iPHONE: Jinsi Ya Kujitengenezea Mwenyewe ‘Sticker’ Za WhatsApp! #iOS
https://teknolojia.co.tz/iphone-jinsi-ya-kujitengenezea-mwenyewe-sticker-za-whatsapp-ios/?utm_source=rss&utm_medium=rss&utm_camLakini vipi kuhusiana na kutengeneza Sticker zako mwenyewe katika mtandao huu wa kijamii (WhatsApp)? Hilo kwa sasa linawezekana kwa watumiaji wa iOS pekee na ni kuanzia iOS 17 na kuendelea.
WhatsApp imeweka mfumo huo ili kuhakikisha kwamba watumiaji wa sticker katika vifaa vya iOS (kwa sasa) wana uwezo wa kutengeneza sticker zao wenyewe.
Ili kuweza kufanikisha hili katika kutengeneza sticker zako unaweza kufanya hivyo kwa kuingia katika eneo la sticker na kisha chagua Create Sticker.
SOMA PIA Nchini Ufilipino mitandao mbalimbali ya video za ngono yafungiwa
Baada ya hapo unaweza ukachagua picha yoyote unayoitaka na kisha unaweza endelea kuhariri (edit) sticker hiyo kwa kuongeza maneno, kubadilisha ukubwa, kuchora juu yake n.k.
Vile vile unaweza Hariri (edit) sticker ambayo tayari ipo, kufanikisha jambo hili itakubidi uiguse sticker husika kwa muda mrefu mpaka neno edit sticker litokee.
Kumbuka kwa upande wa WhatsApp Web tayari huduma hii imewafikia lakini ni vuziri zaidi kufanyia jambo hili katika simu sio?
Kingine ambacho wengi hakiawafurahisha ni kwamba katika WhatsApp Web utakua na uwezo wa kuhariri (edit) tuu lakani hautakua na uwezo wa kutengeneza ya kwako mwenyewe tokea mwanzo.
SOMA PIA 5 Bora ya tovuti zinazotembelewa zaidi Duniani
Kwa sasa hili limeanza kwa watumiaji wa iOS na WhatsApp Web pengine kwa watumiaji wa Android pengine watapata kipegele hiki huko mbeleni.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je ushaanza kutumia mfumo huu wa kutengeneza sticker hizi? Au unausubiria kwa hamu ili uuanze kuutumia?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
SOMA PIA Mitandao ya kijamii yazuiwa Ethiopia kupisha mitihani
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
mtandao wa kijamiiWhatsAppWhatsApp Sticker