Messenger Inataka Kuleta Huduma Ya End-To-End Encryption Kama WhatsApp!
https://teknolojia.co.tz/messenger-inataka-kuleta-huduma-ya-end-to-end-encryption-kama-whatsapp/?utm_source=rss&utm_medium=rss&
Nadhani teknolojia hii kwa sasa sio ngeni mpaka sasa, pengine umeshawahi hata kuisikia tuu na pia hapo nyuma tulishawahi kuandika kuhusu teknolojia ya End-To-End Encryption soma zaidi kwa kuingia >>HAPA<<
App za kutumiana ujumbe na hata mitandao mingi ya kijamii kwa siku za hivi karibuni utagundua kuwa kuna vipengele vingi sana vinafana fanana pengine hata inakua ni ngumu kutofautisha baadhi ya mitandao hata huduma ya End-To-End Encryption iko katika mitandao mingi.

Huduma Ya End-To-End Encryption Katika Messenger
Kwa mfano si unakumbuka huduma ya WhatsApp ile ye Reactions? Sasa kipengele hicho kilikuwepo katika mtandao wa Telegram kwa muda tuu.
Vile vile katika mitandao hii ya kutumiana na kupokea ujumbe kitu muhimu kabisa ni kuhakikisha kuwa mazungumzo hayo yanalindwa hapa ndio teknolojia ya End-To-End Encryption ndio inakuja.
Kwa sasa Messenger inafanya majaribio ya teknolojia hii, na uzuri wa hapa ni kwamba hata hao Meta wenyewe watakua hawana uwezo wa kuweza kuona ujumbe ambao watu wanabadilishana katika mtandao huu.

End-To-End Encryption Katika Messenger
Cha kuvutia kuhusiana na hili ni kwamba Meta wanataka pia kuweza kuruhusu huduma hii ikawepo moja kwa moja bila ya mtu kuchagua uwepo wa huduma hiyo.
Yaani wanataka iwe sio lazima kwa mtu mmoja kuchagua kwamba mazungumzo ya mtu Fulani yawe yanalindwa na teknolojia hii.
Vingine vinavyofanyiwa majaribio kutoka Messenger lakini bado havijapewa muda wa kusikika kwenye masikio ya watu sana ni kama uwezo wa End-To-End Encryption katika huduma ya kupiga simu za sauti katika Messenger.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje, unadhani ni moja kati ya njia sahihi kwa sasa?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
End To End Encryption 3Facebook Messenger 19Messenger 15Meta 6
