MAKATO KINYEMELA KWENYE MITANDAO YA SIMU.
https://kigogoforum.com/index.php?threads/makato-kinyemela-kwenye-mitandao-ya-simu.633/Ndugu wana bodi limeibuka wimbi la kukata salio la muda wa maongezi au vifurushi kutumika tofauti na gharama kwenye mitandao ya vodacom na tigo, mimi binfsi nimekatwa shilingi 400 kwenye tigo usiku wa kuamkia tarehe 27January 2024 na usiku wa kuamkia 28 January 2024 vodacom wamekata muda wangu wa maongezi kiasi cha shilingi 4,396.54!
Lakini kinachoonekana kuwa wamejidhatiti kwa matendo haya ni kuwa wameondoa huduma ya kuongea na wateja na kuacha automated msg!
Wito wangu watumiaji wote wa mitandao hii wafanye kuhakiki matumizi yao ili baadae tuje na jibu la pamoja ikiwa itabainika makato haya kufanyika kwa wengi.