Udukuzi wa data za Pornhub Premium: Watumiaji hatarini

Udukuzi wa data za Pornhub Premium: Watumiaji hatarini

Teknolojia

Ripoti ya uwepo wa udukuzi wa data za Pornhub Premium imeibua mjadala mkubwa katika sekta ya teknolojia na usalama wa mtandao, baada ya kudaiwa kuwa data zilizoibiwa ni pamoja na taarifa za akaunti za watumiaji, historia ya utafutaji, utazamaji na maudhui ya Comments ya watumiaji.

Kwa mujibu wa taarifa za kiufundi, tukio hili la udukuzi wa data za Pornhub halikutokana na kuvamiwa kwa moja kwa moja kwa mifumo ya Pornhub, bali lilitokea kupitia udukuzi uliuofanywa kwa huduma ya uchambuzi wa data (analytics) ya upande wa tatu (Mixpanel) inayotumiwa na tovuti hiyo maarufu kwa maudhui ya kiutu uzima.

Kwa taarifa zilizochapishwa na wachambuzi wa cybersecurity, kundi la wadukuzi linalojulikana kama ShinyHunters linadai kuiba data za kiwango cha juu za watumiaji wa Pornhub Premium, huduma ya kulipia ya tovuti hiyo, udukuzi huo ukiusisha data kuhusu maneno ya utafutaji na jinsi watumiaji wanavyoitumia tovuti hiyo. Pornhub imethibitisha kuwepo kwa tukio la kiusalama lakini imesisitiza kuwa nenosiri(password), taarifa za malipo na data za kifedha za watumiaji hazikuathirika katika uvujaji huu wa data.

Kiteknolojia, tukio hili linaonesha hatari kubwa ya kutegemea watoa huduma kwa huduma muhimu (third-party analytics services) na nyeti kwa majukwaa makubwa ya kidijitali. Hata pale mifumo ya kampuni inapokuwa salama, udhaifu wa mshirika wa data unaweza kusababisha kuvuja kwa taarifa nyeti za watumiaji.

Kwa watumiaji wa intaneti, hasa Afrika Mashariki, tukio hili ni onyo kuhusu umuhimu wa usalama wa data binafsi na faragha mtandaoni. Kwa sasa bado watumiaji wa kulipia wa huduma hiyo wapo kwenye hatari ya kutokuwa na uhakika kama taarifa zao zitavujishwa, inaaminika kundi hilo likipokea malipo kutoka PornHub basi hakutakuwa na uvujaji wa taarifa hizo.

Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.

Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.

Report Page