006-Al-An’aam

006-Al-An’aam

Khamis

Next page 📄 3

 

وَكَيْفَ أَخَافُ مَا أَشْرَكْتُمْ وَلَا تَخَافُونَ أَنَّكُمْ أَشْرَكْتُم بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَانًا ۚ فَأَيُّ الْفَرِيقَيْنِ أَحَقُّ بِالْأَمْنِ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٨١﴾

81. Na vipi nikhofu yale mnayoyashirikisha, nanyi hamkhofu kwamba mnamshirikisha Allaah na ambayo Hakuyateremshia kwenu hoja. Je, basi kundi gani kati ya mawili linastahiki zaidi kuwa katika amani kama nyinyi mnajua?

 

 

 

الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُولَـٰئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٨٢﴾

82. Wale walioamini na hawakuchanganya imaan zao na dhulma,[11] hao ndio watakaopata amani nao ndio waliohidika.

 

 

 

وَتِلْكَ حُجَّتُنَا آتَيْنَاهَا إِبْرَاهِيمَ عَلَىٰ قَوْمِهِ ۚ نَرْفَعُ دَرَجَاتٍ مَّن نَّشَاءُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿٨٣﴾

83. Na hiyo ndio hoja Yetu Tuliyompa Ibraahiym juu ya watu wake. Tunampandisha cheo Tumtakaye. Hakika Rabb wako Ni Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.[12]

 

 

 

وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۚ كُلًّا هَدَيْنَا ۚ وَنُوحًا هَدَيْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِ دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَارُونَ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٤﴾

84. Na Tukamtunukia Is-haaq na Ya’quwb. Wote Tukawahidi. Na Nuwh Tulimhidi kabla. Na katika dhuria wake (Tuliwahidi pia) Daawuwd, na Sulaymaan, na Ayyuwb, na Yuwsuf, na Muwsaa, na Haaruwn. Na hivyo ndivyo Tulipavyo wafanyao ihsaan.

 

 

 

وَزَكَرِيَّا وَيَحْيَىٰ وَعِيسَىٰ وَإِلْيَاسَ ۖ كُلٌّ مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٨٥﴾

85. Na Zakariyyaa, na Yahyaa, na ‘Iysaa, na Ilyaas. Wote ni miongoni mwa Swalihina.

 

 

 

وَإِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطًا ۚ وَكُلًّا فَضَّلْنَا عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٨٦﴾

86. Na Ismaa’iyl, na Al-Yasa’a na Yuwnus, na Luutw. Na wote Tuliwafadhilisha juu ya walimwengu.

 

 

 

 

وَمِنْ آبَائِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ وَإِخْوَانِهِمْ ۖ وَاجْتَبَيْنَاهُمْ وَهَدَيْنَاهُمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٨٧﴾

87. Na katika baba zao, na dhuriya wao, na ndugu zao. Na Tukawateua na Tukawaongoza kuelekea njia iliyonyooka.

 

 

 

 

 

ذَٰلِكَ هُدَى اللَّـهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚ وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٨﴾

88. Hiyo ndiyo Hidaya ya Allaah, Humwongoza kwayo Amtakaye kati ya Waja Wake. Na kama wangemshirikisha basi yangeporomoka yale waliyokuwa wakiyatenda.[13]

 

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ۚ فَإِن يَكْفُرْ بِهَا هَـٰؤُلَاءِ فَقَدْ وَكَّلْنَا بِهَا قَوْمًا لَّيْسُوا بِهَا بِكَافِرِينَ ﴿٨٩﴾

89. Hao ndio Tuliowapa Kitabu na Hikmah na Unabii. Wakiyakanusha hawa (makafiri), basi kwa yakini Tumekwishayawakilisha kwa watu wasioyakanusha.

 

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ هَدَى اللَّـهُ ۖ فَبِهُدَاهُمُ اقْتَدِهْ ۗ قُل لَّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا ۖ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْعَالَمِينَ ﴿٩٠﴾

90. Hao ndio ambao Allaah Amewahidi. Basi fuata kama kigezo uongofu wao. Sema: Sikuombeni ujira kwa hayo. Hayakuwa haya ila ni ukumbusho kwa walimwengu.

 

 

 

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ إِذْ قَالُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ عَلَىٰ بَشَرٍ مِّن شَيْءٍ ۗ قُلْ مَنْ أَنزَلَ الْكِتَابَ الَّذِي جَاءَ بِهِ مُوسَىٰ نُورًا وَهُدًى لِّلنَّاسِ ۖ تَجْعَلُونَهُ قَرَاطِيسَ تُبْدُونَهَا وَتُخْفُونَ كَثِيرًا ۖ وَعُلِّمْتُم مَّا لَمْ تَعْلَمُوا أَنتُمْ وَلَا آبَاؤُكُمْ ۖ قُلِ اللَّـهُ ۖ ثُمَّ ذَرْهُمْ فِي خَوْضِهِمْ يَلْعَبُونَ ﴿٩١﴾

91. Na hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria, pale waliposema: Allaah Hakuteremsha chochote kwa mtu. Sema: Nani aliyeteremsha Kitabu ambacho amekuja nacho Muwsaa, (chenye) nuru na mwongozo kwa watu? Mnakifanya kurasa kurasa mkizifichua na mkificha mengi. Na mkafunzwa yale mliyokuwa hamuyajui nyinyi na baba zenu. Sema: Allaah (Ameiteremsha), kisha waachilie mbali katika shughuliko la porojo lao wakicheza.

 

 

 

وَهَـٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ مُّصَدِّقُ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَلِتُنذِرَ أُمَّ الْقُرَىٰ وَمَنْ حَوْلَهَا ۚ وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۖ وَهُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ ﴿٩٢﴾

92. Na hiki ni Kitabu (Qur-aan) Tumekiteremsha chenye baraka kinachosadikisha yale yaliyokitangulia, na ili uonye (kwacho) Ummul-Quraa[14] (Mama wa miji [Makkah]), na wale ambao wameuzunguka. Na wale wanaoamini Aakhirah wanakiamini. Nao wanahifadhi Swalaah zao.

 

 

 

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ قَالَ أُوحِيَ إِلَيَّ وَلَمْ يُوحَ إِلَيْهِ شَيْءٌ وَمَن قَالَ سَأُنزِلُ مِثْلَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ ۗ وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الظَّالِمُونَ فِي غَمَرَاتِ الْمَوْتِ وَالْمَلَائِكَةُ بَاسِطُو أَيْدِيهِمْ أَخْرِجُوا أَنفُسَكُمُ ۖ الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ وَكُنتُمْ عَنْ آيَاتِهِ تَسْتَكْبِرُونَ ﴿٩٣﴾

93. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyemtungia uongo Allaah au akasema: Nimefunuliwa Wahy na hali hakufunuliwa Wahy wowote.  Na yule asemaye: Nitateremsha mfano wa yale Aliyoyateremsha Allaah.[15] Na lau ungeliona madhalimu pale wakiwa katika mateso makali ya mauti (ungeona jambo la kutisha mno), na Malaika wamenyosha mikono yao (wakiwaambia): Toeni nafsi zenu! Leo mnalipwa adhabu ya kudhalilisha kwa yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Allaah pasi na haki, na mlikuwa mkitakabari msizifuate Aayaat Zake.

 

 

 

وَلَقَدْ جِئْتُمُونَا فُرَادَىٰ كَمَا خَلَقْنَاكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَتَرَكْتُم مَّا خَوَّلْنَاكُمْ وَرَاءَ ظُهُورِكُمْ ۖ وَمَا نَرَىٰ مَعَكُمْ شُفَعَاءَكُمُ الَّذِينَ زَعَمْتُمْ أَنَّهُمْ فِيكُمْ شُرَكَاءُ ۚ لَقَد تَّقَطَّعَ بَيْنَكُمْ وَضَلَّ عَنكُم مَّا كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٩٤﴾

94. Na kwa yakini mmetujia mmoja mmoja kama Tulivyokuumbeni mara ya kwanza[16], na mmeyaacha nyuma yenu yote Tuliyokuruzukuni. Na Hatuwaoni pamoja nanyi waombezi wenu ambao mlidai kwamba wao ni washirika wenu. Kwa yakini yamekatika (mahusiano) baina yenu na yamekupoteeni mliyokuwa mkidai.

 

 

 

إِنَّ اللَّـهَ فَالِقُ الْحَبِّ وَالنَّوَىٰ ۖ يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَمُخْرِجُ الْمَيِّتِ مِنَ الْحَيِّ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ﴿٩٥﴾

95. Hakika Allaah Ni Mpasuaji wa mbegu na kokwa (zikawa miche). Anatoa kilicho hai kutokana na kilicho mfu, na Mtoaji wa kilicho mfu kutokana na kilicho hai.[17] Huyo Ndiye Allaah kwenu. Basi vipi mnaghilibiwa?

 

 

 

 

فَالِقُ الْإِصْبَاحِ وَجَعَلَ اللَّيْلَ سَكَنًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ حُسْبَانًا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ ﴿٩٦﴾

96. Mpasuaji wa mapambazuko ya asubuhi, na Akajaalia usiku kuwa ni   mapumziko, na jua na mwezi kwenda kwa hisabu. Hiyo ndio Takdiri ya Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.[18]

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ النُّجُومَ لِتَهْتَدُوا بِهَا فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٩٧﴾

97. Na Yeye Ndiye Aliyekufanyieni nyota ili zikusaidieni kujua mwendako katika viza vya bara na bahari.[19] Kwa yakini Tumezifasili waziwazi Aayaat (Ishara na vielelezo) kwa watu wanaojua.

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ فَمُسْتَقَرٌّ وَمُسْتَوْدَعٌ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَفْقَهُونَ ﴿٩٨﴾

98. Na Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja, basi (pako) mahali pa kustakiri na pa kuhifadhiwa.[20] Kwa yakini Tumezifasili waziwazi Aayaat (Ishara, Hoja, Dalili) kwa watu wanaofahamu.

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ نَبَاتَ كُلِّ شَيْءٍ فَأَخْرَجْنَا مِنْهُ خَضِرًا نُّخْرِجُ مِنْهُ حَبًّا مُّتَرَاكِبًا وَمِنَ النَّخْلِ مِن طَلْعِهَا قِنْوَانٌ دَانِيَةٌ وَجَنَّاتٍ مِّنْ أَعْنَابٍ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُشْتَبِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ ۗ انظُرُوا إِلَىٰ ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَيَنْعِهِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكُمْ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٩٩﴾

99. Na Yeye Ndiye Ambaye Ameteremsha kutoka mbinguni maji, Tukatoa kwayo mimea ya kila kitu, na Tukatoa kutoka humo mimea ya kijani, Tunatoa kutoka humo punje zinazopandana. Na katika mitende, yanatoka katika makole yake mashada yenye kuning’inia chini kwa chini, na mabustani ya mizabibu na zaytuni, na makomamanga, yanayofanana na yasiyofanana. Tazameni matunda yake yanapozaa na kuiva kwake. Hakika katika hayo mna Aayaat (Ishara, Mazingatio) kwenu kwa watu wanaoamini.

 

 

 

وَجَعَلُوا لِلَّـهِ شُرَكَاءَ الْجِنَّ وَخَلَقَهُمْ ۖ وَخَرَقُوا لَهُ بَنِينَ وَبَنَاتٍ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٠٠﴾

100. Na wakamfanyia Allaah majini kuwa ni washirika Wake ilhali Amewaumba. Na wakampachikia uongo bila ya ujuzi wowote kuwa Ana wana wa kiume na wa kike.[21] Utakasifu ni Wake na Ametukuka kwa ‘Uluwa kutokana na ambayo wanavumisha.

 

 

 

بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ وَلَدٌ وَلَمْ تَكُن لَّهُ صَاحِبَةٌ ۖ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٠١﴾

101. Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Inamkinikaje kuwa Yeye Ana mwana ilhali Hana mke! Naye Ameumba kila kitu, Naye Ni Mjuzi wa kila kitu.

 

 

 

ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ فَاعْبُدُوهُ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ ﴿١٠٢﴾

102. Huyo kwenu Ndiye Allaah, Rabb wenu. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye Muumbaji wa kila kitu, basi mwabuduni Yeye Pekee. Naye Ni Mtegemewa wa kila kitu.

 

 

 

 

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ ﴿١٠٣﴾

103. Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote,[22] Naye Ni Mwenye Kudabiri mambo kwa Ulatifu, Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.

 

 

 

قَدْ جَاءَكُم بَصَائِرُ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَنْ أَبْصَرَ فَلِنَفْسِهِ ۖ وَمَنْ عَمِيَ فَعَلَيْهَا ۚ وَمَا أَنَا عَلَيْكُم بِحَفِيظٍ ﴿١٠٤﴾

104. Kwa yakini zimekujieni hoja, ishara na dalili wazi kutoka kwa Rabb wenu. Atakayeona na kuzitambua, basi ni kwa faida yake mwenyewe, na atakayepofuka asizione basi hasara itamrudia mwenyewe, (sema) nami si msimamizi.

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ وَلِيَقُولُوا دَرَسْتَ وَلِنُبَيِّنَهُ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿١٠٥﴾

105. Na hivyo ndivyo Tunavyosarifu namna kwa namna Aayaat ili (makafiri) waseme: Umedurusu (kutoka kwa Watu wa Kitabu), na ili pia Tuibainishe kwa watu wenye kujua.

 

 

 

اتَّبِعْ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٠٦﴾

106. Fuata (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uliyofunuliwa Wahy toka kwa Rabb wako. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, na jitenge na washirikina.

 

 

 

وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا أَشْرَكُوا ۗ وَمَا جَعَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ۖ وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ ﴿١٠٧﴾

107. Na lau Allaah Angetaka wasingelifanya shirki. Na Hatukukufanya wewe msimamizi wa mambo yao na wala wewe si mdhamini wao.

 

 

 

وَلَا تَسُبُّوا الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ فَيَسُبُّوا اللَّـهَ عَدْوًا بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ كَذَٰلِكَ زَيَّنَّا لِكُلِّ أُمَّةٍ عَمَلَهُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِم مَّرْجِعُهُمْ فَيُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٠٨﴾

108. Na wala msiwatukane wale wanaowaomba asiyekuwa Allaah, wasije nao kumtukana Allaah kwa uadui bila ya ujuzi.[23] Hivyo ndivyo Tumewapambia kila ummah amali zao, kisha kwa Rabb wao Pekee yatakuwa marejeo yao, Atawajulisha yale waliyokuwa wakiyatenda.

 

 

 

 

وَأَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ لَئِن جَاءَتْهُمْ آيَةٌ لَّيُؤْمِنُنَّ بِهَا ۚ قُلْ إِنَّمَا الْآيَاتُ عِندَ اللَّـهِ ۖ وَمَا يُشْعِرُكُمْ أَنَّهَا إِذَا جَاءَتْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٠٩﴾

109. Na wakaapa kwa Allaah, viapo vyao thabiti vya nguvu, kwamba ikiwafikia Aayah (Muujiza) bila shaka wataiamini. Sema: Hakika Aayaat (Miujiza, Ishara) ziko kwa Allaah. Na kitu gani kitakutambulisheni kwamba zitakapokuja hawatoamini?

 

 

 

وَنُقَلِّبُ أَفْئِدَتَهُمْ وَأَبْصَارَهُمْ كَمَا لَمْ يُؤْمِنُوا بِهِ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَنَذَرُهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿١١٠﴾

110. Na Tunazigeuza nyoyo zao na macho yao kama wasivyoiamini mara ya kwanza. Na Tunawaacha katika upindukaji mipaka ya kuasi kwao, wanatangatanga kwa upofu.

 

 

 

وَلَوْ أَنَّنَا نَزَّلْنَا إِلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةَ وَكَلَّمَهُمُ الْمَوْتَىٰ وَحَشَرْنَا عَلَيْهِمْ كُلَّ شَيْءٍ قُبُلًا مَّا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ يَجْهَلُونَ ﴿١١١﴾

111. Na lau kama Sisi Tungeliwateremshia Malaika, na wao wakasemeshwa na wafu, na Tukawakusanyia kila kitu mbele yao, basi bado wasingeliamini ila Allaah Atake, lakini wengi wamo katika ujahili. 

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا شَيَاطِينَ الْإِنسِ وَالْجِنِّ يُوحِي بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ الْقَوْلِ غُرُورًا ۚ وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ مَا فَعَلُوهُ ۖ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ ﴿١١٢﴾

112. Na hivyo ndivyo Tulivyojaalia kwa kila Nabiy maadui mashaytwaan wa kibinaadam na kijini, wanadokezana wenyewe kwa wenyewe maneno ya kupambapamba na ya ghururi. Na lau Angetaka Rabb wako wasingeliyafanya hayo. Basi waachilie mbali na wanayoyatunga (ya uongo).

 

 

 

وَلِتَصْغَىٰ إِلَيْهِ أَفْئِدَةُ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ وَلِيَرْضَوْهُ وَلِيَقْتَرِفُوا مَا هُم مُّقْتَرِفُونَ ﴿١١٣﴾

113. Na ili zielemee katika (udanganyifu) nyoyo za wale wasioamini Aakhirah, na ili waridhike nayo, na ili wachume (madhambi) wanayoyachuma.

 

 

 

أَفَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْتَغِي حَكَمًا وَهُوَ الَّذِي أَنزَلَ إِلَيْكُمُ الْكِتَابَ مُفَصَّلًا ۚ وَالَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْلَمُونَ أَنَّهُ مُنَزَّلٌ مِّن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ ﴿١١٤﴾

114. (Sema): Je, nitafute hakimu ghairi ya Allaah na hali Yeye Ndiye Aliyekuteremshieni Kitabu kilichofasiliwa waziwazi? Na wale Tuliowapa Kitabu (kabla) wanajua kwamba kimeteremshwa kutoka kwa Rabb wako kwa haki. Basi usijekuwa miongoni mwa wanaotia shaka. 

 

 

 

وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدْقًا وَعَدْلًا ۚ لَّا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١١٥﴾

115. Na limetimia Neno la Rabb wako kiukweli na kiadilifu. Hakuna awezaye kuyabadilisha Maneno Yake. Naye Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ ﴿١١٦﴾

116. Na kama ukiwatii wengi walioko ulimwenguni, watakupoteza Njia ya Allaah. Hawafuati isipokuwa dhana tu, na hawakuwa ila wenye kubuni uongo.

 

 

 

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ مَن يَضِلُّ عَن سَبِيلِهِ ۖ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿١١٧﴾

117. Hakika Rabb wako Anajua zaidi mwenye kupotea Njia Yake. Naye Anajua zaidi wenye kuhidika.

 

 

 

فَكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ إِن كُنتُم بِآيَاتِهِ مُؤْمِنِينَ ﴿١١٨﴾

118. Basi kuleni katika ambavyo limetajwa Jina la Allaah (wakati wa kuchinjwa) mkiwa nyinyi ni wenye kuziamini Aayaat (na Hukmu) Zake.

 

 

 

وَمَا لَكُمْ أَلَّا تَأْكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا لَّيُضِلُّونَ بِأَهْوَائِهِم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِالْمُعْتَدِينَ ﴿١١٩﴾

119. Na mna nini hata msile katika ambavyo limetajwa Jina la Allaah na ilhali Ameshafasilisha waziwazi kwenu yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura navyo. Na hakika wengi wanapotoa (wengine) kwa hawaa zao bila ya ilimu. Hakika Rabb wako Yeye Anajua zaidi wenye kutaadi.

 

 

 

وَذَرُوا ظَاهِرَ الْإِثْمِ وَبَاطِنَهُ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَكْسِبُونَ الْإِثْمَ سَيُجْزَوْنَ بِمَا كَانُوا يَقْتَرِفُونَ ﴿١٢٠﴾

120. Na acheni dhambi za dhahiri na zilizofichika. Hakika wale wanaochuma dhambi watalipwa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.

 

 

 

وَلَا تَأْكُلُوا مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَإِنَّهُ لَفِسْقٌ ۗ وَإِنَّ الشَّيَاطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰ أَوْلِيَائِهِمْ لِيُجَادِلُوكُمْ ۖ وَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ ﴿١٢١﴾

121. Na wala msile katika ambavyo halikutajwa Jina la Allaah (wakati wa kuchinjwa), kwani huo ni ukiukaji wa utiifu kwa Allaah. Na hakika mashaytwaan wanawashawishi marafiki wao wandani wabishane nanyi. Na kama mtawatii basi hakika mtakuwa washirikina.

 

 

 

أَوَمَن كَانَ مَيْتًا فَأَحْيَيْنَاهُ وَجَعَلْنَا لَهُ نُورًا يَمْشِي بِهِ فِي النَّاسِ كَمَن مَّثَلُهُ فِي الظُّلُمَاتِ لَيْسَ بِخَارِجٍ مِّنْهَا ۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْكَافِرِينَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٢٢﴾

122. Je, aliyekuwa maiti kisha Tukamhuisha na Tukamjaalia nuru anatembea nayo kati ya watu, ni sawa na yule ambaye yumo katika viza hawezi kutoka humo?[24] Hivyo ndivyo walivyopambiwa makafiri yale waliyokuwa wakiyatenda.

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا فِي كُلِّ قَرْيَةٍ أَكَابِرَ مُجْرِمِيهَا لِيَمْكُرُوا فِيهَا ۖ وَمَا يَمْكُرُونَ إِلَّا بِأَنفُسِهِمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿١٢٣﴾

123. Na hivyo ndivyo Tulivyojaalia katika kila mji wahalifu wake wakuu ili wafanyie makri (njama) humo. Na hawafanyii makri ila nafsi zao, na wala hawahisi.

 

 

 

وَإِذَا جَاءَتْهُمْ آيَةٌ قَالُوا لَن نُّؤْمِنَ حَتَّىٰ نُؤْتَىٰ مِثْلَ مَا أُوتِيَ رُسُلُ اللَّـهِ ۘ اللَّـهُ أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِسَالَتَهُ ۗ سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِندَ اللَّـهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ ﴿١٢٤﴾

124. Na inapowajia Aayah (Muujiza, Ushahidi bayana) husema: Hatutoamini mpaka tupewe mfano wa yale waliopewa Rusuli wa Allaah. Allaah Anajua zaidi wapi Aweke Ujumbe Wake. Utawasibu wale waliohalifu udhalilifu mbele ya Allaah na adhabu kali kwa sababu ya makri (njama) walizokuwa wakifanya.

 

 

 

فَمَن يُرِدِ اللَّـهُ أَن يَهْدِيَهُ يَشْرَحْ صَدْرَهُ لِلْإِسْلَامِ ۖ وَمَن يُرِدْ أَن يُضِلَّهُ يَجْعَلْ صَدْرَهُ ضَيِّقًا حَرَجًا كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِي السَّمَاءِ ۚ كَذَٰلِكَ يَجْعَلُ اللَّـهُ الرِّجْسَ عَلَى الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٢٥﴾

125. Basi yule ambaye Allaah Anataka kumhidi, Humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na yule ambaye Anataka kumpotoa, Hufanya kifua chake kiwe na dhiki chenye kubana kama kwamba anapanda kwa tabu mbinguni. Hivyo ndivyo Allaah Anavyojaalia adhabu (au Anavyowasalitishia shaytwaan) kwa wale wasioamini.  

 

 

 

وَهَـٰذَا صِرَاطُ رَبِّكَ مُسْتَقِيمًا ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَذَّكَّرُونَ ﴿١٢٦﴾

126. Na hii ni Njia ya Rabb wako iliyonyooka. Kwa yakini Tumefasili waziwazi Aayaat kwa watu wanaokumbuka.

 

 

 

لَهُمْ دَارُ السَّلَامِ عِندَ رَبِّهِمْ ۖ وَهُوَ وَلِيُّهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٢٧﴾

127. Watapata Daarus-Salaam (nyumba ya amani Jannah) kwa Rabb wao. Naye Ndiye Rafiki wao Mlinzi kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyatenda. 

 

 

 

وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ قَدِ اسْتَكْثَرْتُم مِّنَ الْإِنسِ ۖ وَقَالَ أَوْلِيَاؤُهُم مِّنَ الْإِنسِ رَبَّنَا اسْتَمْتَعَ بَعْضُنَا بِبَعْضٍ وَبَلَغْنَا أَجَلَنَا الَّذِي أَجَّلْتَ لَنَا ۚ قَالَ النَّارُ مَثْوَاكُمْ خَالِدِينَ فِيهَا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿١٢٨﴾

128. Na Siku Atakapowakusanya wote (Allaah Atasema): Enyi hadhara ya majini! Kwa yakini mmewapoteza wanaadamu wengi sana. Na watasema marafiki wao wandani katika wanaadamu: Rabb wetu! Tulinufaishana sisi kwa sisi, na (leo) tumefikia muda wetu ambao Umetupangia. (Allaah) Atasema: Moto ndio makazi yenu, mtadumu humo, isipokuwa Atakavyo Allaah. Hakika Rabb wako Ni Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ نُوَلِّي بَعْضَ الظَّالِمِينَ بَعْضًا بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿١٢٩﴾

129. Na hivyo ndivyo Tunavyowafanya madhalimu kuwa marafiki wandani wao kwa wao kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.

 

 

 

 

يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِي وَيُنذِرُونَكُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا ۚ قَالُوا شَهِدْنَا عَلَىٰ أَنفُسِنَا ۖ وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَشَهِدُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَنَّهُمْ كَانُوا كَافِرِينَ ﴿١٣٠﴾

130. Enyi hadhara ya majini na wanaadamu! Je hawajakufikieni Rusuli miongoni mwenu wanakusimulieni Aayaat Zangu na wanakuonyeni kukutana na Siku yenu hii? Watasema: Tumeshuhudia dhidi ya nafsi zetu. Na uliwaghuri uhai wa dunia, na wameshuhudia dhidi ya nafsi zao kwamba hakika wao walikuwa ni makafiri.

 

 

 

ذَٰلِكَ أَن لَّمْ يَكُن رَّبُّكَ مُهْلِكَ الْقُرَىٰ بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا غَافِلُونَ ﴿١٣١﴾

131. Hivyo ni kwa kuwa Rabb wako Hakuwa Mwenye Kuangamiza mji kwa dhulma hali wenyewe hawajazindushwa.

 

 

 

وَلِكُلٍّ دَرَجَاتٌ مِّمَّا عَمِلُوا ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ ﴿١٣٢﴾

132. Na wote wana daraja mbalimbali kwa yale waliyoyatenda. Na Rabb wako Si Mwenye Kughafilika na yale wanayoyatenda.

 

 

 

وَرَبُّكَ الْغَنِيُّ ذُو الرَّحْمَةِ ۚ إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَسْتَخْلِفْ مِن بَعْدِكُم مَّا يَشَاءُ كَمَا أَنشَأَكُم مِّن ذُرِّيَّةِ قَوْمٍ آخَرِينَ ﴿١٣٣﴾

133. Na Rabb wako Ni Mkwasi Mwenye Rahmah. Akitaka Atakuondosheni na Aweke wengine Awatakao badala yenu kama Alivyokuzalisheni nyinyi kutokana na vizazi vya watu wengine.

 

 

 

إِنَّ مَا تُوعَدُونَ لَآتٍ ۖ وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ ﴿١٣٤﴾

134. Hakika mnayoahidiwa bila shaka yatakuja tu! Nanyi si wenye kuweza kushinda (kukwepa adhabu). 

 

 

 

قُلْ يَا قَوْمِ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن تَكُونُ لَهُ عَاقِبَةُ الدَّارِ ۗ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ ﴿١٣٥﴾

135. Sema: Enyi kaumu yangu! Tendeni kwa namna yenu, nami pia natenda yangu. Mtakuja kujua nani atakayekuwa na hatima njema ya makazi Aakhirah. Hakika madhalimu hawatofaulu.

 

 

 

وَجَعَلُوا لِلَّـهِ مِمَّا ذَرَأَ مِنَ الْحَرْثِ وَالْأَنْعَامِ نَصِيبًا فَقَالُوا هَـٰذَا لِلَّـهِ بِزَعْمِهِمْ وَهَـٰذَا لِشُرَكَائِنَا ۖ فَمَا كَانَ لِشُرَكَائِهِمْ فَلَا يَصِلُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَمَا كَانَ لِلَّـهِ فَهُوَ يَصِلُ إِلَىٰ شُرَكَائِهِمْ ۗ سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ ﴿١٣٦﴾

136. Na wamemfanyia Allaah fungu katika mimea na wanyama Aliyoumba. Wakasema: Hili ni la Allaah kwa madai yao, na hili ni kwa ajili ya washirika wetu. Basi yaliyokuwa kwa ajili ya washirika wao hayamfikii Allaah. Na yaliyokuwa kwa ajili ya Allaah hufika kwa washirika wao. Uovu ulioje wanayoyahukumu!  

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ زَيَّنَ لِكَثِيرٍ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ قَتْلَ أَوْلَادِهِمْ شُرَكَاؤُهُمْ لِيُرْدُوهُمْ وَلِيَلْبِسُوا عَلَيْهِمْ دِينَهُمْ ۖ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا فَعَلُوهُ ۖ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ ﴿١٣٧﴾

137. Na hivyo ndivyo washirika (mashaytwaan) wao walivyowapambia washirikina wengi kuua watoto wao ili wawateketeze na wawakorogee dini yao. Na lau Allaah Angetaka, wasingeliyafanya hayo. Basi waachilie mbali na wanayoyatunga (ya uongo).

 

 

 

وَقَالُوا هَـٰذِهِ أَنْعَامٌ وَحَرْثٌ حِجْرٌ لَّا يَطْعَمُهَا إِلَّا مَن نَّشَاءُ بِزَعْمِهِمْ وَأَنْعَامٌ حُرِّمَتْ ظُهُورُهَا وَأَنْعَامٌ لَّا يَذْكُرُونَ اسْمَ اللَّـهِ عَلَيْهَا افْتِرَاءً عَلَيْهِ ۚ سَيَجْزِيهِم بِمَا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿١٣٨﴾

138. Na wakasema kwa madai yao: Wanyama hawa (ngamia) na mazao ni marufuku, hawatowala ila wale tuwatakao, na wanyama (hawa) imeharamishwa migongo yao (kuwapanda). Na wanyama (wengine) hawalitaji Jina la Allaah juu yao (wanapowachinja), wanamtungia uongo (Allaah). Atawalipa kwa yale waliyokuwa wakiyatunga.

 

 

 

وَقَالُوا مَا فِي بُطُونِ هَـٰذِهِ الْأَنْعَامِ خَالِصَةٌ لِّذُكُورِنَا وَمُحَرَّمٌ عَلَىٰ أَزْوَاجِنَا ۖ وَإِن يَكُن مَّيْتَةً فَهُمْ فِيهِ شُرَكَاءُ ۚ سَيَجْزِيهِمْ وَصْفَهُمْ ۚ إِنَّهُ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿١٣٩﴾

139. Na wakasema: Waliomo matumboni mwa wanyama hawa ni makhsusi kwa wanaume wetu na marufuku kwa wake zetu. Lakini wakiwa ni nyamafu (wanapozaliwa), basi wanashirikiana katika hao (na wanawake kula). Hakika Atawalipa uvumishi wao. Hakika Yeye Ni Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ قَتَلُوا أَوْلَادَهُمْ سَفَهًا بِغَيْرِ عِلْمٍ وَحَرَّمُوا مَا رَزَقَهُمُ اللَّـهُ افْتِرَاءً عَلَى اللَّـهِ ۚ قَدْ ضَلُّوا وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ ﴿١٤٠﴾

140. Kwa yakini wamekhasirika wale waliowaua watoto wao kwa upumbavu bila ya ujuzi na wakaharamisha vile Alivyowaruzuku Allaah kwa kumtungia uongo Allaah. Kwa yakini wamepotea na wala hawakuwa wenye kuhidika. 

 

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَ جَنَّاتٍ مَّعْرُوشَاتٍ وَغَيْرَ مَعْرُوشَاتٍ وَالنَّخْلَ وَالزَّرْعَ مُخْتَلِفًا أُكُلُهُ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُتَشَابِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ ۚ كُلُوا مِن ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَآتُوا حَقَّهُ يَوْمَ حَصَادِهِ ۖ وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿١٤١﴾

141. Naye (Allaah) Ndiye Aliyezalisha mabustani yanayotambaa na yasiyotambaa. Na mitende na mimea yenye kutofautiana ladha yake, na zaytuni na makomamanga yanayoshabihiana na yasiyoshabihiana. Kuleni katika matunda yake yanapotoa mazao na toeni haki yake (Zakaah) siku ya kuvunwa kwake na wala msifanye israfu. Hakika Yeye Hapendi wafanyao israfu.

 

 

 

وَمِنَ الْأَنْعَامِ حَمُولَةً وَفَرْشًا ۚ كُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿١٤٢﴾

142. Na katika wanyama wa mifugo (Amekuumbieni) wabebao mzigo na wadogodogo. Kuleni katika Alivyokuruzukuni Allaah na wala msifuate hatua za shaytwaan, hakika yeye ni adui bayana kwenu.

 

 

 

ثَمَانِيَةَ أَزْوَاجٍ ۖ مِّنَ الضَّأْنِ اثْنَيْنِ وَمِنَ الْمَعْزِ اثْنَيْنِ ۗ قُلْ آلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ الْأُنثَيَيْنِ أَمَّا اشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ الْأُنثَيَيْنِ ۖ نَبِّئُونِي بِعِلْمٍ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٤٣﴾

143. Jozi nane: (za dume na jike) katika kondoo wawili na katika mbuzi wawili. Sema: Je, Ameharamisha wote madume wawili au majike mawili, au waliomo ndani ya fuko la uzazi mwa majike yote mawili? Nijulisheni kwa ilimu ikiwa nyinyi mnasema kweli.

 

 

 

 

وَمِنَ الْإِبِلِ اثْنَيْنِ وَمِنَ الْبَقَرِ اثْنَيْنِ ۗ قُلْ آلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ الْأُنثَيَيْنِ أَمَّا اشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ الْأُنثَيَيْنِ ۖ أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ وَصَّاكُمُ اللَّـهُ بِهَـٰذَا ۚ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا لِّيُضِلَّ النَّاسَ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿١٤٤﴾

144. Na katika ngamia wawili na katika ng’ombe wawili. Sema: Je, Ameharamisha madume wawili au majike mawili, au waliomo ndani ya fuko la uzazi mwa majike wawili? Au nyinyi mlishuhudia Allaah Alipokuusieni haya? Basi nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemtungia Allaah uongo ili apoteze watu bila ilimu. Hakika Allaah Hawaongozi watu madhalimu.

 

 

 

قُل لَّا أَجِدُ فِي مَا أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلَّا أَن يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَّسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ أَوْ فِسْقًا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ ۚ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ رَبَّكَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٤٥﴾

145. Sema: Sipati katika yale niliyofunuliwa Wahyi kwangu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu au damu inayomwagika au nyama ya nguruwe, kwani hivyo ni vichafu, au kilichochinjwa kinyume na utiifu kwa Allaah kwa kutajiwa asiyekuwa Allaah. Lakini atakayefikwa na dharura bila ya kutamani wala kuvuka mipaka, basi hakika Rabb wako Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

 

وَعَلَى الَّذِينَ هَادُوا حَرَّمْنَا كُلَّ ذِي ظُفُرٍ ۖ وَمِنَ الْبَقَرِ وَالْغَنَمِ حَرَّمْنَا عَلَيْهِمْ شُحُومَهُمَا إِلَّا مَا حَمَلَتْ ظُهُورُهُمَا أَوِ الْحَوَايَا أَوْ مَا اخْتَلَطَ بِعَظْمٍ ۚ ذَٰلِكَ جَزَيْنَاهُم بِبَغْيِهِمْ ۖ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ ﴿١٤٦﴾

146. Na kwa wale walio Mayahudi Tuliharamisha kila (mnyama) mwenye kucha. Na katika ng’ombe na mbuzi Tuliwaharamishia shahamu zao isipokuwa iliyobeba migongo yao au utumbo wao au iliyochanganyika na mifupa. Hivyo ndivyo Tulivyowalipa kwa baghi[25] (dhulma) yao. Na bila shaka Sisi Ni Wakweli.

 

 

 

 

فَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل رَّبُّكُمْ ذُو رَحْمَةٍ وَاسِعَةٍ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُهُ عَنِ الْقَوْمِ الْمُجْرِمِينَ ﴿١٤٧﴾

147. Wakikukadhibisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) basi sema: Rabb wenu Ni Mwenye Rahmah iliyoenea. Na wala haizuiliwi Adhabu Yake kwa watu wahalifu.

 

 

 

 

سَيَقُولُ الَّذِينَ أَشْرَكُوا لَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا أَشْرَكْنَا وَلَا آبَاؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن شَيْءٍ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ حَتَّىٰ ذَاقُوا بَأْسَنَا ۗ قُلْ هَلْ عِندَكُم مِّنْ عِلْمٍ فَتُخْرِجُوهُ لَنَا ۖ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ أَنتُمْ إِلَّا تَخْرُصُونَ ﴿١٤٨﴾

148. Watasema wale walioshirikisha: Lau Allaah Angetaka, tusingelifanya shirki, wala baba zetu pia na wala tusingeliharamisha chochote. Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale wa kabla yao mpaka walipoonja Adhabu Yetu. Sema: Je, mna ilimu yoyote mtutolee? Hamfuati isipokuwa dhana tu, nanyi si lolote ila mnabuni uongo.

 

 

 

قُلْ فَلِلَّـهِ الْحُجَّةُ الْبَالِغَةُ ۖ فَلَوْ شَاءَ لَهَدَاكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿١٤٩﴾

149. Sema: Basi Ni Allaah Pekee Mwenye hoja timilifu. Na Angelitaka Angelikuhidini nyote.

 

 

 

قُلْ هَلُمَّ شُهَدَاءَكُمُ الَّذِينَ يَشْهَدُونَ أَنَّ اللَّـهَ حَرَّمَ هَـٰذَا ۖ فَإِن شَهِدُوا فَلَا تَشْهَدْ مَعَهُمْ ۚ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ وَهُم بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ ﴿١٥٠﴾

150. Sema: Leteni mashahidi wenu wanaoshuhudia kwamba Allaah Ameharamisha (wanyama) hawa. Wakishuhudia, basi usishuhudie pamoja nao. Na wala usifuate hawaa za wale wanaokadhibisha Aayaat Zetu, na wale wasioamini Aakhirah, nao wanawasawazisha wengine na Rabb wao. 

 ☞ Ukurasa wa Tatu

 

 

Report Page