@Furqanbot
وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَلِأُحِلَّ لَكُم بَعْضَ الَّذِي حُرِّمَ عَلَيْكُمْ ۚوَجِئْتُكُم بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿٥٠﴾
50. Na mwenye kusadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat na ili nikuhalalishieni baadhi ya yale yaliyoharamishwa kwenu. Na nimekujieni na Aayah (ishara, hoja) kutoka kwa Rabb wenu. Basi mcheni Allaah na nitiini.
إِنَّ اللَّـهَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۗ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ ﴿٥١﴾
51. Hakika Allaah ni Rabb wangu na Rabb wenu basi mwabuduni. Hii ndio njia iliyonyooka.”
فَلَمَّا أَحَسَّ عِيسَىٰ مِنْهُمُ الْكُفْرَ قَالَ مَنْ أَنصَارِي إِلَى اللَّـهِ ۖ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ اللَّـهِ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَاشْهَدْ بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٥٢﴾
52. Basi alipohisi ‘Iysaa ukafiri kutoka kwao; alisema: “Nani wanusuruji wangu kwa ajili ya Allaah? Wakasema wafuasi watiifu: “Sisi ni wasaidizi wa Allaah. Tumemwamini Allaah na shuhudia kwamba sisi ni Waislamu (tunajisalimisha Kwake).”
رَبَّنَا آمَنَّا بِمَا أَنزَلْتَ وَاتَّبَعْنَا الرَّسُولَ فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ ﴿٥٣﴾
53. “Rabb wetu, tumeamini Uliyoyateremsha na tumemfuata Rasulibasi tuandike pamoja na wanaoshuhudia (haki).”
وَمَكَرُوا وَمَكَرَ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ ﴿٥٤﴾
54. Wakapanga makri lakini Allaah Akapanga kulipiza makri. Na Allaah ni Mbora wa kulipiza mipango ya makri.[6]
إِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَىٰ إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ وَمُطَهِّرُكَ مِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا وَجَاعِلُ الَّذِينَ اتَّبَعُوكَ فَوْقَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۖ ثُمَّ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأَحْكُمُ بَيْنَكُمْ فِيمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿٥٥﴾
55. Pale Allaah Aliposema: “Ee ‘Iysaa, hakika Mimi ni Mwenye kukuchukua usingizini na Mwenye kukupandisha Kwangu na Mwenye kukutakasa kutokana na wale waliokufuru na Nitawafanya wale waliokufuata (kujisalimisha kwa Allaah) kuwa juu ya wale waliokufuru mpaka Siku ya Qiyaamah, kisha Kwangu ndio marejeo yenu Nitahukumu baina yenu katika yale mliyokuwa kwayo mkikhitilafiana.”[7]
فَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَأُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٥٦﴾
56. Basi wale waliokufuru, Nitawaadhibu adhabu kali katika dunia na Aakhirah, na hawatopata yeyote mwenye kunusuru.
وَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُوَفِّيهِمْ أُجُورَهُمْ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ ﴿٥٧﴾
57. Ama wale waliomini na wakatenda mema, basi Atawalipa ujira wao kikamilifu. Na Allaah Hapendi madhalimu.
ذَٰلِكَ نَتْلُوهُ عَلَيْكَ مِنَ الْآيَاتِ وَالذِّكْرِ الْحَكِيمِ ﴿٥٨﴾
58. Hizo Tunakusomea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika Aayaat na ukumbusho wenye hikmah.
إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِندَ اللَّـهِ كَمَثَلِ آدَمَ ۖخَلَقَهُ مِن تُرَابٍ ثُمَّ قَالَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٥٩﴾
59. Hakika mfano wa ‘Iysaa kwa Allaah ni kama mfano wa Aadam. Amemuumba kutokana na udongo kisha Akamwambia: “Kun!”, basi akawa.
الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُن مِّنَ الْمُمْتَرِينَ﴿٦٠﴾
60. Haki kutoka kwa Rabb wako, basi usiwe miongoni mwa wanaotia shaka.
فَمَنْ حَاجَّكَ فِيهِ مِن بَعْدِ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ فَقُلْ تَعَالَوْا نَدْعُ أَبْنَاءَنَا وَأَبْنَاءَكُمْ وَنِسَاءَنَا وَنِسَاءَكُمْ وَأَنفُسَنَا وَأَنفُسَكُمْ ثُمَّ نَبْتَهِلْ فَنَجْعَل لَّعْنَتَ اللَّـهِ عَلَى الْكَاذِبِينَ ﴿٦١﴾
61. Basi yeyote atakayekuhoji kwayo baada ya kukujia elimu, basi sema: “Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsi zetu, na nafsi zenu, kisha tuombe mubaahalah, tuifanye laana ya Allaah iwe juu ya waongo.[8]
إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْقَصَصُ الْحَقُّ ۚ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٦٢﴾
62. Hakika haya ni masimulizi ya haki. Na hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah. Na hakika Allaah Yeye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.
فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِالْمُفْسِدِينَ﴿٦٣﴾
63. Wakikengeuka, basi hakika Allaah ni Mjuzi wa mafisadi.
قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٦٤﴾
64. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaabi! Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu, kwamba tusiabudu isipokuwa Allaah Pekee, na wala tusimshirikishe na chochote, na wala wasichukue baadhi yetu wengine kuwa miola badala ya Allaah.” Wakikengeuka; basi semeni: “Shuhudieni kwamba sisi ni Waislamu.”
يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تُحَاجُّونَ فِي إِبْرَاهِيمَ وَمَا أُنزِلَتِ التَّوْرَاةُ وَالْإِنجِيلُ إِلَّا مِن بَعْدِهِ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٦٥﴾
65. Enyi Ahlal-Kitaabi! Kwanini mnahojiana kuhusu Ibraahiym na hali haikuteremshwa Tawraat na Injiyl isipokuwa baada yake? Je, hamtii akilini?
هَا أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ حَاجَجْتُمْ فِيمَا لَكُم بِهِ عِلْمٌ فَلِمَ تُحَاجُّونَ فِيمَا لَيْسَ لَكُم بِهِ عِلْمٌ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ﴿٦٦﴾
66. Ha! Nyinyi ndio hawa mliohojiana katika yale ambayo mnayo elimu nayo, basi kwa nini mnahojiana katika yale msiyokuwa na elimu nayo? Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui.
مَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَـٰكِن كَانَ حَنِيفًا مُّسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٦٧﴾
67. Hakuwa Ibraahiym Yahudi wala Naswara; lakini alikuwa mwenye kujiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki, Muislamu na hakuwa miongoni mwa washirikna.
إِنَّ أَوْلَى النَّاسِ بِإِبْرَاهِيمَ لَلَّذِينَ اتَّبَعُوهُ وَهَـٰذَا النَّبِيُّ وَالَّذِينَ آمَنُوا ۗوَاللَّـهُ وَلِيُّ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٦٨﴾
68. Hakika watu walio karibu zaidi kwa Ibraahiym ni wale waliomfuata na huyu Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na wale walioamini. Na Allaah ni Mlinzi na Msaidizi wa Waumini.
وَدَّت طَّائِفَةٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يُضِلُّونَكُمْ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿٦٩﴾
69. Linatamani kundi katika Ahlil-Kitaabi kama wangelikupotezeni, lakini hawapotezi ila nafsi zao na hawahisi.
يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَأَنتُمْ تَشْهَدُونَ ﴿٧٠﴾
70. Enyi Ahlal-Kitaabi! Kwanini mnakanusha Aayaat za Allaah na hali nyinyi mnashuhudia?
يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَلْبِسُونَ الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُونَ الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٧١﴾
71. Enyi Ahlal-Kitaabi! Kwanini mnachanganya haki na batili na mnaficha haki na hali nyinyi mnajua?
وَقَالَت طَّائِفَةٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ آمِنُوا بِالَّذِي أُنزِلَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَجْهَ النَّهَارِ وَاكْفُرُوا آخِرَهُ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ﴿٧٢﴾
72. Na kundi miongoni mwa Ahlil-Kitaabi likasema (kuambiana): “Aminini yale ambayo yameteremshwa kwa wale walioamini mwanzo wa mchana na kanusheni mwisho wake, wapate kurejea (waache dini yao).”
وَلَا تُؤْمِنُوا إِلَّا لِمَن تَبِعَ دِينَكُمْ قُلْ إِنَّ الْهُدَىٰ هُدَى اللَّـهِ أَن يُؤْتَىٰ أَحَدٌ مِّثْلَ مَا أُوتِيتُمْ أَوْ يُحَاجُّوكُمْ عِندَ رَبِّكُمْ ۗقُلْ إِنَّ الْفَضْلَ بِيَدِ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٧٣﴾
73. “Na wala msimwamini isipokuwa yule anayefuata dini yenu.” Sema: “Hakika mwongozo wa kweli nimwongozo wa Allaah, (mnakhofu) kwamba atapewa mmoja (elimu) mfano wa yale mliyopewa au wakuhojini mbele ya Rabb wenu” Sema: “Hakika fadhila zi Mkononi mwa Allaah; Humpa Amtakaye. Na Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote.
يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٧٤﴾
74. Humchagua kwa rahmah Yake Amtakaye; na Allaah ni Mwenye fadhila adhimu.
وَمِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مَنْ إِن تَأْمَنْهُ بِقِنطَارٍ يُؤَدِّهِ إِلَيْكَ وَمِنْهُم مَّنْ إِن تَأْمَنْهُ بِدِينَارٍ لَّا يُؤَدِّهِ إِلَيْكَ إِلَّا مَا دُمْتَ عَلَيْهِ قَائِمًا ۗ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لَيْسَ عَلَيْنَا فِي الْأُمِّيِّينَ سَبِيلٌ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٥﴾
75. Na katika Ahlil-Kitaab yuko ambaye ukimpa amana ya mrundi wa mali atakurejeshea, na katika wao yuko ambaye ukimpa amana ya dinari moja tu hatoirudisha kwako isipokuwa utakapodumisha kumsimamia (kumdai). Hilo ni kwa sababu wao wamesema: “Hakuna juu yetu lawama kwa wasiojua kusoma na kuandika” na wanamsingizia uongo Allaah, na hali wao wanajua.
بَلَىٰ مَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ وَاتَّقَىٰ فَإِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ ﴿٧٦﴾
76. Bali ndio! Atakayetimiza ahadi yake akawa na taqwa, basi hakika Allaah Anapenda wamchao Allaah.
إِنَّ الَّذِينَ يَشْتَرُونَ بِعَهْدِ اللَّـهِ وَأَيْمَانِهِمْ ثَمَنًا قَلِيلًا أُولَـٰئِكَ لَا خَلَاقَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّـهُ وَلَا يَنظُرُ إِلَيْهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٧﴾
77. Hakika wale wanaobadilisha ahadi ya Allaah na viapo vyao kwa thamani ndogo; hao hawana sehemu yoyote katika Aakhirah na wala Allaah Hatowasemesha na wala Hatowatazama Siku Ya Qiyaamah na wala Hatowatakasa na watapata adhabu iumizayo.[9]
وَإِنَّ مِنْهُمْ لَفَرِيقًا يَلْوُونَ أَلْسِنَتَهُم بِالْكِتَابِ لِتَحْسَبُوهُ مِنَ الْكِتَابِ وَمَا هُوَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَقُولُونَ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَمَا هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٨﴾
78. Na hakika miongoni mwao kuna kundi wanaopotosha Kitabu kwa ndimi zao (wanaposoma) ili mdhanie kuwa hayo ni yanayotoka katika Kitabu, na hali hayo si yenye kutoka katika Kitabu, na wanasema: “Hayo ni kutoka kwa Allaah”; na hali hayo si kutoka kwa Allaah na wanamsingizia uongo Allaah na wao wanajua.
مَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُؤْتِيَهُ اللَّـهُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ثُمَّ يَقُولَ لِلنَّاسِ كُونُوا عِبَادًا لِّي مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِن كُونُوا رَبَّانِيِّينَ بِمَا كُنتُمْ تُعَلِّمُونَ الْكِتَابَ وَبِمَا كُنتُمْ تَدْرُسُونَ ﴿٧٩﴾
79. Ni mustahili kwa mtu kwamba Allaah Amempa Kitabu na Al-Hukma na Unabii kisha awaambie watu: “Kuweni wenye kuniabudu mimi badala ya Allaah” Bali (atawaambia): “Kuweni Wanachuoni waswalihina kwa yale mliyokuwa mkiyafundisha ya Kitabu na kwa yale mliyokuwa mkiyadurusu.”[10]
وَلَا يَأْمُرَكُمْ أَن تَتَّخِذُوا الْمَلَائِكَةَ وَالنَّبِيِّينَ أَرْبَابًا ۗ أَيَأْمُرُكُم بِالْكُفْرِ بَعْدَ إِذْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿٨٠﴾
80. Na wala hakuamuruni kuwachukua Malaika na Manabii kuwafanya miola. Je, anakuamrisheni ukafiri baada ya nyinyi kuwa mmejisalimisha kwa Allaah?
وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ النَّبِيِّينَ لَمَا آتَيْتُكُم مِّن كِتَابٍ وَحِكْمَةٍ ثُمَّ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مُّصَدِّقٌ لِّمَا مَعَكُمْ لَتُؤْمِنُنَّ بِهِ وَلَتَنصُرُنَّهُ ۚ قَالَ أَأَقْرَرْتُمْ وَأَخَذْتُمْ عَلَىٰ ذَٰلِكُمْ إِصْرِي ۖ قَالُوا أَقْرَرْنَا ۚ قَالَ فَاشْهَدُوا وَأَنَا مَعَكُم مِّنَ الشَّاهِدِينَ﴿٨١﴾
81. Na pindi Alipochukua Allaah fungamano kwa Manabii (akawaambia) “Kwa yale niliyokupeni kutoka kitabu na hikmah, kisha akakujieni Rasuli (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) mwenye kusadikisha yaliyo pamoja nanyi; ni juu yenu kumwamini na kumnusuru.” (Kisha Allaah): Akasema “Je, mmekiri na mmekubali kuchukua juu ya hayo fungamano zito Langu?” Wakasema: “Tumekiri.” (Allaah) Akasema: “Basi shuhudieni na Mimi Niko pamoja nanyi katika wenye kushuhudia.”[11]
فَمَن تَوَلَّىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿٨٢﴾
82. Basi atakayekengeuka baada ya hayo, basi hao ni mafasiki.
أَفَغَيْرَ دِينِ اللَّـهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ ﴿٨٣﴾
83. Je, wanataka dini isiyokuwa ya Allaah, na hali amejisalimisha Kwake kila aliye katika mbingu na katika ardhi akipenda asipende na Kwake watarejeshwa.
قُلْ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ عَلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَالنَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿٨٤﴾
84. Sema: “Tumemwamini Allaah, na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym, na Ismaa’iyl na Is-haaq, na Ya’quwb na Al-Asbaatw na yale aliyopewa Muwsaa na ‘Iysaa na Manabii kutoka kwa Rabb wao, hatutofautishi baina ya mmoja yeyote miongoni mwao, nasi ni Waislamu (tunajisalimisha) Kwake.”[12]
وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٨٥﴾
85. Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake; naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.[13]
كَيْفَ يَهْدِي اللَّـهُ قَوْمًا كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ وَشَهِدُوا أَنَّ الرَّسُولَ حَقٌّ وَجَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٦﴾
86. Vipi Allaah Atawaongoza watu waliokufuru baada ya kuamini kwao na wakashuhudia kwamba Rasuli ni haki na zikawajia hoja bayana? Na Allaah Hawaongozi watu madhalimu.[14]
أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُمْ أَنَّ عَلَيْهِمْ لَعْنَةَ اللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ﴿٨٧﴾
87. Hao jazaa yao ni kwamba juu yao ipo laana ya Allaah na ya Malaika na ya watu wote.
خَالِدِينَ فِيهَا لَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ ﴿٨٨﴾
88. Wenye kudumu humohawatopunguziwa adhabu wala hawatopewa muda wa kuakhirishwa adhabu.
إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٨٩﴾
89. Isipokuwa wale waliotubu baada ya hayo na wakatengenea, basi hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ ثُمَّ ازْدَادُوا كُفْرًا لَّن تُقْبَلَ تَوْبَتُهُمْ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الضَّالُّونَ ﴿٩٠﴾
90. Hakika wale waliokufuru baada ya kuamini kwao kisha wakazidi kukufuru; haitokubaliwa tawbah yao, na hao ndio waliopotoka.[15]
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يُقْبَلَ مِنْ أَحَدِهِم مِّلْءُ الْأَرْضِ ذَهَبًا وَلَوِ افْتَدَىٰ بِهِ ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ﴿٩١﴾
91. Hakika wale waliokufuru na wakafa nao wakiwa makafiri, basi haitakubaliwa kutoka kwa mmoja wao dhahabu ya ujazo wa dunia nzima lau wakitaka kujifidia nayo. Hao watapata adhabu iumizayo na hawatopatamwenye kuwanusuru.
لَن تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِن شَيْءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٩٢﴾
92. Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda. Na kitu chochote mnachotoa basi hakika Allaah kwacho ni Mjuzi.
كُلُّ الطَّعَامِ كَانَ حِلًّا لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ إِلَّا مَا حَرَّمَ إِسْرَائِيلُ عَلَىٰ نَفْسِهِ مِن قَبْلِ أَن تُنَزَّلَ التَّوْرَاةُ ۗ قُلْ فَأْتُوا بِالتَّوْرَاةِ فَاتْلُوهَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٩٣﴾
93. Kila chakula kilikuwa halali kwa wana wa Israaiyl, isipokuwa kile alichojiharamishia Israaiyl (Ya’quwb) mwenyewe kabla ya kuteremshwa Tawraat. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Basi leteni Tawraat kisha muisome mkiwa wakweli.”
فَمَنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٩٤﴾
94. Na yeyote atakayemtungia Allaah uongo baada ya hayo; basi hao ndio madhalimu.
قُلْ صَدَقَ اللَّـهُ ۗ فَاتَّبِعُوا مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٩٥﴾
95. Sema: “Allaah Amesema kweli.” Basi fuateni millah (Dini) ya Ibraahiym aliyejiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki na hakuwa miongoni mwa washirikina.
إِنَّ أَوَّلَ بَيْتٍ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكًا وَهُدًى لِّلْعَالَمِينَ ﴿٩٦﴾
96. Hakika nyumba ya awali iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ‘ibaadah) ni ile ambayo iko Bakkah (Makkah), yenye barakah na mwongozo kwa walimwengu.
فِيهِ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ مَّقَامُ إِبْرَاهِيمَ ۖ وَمَن دَخَلَهُ كَانَ آمِنًا ۗ وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚوَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ﴿٩٧﴾
97. Ndani yake kuna Aayaat (ishara, dalili) zilizo wazi; mahali pa kisimamo cha Ibraahiym. Na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Allaah imewajibika watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo. Na atakayekufuru, basi hakika Allaah ni Mkwasi kwa walimwengu.
قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَاللَّـهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا تَعْمَلُونَ﴿٩٨﴾
98. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaabi! Kwa nini mnakanusha Aayaat za Allaah; na hali Allaah ni Shahiyd juu ya myatendayo?”
قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ مَنْ آمَنَ تَبْغُونَهَا عِوَجًا وَأَنتُمْ شُهَدَاءُ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٩٩﴾
99. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaabi! Kwanini mnamzuilia aliyeamini njia ya Allaah mnaitafutia ionekane kombo na hali nyinyi mashahidi (juu ya haki)? Na Allaah si Mwenye kughafilika kuhusu myatendayo.”