Makampuni Ya Simu Katika Soko la China #Huawei, #Vivo, #Xiaomi, #Oppo Na #Honor Kuja Na Program Endeshi (OS) Yao!

Makampuni Ya Simu Katika Soko la China #Huawei, #Vivo, #Xiaomi, #Oppo Na #Honor Kuja Na Program Endeshi (OS) Yao!


Simu nyingi huwa zinauzika sana na mara nyingi soko hilo ni gumu maana bidhaa nyingi ambazo zinauzika basi asilimia kubwa zinatoka hapo hapo china au nchi zingine za bara la asia.


Kumbuka makampuni haya yapo katika maongozi ya kuwezesha jambo hili baada ya kuona kabisa linawezekana na mfano mzuri wameupata baada ya Huawei kuja na harmonyOS.


harmonyOS ilikuja na wengi waliipokea vizuri huku watu wengi mwanzoni kabisa waliona kuwa haitopata heshima kama ilvyotarajiwa vile vile wengi walikua wanaibeza maana ilikua inashindana moja kwa moja na Android.


SOMA PIA  Samsung Galaxy Z Flip 5 Iko Njiani, Muonekano Wa Nje Umevuja!

Kingine ni kwamba makampuni haya yanafanya hivi ili kuhakikisha kuwa wanaliendesha soko lao wenyewe kama wenyewe maana simu ni zao (asilimia kubwa) lakini programu endheshi ni za wamarekani.


Soko la China ni moja kati ya soko gumu sana kwa teknolojia ya marekani ndio maana vitu vingi huwa havipatikani kwa urahisi kama katika mataifa mengine.


Mpaka sasa inasemekana vifaa milioni 700 vya Huawei vinatumia HarmonyOS na hii ni kwa china pekee ukiachana na nchi zingine.


SOMA PIA  BlackBerry Messenger (BBM) kufungwa Mei 31

Kingine ni kwamba makampuni mengi ya simu nchini humo bado yanatumia mfumo wa uendeshaji wa vifaa vyao wa Android lakini haimaanishi kwamba hilo halitakuja kubadilika.


Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je hili umelipokeaje? Je unshauri kampuni hizo kuja na njia moja au kubaki katika Android tuu?


Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.


Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii


Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn


SOMA PIA  Apple imekuwa kampuni ya kwanza kufikia thamani ya soko la $3tn

Hash

Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.


Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.

ChinaHarmonyOSHonorHuaweiOppoVivoXiaomi

Report Page