007 - Al-A'raaf
الأَعْرَاف
Al-A’raaf: 7
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
المص ﴿١﴾
1. Alif Laam Miym Swaad.[1]
كِتَابٌ أُنزِلَ إِلَيْكَ فَلَا يَكُن فِي صَدْرِكَ حَرَجٌ مِّنْهُ لِتُنذِرَ بِهِ وَذِكْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ﴿٢﴾
2. Kitabu (hiki) kimeteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) basi isiwe katika kifua chako dhiki kwa ajili yake, ili uwaonye kwacho na ni ukumbusho kwa Waumini.
اتَّبِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ﴿٣﴾
3. Fuateni yale mliyoteremshiwa kutoka kwa Rabb wenu na wala msifuate badala Yake marafiki walinzi. Ni machache mnayoyakumbuka.
وَكَم مِّن قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا فَجَاءَهَا بَأْسُنَا بَيَاتًا أَوْ هُمْ قَائِلُونَ ﴿٤﴾
4. Na miji mingapi Tumeiangamiza ikaifikia adhabu Yetu usiku au walipokuwa katika usingizi wa mchana.
فَمَا كَانَ دَعْوَاهُمْ إِذْ جَاءَهُم بَأْسُنَا إِلَّا أَن قَالُوا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ ﴿٥﴾
5. Basi haikuwa kilio chao ilipowajia adhabu Yetu isipokuwa walisema: “Hakika sisi tulikuwa madhalimu.”
فَلَنَسْأَلَنَّ الَّذِينَ أُرْسِلَ إِلَيْهِمْ وَلَنَسْأَلَنَّ الْمُرْسَلِينَ ﴿٦﴾
6. Basi bila ya shaka Tutawauliza wale ambao waliopelekewa (risala) na bila shaka Tutawauliza Rusuli.
فَلَنَقُصَّنَّ عَلَيْهِم بِعِلْمٍ ۖ وَمَا كُنَّا غَائِبِينَ﴿٧﴾
7. Kisha Tutawasimulia kwa elimu (‘amali zao), na hatukuwa wenye kukosekana.
وَالْوَزْنُ يَوْمَئِذٍ الْحَقُّ ۚ فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٨﴾
8. Na kipimo kwa mizani Siku hiyo itakuwa ni haki. Basi ambao mizani yao itakuwa nzito, hao ndio watakaofaulu.
وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُم بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَظْلِمُونَ ﴿٩﴾
9. Na ambao mizani yao itakuwa khafifu, basi hao ni wale waliokhasirika nafsi zao kwa yale waliyokuwa wakizifanyia dhulma Aayaat Zetu.
وَلَقَدْ مَكَّنَّاكُمْ فِي الْأَرْضِ وَجَعَلْنَا لَكُمْ فِيهَا مَعَايِشَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ ﴿١٠﴾
10. Kwa yakini Tumekumakinisheni katika ardhi na Tukawaekea humo mahitaji ya maisha. Kidogo sana mnayoshukuru.
وَلَقَدْ خَلَقْنَاكُمْ ثُمَّ صَوَّرْنَاكُمْ ثُمَّ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ لَمْ يَكُن مِّنَ السَّاجِدِينَ ﴿١١﴾
11. Na kwa yakini Tumekuumbeni kisha Tukakutieni sura; kisha Tukawaambia Malaika: “Msujudieni Aadam.” Wakasujudu isipokuwa Ibliys hakuwa miongoni mwa waliosujudu.
قَالَ مَا مَنَعَكَ أَلَّا تَسْجُدَ إِذْ أَمَرْتُكَ ۖقَالَ أَنَا خَيْرٌ مِّنْهُ خَلَقْتَنِي مِن نَّارٍ وَخَلَقْتَهُ مِن طِينٍ ﴿١٢﴾
12. (Allaah) Akasema: “Nini kilichokuzuia usisujudu Nilipokuamrisha?” (Ibliys) Akasema: “Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye Umemuumba kwa udongo.”
قَالَ فَاهْبِطْ مِنْهَا فَمَا يَكُونُ لَكَ أَن تَتَكَبَّرَ فِيهَا فَاخْرُجْ إِنَّكَ مِنَ الصَّاغِرِينَ ﴿١٣﴾
13. (Allaah) Akasema: “Basi shuka humo, kwani haikupasa kwako utakabari humo. Hivyo toka hakika wewe ni miongoni mwa walio duni na dhalili.”
قَالَ أَنظِرْنِي إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٤﴾
14. (Ibliys) Akasema: “Nipe muhula hadi Siku watakapofufuliwa”
قَالَ إِنَّكَ مِنَ الْمُنظَرِينَ ﴿١٥﴾
15. (Allaah) Akasema: “Hakika wewe ni miongoni mwa waliopewa muhula.”
قَالَ فَبِمَا أَغْوَيْتَنِي لَأَقْعُدَنَّ لَهُمْ صِرَاطَكَ الْمُسْتَقِيمَ ﴿١٦﴾
16. (Ibliys) Akasema: “Basi kwa kuwa Umenihukumia kupotoka, nitawakalia (waja Wako) katika njia Yako iliyonyooka.”
ثُمَّ لَآتِيَنَّهُم مِّن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ وَعَنْ أَيْمَانِهِمْ وَعَن شَمَائِلِهِمْ ۖوَلَا تَجِدُ أَكْثَرَهُمْ شَاكِرِينَ ﴿١٧﴾
17. “Kisha nitawaendea mbele yao na nyuma na kuliani kwao na kushotoni kwao, na wala Hutopata wengi wao wenye kushukuru.”
قَالَ اخْرُجْ مِنْهَا مَذْءُومًا مَّدْحُورًا ۖلَّمَن تَبِعَكَ مِنْهُمْ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿١٨﴾
18. (Allaah) Akasema: “Toka humo ukiwa umeshutumiwa na umefukuzwa. Atakayekufuata miongoni mwao, bila shaka Nitajaza Jahannam kwa nyinyi nyote.”
وَيَا آدَمُ اسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ فَكُلَا مِنْ حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَـٰذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿١٩﴾
19. “Na ee Aadam, ishi wewe na mkeo Jannah na mle humo popote mpendapo; na wala msikaribie huu mti, msijekuwa miongoni mwa madhalimu.”
فَوَسْوَسَ لَهُمَا الشَّيْطَانُ لِيُبْدِيَ لَهُمَا مَا وُورِيَ عَنْهُمَا مِن سَوْآتِهِمَا وَقَالَ مَا نَهَاكُمَا رَبُّكُمَا عَنْ هَـٰذِهِ الشَّجَرَةِ إِلَّا أَن تَكُونَا مَلَكَيْنِ أَوْ تَكُونَا مِنَ الْخَالِدِينَ﴿٢٠﴾
20. Basi shaytwaan (naye ni Ibliys) akawatia wasiwasi ili awafichulie yaliyofichwa kwao ya sehemu zao za siri. Na akasema: “Rabb wenu Hakukukatazeni huu mti isipokuwa msijekuwa Malaika wawili au kuwa miongoni mwa wenye kudumu milele.”
وَقَاسَمَهُمَا إِنِّي لَكُمَا لَمِنَ النَّاصِحِينَ﴿٢١﴾
21. Naye akawaapia: “Hakika mimi kwenu nyinyi wawili ni mwenye kukunasihini kidhati.”
فَدَلَّاهُمَا بِغُرُورٍ ۚ فَلَمَّا ذَاقَا الشَّجَرَةَ بَدَتْ لَهُمَا سَوْآتُهُمَا وَطَفِقَا يَخْصِفَانِ عَلَيْهِمَا مِن وَرَقِ الْجَنَّةِ ۖ وَنَادَاهُمَا رَبُّهُمَا أَلَمْ أَنْهَكُمَا عَن تِلْكُمَا الشَّجَرَةِ وَأَقُل لَّكُمَا إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمَا عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿٢٢﴾
22. Basi akawachota (wote wawili) kwa ghururi. Walipoonja mti ule zikawafichukia sehemu zao za siri; na wakaanza kujibandika majani ya Jannah. Na Rabb wao Akawaita: “Je, kwani Mimi Sikukukatazeni mti huo na kukuambieni kwamba shaytwaan ni adui bayana kwenu?”
قَالَا رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ﴿٢٣﴾
23. Wakasema: “Rabb wetu! Tumedhulumu nafsi zetu, na basi Usipotughufuria na Ukaturehemu; bila shaka tutakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”
قَالَ اهْبِطُوا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖوَلَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ ﴿٢٤﴾
24. (Allaah) Akasema: “Shukeni! Nyinyi kwa nyinyi ni maadui. Na kwenye ardhi ndio itakuwa mastakimu na starehe mpaka muda mahsusi.”
قَالَ فِيهَا تَحْيَوْنَ وَفِيهَا تَمُوتُونَ وَمِنْهَا تُخْرَجُونَ ﴿٢٥﴾
25. Akasema: “Humo mtaishi, na humo mtakufa na kutoka humo mtatolewa (kufufuliwa).”
يَا بَنِي آدَمَ قَدْ أَنزَلْنَا عَلَيْكُمْ لِبَاسًا يُوَارِي سَوْآتِكُمْ وَرِيشًا ۖ وَلِبَاسُ التَّقْوَىٰ ذَٰلِكَ خَيْرٌ ۚ ذَٰلِكَ مِنْ آيَاتِ اللَّـهِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ ﴿٢٦﴾
26. “Enyi wana wa Aadam! Kwa yakini Tumekuteremshieni libasi linaficha sehemu zenu za siri na (nguo) kama pambo. Na libasi la taqwa ndiyo bora zaidi. Hizo ni katika Aayaat (ishara, dalili) za Allaah ili wapate kukumbuka.”
يَا بَنِي آدَمَ لَا يَفْتِنَنَّكُمُ الشَّيْطَانُ كَمَا أَخْرَجَ أَبَوَيْكُم مِّنَ الْجَنَّةِ يَنزِعُ عَنْهُمَا لِبَاسَهُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوْآتِهِمَا ۗ إِنَّهُ يَرَاكُمْ هُوَ وَقَبِيلُهُ مِنْ حَيْثُ لَا تَرَوْنَهُمْ ۗ إِنَّا جَعَلْنَا الشَّيَاطِينَ أَوْلِيَاءَ لِلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٢٧﴾
27. “Enyi wana wa Aadam! Asikufitinisheni kabisa shaytwaan kama alivyowatoa wazazi wenu katika Jannah; akiwavua nguo zao ili awafichulie sehemu zao za siri. Hakika yeye (Ibliys) anakuoneni, yeye na kabila lake (la mashaytwaan) na hali ya kuwa nyinyi hamuwaoni. Hakika Sisi Tumejaalia mashaytwaan kuwa ni marafiki wandani kwa wale wasioamini.”
وَإِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً قَالُوا وَجَدْنَا عَلَيْهَا آبَاءَنَا وَاللَّـهُ أَمَرَنَا بِهَا ۗ قُلْ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَأْمُرُ بِالْفَحْشَاءِ ۖ أَتَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢٨﴾
28. Na wanapofanya jambo chafu husema: “Tumewakuta katika hali hii baba zetu, na Allaah Ametuamrisha kwayo.” Sema: “Hakika Allaah Haamrishi machafu. Je mnasema juu ya Allaah msiyoyajua?”
قُلْ أَمَرَ رَبِّي بِالْقِسْطِ ۖ وَأَقِيمُوا وُجُوهَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ ۚ كَمَا بَدَأَكُمْ تَعُودُونَ ﴿٢٩﴾
29. Sema: “Rabb wangu Ameniamrisha uadilifu; na muelekeze nyuso zenu kwenye kila mahali pa kusujudu na mumuombe Yeye, muwe wenye kumtakasia Yeye Dini. Kama Alivyokuanzisheni mtarudi (tena Kwake).”
فَرِيقًا هَدَىٰ وَفَرِيقًا حَقَّ عَلَيْهِمُ الضَّلَالَةُ ۗ إِنَّهُمُ اتَّخَذُوا الشَّيَاطِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٣٠﴾
30. Kundi Ameliongoa, na kundi (jingine) limethibitikiwa na upotofu. Hakika wao wamefanya mashaytwaan kuwa marafiki wandani badala ya Allaah na wanadhani kwamba wao wamehidika.
يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚإِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿٣١﴾
31. Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu katika kila Masjid; na kuleni na kunyweni; na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu.[2]
قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللَّـهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ ۚ قُلْ هِيَ لِلَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا خَالِصَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٣٢﴾
32. Sema: “Nani aliyeharamisha mapambo ya Allaah ambayo Amewatolea waja Wake na vilivyo vizuri katika riziki?” Sema: “Hivyo ni kwa ajili ya wale walioamini katika uhai wa dunia; makhsusi (kwa Waumini) Siku ya Qiyaamah. Hivyo ndivyo Tunavyofasili waziwazi Aayaat kwa watu wanaojua.”
قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٣٣﴾
33. Sema: “Hakika Rabb wangu Ameharamisha machafu yaliyodhihirika na yaliyofichika na dhambi na ukandamizaji bila ya haki, na kumshirikisha Allaah kwa ambayo Hakukiteremshia mamlaka na kusema juu ya Allaah yale ambayo hamyajui.”[3]
وَلِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ ۖ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ لَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ﴿٣٤﴾
34. Na kwa kila ummah una muda uliokadiriwa. Basi utakapofika muda wao huo, hawatataakhari wala hawatatangulia saa.
يَا بَنِي آدَمَ إِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِي ۙ فَمَنِ اتَّقَىٰ وَأَصْلَحَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٣٥﴾
35. Enyi wana wa Aadam! Watakapokufikieni Rusuli miongoni mwenu wakakusimulieni Aayaat Zangu; basi atakayekuwa na taqwa na akatengenea, haitokuwa khofu juu yao na wala hawatohuzunika.
وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٣٦﴾
36. Na wale waliokadhibisha Aayaat Zetu na wakazifanyia kiburi, hao ni watu wa motoni, wao humo ni wenye kudumu.
فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ ۚ أُولَـٰئِكَ يَنَالُهُمْ نَصِيبُهُم مِّنَ الْكِتَابِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَاءَتْهُمْ رُسُلُنَا يَتَوَفَّوْنَهُمْ قَالُوا أَيْنَ مَا كُنتُمْ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ قَالُوا ضَلُّوا عَنَّا وَشَهِدُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَنَّهُمْ كَانُوا كَافِرِينَ ﴿٣٧﴾
37. Basi nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyemtungia Allaah uongo au aliyekadhibisha Aayaat Zake. Hao itawafikia sehemu yao ya Kitabu (waliyohukumiwa); mpaka watakapowajia Wajumbe Wetu kuwafisha watawaambia: “Wako wapi wale mliokuwa mkiwaomba pasi na Allaah?” Watasema: “Wametupotea.” Na watajishuhudia nafsi zao wenyewe kwamba walikuwa makafiri.
قَالَ ادْخُلُوا فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِكُم مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ فِي النَّارِ ۖكُلَّمَا دَخَلَتْ أُمَّةٌ لَّعَنَتْ أُخْتَهَا ۖ حَتَّىٰ إِذَا ادَّارَكُوا فِيهَا جَمِيعًا قَالَتْ أُخْرَاهُمْ لِأُولَاهُمْ رَبَّنَا هَـٰؤُلَاءِ أَضَلُّونَا فَآتِهِمْ عَذَابًا ضِعْفًا مِّنَ النَّارِ ۖ قَالَ لِكُلٍّ ضِعْفٌ وَلَـٰكِن لَّا تَعْلَمُونَ ﴿٣٨﴾
38. (Allaah) Atasema: “Ingieni motoni pamoja na ummah zilizokwishapita kabla yenu miongoni mwa majini na wana Aadam. Kila utakapoingia ummah utalaani nduguye. Mpaka watakapokusanyika mrundo humo wote pamoja; watasema wa mwisho wao (waliofuata wakuu) kwa wa mwanzo wao (wakuu wao): “Rabb wetu! Hawa wametupoteza; basi Wape adhabu maradufu ya moto.” (Allaah) Atasema: “Kila mmoja atapata (adhabu ya) maradufu lakini hamjui.”
وَقَالَتْ أُولَاهُمْ لِأُخْرَاهُمْ فَمَا كَانَ لَكُمْ عَلَيْنَا مِن فَضْلٍ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْسِبُونَ ﴿٣٩﴾
39. Na wa kwanza wao watawaambia wa mwisho wao: “Basi hamkuwa na fadhila juu yetu. Hivyo onjeni adhabu kwa yale mliyokuwa mkiyachuma.”
إِنَّ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا لَا تُفَتَّحُ لَهُمْ أَبْوَابُ السَّمَاءِ وَلَا يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ حَتَّىٰ يَلِجَ الْجَمَلُ فِي سَمِّ الْخِيَاطِ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُجْرِمِينَ ﴿٤٠﴾
40. Hakika wale waliokadhibisha Aayaat Zetu na wakazifanyia kiburi, hawatofunguliwa milango ya mbingu na wala hawatoingia Jannah mpaka ngamia aingie katika tundu ya sindano. Na hivyo ndivyo Tunavyowalipa wakhalifu.[4]
لَهُم مِّن جَهَنَّمَ مِهَادٌ وَمِن فَوْقِهِمْ غَوَاشٍ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ﴿٤١﴾
41. Jahannam itakuwa ni kitanda chao na juu yao vifuniko (vya moto) na hivyo ndivyo Tunavyowalipa madhalimu.
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿٤٢﴾
42. Na wale walioamini na wakatenda mema, Hatuikalifishi nafsi ila kadiri ya uwezo wake. Hao ni watu wa Jannah, wao humo ni wenye kudumu.
وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ ۖ وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي هَدَانَا لِهَـٰذَا وَمَا كُنَّا لِنَهْتَدِيَ لَوْلَا أَنْ هَدَانَا اللَّـهُ ۖ لَقَدْ جَاءَتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِالْحَقِّ ۖ وَنُودُوا أَن تِلْكُمُ الْجَنَّةُ أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٤٣﴾
43. Na Tutaondosha mafundo ya kinyongo yaliyomo vifuani mwao, zitapita chini yao mito. Na watasema: “AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah), Ambaye Ametuongoza kwa haya; na hatukuwa wenye kuhidika kama Allaah Asingetuongoza. Kwa yakini wamekuja Rusuli wa Rabb wetu kwa haki.” Na wataitwa (kuambiwa): “Hii ndiyo Jannah mliyorithishwa kwa yale mliyokuwa mnayatenda.”[5]
وَنَادَىٰ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ أَصْحَابَ النَّارِ أَن قَدْ وَجَدْنَا مَا وَعَدَنَا رَبُّنَا حَقًّا فَهَلْ وَجَدتُّم مَّا وَعَدَ رَبُّكُمْ حَقًّا ۖ قَالُوا نَعَمْۚ فَأَذَّنَ مُؤَذِّنٌ بَيْنَهُمْ أَن لَّعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الظَّالِمِينَ ﴿٤٤﴾
44. Na watu wa Jannah watawaita watu wa motoni kwamba: “Kwa yakini tumekwishayapata Aliyotuahidi Rabb wetu kuwa ni haki. Je, basi nyinyi mmekwishapata Aliyokuahidini Rabb wenu kuwa ni haki?” Watasema: “Naam!” Basi mtangazaji atatangaza baina yao kwamba: “Laana ya Allaah iwe juu ya madhalimu.”
الَّذِينَ يَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا وَهُم بِالْآخِرَةِ كَافِرُونَ ﴿٤٥﴾
45. Ambao wanazuia njia ya Allaah na wanaitafutia ionekane kombo, na wao kwa Aakhirah ni wenye kuikanusha.
وَبَيْنَهُمَا حِجَابٌ ۚ وَعَلَى الْأَعْرَافِ رِجَالٌ يَعْرِفُونَ كُلًّا بِسِيمَاهُمْ ۚ وَنَادَوْا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ أَن سَلَامٌ عَلَيْكُمْ ۚ لَمْ يَدْخُلُوهَا وَهُمْ يَطْمَعُونَ ﴿٤٦﴾
46. Na baina yao ni kizuizi. Na kwenye Al-A’raaf (ukuta wa mwinuko) patakuweko watu wanaowatambua wote kwa alama zao. Na watawaita watu wa Jannah: “Salaamun ‘Alaykum!” Hawakuingia humo lakini huku wao wanatumaini.[6]
وَإِذَا صُرِفَتْ أَبْصَارُهُمْ تِلْقَاءَ أَصْحَابِ النَّارِ قَالُوا رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٤٧﴾
47. Na yatakapogeuzwa macho yao kuelekea watu wa motoni watasema: “Rabb wetu! Usitujaalie kuwa pamoja na watu madhalimu.”
وَنَادَىٰ أَصْحَابُ الْأَعْرَافِ رِجَالًا يَعْرِفُونَهُم بِسِيمَاهُمْ قَالُوا مَا أَغْنَىٰ عَنكُمْ جَمْعُكُمْ وَمَا كُنتُمْ تَسْتَكْبِرُونَ﴿٤٨﴾
48. Na watu wa Al-A’raaf watawaita watu (wa motoni) wanaowatambua kwa alama zao, watasema: “Hakukufaeni kujumuika kwenu (duniani) na vile mlivyokuwa mkitakabari.”
أَهَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمْتُمْ لَا يَنَالُهُمُ اللَّـهُ بِرَحْمَةٍ ۚ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمْ وَلَا أَنتُمْ تَحْزَنُونَ ﴿٤٩﴾
49. “Je, hawa si wale ambao mliapa kwamba Allaah hatowafikishia kwa rahmah yoyote ile?” (Leo wanaambiwa) “Ingieni Jannah! Hakuna khofu juu yenu na wala nyinyi hamtohuzunika.”
وَنَادَىٰ أَصْحَابُ النَّارِ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ أَنْ أَفِيضُوا عَلَيْنَا مِنَ الْمَاءِ أَوْ مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ ۚ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ حَرَّمَهُمَا عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٥٠﴾
50. Na watu wa motoni watawaita watu wa Jannah: “Tumiminieni maji au katika ambavyo Amekuruzukuni Allaah.” Watasema: “Hakika Allaah Ameviharamisha kwa makafiri.”
الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَهُمْ لَهْوًا وَلَعِبًا وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا ۚ فَالْيَوْمَ نَنسَاهُمْ كَمَا نَسُوا لِقَاءَ يَوْمِهِمْ هَـٰذَا وَمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَجْحَدُونَ ﴿٥١﴾
51. Wale ambao wameifanya dini yao pumbao na mchezo, na ukawaghuri uhai wa dunia. Basi leo Tunawasahau kama walivyosahau kukutana na Siku yao hii; na kwa yale waliyokuwa wakizikanusha kwa jeuri Aayaat (ishara, dalili) Zetu.
وَلَقَدْ جِئْنَاهُم بِكِتَابٍ فَصَّلْنَاهُ عَلَىٰ عِلْمٍ هُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴿٥٢﴾
52. Kwa yakini Tumewaletea Kitabu Tulichokifasili waziwazi kwa ujuzi; ni mwongozo na rahmah kwa watu wanaoamini.
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا تَأْوِيلَهُ ۚ يَوْمَ يَأْتِي تَأْوِيلُهُ يَقُولُ الَّذِينَ نَسُوهُ مِن قَبْلُ قَدْ جَاءَتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِالْحَقِّ فَهَل لَّنَا مِن شُفَعَاءَ فَيَشْفَعُوا لَنَا أَوْ نُرَدُّ فَنَعْمَلَ غَيْرَ الَّذِي كُنَّا نَعْمَلُ ۚ قَدْ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ﴿٥٣﴾
53. Je, wanangojea nini isipokuwa matokeo yake? Siku (ya Qiyaamah) itakapofika matokeo yake watasema wale walioisahau kabla: “Kwa yakini wamekuja Rusuli wa Rabb wetu kwa haki. Je, tuna waombezi wowote watuombee, au turudishwe (duniani) ili tufanye ghairi ya yale tuliyokuwa tunafanya.” Kwa yakini wamekhasiri nafsi zao na imewapotea yale waliyokuwa wakiyatunga.
إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ ۗ أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ۗ تَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٥٤﴾
54. Hakika Rabb wenu ni Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Akawa juu (Istawaa[7]) ya ‘Arsh Anafunika usiku kwa mchana, unaufuatia upesi upesi na (Ameumba) jua na mwezi na nyota (vyote) vimetiishwa kwa amri Yake. Tanabahi! Uumbaji ni Wake Pekee na kupitisha amri. Amebarikika Allaah Rabb wa walimwengu.[8]
ادْعُوا رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿٥٥﴾
55. Muombeni Rabb wenu kwa unyenyekevu na kwa siri, hakika Yeye Hapendi wenye kupindukia mipaka.[9]
وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا وَادْعُوهُ خَوْفًا وَطَمَعًا ۚ إِنَّ رَحْمَتَ اللَّـهِ قَرِيبٌ مِّنَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٥٦﴾
56. Na wala msifanye ufisadi katika ardhi baada ya kutengenea kwake; na muombeni kwa khofu na matumaini. Hakika rahmah ya Allaah iko karibu na wafanyao ihsaan.
وَهُوَ الَّذِي يُرْسِلُ الرِّيَاحَ بُشْرًا بَيْنَ يَدَيْ رَحْمَتِهِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا أَقَلَّتْ سَحَابًا ثِقَالًا سُقْنَاهُ لِبَلَدٍ مَّيِّتٍ فَأَنزَلْنَا بِهِ الْمَاءَ فَأَخْرَجْنَا بِهِ مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ ۚ كَذَٰلِكَ نُخْرِجُ الْمَوْتَىٰ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ ﴿٥٧﴾
57. Naye Ndiye Anayetuma upepo mzuri kuwa bishara kabla ya rahmah Yake; hata unapobeba mawingu mazito Tunayasukuma kwenye nchi iliyokufa. Kisha Tunateremsha kwayo maji na kisha Tunatoa kwayo kila (aina ya) mazao. Hivyo ndivyo Tunavyotoa wafu, ili mpate kukumbuka (au kuwaidhika).
وَالْبَلَدُ الطَّيِّبُ يَخْرُجُ نَبَاتُهُ بِإِذْنِ رَبِّهِ ۖوَالَّذِي خَبُثَ لَا يَخْرُجُ إِلَّا نَكِدًا ۚ كَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَشْكُرُونَ ﴿٥٨﴾
58. Na nchi nzuri hutoa mimea yake kwa idhini ya Rabb wake. Na ile ambayo ni mbaya haitoi ila kwa uadimu. Hivyo ndivyo Tunavyosarifu namna kwa namna Aayaat kwa watu wanaoshukuru.[10]
لَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَقَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿٥٩﴾
59. Kwa yakini Tulimpeleka Nuwh kwa kaumu yake akasema: “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Hakika mimi nakukhofieni adhabu Siku kubwa mno.”
قَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِهِ إِنَّا لَنَرَاكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٦٠﴾
60. Wakasema wakuu katika kaumu yake: “Hakika sisi tunakuona umo katika upotofu bayana.”
قَالَ يَا قَوْمِ لَيْسَ بِي ضَلَالَةٌ وَلَـٰكِنِّي رَسُولٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٦١﴾
61. (Nuwh) Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mimi siko katika upotofu lakini mimi ni Rasuli kutoka kwa Rabb wa walimwengu.”
أُبَلِّغُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَأَنصَحُ لَكُمْ وَأَعْلَمُ مِنَ اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٦٢﴾
62. “Nakubalighishieni risala ya Rabb wangu na nakunasihini, na ninajua kutoka kwa Allaah msiyoyajua.”
أَوَعَجِبْتُمْ أَن جَاءَكُمْ ذِكْرٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنكُمْ لِيُنذِرَكُمْ وَلِتَتَّقُوا وَلَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٦٣﴾
63. “Je, mmestaajabu kwamba imekujieni ukumbusho kutoka kwa Rabb wenu kupitia kwa mtu miongoni mwenu ili akuonyeni na ili muwe na taqwa na mpate kurehemewa?”
فَكَذَّبُوهُ فَأَنجَيْنَاهُ وَالَّذِينَ مَعَهُ فِي الْفُلْكِ وَأَغْرَقْنَا الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۚإِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا عَمِينَ ﴿٦٤﴾
64. Basi walimkadhibisha na Tukamuokoa pamoja na wale waliokuwa naye katika jahazi; na Tukawagharikisha wale waliokadhibisha Aayaat (ishara, dalili) Zetu. Hakika wao walikuwa watu vipofu.
وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمْ هُودًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۚأَفَلَا تَتَّقُونَ ﴿٦٥﴾
65. Na kwa ‘Aad (Tuliwapelekea) kaka yao Huwd. Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Je, basi hamtokuwa na taqwa?”
قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ إِنَّا لَنَرَاكَ فِي سَفَاهَةٍ وَإِنَّا لَنَظُنُّكَ مِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٦٦﴾
66. Wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake: “Hakika sisi tunakuona umo katika upumbavu, na hakiki sisi tunakudhania ni miongoni mwa waongo.”
قَالَ يَا قَوْمِ لَيْسَ بِي سَفَاهَةٌ وَلَـٰكِنِّي رَسُولٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٦٧﴾
67. (Huwd) Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mimi siko katika upumbavu lakini mimi ni Rasuli kutoka kwa Rabb wa walimwengu.”
أُبَلِّغُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَأَنَا لَكُمْ نَاصِحٌ أَمِينٌ ﴿٦٨﴾
68. “Nakubalighishieni risala ya Rabb wangu, nami kwenu ni mtoaji nasiha mwaminifu.”
أَوَعَجِبْتُمْ أَن جَاءَكُمْ ذِكْرٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنكُمْ لِيُنذِرَكُمْ ۚ وَاذْكُرُوا إِذْ جَعَلَكُمْ خُلَفَاءَ مِن بَعْدِ قَوْمِ نُوحٍ وَزَادَكُمْ فِي الْخَلْقِ بَسْطَةً ۖ فَاذْكُرُوا آلَاءَ اللَّـهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٦٩﴾
69. “Je, mmestaajabu kwamba imekujieni ukumbusho kutoka kwa Rabb wenu kupitia kwa mtu miongoni mwenu ili akuonyeni. Na kumbukeni Alipokufanyeni warithi baada ya kaumu ya Nuwh, na Akakuzidisheni kwa ukunjufu katika umbo. Basi kumbukeni neema nyingi za Allaah mpate kufaulu.”
قَالُوا أَجِئْتَنَا لِنَعْبُدَ اللَّـهَ وَحْدَهُ وَنَذَرَ مَا كَانَ يَعْبُدُ آبَاؤُنَا ۖ فَأْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٧٠﴾
70. Wakasema: “Je, umetujia ili tumwambudu Allaah Pekee na tuache yale waliyokuwa wakiabudu baba zetu? Basi tuletee hayo unayotutishia ukiwa ni miongoni mwa wakweli.”
قَالَ قَدْ وَقَعَ عَلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ رِجْسٌ وَغَضَبٌ ۖ أَتُجَادِلُونَنِي فِي أَسْمَاءٍ سَمَّيْتُمُوهَا أَنتُمْ وَآبَاؤُكُم مَّا نَزَّلَ اللَّـهُ بِهَا مِن سُلْطَانٍ ۚ فَانتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُنتَظِرِينَ ﴿٧١﴾
71. (Huwd) Akasema: “Kwa yakini imekwishakuangukieni adhabu na ghadhabu kutoka kwa Rabb wenu. Je, mnabishana nami kuhusu majina (ya masanamu) mliyoyaita nyinyi na baba zenu bila ya Allaah kuyateremshia kwayo mamlaka? Basi ngojeeni, hakika mimi niko pamoja nanyi katika wanaongojea.”
فَأَنجَيْنَاهُ وَالَّذِينَ مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَقَطَعْنَا دَابِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۖ وَمَا كَانُوا مُؤْمِنِينَ ﴿٧٢﴾
72. Basi Tukamuokoa (Huwd) na wale waliokuwa pamoja naye kwa rahmah kutoka Kwetu na Tukakata mizizi ya wale waliokadhibisha Aayaat (ishara, dalili) Zetu na hawakuwa wenye kuamini.
وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ قَدْ جَاءَتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ ۖهَـٰذِهِ نَاقَةُ اللَّـهِ لَكُمْ آيَةً ۖ فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ اللَّـهِ ۖ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٣﴾
73. Na kwa Thamuwd (Tuliwapelekea) kaka yao Swaalih. Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Kwa yakini imekujieni hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu. Huyu ngamia jike wa Allaah ni Aayah (ishara, dalili) kwenu. Basi muacheni ale katika ardhi ya Allaah, na wala msimguse kwa uovu isije ikakuchukueni adhabu iumizayo.”
وَاذْكُرُوا إِذْ جَعَلَكُمْ خُلَفَاءَ مِن بَعْدِ عَادٍ وَبَوَّأَكُمْ فِي الْأَرْضِ تَتَّخِذُونَ مِن سُهُولِهَا قُصُورًا وَتَنْحِتُونَ الْجِبَالَ بُيُوتًا ۖ فَاذْكُرُوا آلَاءَ اللَّـهِ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴿٧٤﴾
74. “Na kumbukeni Alipokujaalieni warithi baada ya ‘Aad, Akakufanyieni makazi katika ardhi mnachukua katika nyanda zake tambarare majumba ya fakhari na mnachonga majumba kutokana na majabali. Basi kumbukeni neema nyingi za Allaah na wala msifanye vitendo vya hujuma katika ardhi mkifisidi.”
قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا مِن قَوْمِهِ لِلَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا لِمَنْ آمَنَ مِنْهُمْ أَتَعْلَمُونَ أَنَّ صَالِحًا مُّرْسَلٌ مِّن رَّبِّهِ ۚقَالُوا إِنَّا بِمَا أُرْسِلَ بِهِ مُؤْمِنُونَ ﴿٧٥﴾
75. Wakasema wakuu waliotakabari katika kaumu yake kuwaambia wale waliokandamizwa ambao walioamini miongoni mwao: “Je, mnajua kwamba Swaalih ametumwa kutoka kwa Rabb wake? Wakasema: “Hakika sisi kwa yale aliyotumwa nayo ni wenye kuyaamini.”
قَالَ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا بِالَّذِي آمَنتُم بِهِ كَافِرُونَ ﴿٧٦﴾
76. Wakasema wale waliotakabari: “Hakika sisi kwa yale mliyoyaamini tunayakanusha.”
فَعَقَرُوا النَّاقَةَ وَعَتَوْا عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ وَقَالُوا يَا صَالِحُ ائْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٧٧﴾
77. Wakamuua yule ngamia jike na wakaasi amri ya Rabb wao; na wakasema: “Ee Swaalih, tuletee hayo unayotutishia ukiwa ni miongoni mwa Rusuli.”
فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ ﴿٧٨﴾
78. Basi ikawachukua tetemeko la ardhi wakawa majumbani mwao wenye kuanguka kifudifudi (wamekufa).
فَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَا قَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَالَةَ رَبِّي وَنَصَحْتُ لَكُمْ وَلَـٰكِن لَّا تُحِبُّونَ النَّاصِحِينَ ﴿٧٩﴾
79. (Swaalih) akajitenga nao na akasema: “Enyi kaumu yangu! Kwa yakini nilishakubalighishieni risala ya Rabb wangu na nilikunasihini, lakini nyinyi hamuwapendi wenye kunasihi.”