Snapchat Ndani Ya Microsoft Store!

Snapchat Ndani Ya Microsoft Store!

https://teknolojia.co.tz/snapchat-ndani-ya-microsoft-store/?utm_source=rss&utm_medium=rss&utm_campaign=snapchat-ndani-ya-micros


Ukiachana na App katika vifaa kama simu na tabiti bado Snapchat ilifanya maboresho katika Snapchat ya mtandao ili angalau iendane na App ya kwenye simu lakini bado kuna baadhi ya vitu havikuendana.


Muonekano Wa Snapchat Ya Kwenye Mtandao

Kwa sasa App inapatikana katika kompyuta ambazo zinatumia programu endeshaji ya Windows na soko ambalo linatumika ni Microsoft Store.



Hii linatokea ikiwa imepishana kidogo sana na App ya WhatsApp ambayo nayo imeanza kupatikana ndani ya miezi michache katika soko hilo la Apps.


SOMA PIA  Jinsi ya kutumia Instagram Kukuza Biashara yako
Snapchat Katika Windows

Ni wazi kwamba kuna App nyingi ambazo bado hazijaanza kupatikana katika soko la Microsoft Store na nyingi zinafanya mpango ili kuanza kupatikana katika soko hilo.



#Snapchat, which avoided the #Windows platform with no official apps or support, has finally arrived on the Microsoft Store as a Progressive Web App.


According to Windows Central, Snapchat's Progressive Web App (PWA) will run through Microsoft Edge on Windows 10 and 11 PCs. pic.twitter.com/sfMJHi024C


— IANS (@ians_india) November 27, 2022

Ni wazi kwamba mtandao huu ulikua unasubiriwa kwa hamu sana kwa miaka na miaka katika soko hili na sasa imekuja huku App yenyewe ikiwa na ukubwa wa 1.4MB.


SOMA PIA  Windows 10 Technical Preview iko Tayari Kupakuliwa

Kwa kupitia Snapchat ya jukwaa hili basi utakua na uwezo wa ku’chat, kuangalia ‘stories’ na hata uweza wa kupigia simu ndugu, jamaa na marafiki.


Snapchat Katika Microsoft Store

Kingine ni kwamba App hii iko katika mfumo wa PWA (progressive web application) na kama inavyojulikana ni kwamba mfumo huu wa App unamaanisha kuwa …


….App zinakua ni za mtandao lakini zinakua na sifa zote sawa na App ambazo zinapatikana katika simu janja.


Ningependa kusikia kutoka kwako,je unaweza kutumia mtandao wa Snapchat katika kompyuta yako? Au ndio umeshazoea mtandao huo katika simu jnaja tuu?


Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.


Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii


Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn


Hash




AppMicrosoft Storemtandao wa kijamiiSnapChatWindows

Report Page