@Furqanbot

@Furqanbot


وَقَالُوا لَن نُّؤْمِنَ لَكَ حَتَّىٰ تَفْجُرَ لَنَا مِنَ الْأَرْضِ يَنبُوعًا ﴿٩٠﴾

90. Na wakasema: “Hatutakuamini (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) mpakautububujie kutoka ardhini chemchemu.”

 

 

 

أَوْ تَكُونَ لَكَ جَنَّةٌ مِّن نَّخِيلٍ وَعِنَبٍ فَتُفَجِّرَ الْأَنْهَارَ خِلَالَهَا تَفْجِيرًا ﴿٩١﴾

91. “Au uwe na bustani ya mitende na mizabibu, kisha utububujie mito kati yake mbubujiko mkubwa.”

 

 

 

أَوْ تُسْقِطَ السَّمَاءَ كَمَا زَعَمْتَ عَلَيْنَا كِسَفًا أَوْ تَأْتِيَ بِاللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ قَبِيلًا﴿٩٢﴾

92. “Au utuangushie mbingu vipande vipande kama ulivyodai, au utuletee Allaah na Malaika uso kwa uso.”

 

 

 

أَوْ يَكُونَ لَكَ بَيْتٌ مِّن زُخْرُفٍ أَوْ تَرْقَىٰ فِي السَّمَاءِ وَلَن نُّؤْمِنَ لِرُقِيِّكَ حَتَّىٰ تُنَزِّلَ عَلَيْنَا كِتَابًا نَّقْرَؤُهُ ۗ قُلْ سُبْحَانَ رَبِّي هَلْ كُنتُ إِلَّا بَشَرًا رَّسُولًا ﴿٩٣﴾

93. “Au uwe na nyumba ya dhahabu, au upae mbinguni. Na wala hatutokuamini kamwe kupaa kwako mpaka ututeremshie kitabu tukisome.” Sema: “Utakasifu ni wa Rabb wangu! Kwani mimi nimekuwa nani isipokuwa ni bin Aadam nimetumwa kuwa Rasuli!”

 

 

 

وَمَا مَنَعَ النَّاسَ أَن يُؤْمِنُوا إِذْ جَاءَهُمُ الْهُدَىٰ إِلَّا أَن قَالُوا أَبَعَثَ اللَّـهُ بَشَرًا رَّسُولًا ﴿٩٤﴾

94. Na hakuna kilichowazuia watu wasiamini ulipowajia mwongozo isipokuwa husema: “Je, Allaah Ametuma bin Aadam kuwa ni Rasuli?”

 

 

 

قُل لَّوْ كَانَ فِي الْأَرْضِ مَلَائِكَةٌ يَمْشُونَ مُطْمَئِنِّينَ لَنَزَّلْنَا عَلَيْهِم مِّنَ السَّمَاءِ مَلَكًا رَّسُولًا ﴿٩٥﴾

95. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Kama ingelikuwa katika ardhi kuna Malaika wanatembea kwa utulivu na amani; basi bila shaka Tungeliwateremshia kutoka mbinguni Malaika kuwa ni Rasuli.”

 

 

 

قُلْ كَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۚإِنَّهُ كَانَ بِعِبَادِهِ خَبِيرًا بَصِيرًا ﴿٩٦﴾

96. Sema: “Anatosheleza Allaah kuwa Shahidi baina yangu na baina yenu. Hakika Yeye daima ni Mwenye khabari za dhahiri na za kufichika za waja Wake, Mwenye kuona yote.

 

 

 

وَمَن يَهْدِ اللَّـهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِ ۖ وَمَن يُضْلِلْ فَلَن تَجِدَ لَهُمْ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِهِ ۖوَنَحْشُرُهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ عُمْيًا وَبُكْمًا وَصُمًّا ۖ مَّأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ كُلَّمَا خَبَتْ زِدْنَاهُمْ سَعِيرًا﴿٩٧﴾

97. Na ambaye Allaah Amemhidi, basi yeye ndiye aliyehidika. Na Anayempotoa, basi hutowapatia walinzi pasi Naye. Na Tutawakusanya Siku ya Qiyaamah juu ya nyuso zao; vipofu, mabubu na viziwi; makazi yao ni (moto wa) Jahannam; kila ukififia Tutawazidishia moto uliowashwa vikali mno.

 

 

 

ذَٰلِكَ جَزَاؤُهُم بِأَنَّهُمْ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا وَقَالُوا أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا وَرُفَاتًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ خَلْقًا جَدِيدًا ﴿٩٨﴾

98. Hiyo ndiyo jazaa yao kwa kuwa wao walizikanusha Aayaat (Wahyi, ishara, dalili) Zetu na wakasema: “Je, hivi sisi tukiwa mifupa na mapande yaliyosagika sagika; hivi kweli sisi tutafufuliwa katika umbo jipya?”

 

 

 

أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ قَادِرٌ عَلَىٰ أَن يَخْلُقَ مِثْلَهُمْ وَجَعَلَ لَهُمْ أَجَلًا لَّا رَيْبَ فِيهِ فَأَبَى الظَّالِمُونَ إِلَّا كُفُورًا ﴿٩٩﴾

99. Je, hawajaona kwamba Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi ni Mweza wa kuumba mfano wao. Na Amewawekea muda maalumu usio na shaka, lakini madhalimu wamekataa kabisa (haki; hawakukubali) isipokuwa kukufuru tu.

 

 

 

قُل لَّوْ أَنتُمْ تَمْلِكُونَ خَزَائِنَ رَحْمَةِ رَبِّي إِذًا لَّأَمْسَكْتُمْ خَشْيَةَ الْإِنفَاقِ ۚوَكَانَ الْإِنسَانُ قَتُورًا ﴿١٠٠﴾

100. Sema: “Ingekuwa nyinyi mnamiliki hazina za rahmah ya Rabb wangu bila shaka hapo mngelizuia kuzitumia kwa ajili ya kukhofu (zisimalizike). Na bin Aadam amekuwa ni mchoyo kupindukia.

 

 

 

وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَىٰ تِسْعَ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ ۖفَاسْأَلْ بَنِي إِسْرَائِيلَ إِذْ جَاءَهُمْ فَقَالَ لَهُ فِرْعَوْنُ إِنِّي لَأَظُنُّكَ يَا مُوسَىٰ مَسْحُورًا ﴿١٠١﴾

101. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Aayaat (miujiza) tisa bayana. Basi waulize wana wa Israaiyl alipowajia; Fir’awn akasema: “Hakika mimi nakuona ewe Muwsaa kuwa umerogwa.”

 

 

 

قَالَ لَقَدْ عَلِمْتَ مَا أَنزَلَ هَـٰؤُلَاءِ إِلَّا رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ بَصَائِرَ وَإِنِّي لَأَظُنُّكَ يَا فِرْعَوْنُ مَثْبُورًا ﴿١٠٢﴾

102. (Muwsaa) Akasema: “Kwa yakini umekwishajua kwamba hakuna Aliyeteremsha haya isipokuwa Rabb wa mbingu na ardhi kuwa ni dalili za kuonekana dhahiri, na hakika mimi bila shaka nakuona ewe Fir’awn kuwa umekwisha angamia.”

 

 

 

فَأَرَادَ أَن يَسْتَفِزَّهُم مِّنَ الْأَرْضِ فَأَغْرَقْنَاهُ وَمَن مَّعَهُ جَمِيعًا ﴿١٠٣﴾

103. Basi akataka awasumbue na kuwafukuza katika nchi, Tukamgharikisha yeye na waliokuwa pamoja naye wote.

 

 

 

وَقُلْنَا مِن بَعْدِهِ لِبَنِي إِسْرَائِيلَ اسْكُنُوا الْأَرْضَ فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ جِئْنَا بِكُمْ لَفِيفًا ﴿١٠٤﴾

104. Na Tukasema baada yake kwa wana wa Israaiyl: “Kaeni katika ardhi; na itakapokuja ahadi ya Aakhirah Tutakuleteni nyote pamoja kwa makundi mchanganyiko.”

 

 

 

وَبِالْحَقِّ أَنزَلْنَاهُ وَبِالْحَقِّ نَزَلَ ۗ وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا مُبَشِّرًا وَنَذِيرًا ﴿١٠٥﴾

105. Na kwa haki Tumeiteremsha (Qur-aan). Na kwa haki imeteremka. Na Hatukukutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa ni mbashiriaji na mwonyaji.

 

 

 

وَقُرْآنًا فَرَقْنَاهُ لِتَقْرَأَهُ عَلَى النَّاسِ عَلَىٰ مُكْثٍ وَنَزَّلْنَاهُ تَنزِيلًا ﴿١٠٦﴾

106. Na Qur-aan Tumeigawanya sehemu mbali mbali ili uwasomee watu kwa vipindi mbali mbali; na Tumeiteremsha mteremsho wa kidogo kidogo.

 

 

 

قُلْ آمِنُوا بِهِ أَوْ لَا تُؤْمِنُوا ۚ إِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ مِن قَبْلِهِ إِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ يَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ سُجَّدًا ﴿١٠٧﴾

107. Sema: “Iaminini au msiamini. Hakika wale waliopewa elimu kabla yake wanaposomewa (Qur-aan) wanaporomoka kifudifudi wanasujudu.”

 

 

 

وَيَقُولُونَ سُبْحَانَ رَبِّنَا إِن كَانَ وَعْدُ رَبِّنَا لَمَفْعُولًا ﴿١٠٨﴾

108. Na wanasema: “Utakasifu ni wa Rabb wetu; hakika ahadi ya Rabb wetu lazima itimizwe.”

 

 

 

وَيَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ يَبْكُونَ وَيَزِيدُهُمْ خُشُوعًا ۩﴿١٠٩﴾

109. Na wanaporomoka kifudifudi huku wanalia na inawazidishia unyenyekevu.

 

 

 

قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا وَابْتَغِ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا ﴿١١٠﴾

110. Sema; “Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan, vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa. Na wala usisome kwa jahara Swalaah yako na wala usiifiche kimya kimya, bali shika njia ya wastani baina yake.

 

 

 

وَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي لَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُن لَّهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَلَمْ يَكُن لَّهُ وَلِيٌّ مِّنَ الذُّلِّ ۖ وَكَبِّرْهُ تَكْبِيرًا﴿١١١﴾

111. Na sema: “AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah) Ambaye Hakujifanyia mwana na wala Hakuwa na mshirika katika ufalme, na wala hakuwa dhalili hata awe (anahitaji) mlinzi msaidizi; basi mtukuze matukuzo makubwa kabisa (sema Allaahu Akbar!)

 


Report Page