وَمِنَ الْأَعْرَابِ مَن يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ قُرُبَاتٍ عِندَ اللَّـهِ وَصَلَوَاتِ الرَّسُولِ ۚ أَلَا إِنَّهَا قُرْبَةٌ لَّهُمْ ۚ سَيُدْخِلُهُمُ اللَّـهُ فِي رَحْمَتِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٩٩﴾
99. Na katika Mabedui, wako wanaomwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na wanachukulia yale wanayoyatoa kuwa ni njia ya makurubisho mbele ya Allaah, na kupata du’aa ya Rasuli. Tanabahi! Hakika hiyo ni njia ya kikurubisho kwao. Allaah Atawaingiza katika rahmah Yake. Hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.
وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١٠٠﴾
100. Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhajirina na Answaar na wale waliowafuata kwa ihsaan; Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Na Amewaandalia Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo abadi. Huko ndiko kufuzu adhimu.
وَمِمَّنْ حَوْلَكُم مِّنَ الْأَعْرَابِ مُنَافِقُونَ ۖوَمِنْ أَهْلِ الْمَدِينَةِ ۖ مَرَدُوا عَلَى النِّفَاقِ لَا تَعْلَمُهُمْ ۖ نَحْنُ نَعْلَمُهُمْ ۚ سَنُعَذِّبُهُم مَّرَّتَيْنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلَىٰ عَذَابٍ عَظِيمٍ﴿١٠١﴾
101. Na katika Mabedui wanaokuzungukeni wako wanafiki. Na katika watu wa Madiynah (pia) walibobea katika unafiki. Huwajui (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Sisi Tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili; kisha watarudishwa katika adhabu kuu.
وَآخَرُونَ اعْتَرَفُوا بِذُنُوبِهِمْ خَلَطُوا عَمَلًا صَالِحًا وَآخَرَ سَيِّئًا عَسَى اللَّـهُ أَن يَتُوبَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١٠٢﴾
102. Na wengineo wamekiri madhambi yao; wamechanganya ‘amali njema na nyinginezo ovu; asaa Allaah Apokee tawbah zao. Hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.
خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّ صَلَاتَكَ سَكَنٌ لَّهُمْ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿١٠٣﴾
103. Chukua (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika mali zao Swadaqah, uwatakase na ziwazidishie kwazo na waombee du’aa (na maghfirah). Hakika du’aa yako ni utulivu kwao. Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.
أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ هُوَ يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَأْخُذُ الصَّدَقَاتِ وَأَنَّ اللَّـهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ﴿١٠٤﴾
104. Je, hawajui kwamba Allaah Ndiye Anayepokea tawbah ya waja Wake, na Anapokea Swadaqah na kwamba Allaah Ndiye Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu.
وَقُلِ اعْمَلُوا فَسَيَرَى اللَّـهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ وَالْمُؤْمِنُونَ ۖ وَسَتُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿١٠٥﴾
105. Na sema: “Fanyeni (mtakavyo). Allaah Ataona ‘amali zenu na Rasuli Wake na Waumini (pia wataona). Na mtarudishwa kwa Mjuzi wa ghayb na dhahiri; kisha Atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.”
وَآخَرُونَ مُرْجَوْنَ لِأَمْرِ اللَّـهِ إِمَّا يُعَذِّبُهُمْ وَإِمَّا يَتُوبُ عَلَيْهِمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿١٠٦﴾
106. Na wengineo wamengojeshewa kwa amri ya Allaah. Ama Atawaadhibu au Atawapokelea tawbah zao. Na Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.
وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مَسْجِدًا ضِرَارًا وَكُفْرًا وَتَفْرِيقًا بَيْنَ الْمُؤْمِنِينَ وَإِرْصَادًا لِّمَنْ حَارَبَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ مِن قَبْلُ ۚوَلَيَحْلِفُنَّ إِنْ أَرَدْنَا إِلَّا الْحُسْنَىٰ ۖ وَاللَّـهُ يَشْهَدُ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ﴿١٠٧﴾
107. Na wale waliojenga Msikiti kwa ajili ya kuleta madhara na kufuru na kufarikisha baina ya Waumini na pa kuvizia waliompiga vita Allaah na Rasuli Wake hapo kabla. Na bila shaka wanaapa: “Hatukukusudia ila jambo zuri.” Na Allaah Anashuhudia kwamba hakika wao ni waongo.
لَا تَقُمْ فِيهِ أَبَدًا ۚ لَّمَسْجِدٌ أُسِّسَ عَلَى التَّقْوَىٰ مِنْ أَوَّلِ يَوْمٍ أَحَقُّ أَن تَقُومَ فِيهِ ۚ فِيهِ رِجَالٌ يُحِبُّونَ أَن يَتَطَهَّرُوا ۚوَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُطَّهِّرِينَ﴿١٠٨﴾
108. Usisimame humo abadani. Bila shaka Msikiti ulioasisiwa juu ya taqwa tokea siku ya kwanza unastahiki zaidi usimame humo. Humo mna watu wanaopenda kujitwaharisha. Na Allaah Anapenda wanaojitwaharisha.
أَفَمَنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَىٰ تَقْوَىٰ مِنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانٍ خَيْرٌ أَم مَّنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَىٰ شَفَا جُرُفٍ هَارٍ فَانْهَارَ بِهِ فِي نَارِ جَهَنَّمَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿١٠٩﴾
109. Je, yule aliyeasisi jengo lake juu ya taqwa ya Allaah na radhi (Zake), ni bora au yule aliyeasisi jengo lake juu ya ukingo wa bonde lenye ufa lenye kuburugunyika likaporomoka pamoja naye katika moto wa Jahannam? Na Allaah Haongozi watu madhalimu.
لَا يَزَالُ بُنْيَانُهُمُ الَّذِي بَنَوْا رِيبَةً فِي قُلُوبِهِمْ إِلَّا أَن تَقَطَّعَ قُلُوبُهُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿١١٠﴾
110. Halitoacha jengo lao hilo walolijenga kuwa ni sababu ya kuwatia shaka katika nyoyo zao mpaka nyoyo zao zikatike katike; na Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.
إِنَّ اللَّـهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ ۚ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ ۖوَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ وَالْقُرْآنِ ۚ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّـهِ ۚ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُم بِهِ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١١١﴾
111. Hakika Allaah Amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwamba watapata Jannah. Wanapigana katika njia ya Allaah, wanaua na wanauawa. Hii ni ahadi ya haki Aliyojiwekea katika Tawraat na Injiyl na Qur-aan. Na nani atimizae zaidi ahadi yake kuliko Allaah? Basi furahieni kwa biashara yenu mliyofungamana Naye. Na huko ndiko kufuzu adhimu.
التَّائِبُونَ الْعَابِدُونَ الْحَامِدُونَ السَّائِحُونَ الرَّاكِعُونَ السَّاجِدُونَ الْآمِرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَالنَّاهُونَ عَنِ الْمُنكَرِ وَالْحَافِظُونَ لِحُدُودِ اللَّـهِ ۗوَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ﴿١١٢﴾
112. (Waumini hao ni;) Wanaotubia, wanaofanya ‘ibaadah, wanaomhimidi (Allaah), wenye swiyaam (au wanaokwenda jihaad), wanaorukuu, wanaosujudu, wanaoamrisha mema na wanaokataza munkari, na wanaohifadhi mipaka ya Allaah. Na wabashirie Waumini.
مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ﴿١١٣﴾
113. Haimpasi Nabiy na wale walioamini kuwaombea maghfirah washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa moto uwakao vikali mno.
وَمَا كَانَ اسْتِغْفَارُ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوْعِدَةٍ وَعَدَهَا إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ أَنَّهُ عَدُوٌّ لِّلَّـهِ تَبَرَّأَ مِنْهُ ۚ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَأَوَّاهٌ حَلِيمٌ ﴿١١٤﴾
114. Na haikuwa Ibraahiym kumuombea maghfirah baba yake isipokuwa kwa sababu ya ahadi aliyoahidiana naye. Lakini ilipombainikia kwamba yeye ni adui wa Allaah, alijiepusha naye. Hakika Ibraahiym ni mwenye huruma mno na mvumilivu.
وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِلَّ قَوْمًا بَعْدَ إِذْ هَدَاهُمْ حَتَّىٰ يُبَيِّنَ لَهُم مَّا يَتَّقُونَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴿١١٥﴾
115. Na haiwi kwa Allaah Awapotoze watu baada ya kuwa Amewaongoa mpaka Awabainishie ya kujikinga nayo. Hakika Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi.
إِنَّ اللَّـهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖيُحْيِي وَيُمِيتُ ۚ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ﴿١١٦﴾
116. Hakika Allaah Anao ufalme wa mbingu na ardhi. Anahuisha na Anafisha. Nanyi hamna pasi na Allaah mlinzi wala mnusuraji yeyote.
لَّقَد تَّابَ اللَّـهُ عَلَى النَّبِيِّ وَالْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ الْعُسْرَةِ مِن بَعْدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٍ مِّنْهُمْ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّهُ بِهِمْ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١١٧﴾
117. Kwa yakini Allaah Amepokea tawbah ya Nabiy na Muhajirina na Answaar ambao wamemfuata (Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) katika saa ya dhiki baada ya nyoyo za kundi miongoni mwao zilikaribia kuelemea mbali na haki Akapokea tawbah yao. Hakika Yeye kwao ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.
وَعَلَى الثَّلَاثَةِ الَّذِينَ خُلِّفُوا حَتَّىٰ إِذَا ضَاقَتْ عَلَيْهِمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ وَضَاقَتْ عَلَيْهِمْ أَنفُسُهُمْ وَظَنُّوا أَن لَّا مَلْجَأَ مِنَ اللَّـهِ إِلَّا إِلَيْهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ لِيَتُوبُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ﴿١١٨﴾
118. Na (Akapokea tawbah) ya wale watatu waliobaki nyuma (wakajuta mno) mpaka ardhi ikadhikika kwao juu ya kuwa ni pana na zikadhikika nafsi zao, na wakatambua kwamba hakuna pa kumkimbia Allaah isipokuwa kuelekea Kwake; kisha (Allaah) Akapokea tawbah yao, ili watubie. Hakika Allaah Yeye Ndiye Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ﴿١١٩﴾
119. Enyi walioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na wakweli.
مَا كَانَ لِأَهْلِ الْمَدِينَةِ وَمَنْ حَوْلَهُم مِّنَ الْأَعْرَابِ أَن يَتَخَلَّفُوا عَن رَّسُولِ اللَّـهِ وَلَا يَرْغَبُوا بِأَنفُسِهِمْ عَن نَّفْسِهِ ۚذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ لَا يُصِيبُهُمْ ظَمَأٌ وَلَا نَصَبٌ وَلَا مَخْمَصَةٌ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَطَئُونَ مَوْطِئًا يَغِيظُ الْكُفَّارَ وَلَا يَنَالُونَ مِنْ عَدُوٍّ نَّيْلًا إِلَّا كُتِبَ لَهُم بِهِ عَمَلٌ صَالِحٌ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ﴿١٢٠﴾
120. Haikuwapasa watu wa Madiynah na Mabedui walio pembezoni mwao kwamba wabakie nyuma wasitoke na Rasuli wa Allaah, wala kujipendelea nafsi zao kuliko nafsi yake. Hivyo ni kwa kuwa wao haiwasibu kiu wala machofu, wala njaa kali katika njia ya Allaah, na wala hawakanyagi njia inayowaghadhibisha makafiri, na wala hawawasibu maadui msiba wowote ila wanaandikiwa kwayo ‘amali njema. Hakika Allaah Hapotezi ujira wa wafanyao ihsaan.
وَلَا يُنفِقُونَ نَفَقَةً صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً وَلَا يَقْطَعُونَ وَادِيًا إِلَّا كُتِبَ لَهُمْ لِيَجْزِيَهُمُ اللَّـهُ أَحْسَنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٢١﴾
121. Na wala hawatoi mchango wowote mdogo au mkubwa na wala hawavuki bonde isipokuwa wameandikiwa ili Allaah Awalipe mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wanayatenda.
وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُوا كَافَّةً ۚفَلَوْلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَائِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُوا فِي الدِّينِ وَلِيُنذِرُوا قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوا إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ﴿١٢٢﴾
122. Na haiwapasi Waumini watoke wote pamoja (kupigana jihaad). Basi kwanini lisitoke katika kila kundi miongoni mwao, kundi (moja tu) wajifunze vyema Dini na ili waonye watu wao watakaporejea kwao ili wapate kujihadharisha.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قَاتِلُوا الَّذِينَ يَلُونَكُم مِّنَ الْكُفَّارِ وَلْيَجِدُوا فِيكُمْ غِلْظَةً ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ﴿١٢٣﴾
123. Enyi walioamini! Piganeni jihaad na wale makafiri walio karibu nanyi na waukute kwenu ukali. Na jueni kwamba Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa.
وَإِذَا مَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ فَمِنْهُم مَّن يَقُولُ أَيُّكُمْ زَادَتْهُ هَـٰذِهِ إِيمَانًا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَزَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَهُمْ يَسْتَبْشِرُونَ﴿١٢٤﴾
124. Na inapoteremshwa Suwrah, basi miongoni mwao wako wanaosema: “Nani kati yenu imemzidishia (Suwrah) hii iymaan?” Ama wale walioamini huwazidishia iymaan nao wanafurahia.
وَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَتْهُمْ رِجْسًا إِلَىٰ رِجْسِهِمْ وَمَاتُوا وَهُمْ كَافِرُونَ﴿١٢٥﴾
125. Na ama wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi, huwazidishia rijs (unafiki, shaka n.k.) juu ya rijs yao, na wakafa hali wao ni makafiri.
أَوَلَا يَرَوْنَ أَنَّهُمْ يُفْتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٍ مَّرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمْ يَذَّكَّرُونَ﴿١٢٦﴾
126. Je, hawaoni kwamba wao wanatahiniwa katika kila mwaka mara moja au mara mbili; kisha hawatubii na wala wao hawakumbuki?
وَإِذَا مَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ نَّظَرَ بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ هَلْ يَرَاكُم مِّنْ أَحَدٍ ثُمَّ انصَرَفُوا ۚ صَرَفَ اللَّـهُ قُلُوبَهُم بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ﴿١٢٧﴾
127. Na inapoteremshwa Suwrah wanatazamana wenyewe kwa wenyewe (wakisema:) “Je, kuna mmoja yeyote anayekuoneni?” Kisha wanageuka kuondokea mbali. Allaah Amewagezua nyoyo zao kwa kuwa wao ni watu wasiofahamu.
لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١٢٨﴾
128. Kwa yakini amekujieni Rasuli anayetokana na nyinyi wenyewe, yanamtia mashaka (na huzuni) yanayokutaabisheni, anakujalini, mwenye huruma kwa Waumini ni mwenye huruma mno, mwenye rahmah.
فَإِن تَوَلَّوْا فَقُلْ حَسْبِيَ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ ۖ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ﴿١٢٩﴾
129. Na wakikengeuka, basi sema: “Amenitosheleza Allaah; Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Kwake nimetawakali. Naye ni Rabb wa ‘Arsh adhimu.