CHAKULA CHA MTOTO
Dr.Mansura M. MtiboraKwanza inabidi tuelewe kuwa mtoto akifikisha miezi sita anatakiwa kuanzishiwa chakula kwani tumbo lake linakua tayari kupokea aina nyingine ya chakula ukiacha mbali na maziwa ya mama pili mtoto anakua hawezi kushiba tena maziwa tu ya mama hata ungemnyonyesha siku nzima bila kupumzika.

Hivyo ni muhimu kupata ndondoo muhimu kuhusu hatua hii ya ukuaji wa mtoto kwani wengi huishia kupata utapiamlo kwa sababu mbalimbali katika uandaji,aina au hata idadi ya mlo wa chakula cha mtoto.
yafuatayo ukiyazingati yatasadia kuimarisha afya ya mwanao
1.Chakula cha mtoto kinatakiwa kuandaliwa kuhifadhiwa na mpaka anapokula katika mazingira yenye usafi wa hali ya juu
2.Usimuachishe mtoto maziwa yako mara tu atakapoanza kula endelea kumnyonyesha

3.Chakula cha mtoto ni lazima kiwe kamili kwa kuwa na aina za vyakula kama protein ,wanga ,mafuta nani vitamini
4.Kama mwanao anakunywa uji basi usimchamganyie nafaka zaidi ya moja kwenye unga wake bali unaweza kuweka makundi yote ya vyakula kama protein (maziwa) mafuta(blueband), vitamini (karoti)

5.Uji uchemke vizuri kuepuka kutoiva hasa kama unga wake una mchanganyiko wa ulezi,ngano nk
6.Muanzishie mtoto chakula kimoja baada y kingine ili ujue kipi hapendi sana au kinachomletea madhara ukichamganya sana hutoweza kujia kipi kimemdhuru kwa muda huo.
7.Usimlazimishe chakula mtoto mpe kidogo kidogo kwa mara nyingi akikataa kabisa badili aina ya chakula unachompa
8. Maji ni muhimu pia kwa mtoto kama ilivo kwa mtu mzima usisahau kumpa maji mwanao kila siku.

9.Watu wengi wamekuwa wakisahau sana mboga za majani kwa watoto jitahidi kumpa mboga za majani mwanao.
10.Weka ratiba nzuri itakayowezesha mwanao kupata uwiano sahihi wa chakula chake mfano asubuhi anaweza kunywa uji baada ya saa mbili akanyonya baadae akalala akaamka akapewa chakula baada ya saa mbili ukampa juisi nk ipange upendavo la msingi ni kijitahidi ale kidogo lakini chenye faida.
