Mbingu imeumbwa kwa nguvu, na si kwa mikono

Mbingu imeumbwa kwa nguvu, na si kwa mikono

Khamis
Swali: Ni nguvu na sifa?

Jibu: Ndio, mkono ni sifa, na pia neno hilo hutumika kumaanisha neema na nguvu:

وَالسَّمَاءَ بَنَيْنَاهَا بِأَيْدٍ

”Mbingu Tumezijenga kwa nguvu.”[1]

Bi maana kwa nguvu.

وَاذْكُرْ عَبْدَنَا دَاوُودَ ذَا الْأَيْدِ

“Mkumbuke mja Wetu Daawuud mwenye nguvu.”[2]

Mwenye nguvu. Mwenye nguvu na uoni wa dini ya Allaah.

Swali: Aayah:

وَالسَّمَاءَ بَنَيْنَاهَا بِأَيْدٍ

”Mbingu Tumezijenga kwa nguvu.”

inafahamisha kuthibitisha mikono kwa Allaah?

Jibu: Hapa inamaanisha nguvu:

وَالسَّمَاءَ بَنَيْنَاهَا بِأَيْدٍ

”Mbingu Tumezijenga kwa nguvu.”

kwa nguvu. Allaah (´Azza wa Jall) ana mikono miwili:

بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ

“Bali mikono Yake imekunjuliwa.”[3]

Hivyo mikono miwili ni jambo tofauti na kilichokusudiwa hapa:

وَالسَّمَاءَ بَنَيْنَاهَا بِأَيْدٍ

”Mbingu Tumezijenga kwa nguvu.”

Bi maana kwa nguvu.

[1] 51:47

[2]38:17

[3] 05:64

https://firqatunnajia.com/mbingu-imeumbwa-kwa-nguvu-na-si-kwa-mikono/

Report Page