Mlango Wa 47
Khamisبَابٌ اِحْتِرَامُ أَسْمَاءِ اللَّهِ تَعَالَى وَتَغْيِيرُ الِاسْمِ لِأَجْلِ ذَلِكَ
Kuheshimu Majina Ya Allaah Ta’aalaa Na Kubadilisha Jina Lake Mtu Kwa Ajili Hiyo
عَنْ أَبِي شُرَيْحٍ: أَنَّهُ كَانَ يُكَنَّى: أَبَا الْحَكَمِ. فَقَالَ لَهُ النَّبِيُّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((إِنَّ اللَّهَ هُوَ الْحَكَمُ وَإِلَيْهِ الْحُكْمُ)) فَقَالَ: إِنَّ قَوْمِي إِذَا اِخْتَلَفُوا فِي شَيْءٍ أَتَوْنِي فَحَكَمْتُ بَيْنَهُمْ فَرَضِي كِلا الْفَرِيقَيْنِ فَقَالَ: ((مَا أَحْسَنَ هَذَا، فَمَا لَكَمِنَ الْوَلَدِ؟)) قُلْتُ: شُرَيْحٌ وَمُسْلِمٌ وَعَبْدُ اللَّهِ. قَالَ: ((فَمَنْ أَكْبَرُهُمْ؟)) قُلْتُ: شُرَيْحٌ. قَالَ: ((فَأَنْتَ أَبُو شُرَيْحٍ)) رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ وَغَيْرُهُ
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Shurayh(رضي الله عنه) kwamba: alikuwa akiitwa Abuu Al-Hakam. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: ((Hakika Allaah ndiye Hakimu na Kwake kuna hukmu zote)) Akasema: Hakika watu wangu wanapokhitilafiana katika jambo, hunijia kisha nikawahukumu baina yao, hapo pande mbili zote zinaridhika. Akasema: ((Uzuri ulioje huo! Je, unao watoto?)) Nikajibu: [Ndio] Shurayh na Muslim na ‘Abdullaah. Akauliza: ((Nani mkubwa wao?)) Nikasema: Shurayh. Akasema: ((Basi wewe ni Abuu Shurayh)) [Abuu Daawuwd na wengineo].
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1-Kuheshimu Majina na Sifa za Allaah (سبحانه وتعالى) japokuwa maana yake halisi haikukusudiwa kujisifia nayo (na Abuu Shurayh)
2-Mtu kubadili jina lake kwa ajili hiyo.
3-Kutumia jina la mtoto mkubwa kwa ajili ya kun-yah.