Tunayoyajua Kuhusiana Na iPhone 15! #Apple

Tunayoyajua Kuhusiana Na iPhone 15! #Apple

https://teknolojia.co.tz/tunayoyajua-kuhusiana-na-iphone-15-apple/?utm_source=rss&utm_medium=rss&utm_campaign=tunayoyajua-kuhus



Ni wazi kila mwaka kuna toleo jipya kutoka makampuni makubwa ya simu, na hili linafanyika pengine ili kuongeza chache ya ushindani katika soko na vile vile kujikusanyia mapato zaidi na mwaka huu tunaisubiria kwa hamu iPhone 15.


Tunayajua Haya Yafuatayo.


MATOLEO MANNE


iPhone nyingi huwa zinakuaja katika matoleo tofauti tofauti na mara nyingi yanakuaga ni zaidi ya mawili, iPhone hii ijayo yenyewe itakuja katika matoleo manne.


iPhone 14

Toleo lake la kwanza linaweza kuwa iPhone 15 (kioo cha inchi 6.1), iPhone 15 Plus (kioo cha inchi 6.7), iPhone 15 Pro (kioo cha inchi 6.1) na vile vile kutakua na toleo la iPhone 15 Ultra (kioo cha inchi 6.7) huku toleo hili likiwa lina sifa nyingi za ziada ukilinganisha na matoleo mengine


MUONEKANO


Kwa miaka mingi sasa matoleo ya iPhone yamekua na muonekano ambao unafanana tuu, na hili halitakua ni jipya kwa toleo la iPhone 15. Kitu ambacho kimebadilika ni lile eneo la kuonyesha notification ambalo linaitwa “Dynamic Island’’ ambalo litaendelea katika matoleo yote ya iPhone zijazo.


SOMA PIA  Matumizi 5 Ya Kamera Ya Simu Janja! #Maujanja

ITAKUA NA RANGI ZA KIPEE


Katike upande wa rangi katika simu hizi ni kwamba itakuja na rangi mpya kabisa ambazo hazijawahi kupatikana katika iPhone zilizopita.


Rangi mpya ambayo inadhaniwa kuongezwa kwa kiasi kikubwa nia rangi nyekundu ambayo inakwenda kwenye weusi hivi, pengine kutakua na rangi zingine mpya.


MABADILIKO KATIKA KAMERA (PERISCOPE)


Simu nyingi sasa hivi zinakuja na lensi katika kamera ambayo inakua na uwezo wa kuvuta (zoom) umbali mrefu sana na bado kuifanya picha/video kuonekana vizuri –hili likifanikiwa litakua la kwanza kwa iPhone.


ITAKUA NA USB TYPE-C



Hii unaweza ukaisoma zaidi  >>HAPA<< na >>HAPA<<


PENGINE HATA CHIP MPYA


Mara nyingi kwa sasa kila Apple wanapotoa toleo jipya huwa wanatoa na chip mpya katika matoleo yao mapya na kwa iPhone 15 pengine tutegemee chip ya A17.


Je unahisi kutakua na sifa gani nyingine katika matoleo haya ambayo unadhani tumeisahau? Niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, ningependa kusikia kutoka kwako.


Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.


Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii


Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn


Hash




Report Page