ibaada ipi iliyo bora?

ibaada ipi iliyo bora?

Hamis

                                                                                                                          Home 🥒

 KITENDO ( AMALI ) IPI ILIYOBORA NA FADHILA ZA GHAZWA ( VITA )





AMALI IPI ILIYO BORA ?

KUSIMAMA MAKKAH AL-MUKARRAMA KWA IBADA - AU - RIBAT ( ULINZI WA MIPAKA ) KATIKA NJIA YA LLAH :





Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote , Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho .

Aliulizwa Shaykh Al-Islam Ahmad Bin Taymiyyah ( Rahimahu-LLAH ) Juu ya Hadiyth : { Kulinda Usiku katika Pwani ya Bahari ni bora kuliko Amali ya mtu katika familia yake kwa miaka Elfu moja } , au Makazi yake kuwa katika Nyumba Tukufu ya Makkah na Baytul-Maqdis na Madina Al-Munawwar kwa Nia ya Ibada na kutokukatika ( Ibada yake ) kwa Allah Ta’ala . au Makazi yake kuwa Damietta ( Misri ) na Alexandria ( Misri ) na Tripoli (Tarablus-Libya) kwa Nia ya Ribat : Je’ Ni Ipi Bora Zaidi ?



AKAJIBU : ALHAMDULILLAH .

Bali kusimama katika Upenyo wa Waislamu (Katika Mipaka baina ya Ardhi ya Waislamu na ya Makafiri , mahala panapoogopewa uvamizi wa Adui ) kama mapenyo ( yaliyo katika pwani ya Bahari ) ya Shamu na Misri ni Bora zaidi kuliko kuwa Jirani na Miskiti mitatu ( Makka , Madina, Baytul-Maqdis ) , Na sijui katika huu mzozo kati ya wanavyuoni , na hiyo imeshanukuliwa isipokuwa mmoja katika Maimamu , hivyo ; kwa sababu Ribat ni katika aina ya Jihaad , na Madhumuni ujirani (na Miskiti Mitukufu) inakuwa katika jinsia ya Hajj .

Kama Alivyosema Allah Ta’ala:

“Je’ mmefanya ( ‘amali ya ) kunywesha Maji Mahujaji na kuamirisha Al-Masjid Al-Haraam kama ( ni sawa na ‘amali za ) Anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho , na Akafanya Jihaad katika njia ya Allaah? ( Hapana! ) Hawawi sawa mbele ya Allaah. Na Allaah Haongoi watu madhalimu” 

[ Attawbah-19 ].

Na katika sahihi mbili ; Nabiy (Swall Allahu ‘alayhi Wasallam) Aliulizwa :

Amali ipi iliyo bora? Akasema : (( Kumuamini Allah na Mtume Wake ))

Akaulizwa: kisha nini?

Akasema: (( Jihaad katika Njia ya Allah ))

Akaulizwa: kisha nini?

Akasema: (( Hajj yenye kukubaliwa )).

NA IMESIMULIWA:

“ { Ghazwa ( Vita ) katika Njia ya Allah ni bora kuliko Kuhiji mara Sabini } ”.

Na imesimuliwa na Muslim katika Sahihi yake Kutoka kwa Salmaan ( Radhiya Allahu ‘Anhu ) amesema kuwa alimsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akisema : 

“ Ribaat ya siku moja na Usiku wake ni Bora kuliko Kufunga Mwezi mzima na Kusali Usiku wake , na mtu akifa ( akiwa katika jukumu hilo ), Amali zake zitaendelea Kuandikwa na Riziki yake ataendelea kupata na atasalimika na Fitna ( za Kaburi ) . ”

Na katika Sunnah kutoka kwa Uthman ( Radhiyallahu ‘Anhu ) Amesema : Nabiy (Swall Allahu ‘alayhi Wasallam) Amesema : “ Kufanya Ribat ya Siku moja katika Njia ya Allah ni Bora kuliko Amali nyingine kwa siku Elfu moja .” Na hivi Alisema Uthman katika Mimbari ya Mtume (Swall Allahu ‘alayhi Wasallam) Alisema kuwa aliwaambia hivyo kuwajulisha Sunnah.

Na Amesema Abu Hurayra : kwa sababu Ribat ya Usiku katika Njia ya Allah ni Bora kwangu kuliko kusimama Usiku wa Laylatul-Qadri katika Hajarul-As-wad (katika Kaaba).

Na Fadhila za Ribat na Ulinzi katika Njia ya Allah ni nyingi haitoshi katika hii karatasi.

NA ALLAH NDIYE MJUZI ZAIDI.

Report Page