031 KUMSAHIHISHA IMAAM

031 KUMSAHIHISHA IMAAM

i live islam


 

Ametoa  (صلى الله عليه وآله وسلم)mfano katika kumsahihisha Imaam anapobabaika au anapochanganyikiwa na kisomo chake. Mara moja aliswali, akasoma ndani yake kisomo, akasahau. Alipomaliza alimwambia Ubayy: ((Uliswali na sisi?)). Alijibu: "Ndio". Akasema: ((Hivyo nini kilichokuzuia [kunisahihisha]?))([1]).

 

 

 

KUJIKINGA NA SHAYTWAAN NA KUTEMA MATE KIDOGO WAKATI WA SWALAH ILI KUONDOSHA WASIWASI

 

'Uthmaan bin Abil-Aasw (رضي الله عنه) alimwambia: "Ewe Mjumbe wa Allaah! Shaytwaan ameingia baina yangu na baina ya Swalah yangu na kisomo changu, ananibabaisha katika kisomo changu!" Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)akasema: ((Huyo ni Shaytwaan anayeitwa Khinzab, hivyo utakapomuhisi jikinge kwa Allaah naye, na tema mate kidogo([2]) upande wa kushoto kwako mara tatu)). Akasema: "Nikafanya hivyo, na Allaah Akamuondoshelea mbali nami".([3]).

 

 





[1] Abu Daawuud, Ibn Hibbaan, Atw-Twabaraaniy, Ibn 'Asaakir (2/296/2) na Adhw-Dhwiyaa katika Al-Mukhtaarah kwa isnaad Swahiyh.

[2] "At-Tafl" ni mpulizo ikiwa na mate kidogo, hivyo ni zaidi ya kupuliza.  (An-Nihaayah).

[3] Muslim na Ahmad. An-Nawawiy (رحمه الله) amesema: "Hadiyth hii ina mapendekezo ya kujikinga na Shaytwaan anaposhawishi, pamoja na kutema mate upande wa kushoto mara tatu".

 

Report Page