@Furqanbot
وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنْ أَحَدٍ مِّنَ الْعَالَمِينَ﴿٨٠﴾
80. Na (Tulimtuma) Luwtw, alipowaambia kaumu yake: “Je, mnafanya uchafu (wa liwati) ambao hajakutangulieni nao yeyote katika walimwengu?”
إِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الرِّجَالَ شَهْوَةً مِّن دُونِ النِّسَاءِ ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ مُّسْرِفُونَ ﴿٨١﴾
81. “Hakika nyinyi mnawaingilia wanaume kwa matamanio badala ya wanawake? Bali nyinyi ni watu wapindukiaji mipaka.”
وَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلَّا أَن قَالُوا أَخْرِجُوهُم مِّن قَرْيَتِكُمْ ۖ إِنَّهُمْ أُنَاسٌ يَتَطَهَّرُونَ ﴿٨٢﴾
82. Na halikuwa jibu la kaumu yake isipokuwa walisema: “Wafukuzeni kutoka mji wenu, kwani hakika wao ni watu wanaojitakasa.”
فَأَنجَيْنَاهُ وَأَهْلَهُ إِلَّا امْرَأَتَهُ كَانَتْ مِنَ الْغَابِرِينَ ﴿٨٣﴾
83. Basi Tukamuokoa (Luwtw) na ahli yake isipokuwa mkewe alikuwa miongoni mwa waliokuwa nyuma.
وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًا ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُجْرِمِينَ ﴿٨٤﴾
84. Na Tukawateremshia mvua (ya mawe); mvua ya aina yake. Basi tazama vipi ilikuwa khatima ya wakhalifu.
وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ قَدْ جَاءَتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ ۖفَأَوْفُوا الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٨٥﴾
85. Na kwa (watu wa) Madyan (Tuliwapelekea) kaka yao Shu’ayb. Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Kwa yakini imekujieni hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu. Basi timizeni kipimo na mizani wala msipunje watu vitu vyao wala msifanye ufisadi ardhini baada ya kutengenea kwake. Hivyo ni bora kwenu ikiwa mmeamini.”
وَلَا تَقْعُدُوا بِكُلِّ صِرَاطٍ تُوعِدُونَ وَتَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ مَنْ آمَنَ بِهِ وَتَبْغُونَهَا عِوَجًا ۚ وَاذْكُرُوا إِذْ كُنتُمْ قَلِيلًا فَكَثَّرَكُمْ ۖ وَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُفْسِدِينَ ﴿٨٦﴾
86. “Na wala msikalie kila njia mkifanya vitisho na kuzuia njia ya Allaah wale wenye kumuamini na mnaitafutia ionekane kombo. Na kumbukeni mlipokuwa wachache Akakukithirisheni. Na tazameni vipi ilikuwa khatima ya mafisadi.”
وَإِن كَانَ طَائِفَةٌ مِّنكُمْ آمَنُوا بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ وَطَائِفَةٌ لَّمْ يُؤْمِنُوا فَاصْبِرُوا حَتَّىٰ يَحْكُمَ اللَّـهُ بَيْنَنَا ۚوَهُوَ خَيْرُ الْحَاكِمِينَ ﴿٨٧﴾
87. “Na kama liko kundi miongoni mwenu limeamini kwa yale niliyotumwa nayo na kundi halikuamini; basi subirini mpaka Allaah Ahukumu baina yetu. Naye ni Mbora wa wenye kuhukumu.”
قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا مِن قَوْمِهِ لَنُخْرِجَنَّكَ يَا شُعَيْبُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَكَ مِن قَرْيَتِنَا أَوْ لَتَعُودُنَّ فِي مِلَّتِنَاۚ قَالَ أَوَلَوْ كُنَّا كَارِهِينَ ﴿٨٨﴾
88. Wakasema wakuu waliotakabari katika kaumu yake: “Tutakutoa ewe Shua’yb na wale walioamini pamoja nawe kutoka mji wetu, au mrejee katika millah yetu.” (Shu’ayb) Akasema: “Japokuwa tumekirihika?”
قَدِ افْتَرَيْنَا عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا إِنْ عُدْنَا فِي مِلَّتِكُم بَعْدَ إِذْ نَجَّانَا اللَّـهُ مِنْهَا ۚوَمَا يَكُونُ لَنَا أَن نَّعُودَ فِيهَا إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّنَا ۚ وَسِعَ رَبُّنَا كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا ۚ عَلَى اللَّـهِ تَوَكَّلْنَا ۚ رَبَّنَا افْتَحْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ قَوْمِنَا بِالْحَقِّ وَأَنتَ خَيْرُ الْفَاتِحِينَ ﴿٨٩﴾
89. “Kwa yakini itakuwa tumemtungia Allaah uongo ikiwa tutarudi katika millah yenu baada ya Allaah kutuokoa nayo. Na haiwi kwetu kurejea humo isipokuwa Akitaka Allaah Rabb wetu. Rabb wetu Amekienea kila kitu kwa ujuzi. Kwa Allaah tunatawakali. Rabbwetu! Hukumu baina yetu na baina ya kaumu yetu kwa haki, Nawe ni Mbora wa wenye kuhukumu.”
وَقَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ لَئِنِ اتَّبَعْتُمْ شُعَيْبًا إِنَّكُمْ إِذًا لَّخَاسِرُونَ﴿٩٠﴾
90. Na wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake: “Mkimfuata Shu’ayb hakika hapo mtakuwa bila shaka wenye kukhasirika.”
فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ ﴿٩١﴾
91. Basi ikawachukua tetemeko la ardhi wakawa majumbani mwao wenye kuanguka kifudifudi (wamekufa).
الَّذِينَ كَذَّبُوا شُعَيْبًا كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۚ الَّذِينَ كَذَّبُوا شُعَيْبًا كَانُوا هُمُ الْخَاسِرِينَ ﴿٩٢﴾
92. Wale waliomkadhibisha Shu’ayb wakawa kama kwamba hawakuishi wakineemeka humo. Waliomkadhibisha Shu’ayb wakawa ndio wenye kukhasirika.
فَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَا قَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَنَصَحْتُ لَكُمْ ۖفَكَيْفَ آسَىٰ عَلَىٰ قَوْمٍ كَافِرِينَ ﴿٩٣﴾
93. Basi (Shu’ayb) akajitenga nao akasema: “Enyi kaumu yangu! Kwa yakini nimeshakubalighishieni risala ya Rabb wangu na nimekunasihini, basi vipi niwe na majonzi juu ya watu makafiri.”
وَمَا أَرْسَلْنَا فِي قَرْيَةٍ مِّن نَّبِيٍّ إِلَّا أَخَذْنَا أَهْلَهَا بِالْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ لَعَلَّهُمْ يَضَّرَّعُونَ ﴿٩٤﴾
94. Na Hatukutuma katika mji Nabiy yeyote (akakanushwa) isipokuwa Tunawashika watu wake, kwa dhiki za ufukara, na maafa ya magonjwa na njaa, huenda wapate kunyenyekea (kwa Allaah).
ثُمَّ بَدَّلْنَا مَكَانَ السَّيِّئَةِ الْحَسَنَةَ حَتَّىٰ عَفَوا وَّقَالُوا قَدْ مَسَّ آبَاءَنَا الضَّرَّاءُ وَالسَّرَّاءُ فَأَخَذْنَاهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٩٥﴾
95. Kisha Tukabadilisha mahali pa hali mbaya kwa nzuri hata wakazidi na wakaneemeka; wakasema: “Kwa yakini iliwagusa baba zetu madhara na raha.” Basi Tukawachukuwa ghafla nao huku hawahisi.
وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَىٰ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِم بَرَكَاتٍ مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ وَلَـٰكِن كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُم بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿٩٦﴾
96. Na lau kama watu wa miji wangeliamimi na wakawa na taqwa, bila ya shaka Tungeliwafungulia baraka kutoka mbinguni na ardhini, lakini walikadhibisha, basi Tukawachukua kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.
أَفَأَمِنَ أَهْلُ الْقُرَىٰ أَن يَأْتِيَهُم بَأْسُنَا بَيَاتًا وَهُمْ نَائِمُونَ ﴿٩٧﴾
97. Je, watu wa miji wameaminisha ya kuwa haitowafikia adhabu Yetu wakati wa usiku hali wao wamelala?
أَوَأَمِنَ أَهْلُ الْقُرَىٰ أَن يَأْتِيَهُم بَأْسُنَا ضُحًى وَهُمْ يَلْعَبُونَ ﴿٩٨﴾
98. Au watu wa miji wameaminisha ya kuwa haitowafikia adhabu Yetu wakati wa kabla ya mchana hali wao wanacheza?
أَفَأَمِنُوا مَكْرَ اللَّـهِ ۚ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٩٩﴾
99. Je, wameaminisha mipango ya (adhabu za) Allaah? Basi hawaaminishi mipango ya Allaah isipokuwa watu wenye kukhasirika.
أَوَلَمْ يَهْدِ لِلَّذِينَ يَرِثُونَ الْأَرْضَ مِن بَعْدِ أَهْلِهَا أَن لَّوْ نَشَاءُ أَصَبْنَاهُم بِذُنُوبِهِمْ ۚ وَنَطْبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ ﴿١٠٠﴾
100. Je, haikubainika kwa wale wanaorithi ardhi baada ya watu wake (wa walioangamizwa) kwamba lau Tungelitaka Tungeliwasibu kwa dhambi zao. Na Tutapiga chapa juu ya nyoyo zao basi hawatosikia?
تِلْكَ الْقُرَىٰ نَقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنبَائِهَا ۚوَلَقَدْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا بِمَا كَذَّبُوا مِن قَبْلُ ۚكَذَٰلِكَ يَطْبَعُ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِ الْكَافِرِينَ ﴿١٠١﴾
101. Hiyo ni miji Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) baadhi ya khabari zake. Na kwa yakini waliwajia Rusuli wao kwa hoja bayana, lakini hawakuwa wenye kuamini kwa yale waliyoyakadhibisha kabla. Hivyo ndivyo Allaah Anavyopiga chapa juu ya nyoyo za makafiri.
وَمَا وَجَدْنَا لِأَكْثَرِهِم مِّنْ عَهْدٍ ۖ وَإِن وَجَدْنَا أَكْثَرَهُمْ لَفَاسِقِينَ ﴿١٠٢﴾
102. Na Hatukuwakuta wengi wao kuwa ni (wakweli) wa ahadi. Bali kwa yakini Tumewakuta wengi wao ni mafasiki.
ثُمَّ بَعَثْنَا مِن بَعْدِهِم مُّوسَىٰ بِآيَاتِنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَظَلَمُوا بِهَا ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُفْسِدِينَ ﴿١٠٣﴾
103. Kisha Tukamtuma baada yao Muwsaa na Aayaat (ishara, dalili) Zetu kwa Fir’awn na wakuu wake wakazifanyia dhulma. Basi tazama vipi ilikuwa khatima ya mafisadi.
وَقَالَ مُوسَىٰ يَا فِرْعَوْنُ إِنِّي رَسُولٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٠٤﴾
104. Na Muwsaa akasema: “Ee Fir’awn! Hakika mimi ni Rasuli kutoka kwa Rabb wa walimwengu.”
حَقِيقٌ عَلَىٰ أَن لَّا أَقُولَ عَلَى اللَّـهِ إِلَّا الْحَقَّ ۚ قَدْ جِئْتُكُم بِبَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ فَأَرْسِلْ مَعِيَ بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿١٠٥﴾
105. “Napaswa nisiseme juu ya Allaah isipokuwa ya haki. Kwa yakini nimekujieni kwa hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu; basi watume pamoja nami wana wa Israaiyl.”
قَالَ إِن كُنتَ جِئْتَ بِآيَةٍ فَأْتِ بِهَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿١٠٦﴾
106. (Fir’awn) Akasema: “Ikiwa umekuja na Aayah (ishara, hoja) basi ilete, ukiwa ni miongoni mwa wakweli.”
فَأَلْقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعْبَانٌ مُّبِينٌ﴿١٠٧﴾
107. Basi (Muwsaa) akaitupa fimbo yake, na mara tahamaki hiyo ni joka bayana.
وَنَزَعَ يَدَهُ فَإِذَا هِيَ بَيْضَاءُ لِلنَّاظِرِينَ﴿١٠٨﴾
108. Na akatoa mkono wake; basi mara tahamaki huo ni mweupe (unang’ara) kwa watazamao.
قَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِ فِرْعَوْنَ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ عَلِيمٌ ﴿١٠٩﴾
109. Wakasema wakuu katika kaumu ya Fir’awn: “Bila shaka huyu ni mchawi mjuzi.”
يُرِيدُ أَن يُخْرِجَكُم مِّنْ أَرْضِكُمْ ۖ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ ﴿١١٠﴾
110. “Anataka kukutoeni kutoka ardhini mwenu; basi mnaamrisha nini?”
قَالُوا أَرْجِهْ وَأَخَاهُ وَأَرْسِلْ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ ﴿١١١﴾
111. Wakasema: “Muahirishe kidogo na kaka yake na tuma katika miji wenye kukusanya.”
يَأْتُوكَ بِكُلِّ سَاحِرٍ عَلِيمٍ ﴿١١٢﴾
112. “Wakujie kila mchawi mjuzi.”
وَجَاءَ السَّحَرَةُ فِرْعَوْنَ قَالُوا إِنَّ لَنَا لَأَجْرًا إِن كُنَّا نَحْنُ الْغَالِبِينَ ﴿١١٣﴾
113. Wakaja wachawi wa Fir’awn; wakasema: “Je, tutapata ujira ikiwa sisi tutashinda?”
قَالَ نَعَمْ وَإِنَّكُمْ لَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ ﴿١١٤﴾
114. (Fir’awn) Akasema: “Naam! Bila shaka nanyi mtakuwa miongoni mwa waliokurubishwa (kwangu).”
قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِمَّا أَن تُلْقِيَ وَإِمَّا أَن نَّكُونَ نَحْنُ الْمُلْقِينَ ﴿١١٥﴾
115. (Wachawi) Wakasema: “Ee Muwsaa, ima utupe wewe au tuwe sisi wa (kwanza) kutupa.”
قَالَ أَلْقُوا ۖ فَلَمَّا أَلْقَوْا سَحَرُوا أَعْيُنَ النَّاسِ وَاسْتَرْهَبُوهُمْ وَجَاءُوا بِسِحْرٍ عَظِيمٍ ﴿١١٦﴾
116. (Muwsaa) Akasema: “Tupeni!” Basi walipotupa, waliyasihiri macho ya watu na wakawatia woga, na wakaja na sihiri kuu.
وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنْ أَلْقِ عَصَاكَ ۖفَإِذَا هِيَ تَلْقَفُ مَا يَأْفِكُونَ ﴿١١٧﴾
117. Na Tukamtia ilhamu Muwsaa ya kwamba: “Tupa fimbo yako!” Basi mara tahamaki ikameza vyote walivyovibuni.
فَوَقَعَ الْحَقُّ وَبَطَلَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١١٨﴾
118. Ukweli ukathibiti na yakabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.
فَغُلِبُوا هُنَالِكَ وَانقَلَبُوا صَاغِرِينَ﴿١١٩﴾
119. Wakashindwa hapo; na wakageuka kuwa wenye kudhalilika.
وَأُلْقِيَ السَّحَرَةُ سَاجِدِينَ ﴿١٢٠﴾
120. Na wachawi wakajiangusha wakisujdu.
قَالُوا آمَنَّا بِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٢١﴾
121. Wakasema: “Tumemwamini Rabbwa walimwengu.”
رَبِّ مُوسَىٰ وَهَارُونَ ﴿١٢٢﴾
122. “Rabb wa Muwsaa na Haaruwn.”
قَالَ فِرْعَوْنُ آمَنتُم بِهِ قَبْلَ أَنْ آذَنَ لَكُمْ ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَمَكْرٌ مَّكَرْتُمُوهُ فِي الْمَدِينَةِ لِتُخْرِجُوا مِنْهَا أَهْلَهَا ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿١٢٣﴾
123. Fir’awn akasema: “Je, mumemwamini kabla sijakupeni rukhsa? Hakika hii bila shaka ni makri mliyoipanga (na Muwsaa) katika mji ili muwatoe watu wake humo. Mtakuja kujua!”
لَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَافٍ ثُمَّ لَأُصَلِّبَنَّكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿١٢٤﴾
124. “Bila shaka niitakatakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutofautisha kisha nitakusulubuni nyote.”[11]
قَالُوا إِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ ﴿١٢٥﴾
125. (Wachawi) Wakasema: “Hakika sisi kwa Rabb wetu tutarudi.”
وَمَا تَنقِمُ مِنَّا إِلَّا أَنْ آمَنَّا بِآيَاتِ رَبِّنَا لَمَّا جَاءَتْنَا ۚ رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَتَوَفَّنَا مُسْلِمِينَ ﴿١٢٦﴾
126. “Na huchukizwi nasi isipokuwa tu kwa kuwa tumeamini Aayaat (dalili, hoja) za Rabb wetu zilipotujia. Ee Rabb wetu! Tumiminie subira na Tufishe tukiwa Waislamu.”
وَقَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِ فِرْعَوْنَ أَتَذَرُ مُوسَىٰ وَقَوْمَهُ لِيُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَيَذَرَكَ وَآلِهَتَكَ ۚ قَالَ سَنُقَتِّلُ أَبْنَاءَهُمْ وَنَسْتَحْيِي نِسَاءَهُمْ وَإِنَّا فَوْقَهُمْ قَاهِرُونَ ﴿١٢٧﴾
127. Na wakasema wakuu katika kaumu ya Fir’awn: “Je, unamwacha Muwsaa na kaumu yake wafisidi katika ardhi; na akuache wewe na waabudiwa wako?” (Fir’awn) Akasema: “Tutawaua watoto wao wa kiume na tutaacha hai wanawake wao; na hakika sisi ni wenye kushinda nguvu juu yao.”
قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ اسْتَعِينُوا بِاللَّـهِ وَاصْبِرُوا ۖ إِنَّ الْأَرْضَ لِلَّـهِ يُورِثُهَا مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۖ وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ﴿١٢٨﴾
128. Muwsaa akawaambia kaumu yake: “Ombeni msaada kwa Allaah na subirini. Hakika ardhi ni ya Allaah; Humrithisha Amtakaye katika waja Wake. Na mwisho (mzuri) ni kwa wenye taqwa.”
قَالُوا أُوذِينَا مِن قَبْلِ أَن تَأْتِيَنَا وَمِن بَعْدِ مَا جِئْتَنَا ۚ قَالَ عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُهْلِكَ عَدُوَّكُمْ وَيَسْتَخْلِفَكُمْ فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ ﴿١٢٩﴾
129. Wakasema: “Tumeudhiwa kabla ya kutujia na baada ya kutujia.” (Muwsaa) akasema: “Asaa Rabb wenu Akamuangamiza adui yenu na Akufanyeni watawala katika ardhi, Atazame mtakavyotenda.”
وَلَقَدْ أَخَذْنَا آلَ فِرْعَوْنَ بِالسِّنِينَ وَنَقْصٍ مِّنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ﴿١٣٠﴾
130. Na kwa yakini Tuliwateka watu wa Fir’awn kwa ukame na upungufu wa mazao ili wapate kukumbuka.
فَإِذَا جَاءَتْهُمُ الْحَسَنَةُ قَالُوا لَنَا هَـٰذِهِ ۖوَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ يَطَّيَّرُوا بِمُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُ ۗ أَلَا إِنَّمَا طَائِرُهُمْ عِندَ اللَّـهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٣١﴾
131. Basi ilipowajia zuri husema: “Hili letu.” Na likiwasibu ovu hunasibisha nuksi kwa Muwsaa na walio pamoja naye. Tanabahi! Hakika nuksi yao iko kwa Allaah lakini wengi wao hawajui.
وَقَالُوا مَهْمَا تَأْتِنَا بِهِ مِنْ آيَةٍ لِّتَسْحَرَنَا بِهَا فَمَا نَحْنُ لَكَ بِمُؤْمِنِينَ ﴿١٣٢﴾
132. Na wakasema: “Chochote utachotuletea kwacho katika Aayah (dalili, hoja) ili utusihiri nacho; basi sisi hatutokuamini.”
فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ الطُّوفَانَ وَالْجَرَادَ وَالْقُمَّلَ وَالضَّفَادِعَ وَالدَّمَ آيَاتٍ مُّفَصَّلَاتٍ فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْمًا مُّجْرِمِينَ ﴿١٣٣﴾
133. Basi Tuliwapelekea tufani na nzige na chawa na vyura na damu Aayaat (ishara, hoja) zilizofasiliwa waziwazi lakini walitakabari wakawa watu makhalifu.
وَلَمَّا وَقَعَ عَلَيْهِمُ الرِّجْزُ قَالُوا يَا مُوسَى ادْعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَ ۖلَئِن كَشَفْتَ عَنَّا الرِّجْزَ لَنُؤْمِنَنَّ لَكَ وَلَنُرْسِلَنَّ مَعَكَ بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿١٣٤﴾
134. Na ilipowaangukia adhabu ya kufadhaika walisema: “Ee Muwsaa! Tuombee kwa Rabb wako kwa yale Aliyokuahidi. Ukituondolea adhabu, bila shaka tutakuamini na bila shaka tutawatuma wana Israaiyl (waje) pamoja nawe.”
فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُمُ الرِّجْزَ إِلَىٰ أَجَلٍ هُم بَالِغُوهُ إِذَا هُمْ يَنكُثُونَ ﴿١٣٥﴾
135. Tulipowaondolea adhabu mpaka muda maalumu wao waufikie; tahamaki wao wanavunja ahadi.
فَانتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَأَغْرَقْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ بِأَنَّهُمْ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا عَنْهَا غَافِلِينَ ﴿١٣٦﴾
136. Basi Tukawalipiza, Tukawagharikisha baharini kwa kuwa wao walikadhibisha Aayaat (ishara, hoja) Zetu na walikuwa ni wenye kughafilika nazo.
وَأَوْرَثْنَا الْقَوْمَ الَّذِينَ كَانُوا يُسْتَضْعَفُونَ مَشَارِقَ الْأَرْضِ وَمَغَارِبَهَا الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا ۖ وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ الْحُسْنَىٰ عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ بِمَا صَبَرُوا ۖ وَدَمَّرْنَا مَا كَانَ يَصْنَعُ فِرْعَوْنُ وَقَوْمُهُ وَمَا كَانُوا يَعْرِشُونَ ﴿١٣٧﴾
137. Na Tukawarithisha watu waliokuwa wakikandamizwa Mashariki ya ardhi na Magharibi yake ambayo Tumeibariki. Na likatimia neno zuri la Rabb wako kwa wana wa Israaiyl kwa kule kusubiri kwao. Na Tukayadamirisha yale waliyokuwa wakitenda Fir’awn na kaumu yake na yale waliyokuwa wakiyajenga.
وَجَاوَزْنَا بِبَنِي إِسْرَائِيلَ الْبَحْرَ فَأَتَوْا عَلَىٰ قَوْمٍ يَعْكُفُونَ عَلَىٰ أَصْنَامٍ لَّهُمْ ۚقَالُوا يَا مُوسَى اجْعَل لَّنَا إِلَـٰهًا كَمَا لَهُمْ آلِهَةٌ ۚ قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ تَجْهَلُونَ﴿١٣٨﴾
138. Na Tukawavusha wana wa Israaiyl bahari wakawafikia watu waliokuwa wanasabilia kwa utiifu masanamu yao. Wakasema: “Ee Muwsaa! Tufanyie nasi mwabudiwa kama walivyokuwa hao wana waabudiwa.” (Muwsaa) Akasema: “Hakika nyinyi ni watu mfanyao ujinga.”
إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ مُتَبَّرٌ مَّا هُمْ فِيهِ وَبَاطِلٌ مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٣٩﴾
139. “Hakika hawa yatateketezwa waliyo nayo, na ni yenye kubatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.”
قَالَ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْغِيكُمْ إِلَـٰهًا وَهُوَ فَضَّلَكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿١٤٠﴾
140. (Muwsaa) Akasema: “Je, nikutafutieni mwabudiwa ghairi ya Allaah, na hali Yeye Amekufadhilisheni juu ya walimwengu?”
وَإِذْ أَنجَيْنَاكُم مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ ۖ يُقَتِّلُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ ۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَاءٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ ﴿١٤١﴾
141. Na Tulipokuokoeni kutoka kwa watu wa Fir’awn walipokusibuni adhabu mbaya wakiwaua watoto wenu wa kiume na wakiacha hai wanawake wenu, na katika hayo kwenu ulikuwa ni mtihani mkuu kutoka kwa Rabb wenu.
وَوَاعَدْنَا مُوسَىٰ ثَلَاثِينَ لَيْلَةً وَأَتْمَمْنَاهَا بِعَشْرٍ فَتَمَّ مِيقَاتُ رَبِّهِ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً ۚ وَقَالَ مُوسَىٰ لِأَخِيهِ هَارُونَ اخْلُفْنِي فِي قَوْمِي وَأَصْلِحْ وَلَا تَتَّبِعْ سَبِيلَ الْمُفْسِدِينَ ﴿١٤٢﴾
142. Na Tukamuahidi Muwsaa misiku thelathini na Tukazitimiza kwa kumi; na ukatimia muda wa miadi wa Rabb wake siku arubaini. Muwsaa akamwambia kaka yake Haaruwn: “Kuwa kaimu wangu kwa watu wangu na tengeneza, na wala usifuate njia ya mafisadi.”
وَلَمَّا جَاءَ مُوسَىٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ قَالَ رَبِّ أَرِنِي أَنظُرْ إِلَيْكَ ۚ قَالَ لَن تَرَانِي وَلَـٰكِنِ انظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي ۚ فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقًا ۚ فَلَمَّا أَفَاقَ قَالَ سُبْحَانَكَ تُبْتُ إِلَيْكَ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٤٣﴾
143. Na alipokuja Muwsaa katika muda na pahala pa miadi Yetu, na Rabb wake Akamsemesha, akasema “Rabb wangu! Nionyeshe ili nikutazame.” (Allaah) Akasema: “Hutoniona! Lakini tazama mlima. Ukitulia mahali pake, basi utaniona.” Basi Rabb wake Alipojidhihirisha katika mlima, Akaufanya uvurugike kuwa vumbi; na Muwsaa akaanguka hali ya kuzimia. Alipozindukana akasema: “Utakasifu ni Wako Nimetubu Kwako, nami ni wa kwanza wa wanaoamini.”
قَالَ يَا مُوسَىٰ إِنِّي اصْطَفَيْتُكَ عَلَى النَّاسِ بِرِسَالَاتِي وَبِكَلَامِي فَخُذْ مَا آتَيْتُكَ وَكُن مِّنَ الشَّاكِرِينَ ﴿١٤٤﴾
144. (Allaah) Akasema: “Ee Muwsaa hakika Mimi Nimekukhitari juu ya watu kwa risala Yangu na maneno Yangu. Basi pokea Niliyokupa na kuwa miongoni mwa wanaoshukuru.”
وَكَتَبْنَا لَهُ فِي الْأَلْوَاحِ مِن كُلِّ شَيْءٍ مَّوْعِظَةً وَتَفْصِيلًا لِّكُلِّ شَيْءٍ فَخُذْهَا بِقُوَّةٍ وَأْمُرْ قَوْمَكَ يَأْخُذُوا بِأَحْسَنِهَا ۚسَأُرِيكُمْ دَارَ الْفَاسِقِينَ ﴿١٤٥﴾
145. Na Tukamwandikia kwenye mbao kila kitu; mawaidha na tafsili ya kila kitu. (Tukamwambia): “Basi yashikilie kwa nguvu na uwaamrishe watu wako wayashike mazuri yake. Nitakuonyesheni miji ya mafasiki.”
سَأَصْرِفُ عَنْ آيَاتِيَ الَّذِينَ يَتَكَبَّرُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَإِن يَرَوْا كُلَّ آيَةٍ لَّا يُؤْمِنُوا بِهَا وَإِن يَرَوْا سَبِيلَ الرُّشْدِ لَا يَتَّخِذُوهُ سَبِيلًا وَإِن يَرَوْا سَبِيلَ الْغَيِّ يَتَّخِذُوهُ سَبِيلًا ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا عَنْهَا غَافِلِينَ ﴿١٤٦﴾
146. Nitawaepusha na Aayaat (ishara, dalili) Zangu wale waliotakabari katika ardhi bila ya haki. Na wanapoona kila Aayah hawaiamini. Na wanapoona njia ya uongofu hawaishiki kuwa ndio njia. Na wanapoona njia ya upotofu wanaishika kuwa ndio njia. Hivyo ni kwa kuwa wao walikadhibisha Aayaat Zetu na walikuwa wenye kughafilika nazo.
وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَلِقَاءِ الْآخِرَةِ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ ۚ هَلْ يُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٤٧﴾
147. Na wale waliokadhibisha Aayaat Zetu na makutano ya Aakhirah, zimeporomoka ‘amali zao. Je, kwani watalipwa isipokuwa yale waliyokuwa wakiyatenda?
وَاتَّخَذَ قَوْمُ مُوسَىٰ مِن بَعْدِهِ مِنْ حُلِيِّهِمْ عِجْلًا جَسَدًا لَّهُ خُوَارٌ ۚ أَلَمْ يَرَوْا أَنَّهُ لَا يُكَلِّمُهُمْ وَلَا يَهْدِيهِمْ سَبِيلًاۘ اتَّخَذُوهُ وَكَانُوا ظَالِمِينَ ﴿١٤٨﴾
148. Na watu wa Muwsaa walijifanyia, baada kuondoka kwake, katika mapambo yao, umbo la ndama - lilikuwa na sauti kama ya ng’ombe. Je, hawakuona kwamba huyo (ndama) hawasemeshi na wala hawaongozi njia? Walimfanya (mwabudiwa) na wakawa madhalimu.
وَلَمَّا سُقِطَ فِي أَيْدِيهِمْ وَرَأَوْا أَنَّهُمْ قَدْ ضَلُّوا قَالُوا لَئِن لَّمْ يَرْحَمْنَا رَبُّنَا وَيَغْفِرْ لَنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿١٤٩﴾
149. Na walipojuta na wakaona kwamba kwa yakini wamepotoka; walisema: “Asipoturehemu Rabb wetu na Akatughufuria, bila shaka tutakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”