034 KUIREFUSHA RUKUU  

034 KUIREFUSHA RUKUU  

i live islam


Alikuwa   (صلى الله عليه وآله وسلم) akifanya rukuu yake, kisimamo chake baada ya rukuu, na sujuud yake na kikao baina sajda mbili, karibu sawa kwa urefu.([1])

 

 

 

KUKATAZWA KUSOMA QUR-AAN KATIKA RUKUU

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)  akikataza kusoma Qur-aan katika rukuu na sujuud.([2])

 

Alikuwa akisema: ((Hakika mimi nimekatazwa kusoma Qur-aan hali ya kuwa nimerukuu au nimesujudu. Hivyo basi katika rukuu mtukuzeni Mola (عزوجل), na (ama) katika sujuud, jitahidini kwa du'aa, kwani ni karibu kukubaliwa humo)).([3])

 

 





[1] Al-Bukhaariy na Muslim. Imetolewa katika IrwaaAl-Ghaliyl (331).      

[2] Muslim na Abu 'Awaanah. Makatazo ni ya ujumla, hivyo inahusisha Swalah za Faradhi na Sunnah. Ziada ya Ibn 'Asaakir (17/299/1): "Ama Swalah za Sunnah, hakuna ubaya", ni (aidha) shaadhah au munkar. Ibn 'Asaakir ameashiria dosari humo, hivyo haijuzu kufanyiwa kazi.

[3] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

   

Report Page