App Bora Kwa Ajili Ya Ku'Edit Picha (#Android #iPhone) #2021!

App Bora Kwa Ajili Ya Ku'Edit Picha (#Android #iPhone) #2021!

Source

Sasa ni App gani ambazo inaidi uzitumie ili kukuwezesha kufanya hili? App ziko nyingi, kuna zile ambazo zinauzwa na kuna zile za bure kabisa…… ni wazi kuwa wengi wetu tunapenda zile za bure sio?


Leo TeknoKona inakuletea listi ya App hizo ambazo unaweza ukatumia kwenye masuala ya picha zako.



  • App Ya Snapseed



Android | iPhone


Hii ni moja kati ya App bora kabisa ambayo nimeshawahi kuitimia katika swala zima la kuhariri picha, App hii ina vipengele vingi ambavyo kwa namna moja au nyingine vitakuhakikishia kuwa unapata picha kali kabisa.


Snapseed inamilikiwa na Google, ndani unaweza ukapata vipengele kama HDR na filter’ zingine za kutosha, rangi n.k… kingine kikubwa ni kwamba ni ya bureeeeeeeeeeee!



  • App Ya Lightroom



Android | iPhone


Sasa hii baadhi ya vipengele unaweza ukavipata bure lakini ukitaka kupata mzigo mzima huna budi kuongeza dola 5 za kimarekani kwa mwezi.


Kama ulishawahi kuona au kutumia Adobe Lightroom katika PC basi hii ni App yake ya simu.. humu utapata kutumia vitu vingi kama mtaalamu na haya yote yatakufanya mwisho wa siku utoke na picha kali sana!


Vitu kama emoji na stika zingine sio kabisa vya kuvitegemea humu lakini mambo mengine mengi tuu unaweza kuyapata, kingnie cha kuvutia ni kwamba unaweza ukaanza ku’edit kwenye kifaa kimoja na ukamalizia kwenye kingine kwa kuwa picha zinaweza kujuhifadhi kwenye hifadhi yake ya kimtandao (Cloud)



  • App Ya Adobe Photoshop Express



Android | iPhone


Hii haina tofauti kubwa sana na Lightroom lakini kuna tofauti kidogo, vipengele kama hifadhi ya kimtandao (cloud) huwezi kuvipata humu.


Adobe Photoshop Express haina mambo mengi kabisa, ni moja kati ya App ambazo ni rahisi kabisa kutumia ukiwa unahariri picha zako. Hii pia inapatakana katika masoko ya android (PlayStore) na iphone (AppStore) bure kabisa



  • App Ya VSCO



Android | iPhone


Baadhi ya vipengele ni bure kabisa ila ukitaka kupata mzigo  wote inagharimu dola 20 kwa mwaka. App hii naweza sema imejikita sana katika swala zima la mionekano (presets) katika picha


Mambo kama Filter na aina nyingine ya mionekano kama vile ‘black and white’ utaipata ya kutosha kabisa. Ijaribu kuitumia kapokua imekaa kitaalamu zaidi kama vile lightroom



  • App Ya PicsArt



Android | iPhone


Na hii pia ina vipengele vingi vya bure lakini pia ukitaka kupata mzigo wote  kwa dola 48 kwa mwaka. App hii inakupa vipengele vingi vya  kucheza  navyo katika picha zako.


PicsArt pia ni mtandao wa kijamii kama vile Instagram, kwamba unaweza piga picha, ukai’edit’ na kui’share katika mtandao huo.


Ningependa kusikia kutoka kwako, wewe umeshawahi kutumia ipi hapa? na unadhani ni ipi bora? niandikie hapoa chini katika eneo la maoni.


Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.


SOMA PIA  Google: Apps kwenye Google Play Store kuchelewa kupewa ruhusa

Report Page