Kigezo cha usahihi wa kuielekea Ka´bah
Khamisar-Raajihiy: Maana ya kuelekea sehemu iliyo wazi ya Ka´bah, kwa maana kwamba ikiwa mtu yuko juu ya mlima ulio juu ya Ka´bah – Je, swalah yake inasihi?
Ibn Baaz: Ndio, akiswali juu ya mlima unaozunguka Ka´bah kuelekea hewani kwake, swalah yake inasihi.
ar-Raajihiy: Je, kwa mtazamo huu inabidi kuelekea sehemu inayoonekana moja kwa moja?
Ibn Baaz: Si lazima, kilicho sahihi ni kwamba hapahitaji sehemu inayoonekana moja kwa moja.
ar-Raajihiy: Basi kwa maoni haya swalah haisihi?
Ibn Baaz: Hewa yake inatosha, kuelekea upande wake kunatosha.
Swali: Ikiwa ataswali karibu na Ka´bah, kisha baada ya kutoa salamu akagundua kwamba ameswali kinyume na Ka´bah, bali amepinda, naye alikuwa karibu nayo?
Jibu: Akiwa ameswali kinyume na Ka´bah, basi arudie swalah.
Swali: Vipi ikiwa amepinda kidogo tu?
Jibu: Upindaji mdogo unasamehewa.
Swali: Ikiwa atatembea kuelekea Ka´bah asigongane nayo?
Jibu: Swalah yake haisihi.
https://firqatunnajia.com/kigezo-cha-usahihi-wa-kuielekea-kabah/