002 - Al-Baqarah

002 - Al-Baqarah


 

الْبَقَرَة

Al-Baqarah: 2 [1]

 

Imeteremka Madiynah, hakuna khilafu katika kauli hii.

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

 الم ﴿١﴾

1. Alif Laam Miym.[2]

 

 

ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٢﴾

2. Hiki ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake, ni mwongozo kwa wenye taqwa.[3]

 

 

 

الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٣﴾

3. Ambao huamini ya ghayb na husimamisha Swalaah na katika vile Tulivyowaruzuku hutoa.[4]

 

 

وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ وَبِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ ﴿٤﴾

4. Na ambao huamini yaliyoteremshwa kwako (ee Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako na ni wenye yakini na Aakhirah.

 

 

 أُولَـٰئِكَ عَلَىٰ هُدًى مِّن رَّبِّهِمْ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٥﴾

5. Hao wako juu ya mwongozo kutoka kwa Rabb wao, na hao ndio wenye kufaulu.

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا سَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٦﴾

6. Hakika wale waliokufuru ni sawa kwao, ukiwaonya au usiwaonye wao hawatoamini.

 

 

خَتَمَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَعَلَىٰ سَمْعِهِمْ ۖ وَعَلَىٰ أَبْصَارِهِمْ غِشَاوَةٌ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿٧﴾

7. Allaah Amepiga mhuri juu ya nyoyo zao, na juu ya masikio yao; na juu ya macho yao pana kifuniko; na watapata adhabu kuu.

 

 

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ ﴿٨﴾ 

8. Na miongoni mwa watu wako wasemao: ”Tumemuamini Allaah na Siku ya Mwisho” hali ya kuwa si wenye kuamini.

 

 

يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَمَا يَخْدَعُونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿٩﴾

9. (Wanadhani) Wanamhadaa Allaah na wale walioamini lakini hawahadai ila nafsi zao na wala hawahisi.

 

 

فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّـهُ مَرَضًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ ﴿١٠﴾

10. Ndani ya nyoyo zao mna maradhi na Allaah Akawazidishia maradhi, na watapata adhabu iumizayo kwa waliyokuwa wakiyakadhibisha.

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ قَالُوا إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ ﴿١١﴾

11. Na wanapoambiwa: “Msifanye ufisadi katika ardhi.” Husema: “Hakika sisi ni watengenezaji.”

 

 أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَلَـٰكِن لَّا يَشْعُرُونَ ﴿١٢﴾

12. Tanabahi! Hakika wao ndio mafisadi lakini hawahisi.

 

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُوا كَمَا آمَنَ النَّاسُ قَالُوا أَنُؤْمِنُ كَمَا آمَنَ السُّفَهَاءُ ۗ أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ السُّفَهَاءُ وَلَـٰكِن لَّا يَعْلَمُونَ ﴿١٣﴾

13. Na wanapoambiwa: “Aminini kama walivyoamini watu.” Husema: “Je, tuamini kama walivyoamini wapumbavu.” Tanabahi! Hakika wao ndio wapumbavu lakini hawajui.

 

 

 وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَوْا إِلَىٰ شَيَاطِينِهِمْ قَالُوا إِنَّا مَعَكُمْ إِنَّمَا نَحْنُ مُسْتَهْزِئُونَ ﴿١٤﴾

14. Na wanapokutana na wale walioamini husema: “Tumeamini.” Na wanapokuwa peke yao pamoja na mashaytwaan wao, husema: “Hakika sisi tuko pamoja nanyi, hakika sisi ni wenye kuwadhihaki tu.”

 

 

 اللَّـهُ يَسْتَهْزِئُ بِهِمْ وَيَمُدُّهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿١٥﴾

15. Allaah Anawadhihaki wao na Atawaendeleza katika hali yao ya upindukiaji mipaka wa kuasi, wakitangatanga kwa upofu.

 

 

 أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الضَّلَالَةَ بِالْهُدَىٰ فَمَا رَبِحَت تِّجَارَتُهُمْ وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ ﴿١٦﴾

16. Hao ndio wale waliobadilisha upotofu badala ya uongofu, basi haikupata faida biashara yao na wala hawakuwa wenye kuongoka.

 

 

مَثَلُهُمْ كَمَثَلِ الَّذِي اسْتَوْقَدَ نَارًا فَلَمَّا أَضَاءَتْ مَا حَوْلَهُ ذَهَبَ اللَّـهُ بِنُورِهِمْ وَتَرَكَهُمْ فِي ظُلُمَاتٍ لَّا يُبْصِرُونَ ﴿١٧﴾

17. Mfano wao ni kama mfano wa aliyekoka moto, ulipoyaangaza yaliyopo pembezoni mwake Allaah Akawaondoshea nuru yao na Akawaacha katika viza; hawaoni.

 

صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَرْجِعُونَ ﴿١٨﴾

18. Viziwi, mabubu, vipofu basi hawatorejea.

 

 

 أَوْ كَصَيِّبٍ مِّنَ السَّمَاءِ فِيهِ ظُلُمَاتٌ وَرَعْدٌ وَبَرْقٌ يَجْعَلُونَ أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِم مِّنَ الصَّوَاعِقِ حَذَرَ الْمَوْتِ ۚ وَاللَّـهُ مُحِيطٌ بِالْكَافِرِينَ ﴿١٩﴾

19. Au ni kama mvua kubwa kutoka mbinguni, ndani yake mna viza na radi na umeme, wanatia vidole vyao katika masikio yao kutokana na mingurumo wakikhofu mauti, na Allaah ni Mwenye kuwazunguka makafiri.  

 

 

يَكَادُ الْبَرْقُ يَخْطَفُ أَبْصَارَهُمْ ۖ كُلَّمَا أَضَاءَ لَهُم مَّشَوْا فِيهِ وَإِذَا أَظْلَمَ عَلَيْهِمْ قَامُوا ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَذَهَبَ بِسَمْعِهِمْ وَأَبْصَارِهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٠﴾

20. Unakaribia umeme kunyakua macho yao, kila unapowaangazia (njia) hutembea humo, na unapowafanyia kiza husimama; na lau Allaah Angelitaka basi Angeliwaondoshea kusikia kwao na kuona kwao. Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Muweza.

 

 

 يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿٢١﴾

21. Enyi watu! Mwabuduni Rabb wenu Ambaye Amekuumbeni na wale wa kabla yenu mpate kuwa na taqwa.

 

 

الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٢﴾

22. Ambaye Amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa, na Akateremsha kutoka mbinguni maji, Akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye na hali ya kuwa nyinyi mnajua.

 

 

 وَإِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّن مِّثْلِهِ وَادْعُوا شُهَدَاءَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٢٣﴾

23. Na ikiwa mko katika shaka kutokana na Tuliyoyateremsha juu ya mja Wetu (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi leteni Suwrah mfano wake, na waiteni mashahidi wenu pasipo na Allaah mkiwa ni wakweli. 

 

 

فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا وَلَن تَفْعَلُوا فَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ ۖ أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ ﴿٢٤﴾

24. Msipofanya, na wala hamtoweza kufanya, basi ogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe, umeandaliwa kwa makafiri.

 

 

وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ كُلَّمَا رُزِقُوا مِنْهَا مِن ثَمَرَةٍ رِّزْقًا ۙ قَالُوا هَـٰذَا الَّذِي رُزِقْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَأُتُوا بِهِ مُتَشَابِهًا ۖ وَلَهُمْ فِيهَا أَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ ۖ وَهُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٥﴾

25. Na wabashirie wale walioamini na wakatenda mema kwamba watapata Jannaat zipitazo chini yake mito, kila watakaporuzukiwa humo katika matunda kuwa ni riziki husema: “Haya ndiyo yale tuliyoruzukiwa kabla.” Na wataletewa hali ya kuwa yanashabihiana, na watapata humo wake waliotakaswa, nao humo ni wenye kudumu.

 

 

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَسْتَحْيِي أَن يَضْرِبَ مَثَلًا مَّا بَعُوضَةً فَمَا فَوْقَهَا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۖ وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَيَقُولُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۘ يُضِلُّ بِهِ كَثِيرًا وَيَهْدِي بِهِ كَثِيرًا ۚ وَمَا يُضِلُّ بِهِ إِلَّا الْفَاسِقِينَ ﴿٢٦﴾

26. Hakika Allaah Haoni hayaa kupiga mfano wa mbu na ulio zaidi yake (kwa udogo). Basi wale walioamini wanajua kwamba hiyo ni haki kutoka kwa Rabb wao; ama wale waliokufuru husema: “Anataka nini Allaah kwa mfano huu?” Kwa (mfano) huo, Huwapoteza wengi na Huwaongoza kwayo wengi na wala Hawapotezi kwavyo ila mafasiki.

 

 

الَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٢٧﴾

27. Wale wanaovunja ahadi ya Allaah baada ya kuifunga Kwake na wanakata Aliyoyaamrisha Allaah kuungwa, na wanafanya ufisadi katika ardhi, hao ndio wenye khasara.

 

 

 كَيْفَ تَكْفُرُونَ بِاللَّـهِ وَكُنتُمْ أَمْوَاتًا فَأَحْيَاكُمْ ۖ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٢٨﴾

28. Vipi mnamkufuru Allaah na hali mlikuwa wafu Akakuhuisheni, kisha Atakufisheni, kisha Atakuhuisheni, kisha Kwake mtarejeshwa?

 

 

هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ فَسَوَّاهُنَّ سَبْع سَمَاوَاتٍ ۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٩﴾ 

29. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbieni vyote vilivyomo ardhini Kisha Akazielekea (Istawaa[5]) mbingu na Akazifanya timilifu mbingu saba, Naye kwa kila kitu ni Mjuzi.

 

 

 وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ۖ قَالُوا أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۖ قَالَ إِنِّي أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٣٠﴾

30. Na pindi Rabb wako Alipowaambia Malaika: “Hakika Mimi Nitaweka katika ardhi khalifa.” Wakasema: “Utaweka humo atakayefanya ufisadi humo na kumwaga damu, na hali sisi tunakusabihi kwa Himidi Zako na tunakutukuza kwa Utakatifu Wako?” (Allaah) Akasema: “Hakika Mimi Nayajua zaidi msiyoyajua.”

 

 

وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلَى الْمَلَائِكَةِ فَقَالَ أَنبِئُونِي بِأَسْمَاءِ هَـٰؤُلَاءِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٣١﴾

31. Na Akamfunza Aadam majina yote (ya kila kitu), kisha Akavionesha mbele ya Malaika; Akasema: “Niambieni majina ya hivi mkiwa ni wakweli.”

 

 

قَالُوا سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَا إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ ﴿٣٢﴾

32. Wakasema: Utakasifu ni Wako hatuna elimu isipokuwa Uliyotufunza; hakika Wewe Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

 قَالَ يَا آدَمُ أَنبِئْهُم بِأَسْمَائِهِمْ ۖ فَلَمَّا أَنبَأَهُم بِأَسْمَائِهِمْ قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ إِنِّي أَعْلَمُ غَيْبَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَأَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ ﴿٣٣﴾

33. Akasema: “Ee Aadam, wajulishe kwa majina yao.” Basi alipowatajia majina yao; (Allaah) Akasema: “Je, Sikuwaambieni kuwa hakika Mimi Najua ghayb ya mbingu na ardhi na Najua mnayoyadhihirisha na mliyokuwa mkiyaficha.

 

 

وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ وَاسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ ﴿٣٤﴾

34. Na pale Tulipowaambia Malaika: “Msujudieni Aadam.” Wakasujudu isipokuwa Ibliys alikataa na akatakabari na akawa miongoni mwa makafiri.

 

 

 وَقُلْنَا يَا آدَمُ اسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ وَكُلَا مِنْهَا رَغَدًا حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَـٰذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٣٥﴾

35. Na Tukasema: “Ee Aadam, kaa wewe na mkeo (Hawaa) Jannah na kuleni humo maridhawa popote mpendapo na wala msiukaribie mti huu; mtakuwa miongoni mwa madhalimu.”

 

 

فَأَزَلَّهُمَا الشَّيْطَانُ عَنْهَا فَأَخْرَجَهُمَا مِمَّا كَانَا فِيهِ ۖ وَقُلْنَا اهْبِطُوا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ وَلَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ ﴿٣٦﴾

36. Shaytwaan akawatelezesha wote wawili kwayo, Akawatoa kutoka katika hali waliyokuwa nayo. Tukasema: “Shukeni mkiwa maadui nyinyi kwa nyinyi, na mtapata katika ardhi makazi na starehe hadi muda maalum.”

 

 

 فَتَلَقَّىٰ آدَمُ مِن رَّبِّهِ كَلِمَاتٍ فَتَابَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿٣٧﴾

37. Kisha Aadam akapokea maneno kutoka kwa Rabb wake; na (Rabb wake) Akapokea tawbah yake, hakika Yeye Ndiye Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu.

 

 

قُلْنَا اهْبِطُوا مِنْهَا جَمِيعًا ۖ فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَن تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٣٨﴾

38. Tukasema: “Shukeni kutoka humo nyote. Utakapokufikieni kutoka Kwangu mwongozo basi yeyote atakayefuata mwongozo Wangu hakutokuwa na khofu juu yao wala hawatohuzunika.”

 

 

وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٣٩﴾

39. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat (ishara, dalili) Zetu hao ni watu wa motoni, wao humo ni wenye kudumu.

 

 

يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَوْفُوا بِعَهْدِي أُوفِ بِعَهْدِكُمْ وَإِيَّايَ فَارْهَبُونِ ﴿٤٠﴾

40. Enyi wana wa Israaiyl! Kumbukeni neema Yangu Niliyokuneemesheni na timizeni ahadi Yangu Nikutimizieni ahadi yenu na Mimi Pekee niogopeni.

 

 

وَآمِنُوا بِمَا أَنزَلْتُ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَكُمْ وَلَا تَكُونُوا أَوَّلَ كَافِرٍ بِهِ ۖ وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا وَإِيَّايَ فَاتَّقُونِ ﴿٤١﴾

41. Na aminini yale Niliyoyateremsha yenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nanyi, na wala msiwe wa kwanza wenye kuzikanusha; na wala msibadilishe Aayaat Zangu kwa thamani ndogo na muwe na taqwa kunikhofu Mimi tu.

 

 

وَلَا تَلْبِسُوا الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُوا الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٤٢﴾

42. Na wala msichanganye haki kwa batili na mkaficha haki; na hali mnajua.

 

 

وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَارْكَعُوا مَعَ الرَّاكِعِينَ ﴿٤٣﴾

43. Na simamisheni Swalaah na toeni Zakaah na rukuuni pamoja na wanaorukuu (katika utiifu).

 

 

أَتَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبِرِّ وَتَنسَوْنَ أَنفُسَكُمْ وَأَنتُمْ تَتْلُونَ الْكِتَابَ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٤٤﴾ 

44. Je, mnaamrisha watu watende mema na mnajisahu nafsi zenu na hali ya kuwa nyinyi mnasoma Kitabu; je hamtii akilini? 

 

 

وَاسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى الْخَاشِعِينَ ﴿٤٥﴾

45. Na tafuteni msaada kupitia subira na Swalaah; na hakika hilo ni kubwa isipokuwa kwa wanyenyekevu.

 

 

الَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَاقُو رَبِّهِمْ وَأَنَّهُمْ إِلَيْهِ رَاجِعُونَ ﴿٤٦﴾

46. Ambao wana yakini kwamba hakika wao ni wenye kukutana na Rabb wao na hakika wao Kwake ni wenye kurejea.

 

 

يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٤٧﴾

47. Enyi wana wa Israaiyl! Kumbukeni neema Yangu Niliyokuneemesheni na hakika Mimi Nimekufadhilisheni juu ya walimwengu wote.[6]

 

 

وَاتَّقُوا يَوْمًا لَّا تَجْزِي نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا شَفَاعَةٌ وَلَا يُؤْخَذُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿٤٨﴾ 

48. Na iogopeni Siku ambayo nafsi haitoifaa nafsi nyingine kwa kitu chochote kile, na wala haitokubaliwa kutoka kwake uombezi wowote na wala hakitochukuliwa kutoka kwake kikomboleo, na wala hawatonusuriwa.

 

 

وَإِذْ نَجَّيْنَاكُم مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ يُذَبِّحُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ ۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَاءٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ ﴿٤٩﴾

49. Na pindi Tulipokuokoeni kutoka kwa watu wa Fir’awn walipokusibuni adhabu mbaya, wakiwachinja watoto wenu wa kiume na wakiacha hai wanawake wenu, na katika hayo kwenu ulikuwa ni mtihani mkuu kutoka kwa Rabb wenu. 

 

 

وَإِذْ فَرَقْنَا بِكُمُ الْبَحْرَ فَأَنجَيْنَاكُمْ وَأَغْرَقْنَا آلَ فِرْعَوْنَ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ ﴿٥٠﴾ 

50. Na pindi Tulipoitenganisha bahari kwa ajili yenu; Tukakuokoeni na Tukawagharikisha watu wa Fir’awn na huku nyinyi mnatazama.

 

 

وَإِذْ وَاعَدْنَا مُوسَىٰ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً ثُمَّ اتَّخَذْتُمُ الْعِجْلَ مِن بَعْدِهِ وَأَنتُمْ ظَالِمُونَ ﴿٥١﴾

51. Na pindi Tulipomuahidi Muwsaa siku arubaini kisha mkamwabudu ndama baada yake na mkawa madhalimu.

 

 

ثُمَّ عَفَوْنَا عَنكُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٥٢﴾ 

52. Kisha Tukawasameheni baada ya hapo ili mpate kushukuru.

 

 

وَإِذْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَالْفُرْقَانَ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿٥٣﴾

 53. Na pindi Tulipompa Muwsaa Kitabu na Furqaan (upambanuo) ili mpate kuongoka.

 

 

 وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ إِنَّكُمْ ظَلَمْتُمْ أَنفُسَكُم بِاتِّخَاذِكُمُ الْعِجْلَ فَتُوبُوا إِلَىٰ بَارِئِكُمْ فَاقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ عِندَ بَارِئِكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ ۚ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿٥٤﴾

54. Na pindi Muwsaa alipowaambia kaumu yake: “Enyi kaumu yangu! Hakika nyinyi mmedhulumu nafsi zenu kwa kuabudu kwenu ndama, basi tubuni kwa Muumbaji wenu; na ziueni nafsi zenu, hivyo ni bora kwenu mbele ya Muumbaji wenu.” Akapokea tawbah yenu; hakika Yeye Ndiye Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu.

 

 

وَإِذْ قُلْتُمْ يَا مُوسَىٰ لَن نُّؤْمِنَ لَكَ حَتَّىٰ نَرَى اللَّـهَ جَهْرَةً فَأَخَذَتْكُمُ الصَّاعِقَةُ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ ﴿٥٥﴾

55. Na pindi mliposema: “Ewe Muwsaa! Hatutokuamini mpaka tumuone Allaah wazi wazi”; ikakuchukueni radi na umeme angamizi nanyi mnatazama.

 

 

ثُمَّ بَعَثْنَاكُم مِّن بَعْدِ مَوْتِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٥٦﴾

56. Kisha Tukakufufueni baada ya kufa kwenu ili mpate kushukuru.

 

 

وَظَلَّلْنَا عَلَيْكُمُ الْغَمَامَ وَأَنزَلْنَا عَلَيْكُمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَىٰ ۖ كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ ۖ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٥٧﴾ 

57. Na Tukakufunikeni kwa mawingu na Tukakuteremshieni Al-Manna na As-Salwaa. (Tukakwambieni): “Kuleni katika vizuri Tulivyokuruzukuni.” Hawakutudhulumu Sisi lakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao.

 

 

 

وَإِذْ قُلْنَا ادْخُلُوا هَـٰذِهِ الْقَرْيَةَ فَكُلُوا مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ رَغَدًا وَادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا وَقُولُوا حِطَّةٌ نَّغْفِرْ لَكُمْ خَطَايَاكُمْ ۚ وَسَنَزِيدُ الْمُحْسِنِينَ ﴿٥٨﴾

58. Na pindi Tuliposema: “Ingieni mji huu (Quds) na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, na ingieni katika mlango wake huku mmeinama kunyenyekea na semeni “Hittwah” (Tuondolee uzito wa madhambi); Tutakughufurieni makosa yenu na Tutawazidishia (thawabu) wafanyao ihsaan.

 

فَبَدَّلَ الَّذِينَ ظَلَمُوا قَوْلًا غَيْرَ الَّذِي قِيلَ لَهُمْ فَأَنزَلْنَا عَلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا رِجْزًا مِّنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿٥٩﴾ 

59. “Basi wale waliodhulumu walibadilisha kauli kinyume na ile waliyoambiwa, Tukateremsha juu ya waliodhulumu adhabu ya kufadhaika kutoka mbinguni kwa yale waliyokuwa wakifanya ya ufasiki.”

 

 

وَإِذِ اسْتَسْقَىٰ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ فَقُلْنَا اضْرِب بِّعَصَاكَ الْحَجَرَ ۖ فَانفَجَرَتْ مِنْهُ اثْنَتَا عَشْرَةَ عَيْنًا ۖ قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَّشْرَبَهُمْ ۖ كُلُوا وَاشْرَبُوا مِن رِّزْقِ اللَّـهِ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴿٦٠﴾

60. Na pindi Muwsaa alipoomba maji kwa ajili ya kaumu yake. Tukasema: “Piga kwa fimbo yako jiwe.” Zikachimbuka na kububujika kutoka kwalo chemchem kumi na mbili. Kila kabila likajua kinywaji chao. Kuleni na kunyweni kutokana na riziki ya Allaah na wala msieneze uovu katika ardhi hali ya kuwa ni wenye kufanya ufisadi.

 

 

وَإِذْ قُلْتُمْ يَا مُوسَىٰ لَن نَّصْبِرَ عَلَىٰ طَعَامٍ وَاحِدٍ فَادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُخْرِجْ لَنَا مِمَّا تُنبِتُ الْأَرْضُ مِن بَقْلِهَا وَقِثَّائِهَا وَفُومِهَا وَعَدَسِهَا وَبَصَلِهَا ۖ قَالَ أَتَسْتَبْدِلُونَ الَّذِي هُوَ أَدْنَىٰ بِالَّذِي هُوَ خَيْرٌ ۚ اهْبِطُوا مِصْرًا فَإِنَّ لَكُم مَّا سَأَلْتُمْ ۗ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ وَالْمَسْكَنَةُ وَبَاءُوا بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّـهِ ۗ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۗ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿٦١﴾

61. Na pindi mliposema: “Ee Muwsaa! Hatuwezi kusubiri kwa chakula cha aina moja tu, tuombee kwa Rabb wako Atutolee katika inavyoviotesha ardhi; kati ya mboga zake, matango yake, thomu (au ngano) yake, adesi zake na vitunguu vyake.” (Muwsaa) Akasema: “Je mnataka kubadilisha yaliyo duni kwa yaliyo bora? Shukeni mjini, hakika huko mtapata mnayoyauliza.” Na ikapigwa juu yao dhila na umaskini na wakastahiki ghadhabu kutoka kwa Allaah, hayo ni kwa kuwa wao walikuwa wakikanusha Aayaat (ishara) za Allaah; na wakiwaua Manabii bila ya haki; hayo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wakitaadi.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالنَّصَارَىٰ وَالصَّابِئِينَ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٦٢﴾

62. Hakika wale walioamini, na wale ambao (kabla ya Uislamu) ni Mayahudi, na Manaswara na Masabai (waabudu nyota); yeyote atakayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na akatenda mema, basi watapata ujira wao kutoka kwa Rabb wao, na hakutokuwa na khofu juu yao, na wala hawatohuzunika.

 

 

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ الطُّورَ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاذْكُرُوا مَا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿٦٣﴾

63. Na pindi Tulipochukua ahadi yenu na Tukaunyanyua juu yenu mlima (Tukasema): “Shikilieni Tuliyokupeni kwa nguvu na kumbukeni yaliyomo humo mpate kuwa na taqwa.”

 

 

ثُمَّ تَوَلَّيْتُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ ۖ فَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَكُنتُم مِّنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٦٤﴾

64. Kisha mkakengeuka baada ya hayo, na lau si fadhila za Allaah juu yenu na rahmah Yake mngekuwa miongoni mwa wenye kukhasirika.

 

 

وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ الَّذِينَ اعْتَدَوْا مِنكُمْ فِي السَّبْتِ فَقُلْنَا لَهُمْ كُونُوا قِرَدَةً خَاسِئِينَ ﴿٦٥﴾

65. Na kwa yakini mlikwishawajua wale miongoni mwenu waliotaadi mipaka ya As-Sabt Tukawaambia: “Kuweni manyani waliobezwa.”[7]

 

 

 

فَجَعَلْنَاهَا نَكَالًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهَا وَمَا خَلْفَهَا وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٦٦﴾

66. Tukaifanya kuwa ni adhabu ya kuonya kwa waliokuweko zama zao na wataokuja baada yao na ni mawaidha kwa wenye taqwa.

 

 

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تَذْبَحُوا بَقَرَةً ۖ قَالُوا أَتَتَّخِذُنَا هُزُوًا ۖ قَالَ أَعُوذُ بِاللَّـهِ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ ﴿٦٧﴾

67. Na pindi Muwsaa alipowaambia kaumu wake: “Hakika Allaah Anakuamuruni mchinje ng’ombe.” Wakasema: “Unatufanyia mzaha?” Akasema: “Najikinga kwa Allaah kuwa miongoni mwa wajinga.”

 

 

قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ ۚ قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ لَّا فَارِضٌ وَلَا بِكْرٌ عَوَانٌ بَيْنَ ذَٰلِكَ ۖ فَافْعَلُوا مَا تُؤْمَرُونَ ﴿٦٨﴾

68. Wakasema: “Tuombee kwa Rabb wako Atubainishie ni ng’ombe wa aina gani huyo?” (Muwsaa) Akasema: “Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ng’ombe mwenyewe si mpevu wala si mchanga, bali ni wa katikati baina ya hao, basi fanyeni mnavyoamrishwa.”

 

 

قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا لَوْنُهَا ۚ قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ صَفْرَاءُ فَاقِعٌ لَّوْنُهَا تَسُرُّ النَّاظِرِينَ ﴿٦٩﴾

69. Wakasema: “Tuombee kwa Rabb wako Atubainishie rangi yake?” (Muwsaa) Akasema: “Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ni ng’ombe wa rangi ya njano iliyoiva mno, rangi yake huwapendeza wanaotazama.”

 

 

 قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ إِنَّ الْبَقَرَ تَشَابَهَ عَلَيْنَا وَإِنَّا إِن شَاءَ اللَّـهُ لَمُهْتَدُونَ ﴿٧٠﴾

70. Wakasema: “Tuombee kwa Rabb wako Atubainishie ni ng’ombe wa aina gani huyo? Kwa hakika ng’ombe wametutatiza na hakika sisi In-Shaa-Allaah tutakuwa wenye kuongoka.”

 

 

قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ لَّا ذَلُولٌ تُثِيرُ الْأَرْضَ وَلَا تَسْقِي الْحَرْثَ مُسَلَّمَةٌ لَّا شِيَةَ فِيهَا ۚ قَالُوا الْآنَ جِئْتَ بِالْحَقِّ ۚ فَذَبَحُوهَا وَمَا كَادُوا يَفْعَلُونَ ﴿٧١﴾

71. (Muwsaa) Akasema: ”Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ni ng’ombe ambaye hakutiishwa; kwa kulima ardhi wala kwa kumwagilia maji shamba; ni kamilifu hana dosari.” Wakasema: “Sasa umekuja na haki.” Basi wakamchinja na hawakuwa wenye kukaribia kufanya hivyo. 

 

 

وَإِذْ قَتَلْتُمْ نَفْسًا فَادَّارَأْتُمْ فِيهَا ۖ وَاللَّـهُ مُخْرِجٌ مَّا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ ﴿٧٢﴾

72. Na pindi mlipoiua nafsi, kisha mkakhitilafiana kwayo, na Allaah ni Mwenye kutoa hayo mliyokuwa mkiyaficha.

 

 

فَقُلْنَا اضْرِبُوهُ بِبَعْضِهَا ۚ كَذَٰلِكَ يُحْيِي اللَّـهُ الْمَوْتَىٰ وَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٧٣﴾

73. Tukasema: “Mpigeni (huyo maiti) kwa kipande chake (huyo ng’ombe).” Hivyo ndivyo Allaah Anavyohuisha wafu na Anakuonyesheni Aayaat (miujiza, dalili) Zake huenda mkatia akilini.

 

 

 ثُمَّ قَسَتْ قُلُوبُكُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ فَهِيَ كَالْحِجَارَةِ أَوْ أَشَدُّ قَسْوَةً ۚ وَإِنَّ مِنَ الْحِجَارَةِ لَمَا يَتَفَجَّرُ مِنْهُ الْأَنْهَارُ ۚ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَشَّقَّقُ فَيَخْرُجُ مِنْهُ الْمَاءُ ۚ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَهْبِطُ مِنْ خَشْيَةِ اللَّـهِ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٧٤﴾

74. Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, zikawa kama mawe au ngumu zaidi. Na kwa hakika katika mawe kuna yanayobubujika humo mito. Na hakika katika hayo kuna yanayopasuka yakatoka humo maji. Na hakika katika hayo kuna mengine yanayoporomoka kutokana na khofu ya Allaah. Na Allaah si Mwenye kughafilika kuhusu myatendayo.

 

 

أَفَتَطْمَعُونَ أَن يُؤْمِنُوا لَكُمْ وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُ مِن بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٥﴾

75. Je, mnatumai kwamba watakuaminini na hali lilikuwa kundi miongoni mwao linasikia maneno ya Allaah kisha linayageuza baada ya kuyaelewa na hali wanajua?

 

 

وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَا بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ قَالُوا أَتُحَدِّثُونَهُم بِمَا فَتَحَ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ لِيُحَاجُّوكُم بِهِ عِندَ رَبِّكُمْ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٧٦﴾

76. Na wanapokutana na wale walioamini husema: “Tumeamini.” Na wanapokuwa peke yao; wao kwa wao; husema: “Hivi mnawasimulia yale Aliyokufungulieni Allaah ili wapate kukuhojini kwayo mbele ya Rabb wenu; hamtii akilini?”

 

 

 أَوَلَا يَعْلَمُونَ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ﴿٧٧﴾

77. Je, hawajui kwamba Allaah Anajua wanayoyaficha na wanayoyatangaza?

 

 

وَمِنْهُمْ أُمِّيُّونَ لَا يَعْلَمُونَ الْكِتَابَ إِلَّا أَمَانِيَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ ﴿٧٨﴾ 

78. Na miongoni mwao wako wasiojua kusoma wala kuandika; hawakijui Kitabu ila matamanio ya kuwaza tu, nao hawana ila kudhania tu.

 

 

فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ يَكْتُبُونَ الْكِتَابَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ هَـٰذَا مِنْ عِندِ اللَّـهِ لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتْ أَيْدِيهِمْ وَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا يَكْسِبُونَ ﴿٧٩﴾

79. Basi ole kwa wale wenye kuandika kitabu kwa mikono yao; kisha wakasema: ”Hiki ni kutoka kwa Allaah” ili wabadilishe kwa thamani ndogo. Basi ole wao kwa yale yaliyoandikwa na mikono yao, na ole wao kwa yale wanayoyachuma.[8]

 

 

وَقَالُوا لَن تَمَسَّنَا النَّارُ إِلَّا أَيَّامًا مَّعْدُودَةً ۚ قُلْ أَتَّخَذْتُمْ عِندَ اللَّـهِ عَهْدًا فَلَن يُخْلِفَ اللَّـهُ عَهْدَهُ ۖ أَمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٨٠﴾

80. Na walisema: “Hautotugusa moto ila siku chache tu.” Sema: “Je, mmechukua ahadi kwa Allaah?” Basi Allaah Hakhalifu ahadi Yake, au mnasema kuhusu Allaah msiyoyajua?

 

 

بَلَىٰ مَن كَسَبَ سَيِّئَةً وَأَحَاطَتْ بِهِ خَطِيئَتُهُ فَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٨١﴾

81. Ndio! Yeyote aliyechuma uovu na yakamzunguka kwayo makosa yake; basi hao ni watu wa motoni, wao humo ni wenye kudumu.

 

 

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٨٢﴾

82. Na wale walioamini na wakatenda mema; hao ni watu wa Jannah, wao humo ni wenye kudumu.

 

 

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ لَا تَعْبُدُونَ إِلَّا اللَّـهَ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَقُولُوا لِلنَّاسِ حُسْنًا وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ ثُمَّ تَوَلَّيْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنكُمْ وَأَنتُم مُّعْرِضُونَ ﴿٨٣﴾ 

83. Na pindi Tulipochukua fungamano ya wana wa Israaiyl (Tukawaambia): “Msiabudu isipokuwa Allaah; na muwafanyie ihsaan wazazi wawili, na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini; na semeni na watu kwa uzuri na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah;” kisha mkakengeuka ila wachache miongoni mwenu na hali nyinyi mnapuuza.

 

 

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ لَا تَسْفِكُونَ دِمَاءَكُمْ وَلَا تُخْرِجُونَ أَنفُسَكُم مِّن دِيَارِكُمْ ثُمَّ أَقْرَرْتُمْ وَأَنتُمْ تَشْهَدُونَ ﴿٨٤﴾

84. Na pindi Tulipochukua fungamano lenu (Tukawaambia): “Msimwage damu zenu, wala msitoe nafsi zenu kutoka miji yenu;” kisha mkakubali nanyi mnashuhudia.

 

 

ثُمَّ أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ تَقْتُلُونَ أَنفُسَكُمْ وَتُخْرِجُونَ فَرِيقًا مِّنكُم مِّن دِيَارِهِمْ تَظَاهَرُونَ عَلَيْهِم بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَإِن يَأْتُوكُمْ أُسَارَىٰ تُفَادُوهُمْ وَهُوَ مُحَرَّمٌ عَلَيْكُمْ إِخْرَاجُهُمْ ۚ أَفَتُؤْمِنُونَ بِبَعْضِ الْكِتَابِ وَتَكْفُرُونَ بِبَعْضٍ ۚ فَمَا جَزَاءُ مَن يَفْعَلُ ذَٰلِكَ مِنكُمْ إِلَّا خِزْيٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرَدُّونَ إِلَىٰ أَشَدِّ الْعَذَابِ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٨٥﴾

85. Kisha nyinyi ndio hao mnaua nafsi zenu na mnalitoa kundi miongoni mwenu kutoka majumbani mwao mnasaidiana dhidi yao kwa dhambi na uadui; na wanapokujieni mateka mnawakomboa na hali hilo limeharamishwa kwenu kuwatoa. Je, mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakanusha baadhi yake? Basi hapana jazaa ya anayefanya hayo miongoni mwenu isipokuwa hizaya katika dunia, na Siku ya Qiyaamah watapelekwa kwenye adhabu kali zaidi, na Allaah si Mwenye kughafilika kuhusu myatendayo.

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا بِالْآخِرَةِ ۖ فَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿٨٦﴾

86. Hao ndio wale waliobadilisha uhai wa dunia badala ya Aakhirah, basi haitopunguzwa kwao adhabu wala hawatonusuriwa.

 

 

وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَقَفَّيْنَا مِن بَعْدِهِ بِالرُّسُلِ ۖ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ ۗ أَفَكُلَّمَا جَاءَكُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَىٰ أَنفُسُكُمُ اسْتَكْبَرْتُمْ فَفَرِيقًا كَذَّبْتُمْ وَفَرِيقًا تَقْتُلُونَ ﴿٨٧﴾

87. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu na Tukafuatisha Rusuli baada yake. Na Tukampa ‘Iysaa mwana wa Maryam hoja bayana na Tukamtia nguvu kwa Ruwhil-Qudus (Jibriyl (عليه السلام. Je, basi kila anapokujieni Rasuli kwa yale yasiyoyapenda nafsi zenu, mlitakabari; hivyo kundi mlilikadhibisha na kundi mnaliua.[9]

 

 

وَقَالُوا قُلُوبُنَا غُلْفٌ ۚ بَل لَّعَنَهُمُ اللَّـهُ بِكُفْرِهِمْ فَقَلِيلًا مَّا يُؤْمِنُونَ ﴿٨٨﴾

88. Na wakasema: “Nyoyo zetu zimefunikwa.” Bali Allaah Amewalaani kwa kufuru zao; basi machache tu wanayoyaamini.

 

 

وَلَمَّا جَاءَهُمْ كِتَابٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ وَكَانُوا مِن قَبْلُ يَسْتَفْتِحُونَ عَلَى الَّذِينَ كَفَرُوا فَلَمَّا جَاءَهُم مَّا عَرَفُوا كَفَرُوا بِهِ ۚ فَلَعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٨٩﴾

89. Na kilipowajia Kitabu kutoka kwa Allaah kisadikishacho yale yaliyo pamoja nao, na japokuwa kabla ya hapo walikuwa wakiomba ushindi dhidi ya wale waliokufuru; basi yalipowajia yale waliyokuwa wakiyatambua waliyakanusha, basi laana ya Allaah iwe juu ya makafiri.[10]

 

 

بِئْسَمَا اشْتَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ أَن يَكْفُرُوا بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ بَغْيًا أَن يُنَزِّلَ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۖ فَبَاءُوا بِغَضَبٍ عَلَىٰ غَضَبٍ ۚ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿٩٠﴾

90. Ubaya ulioje walichojibadilishia nafsi zao, kwamba wakufuru yale Aliyoyateremsha Allaah wakichukizwa na uhasidi kwa kuwa Allaah Kateremsha katika fadhila Zake juu ya Amtakae katika waja Wake. Basi wakarudi kwa kustahiki ghadhabu juu ya ghadhabu. Na makafiri watapata adhabu ya kudhalilisha.

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُوا بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ قَالُوا نُؤْمِنُ بِمَا أُنزِلَ عَلَيْنَا وَيَكْفُرُونَ بِمَا وَرَاءَهُ وَهُوَ الْحَقُّ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَهُمْ ۗ قُلْ فَلِمَ تَقْتُلُونَ أَنبِيَاءَ اللَّـهِ مِن قَبْلُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٩١﴾

91. Na wanapoambiwa: “Aminini yale Aliyoyateremsha Allaah”, husema: “Tunaamini yale yaliyoteremshwa kwetu” na wanayakanusha yale yaliyokuja baada yake, na hali ya kuwa hayo ni haki yenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nao. Sema: “Kwa nini basi mnawaua Manabii wa Allaah toka hapo kabla kama kweli mlikuwa waumini?

 

 

وَلَقَدْ جَاءَكُم مُّوسَىٰ بِالْبَيِّنَاتِ ثُمَّ اتَّخَذْتُمُ الْعِجْلَ مِن بَعْدِهِ وَأَنتُمْ ظَالِمُونَ ﴿٩٢﴾

92. Na kwa yakini alikujieni Muwsaa kwa hoja bayana kisha mkamwabudu ndama baada yake na hali ya kuwa nyinyi ni madhalimu.

 

 

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ الطُّورَ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاسْمَعُوا ۖ قَالُوا سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَأُشْرِبُوا فِي قُلُوبِهِمُ الْعِجْلَ بِكُفْرِهِمْ ۚ قُلْ بِئْسَمَا يَأْمُرُكُم بِهِ إِيمَانُكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٩٣﴾

93. Na Tulipochukua fungamano lenu na Tukaunyanyua juu yenu mlima; (Tukasema): “Shikilieni Tuliyokupeni kwa nguvu na sikilizeni.” Wakasema: ”Tumesikia na tumeasi.” Wakanyweshwa katika nyoyo zao (kumwabudu) ndama kwa kufuru yao. Sema: “Ubaya ulioje inakuamrisheni kwayo imani yenu mkiwa ni waumini.”

 

 

 

قُلْ إِن كَانَتْ لَكُمُ الدَّارُ الْآخِرَةُ عِندَ اللَّـهِ خَالِصَةً مِّن دُونِ النَّاسِ فَتَمَنَّوُا الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٩٤﴾

94. Sema: ”Ikiwa nyumba ya Aakhirah iliyoko kwa Allaah ni makhsusi kwenu pekee pasi na watu wengine; basi tamanini mauti mkiwa ni wakweli.

 

 

وَلَن يَتَمَنَّوْهُ أَبَدًا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ ﴿٩٥﴾

95. Na hawatoyatamani abadani kutokana na iliyoyatanguliza mikono yao. Na Allaah ni Mjuzi wa madhalimu.

 

 

 

وَلَتَجِدَنَّهُمْ أَحْرَصَ النَّاسِ عَلَىٰ حَيَاةٍ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا ۚ يَوَدُّ أَحَدُهُمْ لَوْ يُعَمَّرُ أَلْفَ سَنَةٍ وَمَا هُوَ بِمُزَحْزِحِهِ مِنَ الْعَذَابِ أَن يُعَمَّرَ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ ﴿٩٦﴾

96. Na kwa yakini utawakuta wao (Mayahudi) ni watu wenye pupa mno kuliko yeyote juu ya uhai na kuliko wale walioshirikisha. Anapenda mmoja wao lau angelipewa umri mrefu wa miaka elfu. Na wala huko hakutamuondoshea adhabu kwa kupewa umri mrefu. Na Allaah ni Mwenye kuona wanayoyatenda. 

 

 

قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّـهِ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ ﴿٩٧﴾

97. Sema: “Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika yeye ameiteremsha Qur-aan katika moyo wako (ee Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) kwa idhini ya Allaah inayosadikisha yaliyo kabla yake, na mwongozo na bishara kwa Waumini.[11]

 

 مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّـهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ ﴿٩٨﴾

98. Yeyote aliyekuwa adui wa Allaah na Malaika Wake, na Rusuli Wake, na Jibriyl, na Miykaala, basi hakika Allaah ni adui kwa makafiri.

 

 

وَلَقَدْ أَنزَلْنَا إِلَيْكَ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ ۖ وَمَا يَكْفُرُ بِهَا إِلَّا الْفَاسِقُونَ ﴿٩٩﴾

99. Na kwa yakini Tumeteremsha kwako Aayaat bayana, na hawazikanushi isipokuwa mafasiki.



Endelea Kusoma Kwa Kugusa Hapa 👈

Ukishaa Gusa Hapo 👆 Kufunguka Utasubilia kidogo kwa baazi ya App na simu




Report Page