iPhone Air mauzo chali! Apple yapunguza uzalishaji wake kwa 80%

iPhone Air mauzo chali! Apple yapunguza uzalishaji wake kwa 80%

Teknolojia

Kampuni ya Apple imeanza kupunguza uzalishaji wa simu yake mpya ya iPhone Air kwa zaidi ya asilimia 80, baada ya mauzo yake kuwa chini ya malengo.

Ripoti kutoka tovuti ya MacRumors zinasema wasambazaji wa Apple wameshaanza kupunguza uzalishaji na usafirishaji wa vifaa vya iPhone Air, huku baadhi ya vipuri vinavyotumika katika utengenezaji wa simu hiyo vikitarajiwa kusitishwa utengenezaji wake kabla ya mwisho wa mwaka 2025.

Kwanini iPhone Air Imeshindwa?

Kushindwa kwa iPhone Air kunaonesha kuwa wateja wa simu za hadhi ya juu tayari wameridhika na safu ya iPhone 17 na iPhone 17 Pro, hivyo hakuna nafasi kubwa ya soko jipya kwa kutoa toleo spesheli lililojikita katika uwembamba wake kama sifa ya kipekee ya simu hiyo.

iPhone Air inapatikana Tanzania kwa bei ya kati ya Tsh 2,600,000/= hadi Tsh 3,500,000/=

iPhone Air inapatikana Tanzania kwa bei ya kati ya Tsh 2,600,000/= hadi Tsh 3,500,000/=

IPhone Air ilizinduliwa kama simu nyembamba zaidi kuwahi kutolewa na Apple, ikiwa na unene wa karibu mm 5.6 lakini ilijaribu kuvutia soko kwa muonekano badala ya utendaji. Simu hii ilipunguza baadhi ya vipengele kwa wateja kwa sasa kama vile kamera za ziada na betri kubwa, haya yalifanyika ili kuzidi kuifanya simu iwe nyembamba lakini walisahau wateja kwa sasa wanathamini sana uwezo wa kamera na uwezo wa simu kukaa na chaji.

Samsung Pia Yashindwa Kwenye Soko Hilo

Sio Apple pekee. Ripoti pia zinaonesha kuwa Samsung imekumbwa na changamoto kama hiyo kupitia simu yake nyembamba Galaxy S25 Edge, na tayari imefuta muendelezo wa matoleo mapya kutokana mauzo hafifu.

Apple Kutafuta Mwelekeo Mpya

Hii si mara ya kwanza kwa Apple kupitia changamoto kwenye kuja na kitu kipya.

  • Kwanza ilikuwa iPhone mini (5.4-inch) ambayo haikupata mauzo mazuri.
  • Kisha iPhone Plus ikazinduliwa kama chaguo nafuu kwa wapenzi wa skrini kubwa, nayo ikashindwa.
  • Sasa iPhone Air, toleo la iPhone nyembamba na nyepesi zaidi, nayo inaonekana imeshindwa.
  • Kwanza ilikuwa iPhone mini (5.4-inch) ambayo haikupata mauzo mazuri.
  • Kisha iPhone Plus ikazinduliwa kama chaguo nafuu kwa wapenzi wa skrini kubwa, nayo ikashindwa.
  • Sasa iPhone Air, toleo la iPhone nyembamba na nyepesi zaidi, nayo inaonekana imeshindwa.
  • Watumiaji wa sasa wanathamini zaidi betri kubwa, kamera bora na thamani ya fedha, kuliko unene mdogo au muonekano wa kuvutia tu.

    Watumiaji wa sasa wanathamini zaidi betri kubwa, kamera bora na thamani ya fedha, kuliko unene mdogo au muonekano wa kuvutia tu.

    Ripoti zinaashiria kuwa Apple sasa inaelekeza nguvu zake kwenye iPhone inayokunjika, ambayo huenda ikawa sehemu ya mfululizo wa iPhone 18 mwaka 2026. Fahamu kuhusu simu za mkunjo na kwa kusoma hapa -> Simu za mkunjo, je tunazihitaji?

    Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.

    Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.

    Report Page