Istikhaarah
🔙 Homeاللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْتَخيـرُكَ بِعِلْمِك، وَأسْتَقْـدِرُكَ بِقُـدْرَتِـك، وَأَسْـألُـكَ مِنْ فَضْـلِكَ العَظـيم، فَإِنَّـكَ تَقْـدِرُ وَلا أَقْـدِر، وَتَـعْلَـمُ وَلا أَعْلَـم، وَأَنْـتَ عَلاّمُ الغُـيوب، اللّهُـمَّ إِنْ كُنْـتَ تَعْـلَمُ أَنَّ هـذا الأمْـرَ (وَيُسَـمِّي حاجته) خَـيْرٌ لي في دينـي وَمَعـاشي وَعاقِـبَةِ أَمْـري، عَاجِلِهِ و آجِلِه , فَاقْـدُرْهُ لي وَيَسِّـرْهُ لي ثـمَّ بارِكْ لي فيـه، وَإِنْ كُنْـتَ تَعْـلَمُ أَنَّ هـذا الأمْـرَ شَـرٌ لي في دينـي وَمَعـاشي وَعاقِـبَةِ أَمْـري، عَاجِلِهِ و آجِلِه فَاصْرِفْـهُ عَنّيِ وَاصْرِفْني عَنْـهُ وَاقْـدُرْ ليَ الخَـيْرَ حَيْـثُ كانَ ثُـمَّ أَرْضِـني بِـه.
Ee Allaah hakika mimi nakutaka (muongozo) unichagulie kwa ujuzi Wako, na nakuomba Uniwezeshe kwa uwezo Wako, na nakuomba fadhila Zako kubwa, hakika Wewe Unaweza, nami siwezi, Nawe unajua nami sijui, Nawe ni Mjuzi wa ya ghayb. Ee Allaah, iwapo jambo hili kutokana na ujuzi Wako (utalitaja jambo lako) lina kheri na mimi katika Dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu, karibu na mbali, basi nakuomba Uniwezeshe nilipate, na Unifanyie wepesi, kisha Unibariki. Na iwapo Unajua kwamba jambo hili ni shari kwangu katika Dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu (karibu na mbali) basi liepushe na mimi nami niepushe nalo, na nipangie jambo jengine lenye kheri nami popote lilipo, kisha niridhishe kwalo. [Al-Bukhaariy]
❍ Swalaah Ya Istikhaarah Iswaliwe Kwa Ajili Ya Nini Na Ipi Du'aa Yake?
❍ Muda Wa Swalaah ya Istikhaarah
❍ Istikhaarah Ni Kabla Ya Salaam Au Baada Ya Kumaliza Swalaah
❍ Dalili Gani Baada Ya Swalaah ya Istikhaarah Je Kuna Muda Maalumu Wa Kuiswali