Mbunifu wa iPhone Air kuondoka Apple - TeknoKona Teknolojia Tanzania
TeknolojiaMbunifu wa iPhone Air aliyetumika katika utambulisho wa simu hiyo katika uzinduzi rasmi anaondoka kampuni hiyo. Wabunifu mbalimbali na wafanyakazi wa kwenye sekta muhimu kama vile AI wengi wamekuwa wakivutiwa na ofa nyingi kutoka makampuni mengine, na hii inapelekea wengi kuacha kazi Apple.
Abidur Chowdhury alikuwa mfanyakazi mbunifu ambaye alianza kuonekana ni mkali katika sekta hiyo na alikuwa mmoja kati ya watu muhimu katika ubunifu wa toleo jipya la iPhone ya kipekee iliyopewa jina la iPhone Air na ilitambulishwa mwezi wa tisa mwaka huu.

Ata hivyo mapokezi ya simu hiyo sokoni hayajawa mazuri sana kimauzo, bado simu hiyo inapata changamoto kukubalika sokoni kutokana na Apple kuondoa vitu muhimu kama vile utumiaji wa kamera nyingi na hivyo kuifanya simu hiyo kukosa mvuto wa kiufanisi ukilinganisha na matoleo mengine ya iPhone au yale ya Android.
Ni muda sasa Apple inajikuta inapoteza wafanyakazi wazuri kwenye sekta ya teknolojia na ubunifu, huku wengi wakivutiwa na ofa kubwa kutoka makampuni mengine ambayo yanayonekana yapo mbele katika sekta za teknolojia kama vile Akili Unde (AI). Apple bado wapo nyuma katika eneo hilo na hivi karibuni waliingia makataba na kampuni ya Google kwa ajili ya huduma ya Gemini AI kuingizwa na kutumia katika huduma ya AI katika vifaa vya Apple.
Kwa wanahabari wengi bado dalili ya Apple kuendelea kuwa na wafanyakazi bora ipo hatarini, hali inaweza kubadilika kama uongozi mkuu wa juu nao utabadilika na kuleta hali na mtazamo mpya katika kampuni hiyo.
Vyanzo: Macrumors na vyanzo mbalimbali
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.