Realme P4 Power – Simu yenye betri kubwa haijawahi tokea | SimuNzuri

Realme P4 Power – Simu yenye betri kubwa haijawahi tokea | SimuNzuri

Teknolojia

Unatamani kutumia simujanja masaa karibu 24 kwenye intaneti bila kuwaza chaji kuisha?

Kama ni hivyo Realme P4 Power ndio simu sahihi

Realme P4 Power ndio simu ya kwanza kuja na bonge labetri la ukubwa wa mAh 10,001

Ukubwa wake wa betri unaifanya simu kudumu na chaji masaa mengi kwenye kucheza gemu na kutumuia intaneti muda wote

Hata hivyo bei yake pia imechangamka

Bei ya Realme P4 Power GB 128

Kwa hapa Tanzania realme p4 power haijaingia rasmi

Lakini gharama zake mpaka kukufikia inafika laki nane na nusu (850,000)

Inapatikana kwenye masoko ya India

Na ukubwa wa RAM unaanzia GB 8 na zingine GB 12

Kwa hiyo bei inabadilika kutokana na ukubwa wa memori na RAM

Aina ya betri

Ukubwa wa betri wa Realme P4 Power ni mAh 10,001

Mara nyingi simu tunazotumia betri zake huwa na mAh 5000

Ukubwa wa betri umechangiwa na aina mpya betri

Aina hiyo ya betri inatambulika kama silicon cabon

Si/C nishati yake ni kubwa ukilinganisha na betri zilizozoeleka

Hivyo simu nyingi kwa sasa zinaambatana na aina hii ya betri

Usije kushangaa kutokea kwa simu yenye betri kubwa zaidi ya hii

Uwezo wa kukaa na chaji

Simu inaweza kukaa na chaji masaa 14 ukiwa unacheza magemu muda wote

Ukiwa unatumia intaneti muda wote inakaa siku nzima

Kwa sababu ya betri kubwa sana chaji yake inachukuwa muda kujaa

Kutoka 0% hadi 100% inachukua takribani dakika 90

Na chaji yake inaweza kupeleka umeme hadi wa wati 80

Kama ingekuwa ni betri ndogo ya mAh ingechukua karibu dakika 45

Report Page