003 - Aal-'Imraan

003 - Aal-'Imraan

 

آل عِمْران

Aal-‘Imraan: 3[1]

Imeteremka Madiynah Kwa Ijmaa’

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

الم ﴿١﴾

1. Alif Laam Miym.

 

 

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ﴿٢﴾

2. Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliye hai daima, Msimamia kila kitu.

 

 

 

 نَزَّلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَأَنزَلَ التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ﴿٣﴾

3. Amekuteremshia Kitabu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki kinachosadikisha yaliyo kabla yake na AkateremshaTawraat na Injiyl.

 

 

 

 

مِن قَبْلُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَأَنزَلَ الْفُرْقَانَ ۗإِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ﴿٤﴾

4. Kabla (ya kuteremshwa Qur-aan), iwe ni mwongozo kwa watu na Akateremsha Furqaan (upambanuo). Hakika wale waliokufuru Aayaat za Allaah watapata adhabu kali. Na Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kuangamiza.

 

 

 

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَخْفَىٰ عَلَيْهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ ﴿٥﴾

5. Hakika Allaah Hakifichiki Kwake chochote katika ardhi wala katika mbingu. 

 

 

 هُوَ الَّذِي يُصَوِّرُكُمْ فِي الْأَرْحَامِ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٦﴾

6. Yeye Ndiye Aliyekusawirini umbo katika matumbo ya uzazi vile Atakavyo. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.[2]

 

 

 

 

هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ ۖ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ ۗ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّـهُ ۗ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٧﴾

7. Yeye Ndiye Aliyeteremsha kwako Kitabu humo mna Aayaat zenye maana wazi, hizo ndio msingi wa Kitabu, na nyinginezo zisizokuwa wazi maana zake. Basi wale ambao katika nyoyo zao mna upotovu hufuata zile zisizokuwa wazi maana zake kutafuta fitnah (upotofu) na kutafuta maana zake zilofichika, na hakuna ajuae maana zake isipokuwa Allaah. Na wenye msingi madhubuti katika elimu husema: “Tumeziamini, zote ni kutoka kwa Rabb wetu.” Na hawakumbuki ila wenye akili.[3]

 

 

رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ ﴿٨﴾

8. (Husema): “Rabb wetu, Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kuwa Umetuhidi na Tutunukie kutoka kwako rahmah. Hakika Wewe ni Mwingi wa kutunuku na kuneemesha.”

 

 

رَبَّنَا إِنَّكَ جَامِعُ النَّاسِ لِيَوْمٍ لَّا رَيْبَ فِيهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُخْلِفُ الْمِيعَادَ ﴿٩﴾ 

9. “Rabb wetu! Hakika Wewe ni Mkusanyaji watu Siku isiyo na shakandani yake. Hakika Allaah Havunji miadi.”

 

 

 

 إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَن تُغْنِيَ عَنْهُمْ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُم مِّنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۖوَأُولَـٰئِكَ هُمْ وَقُودُ النَّارِ ﴿١٠﴾

10. Hakika wale waliokufuru hazitowafaa kitu mali zao na wala watoto wao mbele ya Allaah, na hao ndio kuni za moto.

 

 

كَدَأْبِ آلِ فِرْعَوْنَ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا فَأَخَذَهُمُ اللَّـهُ بِذُنُوبِهِمْ ۗوَاللَّـهُ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿١١﴾

11. Kama mwenendo wa watu wa Fir’awn na wale waliokuwa kabla yao. Wamekadhibisha Aayaat Zetu basi Allaah Aliwaadhibu kwa madhambi yao, na Allaah ni Mkali wa kuakibu.

 

 

قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا سَتُغْلَبُونَ وَتُحْشَرُونَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ ۚ وَبِئْسَ الْمِهَادُ﴿١٢﴾

12. Waambie waliokufuru: “Mtashindwa na mtakusanywa katika Jahannam, na ni pabaya mno mahala hapo pa kupumzika.”

 

 

 

 قَدْ كَانَ لَكُمْ آيَةٌ فِي فِئَتَيْنِ الْتَقَتَا ۖفِئَةٌ تُقَاتِلُ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَأُخْرَىٰ كَافِرَةٌ يَرَوْنَهُم مِّثْلَيْهِمْ رَأْيَ الْعَيْنِ ۚوَاللَّـهُ يُؤَيِّدُ بِنَصْرِهِ مَن يَشَاءُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّأُولِي الْأَبْصَارِ ﴿١٣﴾

13. Kwa hakika ilikuwa ni Aayah (ishara) kwenu katika makundi mawili; yalipokutana (vita vya Badr). Kundi linapigana katika njia ya Allaah na jingine ni makafiri ambao wanawaona (Waislamu) mara mbili yao kwa mtazamo wa macho. Na Allaah Humsaidia kwa nusura Yake Amtakaye. Hakika katika hayo bila shaka ni zingatio kwa wenye utambuzi.

 

 

زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ الشَّهَوَاتِ مِنَ النِّسَاءِ وَالْبَنِينَ وَالْقَنَاطِيرِ الْمُقَنطَرَةِ مِنَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ وَالْخَيْلِ الْمُسَوَّمَةِ وَالْأَنْعَامِ وَالْحَرْثِ ۗ ذَٰلِكَ مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الْمَآبِ﴿١٤﴾

14. Watu wamepambiwa huba ya matamanio miongoni mwa wanawake, na watoto, na mirundi ya mali iliyorundikwa ya dhahabu na fedha na farasi wenye chapa ya aina bora na wanyama wa mifugo na mashamba. Hayo ni starehe za uhai wa dunia, na Allaah Kwake kuna marejeo mazuri.

 

 

 قُلْ أَؤُنَبِّئُكُم بِخَيْرٍ مِّن ذَٰلِكُمْ ۚ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَأَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ وَرِضْوَانٌ مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ ﴿١٥﴾

15. Sema: “Je, nikujulisheni yaliyo bora kuliko hayo? Kwa wale waliokuwa na taqwa kwa Rabb wao watapata Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo na wake waliotakasika na radhi kutoka kwa Allaah. Na Allaah ni Mwenye kuwaona waja.”

 

 

الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا إِنَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ﴿١٦﴾ 

16. Wale wasemao: “Rabb wetu, hakika sisi tumeamini, basi Tughufurie madhambi yetu na Tukinge na adhabu ya moto.”

 

 

 الصَّابِرِينَ وَالصَّادِقِينَ وَالْقَانِتِينَ وَالْمُنفِقِينَ وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ﴿١٧﴾

17. Wenye kusubiri na wasemao kweli, na watiifu, na watoaji mali katika njia ya Allaah na waombao maghfirah kabla ya Alfajiri.

 

 

 

شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٨﴾

18. Allaah Ameshuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye; na (pia) Malaika na wenye elimu (kwamba Allaah) ni Mwenye kusimamisha (uumbaji Wake) kwa uadilifu. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

 

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ ۗ وَمَا اخْتَلَفَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۗوَمَن يَكْفُرْ بِآيَاتِ اللَّـهِ فَإِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿١٩﴾

19. Hakika Dini mbele ya Allaah ni Uislamu. Na hawakukhitilafiana wale waliopewa Kitabu ila baada ya kuwajia elimu kwa kufanyiana baghi na uhusuda baina yao. Na atakayekanusha Aayaat za Allaah basi hakika Allaah ni Mwepesi wa kuhesabu.

 

 

 فَإِنْ حَاجُّوكَ فَقُلْ أَسْلَمْتُ وَجْهِيَ لِلَّـهِ وَمَنِ اتَّبَعَنِ ۗ وَقُل لِّلَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْأُمِّيِّينَ أَأَسْلَمْتُمْ ۚ فَإِنْ أَسْلَمُوا فَقَدِ اهْتَدَوا ۖ وَّإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ﴿٢٠﴾

20. Na wakikuhoji, basi sema: “Nimejisalimisha kwa Allaah na ambao walionifuata” Na waambie waliopewa Kitabu na wasiojua kusoma na kuandika: “Je, mmesilimu?” Wakisilimu basi wameongoka, na wakikengeuka basi hakika juu yako ni kubalighisha. Na Allaah ni Mwenye kuwaona waja.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَيَقْتُلُونَ الَّذِينَ يَأْمُرُونَ بِالْقِسْطِ مِنَ النَّاسِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٢١﴾ 

21. Hakika waliokanusha Aayaat za Allaah na wakaua Manabii bila ya haki, na wakaua wale wanaoamrisha haki miongoni mwa watu, basi wabashirie adhabu iumizayo.

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ﴿٢٢﴾

22. Hao ni wale ambao zimeporomoka ‘amali zao katika dunia na Aakhirah na hawatopata yeyote mwenye kuwanusuru.

 

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُدْعَوْنَ إِلَىٰ كِتَابِ اللَّـهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ يَتَوَلَّىٰ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ وَهُم مُّعْرِضُونَ ﴿٢٣﴾ 

23. Je, hukuzingatia wale waliopewa sehemu katika Kitabu wanaitwa katika Kitabu cha Allaah ili kiwahukumu baina yao; kisha kundi miongoni mwao linageuka na huku wanapuuza.

 

 

 ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لَن تَمَسَّنَا النَّارُ إِلَّا أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ ۖ وَغَرَّهُمْ فِي دِينِهِم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٢٤﴾

24. Hivyo ni kwa sababu wamesema: “Hautotugusa moto isipokuwa siku chache za kuhesabika.” Na yakawadanganya katika dini yao yale waliyokuwa wakiyazua.

 

 

فَكَيْفَ إِذَا جَمَعْنَاهُمْ لِيَوْمٍ لَّا رَيْبَ فِيهِ وَوُفِّيَتْ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٢٥﴾

25. Basi itakuwa vipi Tutakapowakusanya katika Siku ambayo haina shaka ndani yake, na kila nafsi italipwa kikamilifu yale iliyochuma; nao hawatodhulumiwa.

 

 

قُلِ اللَّـهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَن تَشَاءُ وَتَنزِعُ الْمُلْكَ مِمَّن تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَاءُ ۖ بِيَدِكَ الْخَيْرُ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٢٦﴾

26. Sema: “Ee Allaah Mfalme Uliyemiliki ufalme wote, Unampa ufalme Umtakaye, na Unamuondoshea ufalme Umtakaye, na Unamtukuza Umtakaye, na Unamdhalilisha Umtakaye, khayr imo Mkononi Mwako. Hakika Wewe juu ya kila kitu ni Muweza.

 

 

 تُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَتُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ ۖ وَتُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَتُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ ۖ وَتَرْزُقُ مَن تَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٢٧﴾

27. Unauingiza usiku katika mchana na Unauingiza mchana katika usiku; na Unatoa kilicho hai kutokana na kilicho mfu na Unatoa kilicho mfu kutokana na kilicho hai na Unamruzuku Umtakaye bila ya hesabu.

 

 

لَّا يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَلَيْسَ مِنَ اللَّـهِ فِي شَيْءٍ إِلَّا أَن تَتَّقُوا مِنْهُمْ تُقَاةً ۗ وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ ۗ وَإِلَى اللَّـهِ الْمَصِيرُ ﴿٢٨﴾ 

28. Waumini hawawafanyi makafiri kuwa marafiki wandani badala ya Waumini. Na atakayefanya hivyo, basi hatokua na chochote mbele ya Allaah, isipokuwa mkiwa mnaogopa khatari kutoka kwao. Na Allaah Anakutahadharisheni na Nafsi yake. Na kwa Allaah ni mahali pa kuishia.

 

 

 قُلْ إِن تُخْفُوا مَا فِي صُدُورِكُمْ أَوْ تُبْدُوهُ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ ۗ وَيَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٩﴾

29. Sema: “Mkificha yale yaliyomo katika vifua vyenu au mkiyafichua, Allaah Anayajua. Na Anajua yale yaliyomo katika mbingu na yale yaliyomo katika ardhi. Na Allaah juu ya kila kitu ni Muweza.

 

 

يَوْمَ تَجِدُ كُلُّ نَفْسٍ مَّا عَمِلَتْ مِنْ خَيْرٍ مُّحْضَرًا وَمَا عَمِلَتْ مِن سُوءٍ تَوَدُّ لَوْ أَنَّ بَيْنَهَا وَبَيْنَهُ أَمَدًا بَعِيدًا ۗوَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ ۗ وَاللَّـهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ ﴿٣٠﴾

30. Siku itayokuta kila nafsi yale iliyoyatenda katika khayr yamehudhurishwa, na yale iliyoyatenda katika maovu, itatamani nafsi lau kama ingelikuwa baina yake na baina hayo (maovu) masafa ya mbali. Na Allaah Anakutahadharisheni na Nafsi yake. Na Allaah ni Raufu mno kwa waja.

 

 

 قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗوَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾

31. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.”[4]

 

 

قُلْ أَطِيعُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْكَافِرِينَ ﴿٣٢﴾

32. Sema: “Mtiini Allaah na Rasuli, lakini mkikengeuka basi hakika Allaah Hapendi makafiri.”

 

 

إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ آدَمَ وَنُوحًا وَآلَ إِبْرَاهِيمَ وَآلَ عِمْرَانَ عَلَى الْعَالَمِينَ﴿٣٣﴾

33. Hakika Allaah Amemkhitari Aadam na Nuwh na kizazi cha Ibraahiym na kizazi cha ‘Imraan juu ya walimwengu.

 

 

 ذُرِّيَّةً بَعْضُهَا مِن بَعْضٍ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٣٤﴾

34. Kizazi cha wao kwa wao na Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

 

إِذْ قَالَتِ امْرَأَتُ عِمْرَانَ رَبِّ إِنِّي نَذَرْتُ لَكَ مَا فِي بَطْنِي مُحَرَّرًا فَتَقَبَّلْ مِنِّي ۖ إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٣٥﴾ 

35. Pale aliposema mke wa ‘Imraan: “Rabb wangu, hakika mimi nimeweka nadhiri Kwako kilichomo katika tumbo langu kuwa ni wakfu kukutumikia, basi nitakabalie. Hakika wewe ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

 فَلَمَّا وَضَعَتْهَا قَالَتْ رَبِّ إِنِّي وَضَعْتُهَا أُنثَىٰ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا وَضَعَتْ وَلَيْسَ الذَّكَرُ كَالْأُنثَىٰ ۖ وَإِنِّي سَمَّيْتُهَا مَرْيَمَ وَإِنِّي أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ ﴿٣٦﴾

36. Basi alipomzaa akasema: “Rabb wangu, hakika mimi nimezaa mwanamke,” na Allaah Anajua zaidi alichokizaa. “Na mwanamme si kama mwanamke. Nami nimemwita Mayram nami namkinga Kwako na dhuria wake kutokana na shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa.

 

 

فَتَقَبَّلَهَا رَبُّهَا بِقَبُولٍ حَسَنٍ وَأَنبَتَهَا نَبَاتًا حَسَنًا وَكَفَّلَهَا زَكَرِيَّا ۖ كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيْهَا زَكَرِيَّا الْمِحْرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزْقًا ۖ قَالَ يَا مَرْيَمُ أَنَّىٰ لَكِ هَـٰذَا ۖقَالَتْ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ ۖ إِنَّ اللَّـهَ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٣٧﴾ 

37. Basi Rabb wake Akampokea kwa kabuli njema na Akamkuza mkuzo mzuri na Akamfanya Zakariyyaa kuwa mlezi wake. Kila Zakariyyaa alipoingia kwake katika chumba cha kuswalia alikuta kwake kuna riziki Akasema: “Ee Maryam! Umepata wapi hivi? ”Akasema: “Hivi ni kutoka kwa Allaah. Hakika Allaah Anamruzuku Amtakaye bila ya hesabu.”

 

 

 هُنَالِكَ دَعَا زَكَرِيَّا رَبَّهُ ۖ قَالَ رَبِّ هَبْ لِي مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً ۖ إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاءِ ﴿٣٨﴾

38. Hapo hapo Zakariyyaa akamwomba Rabb wake, akasema: “Rabb wangu Nitunukie kutoka Kwako kizazi chema hakika Wewe ni Mwenye kusikia du’aa yangu.”

 

فَنَادَتْهُ الْمَلَائِكَةُ وَهُوَ قَائِمٌ يُصَلِّي فِي الْمِحْرَابِ أَنَّ اللَّـهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحْيَىٰ مُصَدِّقًا بِكَلِمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَسَيِّدًا وَحَصُورًا وَنَبِيًّا مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٣٩﴾

39. Basi mara Malaika akamwita (Zakariyyaa) naye akiwa amesimama anaswali katika chumba kwamba: “Hakika Allaah Anakubashiria Yahyaa mwenye kusadikisha Neno (la Kun!) kutoka kwa Allaah na ni mwenye sharaf, busara na taqwa, na anayejitenga mbali na matamanio na Nabiy miongoni mwa Swalihina.”[5]

 

 

قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَقَدْ بَلَغَنِيَ الْكِبَرُ وَامْرَأَتِي عَاقِرٌ ۖ قَالَ كَذَٰلِكَ اللَّـهُ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ ﴿٤٠﴾

40. (Zakariyyaa) Akasema: “Nitapataje ghulamu na hali uzee umeshanifikia na mke wangu ni tasa?!” Akasema: “Hivyo ndivyo Allaah Anafanya Atakavyo”

 

 

قَالَ رَبِّ اجْعَل لِّي آيَةً ۖ قَالَ آيَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ النَّاسَ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ إِلَّا رَمْزًا ۗوَاذْكُر رَّبَّكَ كَثِيرًا وَسَبِّحْ بِالْعَشِيِّ وَالْإِبْكَارِ ﴿٤١﴾ 

41. (Zakariyyaa) Akasema: “Rabb wangu niwekee Aayah (ishara)” Akasema: Ishara yako ni kwamba hutoweza kuwasemesha watu siku tatu ila kwa kuashiria tu. Na mdhukuru Rabb wako kwa wingi na msabihi jioni na asubuhi.”

 

 

وَإِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَاكِ وَطَهَّرَكِ وَاصْطَفَاكِ عَلَىٰ نِسَاءِ الْعَالَمِينَ ﴿٤٢﴾

42. Na pale Malaika waliposema: “Ee Maryam! Hakika Allaah Amekuteua na Amekutakasa na Amekukhitari juu ya wanawake wa walimwengu.”

 

 

 يَا مَرْيَمُ اقْنُتِي لِرَبِّكِ وَاسْجُدِي وَارْكَعِي مَعَ الرَّاكِعِينَ ﴿٤٣﴾

43. “Ee Maryam! Kuwa mtiifu kwa Rabb wako, na sujudu, na rukuu pamoja na wanaorukuu.”

 

 

ذَٰلِكَ مِنْ أَنبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهِ إِلَيْكَ ۚوَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يُلْقُونَ أَقْلَامَهُمْ أَيُّهُمْ يَكْفُلُ مَرْيَمَ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يَخْتَصِمُونَ ﴿٤٤﴾ 

44. Hizo ni khabari za ghayb Tunakufunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).  Na hukuwa pamoja nao walipotupa kalamu zao, ili nani kati yao amlee Maryam. Na hukuwa pamoja nao walipokhasimiana.

 

 

 

 إِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللَّـهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٍ مِّنْهُ اسْمُهُ الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ وَجِيهًا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ ﴿٤٥﴾

45. Na pale Malaika waliposema: “Ee Maryam! Hakika Allaah Anakubashiria Neno (la Kun!) kutoka Kwake (umzae mtoto), jina lake ni Al-Masiyhu ‘Iysaa mwana wa Maryam, mwenye taadhima katika dunia na Aakhirah na ni miongoni mwa waliokurubishwa (kwa Allaah).

 

 

وَيُكَلِّمُ النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلًا وَمِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٤٦﴾

46. Na Atawasemesha watu katika utoto wake na utu uzima wake na ni miongoni mwa Swalihina.

 

 

قَالَتْ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي وَلَدٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ ۖ قَالَ كَذَٰلِكِ اللَّـهُ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ إِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٤٧﴾

47. (Maryam) Akasema: “Itakuwaje nipate mtoto na hali hakunigusa mtu?” (Malaika) Akasema: “Hivyo ndivyo Allaah Huumba Akitakacho. Anapokidhia jambo basi huliambia: "Kun!" (Kuwa!) Basi nalo huwa.

 

 

 وَيُعَلِّمُهُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَالتَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ﴿٤٨﴾

48. Na Atamfunza Kitabu na Hikmah na Tawraat na Injiyl.

 

 

 وَرَسُولًا إِلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنِّي قَدْ جِئْتُكُم بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ أَنِّي أَخْلُقُ لَكُم مِّنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ فَأَنفُخُ فِيهِ فَيَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۖ وَأُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ وَأُحْيِي الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۖ وَأُنَبِّئُكُم بِمَا تَأْكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِي بُيُوتِكُمْ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٤٩﴾

49. Na ni Rasuli kwa wana wa Israaiyl (akisema): “Hakika mimi nimekujieni na Aayah (ishara, dalili) kutoka kwa Rabb wenu, kwamba mimi nakuundieni kutokana na udongo kama umbo la ndege, kisha napuliza humo basi huwa ndege kwa idhini ya Allaah. Na naponyesha vipofu na wenye ubarasi na nahuisha wafu kwa idhini ya Allaah. Na nakujulisheni mtakavyokula na mtakavyoweka akiba majumbani mwenu. Hakika katika hayo bila shaka kuna Aayah kwenumkiwa Waumini.

 

 

 وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَلِأُحِلَّ لَكُم بَعْضَ الَّذِي حُرِّمَ عَلَيْكُمْ ۚوَجِئْتُكُم بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿٥٠﴾

50. Na mwenye kusadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat na ili nikuhalalishieni baadhi ya yale yaliyoharamishwa kwenu. Na nimekujieni na Aayah (ishara, hoja) kutoka kwa Rabb wenu. Basi mcheni Allaah na nitiini.



Endelea Kusoma Kwa Kugusa HAPA

Report Page