Gmail (Katika Kompyuta) Yapata Muonekano Mpya!
https://teknolojia.co.tz/gmail-yapata-muonekano-mpya/?utm_source=rss&utm_medium=rss&utm_campaign=gmail-yapata-muonekano-mpya
Google ilitangaza kubadiisha muonekano wa Gmail tangia mwezi januari mwaka huu, na toleo hilo likatoka lakini kwa baadhi ya watumiaji waliochaguliwa.
Sio mara ya kwanza kwa kampuni ya Google kubadilisha muonekano wa baadhi ya huduma zake, sasa muonekano huu mpya utaonekana na utakuwa ukitumika na watumiaji wote ambao wamewasha huduma ya Google Chat

Muonekano Mpya Wa Gmail
Kabla ya kuanza kufikiria mbali zaidi, subiri kwanza. Hapa huduma haijafanyiwa mabadiliko makubwa sana maana imejikita tu katika muonekano na mpangilio wa vitu.
Ni ishu ya muonekano tuu, na muonekano huu utasaidia kwa namna moja au nyingine huduma za Chat, Spaces, na Meet n.k ziweze kupatikana vizuri ndani ya huduma hiyo.
SOMA PIA Kuna uwezekano Google kutengeneza simu yake mwaka huu! #Ripoti
Kingine kizuri ni kwamba kama ukiwa hujapenda muonekano huo basi unaweza kurudia muonekano wa zamani, Hapa unaweza kwenda katika eneo la settings na kuingia katika “Go back to the original Gmail view,”
Ili kutumia huduma hii ni lazima uingie katika huduma hii ya barua pepe ya kwenye mtandao (kompyuta).

Jinsi Ya Kuwasha Muonekano Mpya Ndani Ya Gmail
Ili kutumia huduma hii kama bado haijawezeshwa katika Gmail yako nenda katika eneo la Settings na kasha ingia katika upande wa Settings na kisha Try out the new Gmail view.
SOMA PIA Ukitumia Skype Ethiopia Jua Una Miaka 15 Jela!
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, Je umeshaanza kutumia huduma hii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
