006 - Al-An'aam

006 - Al-An'aam

       

 الأنْعَام

Al-An’aam: 6[1]

 

Imteremshwa Makkah

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

 

الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَجَعَلَ الظُّلُمَاتِ وَالنُّورَ ۖ ثُمَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ ﴿١﴾

1. AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah), Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na Akajaalia viza na nuru; kisha wale ambao wamekufuru wanawasawazisha wengine na Rabb wao.

 

 

 

هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن طِينٍ ثُمَّ قَضَىٰ أَجَلًا ۖ وَأَجَلٌ مُّسَمًّى عِندَهُ ۖ ثُمَّ أَنتُمْ تَمْتَرُونَ ﴿٢﴾

2. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na udongo kisha Akahukumu muda maalumu, na uko Kwake muda maalumu uliokadiriwa, kisha nyinyi mnatilia shaka.

 

 

 

وَهُوَ اللَّـهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَفِي الْأَرْضِۖ يَعْلَمُ سِرَّكُمْ وَجَهْرَكُمْ وَيَعْلَمُ مَا تَكْسِبُونَ ﴿٣﴾

3. Na Yeye ni Allaah mbinguni na ardhini; Anajua ya siri yenu na ya dhahiri yenu; na Anajua yale mnayoyachuma.[2]

 

 

 

وَمَا تَأْتِيهِم مِّنْ آيَةٍ مِّنْ آيَاتِ رَبِّهِمْ إِلَّا كَانُوا عَنْهَا مُعْرِضِينَ ﴿٤﴾

4. Na haiwafikii Aayah yoyote ile katika Aayaat za Rabb wao isipokuwa huwa ni wenye kuipuuza.

 

 

فَقَدْ كَذَّبُوا بِالْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ ۖفَسَوْفَ يَأْتِيهِمْ أَنبَاءُ مَا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٥﴾

5. Kwa yakini wameikadhibisha haki ilipowajia; basi zitawafikia khabari muhimu za yale waliyokuwa kwayo wakiyafanyia istihzai.

 

 

 

أَلَمْ يَرَوْا كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّن قَرْنٍ مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ مَا لَمْ نُمَكِّن لَّكُمْ وَأَرْسَلْنَا السَّمَاءَ عَلَيْهِم مِّدْرَارًا وَجَعَلْنَا الْأَنْهَارَ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمْ فَأَهْلَكْنَاهُم بِذُنُوبِهِمْ وَأَنشَأْنَا مِن بَعْدِهِمْ قَرْنًا آخَرِينَ ﴿٦﴾

6. Je, hawaoni ni karne ngapi Tumeziangamiza kabla yao? Tuliwamakinisha katika ardhi yale ambayo Hatujapata kuwamakinisha nyinyi; na Tukawapelekea mvua tele iendeleayo; na Tukajaalia mito ipitayo chini yao. Tukawaangamiza kwa dhambi zao na Tukaanzisha baada yao karne nyingine.

 

 

 

وَلَوْ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ كِتَابًا فِي قِرْطَاسٍ فَلَمَسُوهُ بِأَيْدِيهِمْ لَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿٧﴾

7. Na lau Tungelikuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu katika karatasi, kisha wakakigusa kwa mikono yao; bila shaka wale waliokufuru wangelisema: “Hii si chochote isipokuwa ni sihiri bayana.”

 

 

 

وَقَالُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ مَلَكٌ ۖ وَلَوْ أَنزَلْنَا مَلَكًا لَّقُضِيَ الْأَمْرُ ثُمَّ لَا يُنظَرُونَ ﴿٨﴾

8. Na wakasema: “Mbona hakuteremshiwa Malaika?” Na lau Tungeliteremsha Malaika; basi ingelihukumiwa amri kisha wasingelipewa muhula.

 

 

 

وَلَوْ جَعَلْنَاهُ مَلَكًا لَّجَعَلْنَاهُ رَجُلًا وَلَلَبَسْنَا عَلَيْهِم مَّا يَلْبِسُونَ ﴿٩﴾

9. Na lau Tungelimfanya Malaika, bila shaka Tungelimfanya mtu na Tungeliwatatanishia yale wanayojitatanisha.

 

 

 

وَلَقَدِ اسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِّن قَبْلِكَ فَحَاقَ بِالَّذِينَ سَخِرُوا مِنْهُم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿١٠﴾

10. Na kwa yakini walifanyiwa istihzai Rusuli kabla yako, lakini wale waliofanya kejeli, yaliwazunguka yale yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.

 

 

 

قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ ثُمَّ انظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ ﴿١١﴾

11. Sema: “Nendeni katika ardhi, kisha mtazame vipi ilikuwa hatima ya wenye kukadhibisha.”

 

 

 

قُل لِّمَن مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖقُل لِّلَّـهِ ۚ كَتَبَ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ۚلَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۚ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٢﴾

12. Sema: “Ni vya nani vilivyomo mbinguni na ardhini?” Sema: “Ni vya Allaah. Ameandika juu ya Nafsi Yake rahmah. Bila shaka Atakukusanyeni Siku ya Qiyaamah; hapana shaka yoyote ndani yake.” Wale ambao wamekhasiri nafsi zao basi wao hawaamini.

 

 

 

وَلَهُ مَا سَكَنَ فِي اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٣﴾

13. Na ni Vyake vyote vinavyotulia katika usiku na mchana. Naye ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

قُلْ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَتَّخِذُ وَلِيًّا فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ يُطْعِمُ وَلَا يُطْعَمُ ۗ قُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ أَوَّلَ مَنْ أَسْلَمَ ۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١٤﴾

14. Sema: “Je, nimfanye mlinzi asiyekuwa Allaah; Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Naye Ndiye Anayelisha na wala halishwi?” Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu.” Na wala usijekuwa kabisa miongoni mwa washirikina.

 

 

 

قُلْ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٥﴾

15. Sema: “Hakika mimi nakhofu, ikiwa nitamuasi Rabb wangu, adhabu ya Siku adhimu.”

 

 

 

مَّن يُصْرَفْ عَنْهُ يَوْمَئِذٍ فَقَدْ رَحِمَهُ ۚوَذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْمُبِينُ ﴿١٦﴾

16. Atakayeepushwa nayo (adhabu) Siku hiyo; basi kwa yakini (Allaah) Amemrehemu. Na huko ndiko kufuzu bayana.

 

 

 

وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يَمْسَسْكَ بِخَيْرٍ فَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٧﴾

17. Na Allaah Akikugusisha kwa dhara, basi hakuna yeyote wa kukuondolea hiyo isipokuwa Yeye; na Akikugusisha khayr, basi Yeye juu ya kila kitu ni Muweza.

 

 

 

وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ ﴿١٨﴾

18. Naye ni Mwenye kudhibiti juu ya waja Wake; Naye ni Mwenye hikmah wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.

 

 

 

قُلْ أَيُّ شَيْءٍ أَكْبَرُ شَهَادَةً ۖ قُلِ اللَّـهُ ۖشَهِيدٌ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۚ وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ ۚأَئِنَّكُمْ لَتَشْهَدُونَ أَنَّ مَعَ اللَّـهِ آلِهَةً أُخْرَىٰ ۚ قُل لَّا أَشْهَدُ ۚ قُلْ إِنَّمَا هُوَ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ وَإِنَّنِي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ﴿١٩﴾

19. Sema: “Kitu gani ushahidi wake ndio mkubwa zaidi?” Sema: “Allaah; ni Mwenye kushuhudia yote baina yangu na baina yenu. Na nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayomfikia. Je, hivi nyinyi hakika mnashuhudia kwamba wako waabudiwa wengine pamoja na Allaah?” Sema: “Mimi sishuhudii (hayo).” Sema: “Hakika Yeye ni Mwabudiwa wa haki Mmoja (Pekee), na kwamba hakika mimi sihusiki na mnavyomfanyia shirki.”

 

 

 

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمُ ۘ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٢٠﴾

20. Wale Tuliowapa Kitabu wanaitambua (Tawhiyd au Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kama wanavyotambua watoto wao. Wale ambao wamekhasiri nafsi zao basi wao hawaamini.

 

 

 

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ ۗ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ ﴿٢١﴾

21. Na nani mdhalimu zaidi kuliko yule anayemtungia Allaah uongo au anayekadhibisha Aayaat Zake? Hakika madhalimu hawatofaulu.

 

 

 

وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا أَيْنَ شُرَكَاؤُكُمُ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٢٢﴾

22. Na Siku Tutakayowakusanya wote pamoja, kisha Tutawaambia wale walioshirikisha: “Wako wapi washirika wenu ambao mlikuwa mnadai (kuwashirikisha na Allaah)?”

 

 

 

ثُمَّ لَمْ تَكُن فِتْنَتُهُمْ إِلَّا أَن قَالُوا وَاللَّـهِ رَبِّنَا مَا كُنَّا مُشْرِكِينَ ﴿٢٣﴾

23. Kisha haitokuwa fitnah yao isipokuwa kusema: “Wa-Allaahi Rabb wetu, hatukuwa washirikina.”

 

 

 

انظُرْ كَيْفَ كَذَبُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ ۚوَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٢٤﴾

24. Tazama vipi wamesema uongo juu ya nafsi zao; na yamewapotea yale waliyokuwa wakiyatunga.

 

 

 

وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ ۖ وَجَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ وَقْرًا ۚ وَإِن يَرَوْا كُلَّ آيَةٍ لَّا يُؤْمِنُوا بِهَاۚ حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوكَ يُجَادِلُونَكَ يَقُولُ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ ﴿٢٥﴾

25. Na miongoni mwao, wanaotega sikio kukusikiliza. Na Tumejaalia juu ya nyoyo zao vifuniko wasiyafahamu; na katika masikio yao uziwi. Na wanapoona kila Aayah (ishara, dalili) hawaiamini; hata wanapokujia kukubishia husema wale waliokufuru: “Hizi si chochote ila ni hekaya za watu wa kale.” 

 

 

 

وَهُمْ يَنْهَوْنَ عَنْهُ وَيَنْأَوْنَ عَنْهُ ۖ وَإِن يُهْلِكُونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ﴿٢٦﴾

26. Nao wanazuia wengine (kufuata haki) naye; nao wenyewe wanajiweka mbali naye. Na (hivyo) hawaangamizi isipokuwa nafsi zao na wala hawahisi. 

 

 

 

وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ وُقِفُوا عَلَى النَّارِ فَقَالُوا يَا لَيْتَنَا نُرَدُّ وَلَا نُكَذِّبَ بِآيَاتِ رَبِّنَا وَنَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢٧﴾

27. Na lau ungeliona watakaposimamishwa kwenye moto; kisha wakasema: “Laiti tungelirudishwa (duniani) na wala hatutakadhibisha Aayaat za Rabb wetu, na tutakuwa miongoni mwa waumini.”

 

 

 

بَلْ بَدَا لَهُم مَّا كَانُوا يُخْفُونَ مِن قَبْلُ ۖوَلَوْ رُدُّوا لَعَادُوا لِمَا نُهُوا عَنْهُ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿٢٨﴾

28. Bali yamewadhihirikia yale waliyokuwa wakiyaficha kabla. Na lau wangelirudishwa; kwa yakini wangeyarudia yale waliyokatazwa; na hakika wao ni waongo.

 

 

 

وَقَالُوا إِنْ هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ ﴿٢٩﴾

29. Na walisema: “Haya si chochote isipokuwa ni uhai wetu wa dunia tu; na wala sisi hatutofufuliwa.”

 

 

 

وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ وُقِفُوا عَلَىٰ رَبِّهِمْ ۚ قَالَ أَلَيْسَ هَـٰذَا بِالْحَقِّ ۚ قَالُوا بَلَىٰ وَرَبِّنَا ۚقَالَ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ ﴿٣٠﴾

30. Na lau ungeliona watakaposimamishwa mbele ya Rabb wao. Atasema: Je, haya si ya kweli? Watasema: “Ndio, tunaapa kwa Rabb wetu.” Atasema: “Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkikufuru.”

 

 

 

قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِلِقَاءِ اللَّـهِ ۖحَتَّىٰ إِذَا جَاءَتْهُمُ السَّاعَةُ بَغْتَةً قَالُوا يَا حَسْرَتَنَا عَلَىٰ مَا فَرَّطْنَا فِيهَا وَهُمْ يَحْمِلُونَ أَوْزَارَهُمْ عَلَىٰ ظُهُورِهِمْ ۚ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ ﴿٣١﴾

31. Kwa yakini wamekhasirika wale waliokadhibisha kukutana na Allaah; hata itakapowajia Saa (mauti) kwa ghafla; watasema: “Ee majuto yetu kwa yale tuliyokusuru humo”, na ilhali wao wanabeba mizigo yao (ya dhambi) migongoni mwao. Tanabahi! Uovu ulioje wanayobeba!

 

 

 

وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَعِبٌ وَلَهْوٌ ۖوَلَلدَّارُ الْآخِرَةُ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ ۗأَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٣٢﴾

32. Na uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni mchezo na pumbao. Na bila shaka nyumba ya Aakhirah ni bora zaidi kwa wenye taqwa. Je, basi hamtii akilini?

 

 

 

قَدْ نَعْلَمُ إِنَّهُ لَيَحْزُنُكَ الَّذِي يَقُولُونَ ۖفَإِنَّهُمْ لَا يُكَذِّبُونَكَ وَلَـٰكِنَّ الظَّالِمِينَ بِآيَاتِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَ ﴿٣٣﴾

33. Kwa yakini Tunajua (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba yanakuhuzunisha yale wanayoyasema. Basi hakika wao hawakukadhibishi wewe lakini madhalimu wanakanusha Aayaat za Allaah.

 

 

 

وَلَقَدْ كُذِّبَتْ رُسُلٌ مِّن قَبْلِكَ فَصَبَرُوا عَلَىٰ مَا كُذِّبُوا وَأُوذُوا حَتَّىٰ أَتَاهُمْ نَصْرُنَا ۚ وَلَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِ اللَّـهِ ۚ وَلَقَدْ جَاءَكَ مِن نَّبَإِ الْمُرْسَلِينَ ﴿٣٤﴾

34. Na kwa yakini walikadhibishwa Rusuli kabla yako, wakasubiri juu ya yale waliyokadhibishwa; na wakaudhiwa hata ilipowafikia nusura Yetu. Na hakuna abadilishaye maneno ya Allaah. Zimekwishakujia khabari za Rusuli (waliopita).

 

 

 

وَإِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكَ إِعْرَاضُهُمْ فَإِنِ اسْتَطَعْتَ أَن تَبْتَغِيَ نَفَقًا فِي الْأَرْضِ أَوْ سُلَّمًا فِي السَّمَاءِ فَتَأْتِيَهُم بِآيَةٍ ۚوَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَجَمَعَهُمْ عَلَى الْهُدَىٰ ۚفَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْجَاهِلِينَ ﴿٣٥﴾

35. Na kama imekuwa kukengeuka kwao ni mashaka mno kwako, basi ukiweza kutafuta upenyo chini kwa chini katika ardhi au ngazi kwendea mbinguni ili uwaletee Aayah (basi fanya). Na kama Angetaka Allaah Angeliwakusanya katika uongofu. Basi usiwe miongoni mwa majahili.

 

 

 

إِنَّمَا يَسْتَجِيبُ الَّذِينَ يَسْمَعُونَ ۘوَالْمَوْتَىٰ يَبْعَثُهُمُ اللَّـهُ ثُمَّ إِلَيْهِ يُرْجَعُونَ ﴿٣٦﴾

36. Hakika wanaitikia wale wanaosikia (kwa nyoyo za iymaan). Ama wafu (wa nyoyo) Allaah Atawafufua, kisha Kwake watarejeshwa.

 

 

وَقَالُوا لَوْلَا نُزِّلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِّن رَّبِّهِ ۚقُلْ إِنَّ اللَّـهَ قَادِرٌ عَلَىٰ أَن يُنَزِّلَ آيَةً وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٣٧﴾

37. Na walisema: “Kwa nini hakuteremshiwa Aayah (muujiza, ishara) kutoka kwa Rabb wake?” Sema: “Hakika Allaah ni Muweza wa kuteremsha Aayah lakini wengi wao hawajui.” 

 

 

 

وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا طَائِرٍ يَطِيرُ بِجَنَاحَيْهِ إِلَّا أُمَمٌ أَمْثَالُكُم ۚ مَّا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِن شَيْءٍ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِمْ يُحْشَرُونَ ﴿٣٨﴾

38. Na hakuna kiumbe chochote kinachotembea katika ardhi na wala ndege anayeruka kwa mbawa zake mbili, isipokuwa ni umati mfano wenu. Hatukusuru katika Kitabu kitu chochote. Kisha kwa Rabb wao watakusanywa.

 

 

 

وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا صُمٌّ وَبُكْمٌ فِي الظُّلُمَاتِ ۗ مَن يَشَإِ اللَّـهُ يُضْلِلْـهُ وَمَن يَشَأْ يَجْعَلْهُ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٣٩﴾

39. Na wale waliokadhibisha Aayaat Zetu ni viziwi na mabubu katika viza. Allaah Humpotoa Amtakaye na Humweka Amtakaye juu ya njia iliyonyooka. 

 

 

 

قُلْ أَرَأَيْتَكُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُ اللَّـهِ أَوْ أَتَتْكُمُ السَّاعَةُ أَغَيْرَ اللَّـهِ تَدْعُونَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٤٠﴾

40. Sema: “Je, mnaonaje ikikufikieni adhabu ya Allaah au ikakufikieni Saa, je, mtamwomba ghairi ya Allaah? (Jibuni) mkiwa ni wakweli.”

 

 

 

بَلْ إِيَّاهُ تَدْعُونَ فَيَكْشِفُ مَا تَدْعُونَ إِلَيْهِ إِن شَاءَ وَتَنسَوْنَ مَا تُشْرِكُونَ﴿٤١﴾

41. Bali Yeye Pekee Ndiye mtayemwomba, kisha Akitaka Ataondoa yale (ya dhiki) mliyomwomba; na mtasahau mnayoyashirikisha (pamoja Naye).

 

 

 

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ أُمَمٍ مِّن قَبْلِكَ فَأَخَذْنَاهُم بِالْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ لَعَلَّهُمْ يَتَضَرَّعُونَ ﴿٤٢﴾

42. Na kwa yakini Tulipeleka (Rusuli) kwa ummah nyingi kabla yako; Tukawatia katika dhiki za ufukara na madhara ya magonjwa na misiba ili wapate kunyenyekea.

 

 

 

 فَلَوْلَا إِذْ جَاءَهُم بَأْسُنَا تَضَرَّعُوا وَلَـٰكِن قَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٤٣﴾

43. Basi kwa nini ilipowafikia adhabu Yetu wasinyenyekee? Lakini nyoyo zao zimekuwa ngumu na shaytwaan akawapambia yale waliyokuwa wakitenda.

 

 

 

فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ أَبْوَابَ كُلِّ شَيْءٍ حَتَّىٰ إِذَا فَرِحُوا بِمَا أُوتُوا أَخَذْنَاهُم بَغْتَةً فَإِذَا هُم مُّبْلِسُونَ ﴿٤٤﴾

44. Waliposahau yale waliyokumbushwa nayo; Tuliwafungulia milango ya (taanisi za) kila kitu, mpaka walipofurahia kwa yale waliyopewa; Tukawachukua ghafla (kawaadhibu), basi mara wao wakawa wenye kukata tamaa.

 

 

 

فَقُطِعَ دَابِرُ الْقَوْمِ الَّذِينَ ظَلَمُوا ۚوَالْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٤٥﴾

45. Basi ikakatwa mizizi ya watu waliodhulumu; na AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah); Rabb wa walimwengu.

 

 

 

قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَخَذَ اللَّـهُ سَمْعَكُمْ وَأَبْصَارَكُمْ وَخَتَمَ عَلَىٰ قُلُوبِكُم مَّنْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ يَأْتِيكُم بِهِ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ ثُمَّ هُمْ يَصْدِفُونَ﴿٤٦﴾

46. Sema: “Mnaonaje ikiwa Allaah Atakuondoleeni kusikia kwenu na kuona kwenu na Akapiga mhuri juu ya nyoyo zenu; je, ni mwabudiwa wa haki yupi ghairi ya Allaah Atakuleteeni hayo?” Tazama jinsi Tunavyosarifu namna kwa namna Aayaat kisha wao wanakengeuka.

 

 

 

قُلْ أَرَأَيْتَكُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُ اللَّـهِ بَغْتَةً أَوْ جَهْرَةً هَلْ يُهْلَكُ إِلَّا الْقَوْمُ الظَّالِمُونَ ﴿٤٧﴾

47. Sema: “Mnaonaje ikikufikieni adhabu ya Allaah ghafla au kwa dhahiri; Je, kwani huangamizwa isipokuwa watu madhalimu?”

 

 

 

وَمَا نُرْسِلُ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ ۖ فَمَنْ آمَنَ وَأَصْلَحَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٤٨﴾

48. Na Hatupeleki Rusuli isipokuwa ni wabashiriaji na waonyaji. Basi yeyote atakayeamini na kutengenea; haitokuwa khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika.

 

 

 

وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا يَمَسُّهُمُ الْعَذَابُ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿٤٩﴾

49. Na wale waliokadhibisha Aayaat Zetu itawagusa adhabu kwa yale waliyokuwa wakifanya ufasiki.

 

 

Endelea Kusoma Kwa Kugusa Hapa 👈



Report Page