Swalah kwa mfungwa ndani ya choo
KhamisSwali: Je, ni choo cha haja au ni choo cha kuogea?
Jibu: Ni choo cha haja.
Swali: Ikiwa mbele ya msimamo wa kuswali kuna choo, je, inadhuru?
Jibu: Haidhuru, akiliswali nacho kiko mbele yake haidhuru.
Swali: Je, ndani ya choo swalah inasihi?
Jibu: Swalah haisihi ndani ya choo; Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza, akasema:
”Ardhi yote ni msikiti isipokuwa makaburi na vyoo.”
Kwa sababu ni mahali panapodhaniwa kuwa na najisi.
Swali: Vipi ikiwa mtu amefungwa ndani ya choo na hawezi kutoka hadi wakati wa swalah ukaisha?
Jibu: Allaah amesema:
وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ
”… na ilihali ameshapambanua kwenu yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura.”[1]
Hivyo dharurah ina hukumu zake.
[1] 06:119
https://firqatunnajia.com/swalah-kwa-mfungwa-ndani-ya-choo/