COVID19

COVID19

Mansura Mtibora

COVID 19 (CORONA VIRUS DISEASE 2019) huu ni ugonjwa hatari wa kuambukiza amabao hushambulia njia ya hewa na kusababisha mtu kupata shida katika kupumua(severe acute resporatory syndrome)

Ugonjwa huu husababishwa na kirusi aina ya CORONA kama inavojieleza

Hivi sasa umekua ni ugonjwa wa kidunia(Pandemic disease)

CORONA VIRUS


NJIA ZA KUAMBUKIZA

Ugonjwa huu ni mpya katika dunia hivo basi unafanyiwa utafiti wa kutosha ila kwa sasa imethibitishwa kuwa huambukiza kwa njia ya majimaji(droplets) yatokayo kwa mgonjwa mwenye COVID19

Kwa njia ya kuongea ,kupiga chafya ,kukohoa au kupika mwayo bila kujiziba pua au mdomo wake

Ugonjwa huu haumbukizi kwa njia ya hewa (air born disease)

DALILI ZAKE

kwa kuwa ugonjwa huu unasababishwa na kirusi haina dalili moja bali nyingi kutokana na tabia ya kirusi kujibadilisha umbile lake na tabia yake ya kubadilika kulingana na mazingira aliyopo

Lakini dalili kubwa imeonekana ni kupata homa kali sana inayopanda kadri ya muda unavopita dalili nyingine ni kama

kuchuruzika kamasi

kikohozi

kupumua kwa shida pale virusi hivi vinapoendelea kushambulia mwili ,(dalili hii ndio inaonekana kwa watu wengi pamoja na homa kali kwani ximethibitika kuwa mgonjwa wa COVID19 anaweza kuonesha yuko sawa kwa kumtazama lakini ukipima kiwango cha oxygen mwilini utapata majibu ya kushangaza maana oxygen inakua chini ya kiwango mwili unachohitaji (silent hypoxia)

Hivo kadri muda unavopita na mapafu yanaendelea kuishiwa uwezo wake wa kutengeneza oxygen hivo mgonjwa anaweza kuonesha dalili moja tu ya kupumua kwa shida sana.

Dalili nyingine zimegunduliwa hivi karibuni ni

kukosa hamu ya kula

mwili kuchoka sana bila kuwa umefanya kazi nzito ya kuuchosha

Kushindwa kutambua harufu mbalimbali

kutapika na kuharisha hasa kwa watoto.


TIBA YA COVID19

Mpaka sasa hakuna tiba iliyopatikana kutokana na tabia ya kirusi hivo tiba pekee hapa ni kujikinga dhidi ya maambukizi kwa

Kunawa mikono mara kwa mara kwa maji na sabani au vitakasa mikono(sanitizers)

Kuepuka msongamano mkubwa wa watu

Kuziba mdomo na pua unapopiga chafya au kukohoa kwa barakoa (mask) wakati wote unapokua na watu hata wawili.

Epuka kujifukiza kama huna utaalamu huo maana ni hatari sana moto au mvuke wenye joto kubwa ni hatari sana kwa njoa ya hewa hivo inaweza kuleta tatizo lingine mbali na hiyo COVID19.

Mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na COVID 19 hutibiwa dalili anazonesha kwa muda huo hivo kama ana homa kali itatulizwa kwa dawa za kushusha homa kama atakua anapumua kwa shida atasaidiwa kupuma kwa kuwekewa oxyegen nk.


JIKINGE NA WAKINGE WENGINE DHIDI YA COVID19.


Report Page