Mlango Wa 46

Mlango Wa 46

Khamis


بَابٌ التَّسَمِّي بِقَاضِي الْقُضَاةِ وَنَحْوِهِ

Kujiita Qadhi Wa Maqadhi Na Mfano Wake


 

 

 

فِي الصَّحِيحِ: عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنِ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((إِنَّ أَخْنَعَ اِسْمٍ عِنْدَ اللَّهِ رَجُلٌ تَسَمَّى مَلَكَ الأَمْلاكِ، لاَ مَالِكَ إِلاَّ اللَّهَ))

Katika Swahiyh Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah(رضي الله عنه)  kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Jina ovu na  la kuchukiza mno kwa Allaah ni mtu kujiita MalakAl-Amlaak [mfalme wa milki zote]. Hakuna Maalik isipokuwa Allaah))

 

قَالَ سُفْيَانُ مِثْلُ شَاهَانْ شَاهْ .

Sufyaan amesema: mfano: “Shaahaan Shaah” (mfalme wa wafalme kwa Wafursi).

 

وَفِي رِوَايَةٍ: ((أَغْيَظُ رَجُلٍ عَلَى اللَّهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَأَخْبَثُهُ ))

Na katika riwaayah nyingine:

((Mtu mwenye kuchukiwa mno na muovu kabisa mbele ya Allaah Siku ya Qiyaamah [ni mtu anayejiita: mfalme wa wafalme]))[Al-Bukhaariy]

Na maana ya  أخنع  ni   أوضع:  duni, aliyedhalilika kabisa.

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Kukatazwa kutumia cheo cha ‘mfalme wa wafalme’ kwa yeyote.

 

2-Kukatazwa mfano wake kama mfano uliotolewa na Sufyaan (رضي الله عنه).

 

3-Ufahamu na kuelewa uzito wa kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) licha ya kuwa mtu anaweza asidhamirie maana mbaya moyoni mwake.

 

4-Utambuzi na ufahamu kwamba kutukuzwa kiuabudiwa ni kwa Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee Mtukufu kuliko wote, Asiyefikiwa hata chembe ‘Uluwa Yake, Ametakasika na kila kitu (tofauti na ‘mfalme’ wa kidunia).

 

 

Report Page