Pixel 10 Sasa Inashare Mafaili Moja kwa Moja na iPhone Kupitia AirDrop - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Teknolojia

Kuna habari njema kwa watumiaji wa simu za Pixel 10. Sasa unaweza kutuma na kupokea faili — kama picha, video, na document — kwenda kwenye iPhone bila kutuma kupitia WhatsApp au kuupload kwenye cloud. Hii ni kupitia Quick Share ambayo sasa inafanya kazi kama AirDrop, bila longolongo.

Kwa miaka mingi, kushare faili kirahisi kulikuwa ubora wa upande wa iPhone pekee. Lakini leo, mambo yamebadilika.

Inafanya Kazi Vipi?

  • Mmiliki wa iPhone anafungua AirDrop na kuweka “Everyone for 10 minutes”

  • Pixel inaona iPhone ndani ya Quick Share

  • Unaomba kutuma → anathibitisha → faili linaenda haraka ndani ya sekunde

    • Pixel inawashwa kwenye “Receive mode”

    • Mmiliki wa iPhone anatuma kama kawaida

    • Unakubali → shughuli imekamilika

    Hakuna internet inahitajika. Kifaa tu kiwe karibu.

    Kwa Nini Hii Ni Habari Kubwa?

    • Kuondoa vizingiti kati ya simu mbili kubwa duniani

    • Hakuna tena “nitakutumia kwa WhatsApp ikishuka ubora”

    • Hakuna tena “nitupie kwa Telegram kisha download”

    • Hakuna tena kuomba mtu afungue iCloud au Google Drive

    Teknolojia inakuwa rafiki kwa wote, haijalishi unatumia nini.

    Vipi Kuhusu Usalama?

    • Faili linatoka simu moja kwenda nyingine moja kwa moja

    • Hakuna server ya kati inayohifadhi taarifa

    • Unadhibiti nani anaweza kukuona kwa kuweka muda mfupi wa kuonekana

    Hivyo, endelea kuwa makini unapotumia sehemu yenye watu wengi, lakini muunganisho wenyewe ni salama.

    Hii Inapatikana Kwa Nani Kwa Sasa?

    Kwa sasa, ni familia nzima ya Pixel 10 pekee inayopata uwezo huu.
    Simu nyingine za Android bado zinasubiri nafasi.

    Lakini hii ni dalili kwamba siku si nyingi simu nyingi za Android zitafaidika pia.

    Hatimaye, watumiaji wa Android na iPhone wanaanza kuishi kama majirani wema — bila mipaka isiyo ya lazima. Kama una Pixel 10, jaribu leo na uone urahisi wake. Kama bado hujanunua, pengine hii ndiyo sababu yako ya kupandisha ngazi.

    Ushirikiano huu ni mwanzo tu wa dunia isiyoweka mipaka katika kushare teknolojia.

    Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.

    Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.

    Report Page