Simu za Google Pixel sahihi za kununua (2026) | SimuNzuri

Simu za Google Pixel sahihi za kununua (2026) | SimuNzuri

Teknolojia

Hapa Tanzania Google Pixel imeshika kwa sasa

Ni simu zilizovuta wengi na kununua kama vipofu

Matokeo yake wengine wameibuka kununua Google Pixel ambazo hazifai kwa sasa

Baadhi za Google zina mapungufu upande wa utendaji, software na utunzaji wa chaji

Kwa sababu Pixel nyingi zinazonunuliwa hapa Tanzania ni za zamani

Zijue zipi sahihi usije ukajichanganya huko mbeleni

Hizi hapa Google Pixel Sahihi

  • Google Pixel 5
  • Google Pixel 6
  • Google Pixel 6 Pro
  • Google Pixel 7
  • Google Pixel 7a
  • Google Pixel 7 Pro
  • Google Pixel 6a
  • Google Pixel 8
  • Google Pixel 8a
  • Google Pixel 8 Pro
  • Kuna mamilioni ya sababu kwa nini ununue hizi Google Pixel

    Na ni nafuu mara mia kuepuka matole kuanzia Google Pixel 4 kwenda chini ikiwezekana

    Hizi ndio sababu na naamini utanishukuru kukuepushia hasara mbeleni

    Ukubwa wa betri

    Simu za Google Pixel ya mwaka 2019 kuja chini zina betri ndogo sana

    Kwa mfano Google Pixel 4 ukubwa wa betri ni mAh 2800

    Hii betri kiuhalisia haiwezi kudumu na chaji hata kwa masaa nane

    Simu nyingi kwa sasa kufikisha masaa 12 ni jambo la kawaida

    Kumbuka Google Pixel 4 inakaribia miaka 7 tangu itoke

    Hivyo ubora hauwezi kuwa sawa kama awali

    Hivyo kama bajeti yako ni chini ya laki tano walau unapaswa ununue Google Pixel 5

    Nguvu ya utendaji

    Google Pixel zilizotoka mwaka 2021 zina pafomansi kubwa sana

    Pamoja na utendaji mkubwa hazitumii kiwango kikubwa cha chaji

    Mwaka 2021 Google walianza kutumia prosesa wanazoziunda wao wenyewe

    Prosesa hizo Zinaitwa Google Tensor

    Zinaambatana na core aina ya Cortex X1 kwa ajili ya kazi zinazohitaji nguvu kubwa

    Kwa kufipi kama unataka kuitumia simu kwa mambo mengi basi Google Pixel 6 kwenda mbele chaguo zuri zaidi

    Na uzuri bajeti ya hizi simu zipo kati ya 500,000 hadi 600,000

    Ukubwa wa RAM

    Unajua katika kipindi cha miaka 2 iliyopita simu zinakuja na mifumo mingi ya AI

    Mifumo ya AI inatumia sana RAM

    RAM ikiwa ndogo baada ya muda simu inaanza kuwa nzito

    Google Pixel 3, kwa mfano, ina kiasi cha RAM ya GB 4

    Kwa sasa hiki ni kiwango kidogo

    Wakati kuanzia Google Pixel 5 zinakuwekea RAM ya GB 8 na kuendelea

    Zipo Google Pixel hadi za GB 12

    Maboresho ya Software

    Simu nzuri ni ile inayotunza thamani yake muda mrefu

    Simu inayokupa nafasi ya kuweza kutumia teknolojia mpya kwa kupata toleo jipya la mfumo endeshi

    Kuna baadhi ya simu za Google Pixel hazitopoeki tena toleo la android jipya

    Kwa sasa Android mpya kabisa ni Android 16

    Google Pixel 5 kwa mfano inapokea mwisho Android 14

    Wakati huo Google Pixel 6 inapokea Android 16 na matoleo yatakayofuata

    Matoleo mapya ya Android huasidia kuboresha pia usalama wa simu

    Mifumo ya kamera

    Simu za Google Pixel kabla 2020 zina machaguo machache ya aina ya kamera

    Kwa mfano Google Pixel 4 ina kamera mbili tu haina kamera aina telephoto

    Lakini Google Pixel 6 Pro inakuja na kamera tatu

    Huku ikiwa na kamera ya ziada ya lenzi ya ultrawide

    Kwa hiyo kwa mpenzi wa kamera hana budi kununua Google Pixel 6 Pro kwenda mbele

    Ubora wa display(kioo)

    Vioo vya simu miaka hii vya daraja kati vinatumia refresh rate ya 120Hz

    Hii inafanya tachi kuwa nyepesi na muonekano mzuri unapo-scroll

    Pia Google Pixel za zamani vioo havina muangaza mkubwa

    Mara nyingi muangaza huwa ni chini ya nits 1000

    Lakini vioo vya goole pixel 6 nits ni kubwa

    Na kioo cha hdr10+ hivyo vitu vinaokana kwa kina kikubwa cha rangi

    Report Page