Maujanja Ndani Ya Jukwaa La Barua Pepe La Gmail! #Maujanja #2023

Maujanja Ndani Ya Jukwaa La Barua Pepe La Gmail! #Maujanja #2023

https://teknolojia.co.tz/maujanja-ndani-ya-jukwaa-la-barua-pepe-la-gmail/?utm_source=rss&utm_medium=rss&utm_campaign=maujanja-n




Ni wazi kwamba wengi wetu kwa kupitia Gmail huwa tunatuma na kupokea barua pepe tuu, lakini kumbuka wakati ukifanya hivyo kuna vitu kadha wa kadha unaweza fanya ilimradi vikawa vinarahisisha mchakato huo mzima.


Licha ya hivyo kuna baadhi ya mambo pia ambayo ni maujanja ambayo unaweza fanya wakati ukiwa unatumia huduma hiyo.


Haya Ni Baadhi Ya Mambo.

Futa Barua Pepe (Email) Uliyokosea Kutuma.


Kukosea kupo, katika mtandao wa Gmail pale tuu unapomaliza kutuma barua pepe kwa mtu huwa kuna ujumbe unatokea ukielea kwa sekunde kadhaa ukisema “Undo Send’ ambapo ukiochagua basi barua pepe hiyo haitaenda.


Kingine kizuri kuhusu kipengele hiki ni kwamba unaweza chagua muda wa hili yaani unaweza ukachagua kati ya sekunde 5 mpaka 30 ili uwe na uwezo wa kutumia kipengele hiki.


Ili kufanikisha kwa tumia kompyuta ingia katika eneo la setting ndani ya Gmail na kisha katika upande wa General nenda mpaka sehemu ya ‘Undo Send’ na kisha chagua muda.

Tuma Barua Pepe Yenye Usiri Wa Hali Ya Juu


Ni wazi kwamba kuna barua pepe huwa zinatumwa na vipengele kama vile vya ‘’Print, copu, forward na download” vinakua vimefungiwa ili kulinda usiri huo.


Sasa ili kufanikisha hili, wakati unaandika barua pepe mpya hakikisha kwamba umechagua/umewasha kile kikufuli pale chini

Andaa Barua Pepe Na Kisha Itume Baadae


Hiki kipengele kipo katika mitandao mingi sana, yaani hapa unaweza ukatuma email na ukawa umeiweka muda wa kutoka katika akaunti yako na kwenda katika akaunti ya mlengwa.


Mfano unaweza ukapanga muda wa email kutoka kesho lakini ukawa umeiandika leo. Ili kuwezesha hili wakati unataka kutuma chagua sehemu ya “schedule Send’ ambayo iko ndani ya Send, cha kufanya gusa kile kimshale kinachoangalia chini pembeni yake.


Baada ya hapo unaweza chagua tarehe na muda ambao unataka barua pepe hiyo kutoka.

Andaa Barua Pepe (Iliyoingia Kwako) Ili Uisome Baadae


Ushawahi kupata barua pepe na kisha ukaamua kwamba usiisome kwanza na utaisoma baadae? Unaweza ukaweka kumbukumbu ya kukukumbusha kuisoma baadae kwani itarudi kama barua pepe mpya.


SOMA PIA Ijue tofauti ya 32-Bit na 64-Bit katika kompyuta yako

Ni rahisi cha kufanya chagua katika alama ya saa na kisha chagua muda ambao unataka ukumbushwe na kuisoma barua pepe hiyo kumbuka inaweza kuchukua muda wowote ambao umechagua wewe hata kama ni mwezi

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je hili umelipokeaje? Ni njia gani ambayo ulikua unaitumia kati ya hizo hapo juu? Je kuna maujanja mengine katika Gmail ambayo unayajua na nimeyaacha?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.


Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii


Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn


Hash









Report Page