Oktoba 20: Mfumo wa AWS wasababisha hitilafu kubwa ya huduma za mtandao

Oktoba 20: Mfumo wa AWS wasababisha hitilafu kubwa ya huduma za mtandao

Teknolojia

Sehemu kubwa ya mtandao duniani ilipata usumbufu mkubwa jana baada ya Amazon Web Services (AWS) kupata hitilafu kwenye miundombinu yake ya Cloud, hasa katika kituo chake cha US-EAST-1 huko Virginia, Marekani.

Nini Kilitokea

Kuanzia majira ya asubuhi kwa saa za Tanzania katika siku ya jana, huduma nyingi za mitandao ya kijamii na tovuti maarufu za kimataifa zilianza kuwa na hali isiyo ya kawaida kwenye utendaji kazi. Katika huduma zote zilizokuwa na changamoto, sifa moja iliwaunganisha, utumiaji wa huduma ya mtandao ya AWS (Amazon Web Services).

AWS zilianza kuripoti tatizo la DNS na mfumo wa huduma za tovuti . Hii ilisababisha watumiaji wengi kushindwa kufikia huduma nyingi za mtandao zinazotegemea mifumo ya AWS kwa ufanisi.

Huduma Zilizoguswa

Mitandao na app kama Snapchat, Fortnite, WhatsApp, Venmo, Alexa, Ring, pamoja na huduma kadhaa za benki na biashara mtandaoni, zilipata hitilafu au zilikosa kufunguka kabisa kwa saa kadhaa.

Nini Kina maana kwa Watumiaji na Biashara

Kwa watumiaji wa kawaida, hili lilimaanisha kushindwa kufikia huduma za kila siku kama mawasiliano, michezo na malipo ya kidijitali. Kwa biashara, tukio hili limeonesha udhaifu wa kutegemea mtoa huduma mmoja wa kwa huduma muhimu za mtandao.

Wataalamu wanasema hili ni kumbusho muhimu kwa kampuni na taasisi kujenga mikakati mizuri ya kuhakikisha urahisi wa upatikanaji wa huduma hata pale mtoa huduma mmoja anapopatwa na changamoto.(backup & redundancy).

Kwa ufupi: Tukio hili limeonyesha jinsi dunia inavyotegemea miundombinu michache ya wingu, na jinsi hitilafu moja inaweza kuvuruga huduma mamilioni kwa sekunde chache.

Chanzo: Digital Trends, TechRadar, The Guardian.

Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.

Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.

Report Page