002-Kutoa Zakaah: Utangulizi

002-Kutoa Zakaah: Utangulizi

i love islam ๐Ÿ•‹

ย 

Utangulizi

ย 

Kutoa Zakaah ni nguzo ya tatu ya Islam. Mtume (Swalla Allaahu โ€˜alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

"Nguzo za Uislam ni tano. Shahada kuwa hapana muabudiwa wa haki ila Allaah, na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaahu, na Kusimaamisha Swalaah, na Kutoa Zakaah, na Kufunga mwezi wa Ramadhwaan na Kuhiji Makkah kwa mwenye uwezo wa kufika huko".

ย 

Kufaridhishwa kwa Zakaah ni jambo muhimu na tukufu sana kwa Waislam kwa sababu ya wingi wa faida yake na kwa ajili ya haja kubwa ya kuwepo kwa jambo hilo, kutokana na masikini na mafakiri wanaohitajia sana msaada wa ndugu zao wenye uwezo, kwani katika Kutoa Zakaah uhusiano mzuri unajengeka baina ya Waislam matajiri na Waislam masikini, na hii ni kwa sababu siku zote moyo wa mtu huelekea na kumpenda yule anayemfanyia wema na ihsani. Zakaah inasaidia pia katika kuzisafisha na kuzitakasa nyoyo.

Allaahย Anasema:

ุฎูุฐู’ ู…ูู†ู’ ุฃูŽู…ู’ูˆูŽุงู„ูู‡ูู…ู’ ุตูŽุฏูŽู‚ูŽุฉู‹ ุชูุทูŽู‡ู‘ูุฑูู‡ูู…ู’ ูˆูŽุชูุฒูŽูƒู‘ููŠู‡ูู… ุจูู‡ูŽุง

"Chukuwa Swadaqah katika mali zao, uwasafishe na kuwatakasa kwa ajili ya hizo (Swadaqah zao)".

[At-Tawbah: 103]

ย 

Katika kutoa Zakaah au Swadaqah kunaizoesha nafsi katika kuwapendelea kheri watu wenye haja na katika kuwaonea huruma na pia kunaipatia nafsi baraka nyingi kutoka kwa Allaahu Subhanaahu wa Taโ€™ala.

Allaahย Anasema:

ูˆูŽู…ูŽุง ุฃูŽู†ููŽู‚ู’ุชูู… ู…ู‘ูู† ุดูŽูŠู’ุกู ููŽู‡ููˆูŽ ูŠูุฎู’ู„ูููู‡ู ูˆูŽู‡ููˆูŽ ุฎูŽูŠู’ุฑู ุงู„ุฑู‘ูŽุงุฒูู‚ููŠู†ูŽ

"Na chochote mtakachotoa, basi Yeye Atakilipa; naye ni Mbora wa wanaoruzuku".

Saba-a - 39

ย 

Na Mtume (Swalla Allaahu โ€˜alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

"Allaahu Anasema:ย 'Ewe mwana Aadam, toa na sisi tutakupa"

ย 

Anasema Ibn Uthaymiyn:

"Kutoa Zakaah ni jambo liliofaradhishwa katika Uislam, na ni nguzo muhimu sana baada ya Shahada mbili na Swalaah, na dalili ya kuwajibika kwake imo ndani ya Qur-aan na pia katika mafundisho ya Mtume (Swalla Allaahu โ€˜alayhi wa aalihi wa sallam), pamoja na ijmai ya Waislam, na yeyote anayeikanusha nguzo hii anakuwa Kafir aliyertadi katika Uislam, na hukumu yake ni kutubishwa, na akitubu anasamehewa. Ama akikataa kutubu na akaendelea kuikanusha basi hukmu yake ni kuuliwa.

Ama anayeifanyia ubakhili au akapunguza katika Zakaah yake, huyo anakuwa miongoni mwa madhalimu wanaostahiki adhabu ya Allaahu.

ย 

Allaahu Anasema:

ูˆูŽุงู„ู‘ูŽุฐููŠู†ูŽ ูŠูŽูƒู’ู†ูุฒููˆู†ูŽ ุงู„ุฐู‘ูŽู‡ูŽุจูŽ ูˆูŽุงู„ู’ููุถู‘ูŽุฉูŽ ูˆูŽู„ุงูŽ ูŠูู†ููู‚ููˆู†ูŽู‡ูŽุง ูููŠ ุณูŽุจููŠู„ู ุงู„ู„ู‘ู‡ู ููŽุจูŽุดู‘ูุฑู’ู‡ูู… ุจูุนูŽุฐูŽุงุจู ุฃูŽู„ููŠู…ู. ูŠูŽูˆู’ู…ูŽ ูŠูุญู’ู…ูŽู‰ ุนูŽู„ูŽูŠู’ู‡ูŽุง ูููŠ ู†ูŽุงุฑู ุฌูŽู‡ูŽู†ู‘ูŽู…ูŽ ููŽุชููƒู’ูˆูŽู‰ ุจูู‡ูŽุง ุฌูุจูŽุงู‡ูู‡ูู…ู’ ูˆูŽุฌูู†ูˆุจูู‡ูู…ู’ ูˆูŽุธูู‡ููˆุฑูู‡ูู…ู’ ู‡ูŽู€ุฐูŽุง ู…ูŽุง ูƒูŽู†ูŽุฒู’ุชูู…ู’ ู„ุฃูŽู†ููุณููƒูู…ู’ ููŽุฐููˆู‚ููˆุงู’ ู…ูŽุง ูƒูู†ุชูู…ู’ ุชูŽูƒู’ู†ูุฒููˆู†ูŽ

"Na wale wakusanyao dhahabu na fedha wala hawazitoi katika njia ya Allaahu, wape habari za adhabu inyoumiza inayowangoja.

Siku (mali yao) yatakapotiwa moto katika moto wa Jahanamu, na kwa hayo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, (na huku wanaambia); "Haya ndiyo (yale mali) mliyojilimbikia (mliyojikusanyia) nafsi zenu, basi onjeni (adhabu ya) yale mliyokuwa mkikusanya."

[At-Tawbah - 34 - 35]

ย 

"Miongoni mwa faida za kutoa Zakaah anazozipata mtu katika dini yake"ย anaendelea kusema Shaykh Ibn โ€˜Uthaymiyn (Rahimahu Allaah),ย "Ni kuitimiza nguzo katika nguzo za Kiislam, jambo litakalomletea mtu furaha katika dunia yake na katika akhera yake, na pia inazidi kumkaribisha mja kwa Mola wake na kumuongezea Imani, kama ilivyo katika mambo yote ya kumtii Allaahu Subhanaahu wa Taโ€™ala."

ย 

ย 

Report Page