@Furqanbot
وَاسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّي رَحِيمٌ وَدُودٌ﴿٩٠﴾
90. “Na ombeni maghfirah kwa Rabb wenu, kisha tubieni Kwake. Hakika Rabb wangu ni Mwenye kurehemu, Mwenye upendo khalisi.”
قَالُوا يَا شُعَيْبُ مَا نَفْقَهُ كَثِيرًا مِّمَّا تَقُولُ وَإِنَّا لَنَرَاكَ فِينَا ضَعِيفًا ۖ وَلَوْلَا رَهْطُكَ لَرَجَمْنَاكَ ۖ وَمَا أَنتَ عَلَيْنَا بِعَزِيزٍ﴿٩١﴾
91. Wakasema: “Ee Shu’ayb! Hatufahamu mengi unayoyasema, na hakika sisi tunakuona ni dhaifu kati yetu. Na lau si jamaa zako tungelikupiga mawe. Nawe si azizi kwetu.”
قَالَ يَا قَوْمِ أَرَهْطِي أَعَزُّ عَلَيْكُم مِّنَ اللَّـهِ وَاتَّخَذْتُمُوهُ وَرَاءَكُمْ ظِهْرِيًّا ۖ إِنَّ رَبِّي بِمَا تَعْمَلُونَ مُحِيطٌ﴿٩٢﴾
92. (Shu’ayb) Akasema: “Enyi kaumu yangu! Je, jamaa zangu wana utukufu zaidi kwenu kuliko Allaah, na mmemuweka Yeye (Allaah) nyuma ya migongo yenu? Hakika Rabb wangu ni Mwenye kuyazunguka yale myatendayo.”
وَيَا قَوْمِ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ ۖ سَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَمَنْ هُوَ كَاذِبٌ ۖوَارْتَقِبُوا إِنِّي مَعَكُمْ رَقِيبٌ﴿٩٣﴾
93. “Na enyi kaumu yangu! Tendeni kwa tamkini zenu, hakika mimi mtendaji. Mtakuja kujua nani itamfika adhabu itakayomhizi, na ni nani aliye muongo. Na ngojeeni mchunge. Hakika mimi niko pamoja nanyi nikingojea na kuchunga.”
وَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا شُعَيْبًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَأَخَذَتِ الَّذِينَ ظَلَمُوا الصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دِيَارِهِمْ جَاثِمِينَ﴿٩٤﴾
94. Na ilipokuja amri Yetu; Tulimuokoa Shu’ayb na wale walioamini pamoja naye kwa rahmah kutoka Kwetu. Na ukawachukuwa wale waliodhulumu ukelele angamizi wakapambazukiwa wameanguka kifudifudi majumbani mwao (wamekufa).
كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۗ أَلَا بُعْدًا لِّمَدْيَنَ كَمَا بَعِدَتْ ثَمُودُ﴿٩٥﴾
95. Kama kwamba hawakuishi wakineemeka humo. Tanabahi! Watokomee mbali (watu wa) Madyan kama walivyotokomea Thamuwd.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا وَسُلْطَانٍمُّبِينٍ﴿٩٦﴾
96. Na kwa yakini Tulimpeleka Muwsaa kwa Aayaat (miujiza, ishara) Zetu na dalili bayana.
إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَاتَّبَعُوا أَمْرَ فِرْعَوْنَ ۖ وَمَا أَمْرُ فِرْعَوْنَبِرَشِيدٍ﴿٩٧﴾
97. Kwa Fir’awn na wakuu wake, lakini walifuata amri ya Fir’awn. Na amri ya Fira’wn haikuwa yenye uongofu.
يَقْدُمُ قَوْمَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَأَوْرَدَهُمُ النَّارَ ۖ وَبِئْسَ الْوِرْدُ الْمَوْرُودُ﴿٩٨﴾
98. (Fira’wn) Atawatangulia watu wake Siku ya Qiyaamah, na atawafikisha motoni. Na ubaya ulioje mahali pa maingio watakapoingizwa.
وَأُتْبِعُوا فِي هَـٰذِهِ لَعْنَةً وَيَوْمَ الْقِيَامَةِۚ بِئْسَ الرِّفْدُ الْمَرْفُودُ﴿٩٩﴾
99. Na wamefuatishwa na laana katika (dunia) hii na Siku ya Qiyaamah. Ubaya ulioje wa watakayotunukiwa; laana ya dunia na ya Aakhirah.
ذَٰلِكَ مِنْ أَنبَاءِ الْقُرَىٰ نَقُصُّهُ عَلَيْكَ ۖمِنْهَا قَائِمٌ وَحَصِيدٌ﴿١٠٠﴾
100. Hizo ni baadhi ya khabari za miji Tunakusimulia kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم); miongoni mwake ingalipo bado, na iliyofekwa.
وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَـٰكِن ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ۖفَمَا أَغْنَتْ عَنْهُمْ آلِهَتُهُمُ الَّتِي يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ لَّمَّا جَاءَ أَمْرُ رَبِّكَ ۖ وَمَا زَادُوهُمْ غَيْرَ تَتْبِيبٍ﴿١٠١﴾
101. Na hatukuwadhulumu, lakini wamejidhulumu nafsi zao wenyewe. Basi hawakuwafaa kitu chochote waabudiwa wao waliokuwa wakiwaomba badala ya Allaah ilipokuja amri ya Rabb wako. Na wala hawakuwazidishia isipokuwa mateketezo.
وَكَذَٰلِكَ أَخْذُ رَبِّكَ إِذَا أَخَذَ الْقُرَىٰ وَهِيَ ظَالِمَةٌ ۚ إِنَّ أَخْذَهُ أَلِيمٌ شَدِيدٌ﴿١٠٢﴾
102. Na hivyo ndivyo mkamato wa Rabb wako unavyokuwa Anapokamata miji na huku ikifanya dhulma. Hakika mkamato Wake unaumiza vikali.
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّمَنْ خَافَ عَذَابَ الْآخِرَةِ ۚ ذَٰلِكَ يَوْمٌ مَّجْمُوعٌ لَّهُ النَّاسُ وَذَٰلِكَ يَوْمٌ مَّشْهُودٌ﴿١٠٣﴾
103. Hakika katika hayo mna Aayah (funzo, zingatio, dalili) kwa anayekhofu adhabu ya Aakhirah. Hiyo ni Siku ya kujumuishwa watu, na hiyo ni Siku ya kushuhudiwa.
وَمَا نُؤَخِّرُهُ إِلَّا لِأَجَلٍ مَّعْدُودٍ﴿١٠٤﴾
104. Na hatuiakhirishi isipokuwa kwa muda maalumu unaohesabiwa.
يَوْمَ يَأْتِ لَا تَكَلَّمُ نَفْسٌ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚفَمِنْهُمْ شَقِيٌّ وَسَعِيدٌ﴿١٠٥﴾
105. Siku itakapofika; haitosema nafsi yeyote isipokuwa kwa idhini Yake (Allaah). Basi miongoni mwao ni wenye mashaka wanaostahiki adhabu, na wenye furaha na neema.
فَأَمَّا الَّذِينَ شَقُوا فَفِي النَّارِ لَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَشَهِيقٌ﴿١٠٦﴾
106. Basi ama wale walio mashakani, basi watakuwa motoni, lao humo ni upumuaji pumzi kwa mngurumo na uvutaji pumzi kwa mkoromo.
خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ﴿١٠٧﴾
107. Ni wenye kudumu humo zitakavyodumu mbingu na ardhi isipokuwa Atakavyo Rabb wako. Hakika Rabb wako Anafanya Atakavyo.
وَأَمَّا الَّذِينَ سُعِدُوا فَفِي الْجَنَّةِ خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ ۖ عَطَاءً غَيْرَ مَجْذُوذٍ﴿١٠٨﴾
108. Na ama wale walio furahani, basi watakuwa katika Jannah, ni wenye kudumu humo zitakavyodumu mbingu na ardhi isipokuwa Atakavyo Rabb wako. Ni hiba isiyokatizwa.
فَلَا تَكُ فِي مِرْيَةٍ مِّمَّا يَعْبُدُ هَـٰؤُلَاءِ ۚمَا يَعْبُدُونَ إِلَّا كَمَا يَعْبُدُ آبَاؤُهُم مِّن قَبْلُ ۚ وَإِنَّا لَمُوَفُّوهُمْ نَصِيبَهُمْ غَيْرَمَنقُوصٍ﴿١٠٩﴾
109. Basi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) usiwe katika shaka kutokana na wanayoyaabudu hao (washirikina). Hawaabudu ila kama walivyoabudu baba zao kabla. Na hakika Tutawalipa kikamilifu fungu lao bila ya kupunguzwa.
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ فَاخْتُلِفَ فِيهِ ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُمُرِيبٍ﴿١١٠﴾
110. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu, zikatiwa ikhtilaafu ndani yake. Na kama si neno lilotangulia kutoka kwa Rabb wako, bila shaka ingelihukumiwa baina yao. Na hakika wao wako katika shaka juu yake (hii Qur-aan) inayowatia wasiwasi.
وَإِنَّ كُلًّا لَّمَّا لَيُوَفِّيَنَّهُمْ رَبُّكَ أَعْمَالَهُمْ ۚإِنَّهُ بِمَا يَعْمَلُونَ خَبِيرٌ﴿١١١﴾
111. Na hakika wote Rabb wako Atawalipa kikamilifu ‘amali zao. Hakika Yeye kwa yale wayatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.
فَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ وَمَن تَابَ مَعَكَ وَلَا تَطْغَوْا ۚ إِنَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَبَصِيرٌ﴿١١٢﴾
112. Basi thibitika imara kama ulivyoamrishwa na aliyetubia pamoja nawe, na wala msiruke mipaka. Hakika Yeye kwa myatendayo ni Mwenye kuona.
وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ﴿١١٣﴾
113. Na wala msielemee kwa wale waliodhulumu utakuguseni moto, na hamtokuwa na walinzi badala ya Allaah, kisha hamtonusuriwa.
وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ﴿١١٤﴾
114. Na simamisha Swalaah katika ncha mbili za mchana na sehemu ya kwanza ya usiku; hakika mema yanaondosha maovu. Hivyo ni ukumbusho kwa wanaokumbuka.
وَاصْبِرْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَالْمُحْسِنِينَ﴿١١٥﴾
115. Na vuta subira kwani hakika Allaah Hapotezi ujira wa wafanyao ihsaan.
فَلَوْلَا كَانَ مِنَ الْقُرُونِ مِن قَبْلِكُمْ أُولُو بَقِيَّةٍ يَنْهَوْنَ عَنِ الْفَسَادِ فِي الْأَرْضِ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّنْ أَنجَيْنَا مِنْهُمْ ۗوَاتَّبَعَ الَّذِينَ ظَلَمُوا مَا أُتْرِفُوا فِيهِ وَكَانُوا مُجْرِمِينَ﴿١١٦﴾
116. Basi kwanini hawakuweko katika karne za kabla yenu, walio weledi na wasaa wanakataza ufisadi katika ardhi isipokuwa wachache kati ya Tuliowaokoa miongoni mwao? Na wale waliodhulumu wakafuata anasa walizostareheshwa nazo na wakawa wakhalifu.
وَمَا كَانَ رَبُّكَ لِيُهْلِكَ الْقُرَىٰ بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا مُصْلِحُونَ﴿١١٧﴾
117. Na Rabb wako hakuwa Mwenye kuangamiza miji kwa dhulma na hali watu wake ni wenye kutengenea.
وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ لَجَعَلَ النَّاسَ أُمَّةً وَاحِدَةً ۖ وَلَا يَزَالُونَ مُخْتَلِفِينَ﴿١١٨﴾
118. Na kama Angetaka Rabb wako, basi Angejaalia watu wote kuwa ni ummah mmoja. Na hawatoacha kukhitilafiana.
إِلَّا مَن رَّحِمَ رَبُّكَ ۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمْ ۗوَتَمَّتْ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ﴿١١٩﴾
119. Isipokuwa yule Aliyemrehemu Rabb wako. Na kwa hivyo ndivyo Amewaumba. Na limetimia neno la Rabb wako (kwamba): “Bila shaka Nitajaza Jahannam kwa majini na watu wote pamoja.”
وَكُلًّا نَّقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنبَاءِ الرُّسُلِ مَا نُثَبِّتُ بِهِ فُؤَادَكَ ۚ وَجَاءَكَ فِي هَـٰذِهِ الْحَقُّ وَمَوْعِظَةٌ وَذِكْرَىٰلِلْمُؤْمِنِينَ﴿١٢٠﴾
120. Na yote Tunayokusimulia katika khabari muhimuu za Rusuli, Tunathibitisha kwazo moyo wako. Na imekujia katika hii haki na mawaidha na ukumbusho kwa Waumini.
وَقُل لِّلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنَّا عَامِلُونَ﴿١٢١﴾
121. Na waambie wale wasioamini: “Tendeni kwa tamkini zenu, nasi pia tunatenda.”
وَانتَظِرُوا إِنَّا مُنتَظِرُونَ﴿١٢٢﴾
122. Na ngojeeni, nasi tunangojea.”
وَلِلَّـهِ غَيْبُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَإِلَيْهِ يُرْجَعُ الْأَمْرُ كُلُّهُ فَاعْبُدْهُ وَتَوَكَّلْ عَلَيْهِۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ﴿١٢٣﴾
123. Na ni ya Allaah (Pekee) ghayb ya mbingu na ardhi, na Kwake hurudishwa mambo yote; basi mwabudu Yeye na tawakali Kwake. Na Rabb wako si Mwenye kughafilika na yale myatendayo.
[1] Faida: Mahali pa kustakiri ni tumboni mwa mama au duniani. Mahali pa kuhifadhiwa ni ima migongoni mwa baba au kaburini.