Coca-cola Kuja Na Simu Janja Yao!
https://teknolojia.co.tz/coca-cola-kuja-na-simu-janja-yao/?utm_source=rss&utm_medium=rss&utm_campaign=coca-cola-kuja-na-simu-ja
Tumeshaona simu tofauti tofauti ambazo zinakujaga kubeba chapa fulani kwa muda na huo kunakua na matoleo maalamu, mfano
TECNO – (Tecno Camon CX) Toleo La Manchester City
SAMSUNG – (Galaxy Z Flip 4) Toleo la Maison Margiela
OPPO – (Oppo Reno 10X Zoom) Toleo la Barcelona
N.k
Na matoleo mengine mengi tuu ambayo makampuni mengi huwa yanatoa, kwa haraka haraka ni kwamba matoleo haya huwa tayari yapo katika soko na kampuni nyingine huwa inakuja kuweka chapa (brand) yake tuu.
SOMA PIA WhatsApp kuja na muonekano wa giza
Huwa ni vigumu kabisa kwa kampuni ambayo haijihusishi kabisa katika soko la simu kuja kusikia kuwa imezindua simu yake.
Pengine hili linakuja kubadilishwa na Coca-cola, maana wako mbioni katika kuzalisha simu yao ya kwanza kabisa.
Lakini hata hivyo hili sio la kushangaza sana maana hata miaka kadhaa iliyopita Pepsi nao waliachiwa simu janja mbili Yaani Pepsi P1 na Pepsi P1s japo simu hizi zilikua kwa ajili ya soko la china. Soma zaidi >>HAPA<<
SOMA PIA YouTube ya kwenye Android na iOS yaboreshwa
Kwa sasa swala hili limetoka kama fununu lakini viashiria vyote vinaonyesha kwamba sio siri tena jambo hili linaenda kufanyika.
Ushahidi kama akaunti ya Twitter ya simu janja hiyo kutoka Coca-cola imefunguliwa na inaitwa @colaphoneglobal lakini vile vile usishangae simu hii nayo ikawa ni kama zile zinazobeba chapa (brand) tuu.
Yaani pengine coca-cola hawatakaa chini na kuanza kutengeneza simu hii kutoka mwanzo hadi mwisho.
Kwa sasa kuna picha inayosambaa katika mtandao huku ikiwa inayonyesha upande wa nyuma –muonekano wa kamera – bila kuonyesha upande wa mbele wa simu hiyo.
SOMA PIA Sony Xperia 1: Simu yenye upekee wa aina yake
Kwa sasa hakuna taarifa zozote za undani juu ya simu janja hii na hata bei haipo wazi lakini vyanzo mbalimbali vinadai kuwa itakua ni moja kati ya zile simu janja ambazo haina gharama kubwa
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je uko tayari kuanza kutumia simu yenye chapa la soda ya Coca-cola?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
