005-Al-Maaidah

005-Al-Maaidah

Khamis

Next page 📄 3

 

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَسْتُمْ عَلَىٰ شَيْءٍ حَتَّىٰ تُقِيمُوا التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ ۗ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم مَّا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ طُغْيَانًا وَكُفْرًا ۖ فَلَا تَأْسَ عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٦٨﴾

68. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Hamtaambulia chochote mpaka muishike ipasavyo Tawraat na Injiyl na yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Rabb wenu. Kwa yakini yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako, yatawazidisha wengi miongoni mwao upindukaji mipaka ya kuasi na kufuru. Basi usisikitike juu ya watu makafiri.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالصَّابِئُونَ وَالنَّصَارَىٰ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٦٩﴾

69. Hakika wale walioamini na Mayahudi na Wasabai[16] na Manaswara; atakayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho na akatenda mema, basi hawatokuwa na khofu na wala hawatohuzunika.

 

   

 

لَقَدْ أَخَذْنَا مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَأَرْسَلْنَا إِلَيْهِمْ رُسُلًا ۖ كُلَّمَا جَاءَهُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَىٰ أَنفُسُهُمْ فَرِيقًا كَذَّبُوا وَفَرِيقًا يَقْتُلُونَ ﴿٧٠﴾

70. Kwa yakini Tulichukua agano la wana wa Israaiyl na Tukawapelekea Rusuli. Basi kila alipowajia Rasuli kwa yale yasiyopenda nafsi zao, kundi waliwakadhibisha na kundi wakawaua.

 

 

 

وَحَسِبُوا أَلَّا تَكُونَ فِتْنَةٌ فَعَمُوا وَصَمُّوا ثُمَّ تَابَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ ثُمَّ عَمُوا وَصَمُّوا كَثِيرٌ مِّنْهُمْ ۚ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ ﴿٧١﴾

71. Na walidhani kwamba yatapita hayo bila adhabu, basi wakawa vipofu na wakawa viziwi, kisha Allaah Akapokea tawbah yao. Tena wengi wao wakawa vipofu na wakawa viziwi. Na Allaah Ni Mwenye Kuona yale wayatendayo.

 

 

لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۖ وَقَالَ الْمَسِيحُ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۖ إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ﴿٧٢﴾

72. Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: Allaah ni Al-Masiyh mwana wa Maryam. Na ilhali Al-Masiyh alisema (kukadhibisha madai yao): Enyi wana wa Israaiyl! Mwabuduni Allaah, Rabb wangu na Rabb wenu. Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni.[17] Na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kunusuru.

 

 

لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ ۘ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۚ وَإِن لَّمْ يَنتَهُوا عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٣﴾

73. Kwa yakini wamekufuru wale waliosema Allaah ni wa tatu wa watatu. Ilhali hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Ilaah Mmoja Pekee. Na wasipoacha yale wanayoyasema, bila ya shaka itawagusa adhabu iumizayo wale waliokufuru miongoni mwao.

 

 

أَفَلَا يَتُوبُونَ إِلَى اللَّـهِ وَيَسْتَغْفِرُونَهُ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٧٤﴾

74. Je, hawatubii kwa Allaah na wakamwomba maghfirah? Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

مَّا الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ وَأُمُّهُ صِدِّيقَةٌ ۖ كَانَا يَأْكُلَانِ الطَّعَامَ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُبَيِّنُ لَهُمُ الْآيَاتِ ثُمَّ انظُرْ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴿٧٥﴾

75. Al-Masiyh mwana wa Maryam si chochote ila ni Rasuli tu, wamekwishapita kabla yake Rusuli (wengine). Na mama yake ni Muumini mkweli wa dhati. Wote wawili walikuwa wanakula chakula. Tazama jinsi Tunavyowabainishia Aayaat (Ishara, Hoja, Dalili) kisha tazama vipi wanavyoghilibiwa.

 

 

قُلْ أَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا ۚ وَاللَّـهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٧٦﴾

76. Sema: Vipi mnaabudu visivyokuwa na uwezo wa kukudhuruni wala kukunufaisheni badala ya Allaah! Na Allaah Ndiye Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ غَيْرَ الْحَقِّ وَلَا تَتَّبِعُوا أَهْوَاءَ قَوْمٍ قَدْ ضَلُّوا مِن قَبْلُ وَأَضَلُّوا كَثِيرًا وَضَلُّوا عَن سَوَاءِ السَّبِيلِ ﴿٧٧﴾

77. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Msipindukie mipaka katika dini yenu bila ya haki, na wala msifuate hawaa za watu waliokwishapotea kabla na wakapotosha wengi na wakapotea njia iliyo sawa.

 

 

لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿٧٨﴾

78. Wamelaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israaiyl kwa lisani ya Daawuwd na ‘Iysaa mwana wa Maryam. Hivyo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wakitaadi.

 

 

كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿٧٩﴾

79. Walikuwa hawakatazani munkari yoyote waliyofanya. Uovu ulioje waliyokuwa wakiyafanya!  

 

 

تَرَىٰ كَثِيرًا مِّنْهُمْ يَتَوَلَّوْنَ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ لَبِئْسَ مَا قَدَّمَتْ لَهُمْ أَنفُسُهُمْ أَن سَخِطَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ وَفِي الْعَذَابِ هُمْ خَالِدُونَ ﴿٨٠﴾

80. Utawaona wengi miongoni mwao wanawafanya marafiki wandani na walinzi wale waliokufuru. Ubaya ulioje yale yaliyowatangulizia nafsi zao, hata Allaah Amewaghadhibikia na katika adhabu wao watadumu.

 

 

وَلَوْ كَانُوا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالنَّبِيِّ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مَا اتَّخَذُوهُمْ أَوْلِيَاءَ وَلَـٰكِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ ﴿٨١﴾

81. Na lau wangelikuwa wanamwamini Allaah na Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kwake, wasingeliwafanya hao marafiki wandani na walinzi, lakini wengi miongoni mwao ni mafasiki.

 

 

لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا ۖ وَلَتَجِدَنَّ أَقْرَبَهُم مَّوَدَّةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ قَالُوا إِنَّا نَصَارَىٰ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّ مِنْهُمْ قِسِّيسِينَ وَرُهْبَانًا وَأَنَّهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ ﴿٨٢﴾

82. Bila shaka utawakuta walio na uadui mkali zaidi kuliko watu wote, kwa walioamini, ni Mayahudi na wale walioshirikisha. Na bila shaka utawakuta walio karibu zaidi kimapenzi kwa Waumini ni wale wanaosema: Sisi ni Manaswara. Hivyo ni kwa kuwa miongoni mwao kuna Qissiysiyna[18] (Makasisi) na Ruhbaan[19] (Wamonaki) na kwamba wao hawatakabari.

 

 

 

 

وَإِذَا سَمِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَى الرَّسُولِ تَرَىٰ أَعْيُنَهُمْ تَفِيضُ مِنَ الدَّمْعِ مِمَّا عَرَفُوا مِنَ الْحَقِّ ۖ يَقُولُونَ رَبَّنَا آمَنَّا فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ ﴿٨٣﴾

83. Na wanaposikia yale yaliyoteremshwa kwa Rasuli utaona macho yao yanachuruzika machozi kutokana na yale waliyoyatambua ya haki. Wanasema: Rabb wetu tumeamini, basi Tuandike pamoja na wenye kushuhudia.

 

 

 

 

وَمَا لَنَا لَا نُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَمَا جَاءَنَا مِنَ الْحَقِّ وَنَطْمَعُ أَن يُدْخِلَنَا رَبُّنَا مَعَ الْقَوْمِ الصَّالِحِينَ ﴿٨٤﴾

84. Na kwa nini Tusimwamini Allaah na haki iliyotufikia na hali tunatumai Rabb wetu Atuingize (Jannah) pamoja na watu Swalihina?

 

 

 

 

فَأَثَابَهُمُ اللَّـهُ بِمَا قَالُوا جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٥﴾

85. Basi Allaah Akawalipa tuzo ya Jannaat zipitazo chini yake mito kwa yale waliyoyasema, wadumu humo. Na hiyo ndio jazaa ya wafanyao ihsaan.

 

 

 

 

وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴿٨٦﴾

86. Na wale waliokufuru na wakazikadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) Zetu hao ni watu wa moto uwakao vikali mno. 

 

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُحَرِّمُوا طَيِّبَاتِ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿٨٧﴾

87. Enyi walioamini! Msiharamishe vilivyo vizuri Alivyokuhalalishieni Allaah, na wala msipindukie mipaka. Hakika Allaah Hapendi wapindukao mipaka. 

 

 

 

وَكُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ حَلَالًا طَيِّبًا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي أَنتُم بِهِ مُؤْمِنُونَ ﴿٨٨﴾

88. Na kuleni katika vile Alivyowaruzukuni Allaah vya halali na vizuri. Na mcheni Allaah Ambaye nyinyi mnamwamini. 

 

 

 

لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٨٩﴾

89. Allaah Hatokuchukulieni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini Atakuchukulieni kwa (kuvunja) viapo mlivyoapa kwa niya mlioifunga thabiti. Basi kafara yake ni kulisha maskini kumi chakula cha wastani mnachowalisha ahli zenu, au kuwavisha nguo, au kuacha huru mtumwa. Lakini asiyeweza kupata (katika hayo), basi (afunge) Swiyaam siku tatu. Hiyo ndio kafara ya viapo vyenu mnapoapa. Na hifadhini yamini zenu.[20] Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na Hukmu, Sharia) Zake ili mpate kushukuru.

 

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٩٠﴾

90. Enyi walioamini! Hakika pombe na kamari na masanamu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli, ni najisi na chukizo kutokana na kazi ya shaytwaan. Basi jiepusheni navyo mpate kufaulu.[21]

 

 

إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ ﴿٩١﴾

91. Hakika shaytwaan anataka kukutilieni baina yenu uadui na bughudha, katika pombe na kamari na akuzuieni kumdhukuru Allaah na Swalaah, basi je mtakoma?

 

 

 

وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَاحْذَرُوا ۚ فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ ﴿٩٢﴾

92. Na mtiini Allaah na mtiini Rasuli na tahadharini! Mkikengeuka, basi jueni kwamba juu ya Rasuli Wetu ni kubalighisha ujumbe tu ulio bayana.

 

 

 

 

 

لَيْسَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جُنَاحٌ فِيمَا طَعِمُوا إِذَا مَا اتَّقَوا وَّآمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ ثُمَّ اتَّقَوا وَّآمَنُوا ثُمَّ اتَّقَوا وَّأَحْسَنُوا ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿٩٣﴾

93. Hakuna lawama juu ya wale walioamini na wakatenda mema katika vile walivyokula (kabla ya kuharimishwa) ikiwa watakuwa na taqwa na wakaamini na wakatenda mema, kisha wakawa na taqwa na wakaamini, kisha wakawa na taqwa na wakafanya ihsaan. Na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَيَبْلُوَنَّكُمُ اللَّـهُ بِشَيْءٍ مِّنَ الصَّيْدِ تَنَالُهُ أَيْدِيكُمْ وَرِمَاحُكُمْ لِيَعْلَمَ اللَّـهُ مَن يَخَافُهُ بِالْغَيْبِ ۚ فَمَنِ اعْتَدَىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَلَهُ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٩٤﴾

94. Enyi walioamini! Bila shaka Allaah Atakujaribuni mtihani mdogo kwa baadhi ya wanyama wa kuwinda inayowafikia mikono yenu na mikuki yenu, ili Allaah Ampambanue mwenye kumkhofu bila kumwona. Na atakayetaadi baada ya hayo, basi atapata adhabu iumizayo. 

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْتُلُوا الصَّيْدَ وَأَنتُمْ حُرُمٌ ۚ وَمَن قَتَلَهُ مِنكُم مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاءٌ مِّثْلُ مَا قَتَلَ مِنَ النَّعَمِ يَحْكُمُ بِهِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ هَدْيًا بَالِغَ الْكَعْبَةِ أَوْ كَفَّارَةٌ طَعَامُ مَسَاكِينَ أَوْ عَدْلُ ذَٰلِكَ صِيَامًا لِّيَذُوقَ وَبَالَ أَمْرِهِ ۗ عَفَا اللَّـهُ عَمَّا سَلَفَ ۚ وَمَنْ عَادَ فَيَنتَقِمُ اللَّـهُ مِنْهُ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٩٥﴾

95. Enyi walioamini! Msiue mawindo na hali mko katika ihraam.[22] Na atakayemuua (mnyama) miongoni mwenu kwa kusudi, basi malipo yake itakuwa ni kilicho sawa na alichokiua katika wanyama wa mifugo. Watamkadiria anayelingana naye wajuzi wawili waadilifu miongoni mwenu. Mnyama huyo afikishwe Ka’bah, au atoe kafara ya kulisha maskini, au badala ya hayo, (afunge) Swiyaam ili aonje matokeo maovu ya jambo lake. Allaah Ameshasamehe yaliyopita, na yeyote atakayerudia tena, basi Allaah Atamlipiza (kumuadhibu). Na Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kulipiza.

 

 

 

أُحِلَّ لَكُمْ صَيْدُ الْبَحْرِ وَطَعَامُهُ مَتَاعًا لَّكُمْ وَلِلسَّيَّارَةِ ۖ وَحُرِّمَ عَلَيْكُمْ صَيْدُ الْبَرِّ مَا دُمْتُمْ حُرُمًا ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٩٦﴾

96. Mmehalalishiwa mawindo ya bahari, na chakula chake ni manufaa kwenu na kwa wasafiri. Na mmeharamishiwa mawindo ya nchi kavu madamu mtakuwa katika ihraam. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mtakusanywa.

 

 

 

 

جَعَلَ اللَّـهُ الْكَعْبَةَ الْبَيْتَ الْحَرَامَ قِيَامًا لِّلنَّاسِ وَالشَّهْرَ الْحَرَامَ وَالْهَدْيَ وَالْقَلَائِدَ ۚ ذَٰلِكَ لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَأَنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٩٧﴾

97. Allaah Amejaalia Ka’bah ambayo ni Nyumba Tukufu kuwa kiini cha manufaa na matengeneo kwa watu, na pia Miezi Mitukufu na wanyama wa kafara na vigwe. Hivyo ili mpate kujua kuwa Allaah Anajua yale yaliyomo mbinguni na ardhini na kwamba Allaah Ni Mjuzi kwa kila kitu.

 

 

 

 

اعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ وَأَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٩٨﴾

98. Jueni kuwa Allaah Ni Mkali wa Kuakibu[23] na kwamba Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

مَّا عَلَى الرَّسُولِ إِلَّا الْبَلَاغُ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا تَكْتُمُونَ ﴿٩٩﴾

99. Rasuli hana jingine zaidi ila kubalighisha tu. Na Allaah Anayajua yale mnayoyadhihirisha na yale mnayoyaficha.

 

 

 

 

قُل لَّا يَسْتَوِي الْخَبِيثُ وَالطَّيِّبُ وَلَوْ أَعْجَبَكَ كَثْرَةُ الْخَبِيثِ ۚ فَاتَّقُوا اللَّـهَ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٠٠﴾

100. Sema: Haviwi sawasawa viovu na vizuri japokuwa utakupendezea wingi wa viovu. Basi mcheni Allaah, enyi wenye akili ili mpate kufaulu.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ وَإِن تَسْأَلُوا عَنْهَا حِينَ يُنَزَّلُ الْقُرْآنُ تُبْدَ لَكُمْ عَفَا اللَّـهُ عَنْهَا ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿١٠١﴾

101. Enyi walioamini! Msiulizie mambo ambayo mkifichuliwa yatakuchukizeni. Na mkiyaulizia pale inapoteremshwa Qur-aan mtafichuliwa. Allaah Ameyasamehe hayo. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mvumilivu.

 

 

 

 

قَدْ سَأَلَهَا قَوْمٌ مِّن قَبْلِكُمْ ثُمَّ أَصْبَحُوا بِهَا كَافِرِينَ ﴿١٠٢﴾

102. Walikwishayauliza hayo watu wa kabla yenu, kisha kutokana nayo, wakawa makafiri.

 

 

 

مَا جَعَلَ اللَّـهُ مِن بَحِيرَةٍ وَلَا سَائِبَةٍ وَلَا وَصِيلَةٍ وَلَا حَامٍ ۙ وَلَـٰكِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ ۖ وَأَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿١٠٣﴾

103. Allaah Hakuweka sharia yoyote ya kuharamisha bahiyrah[24], wala saaibah[25] wala waswiylah[26] wala haam[27] lakini wale waliokufuru wanamtungia Allaah uongo, na wengi wao hawatumii akili.

 

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ قَالُوا حَسْبُنَا مَا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۚ أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ ﴿١٠٤﴾

104. Na wanapoambiwa: Njooni katika yale Aliyoyateremsha Allaah na kwa Rasuli Husema: Yanatutosheleza yale tuliyowakuta nayo baba zetu. Je, japokuwa walikuwa baba zao hawajui chochote na wala hawakuhidika?

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنفُسَكُمْ ۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ ۚ إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٠٥﴾

105. Enyi walioamini! Jiangalieni nafsi zenu. Hawakudhuruni waliopotoka ikiwa mmehidika. Kwa Allaah Pekee ndio marejeo yenu nyote, kisha Atakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda.[28]

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا شَهَادَةُ بَيْنِكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ حِينَ الْوَصِيَّةِ اثْنَانِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ أَوْ آخَرَانِ مِنْ غَيْرِكُمْ إِنْ أَنتُمْ ضَرَبْتُمْ فِي الْأَرْضِ فَأَصَابَتْكُم مُّصِيبَةُ الْمَوْتِ ۚ تَحْبِسُونَهُمَا مِن بَعْدِ الصَّلَاةِ فَيُقْسِمَانِ بِاللَّـهِ إِنِ ارْتَبْتُمْ لَا نَشْتَرِي بِهِ ثَمَنًا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۙ وَلَا نَكْتُمُ شَهَادَةَ اللَّـهِ إِنَّا إِذًا لَّمِنَ الْآثِمِينَ ﴿١٠٦﴾

106. Enyi walioamini! Ushahidi uliofaradhishwa kati yenu ni wa watu wawili waadilifu wakati wa kuandika (au kutamka) usia, anapohisi mmoja wenu dalili za kukurubia kufa, au wawili wengineo wasiokuwa nyinyi pale mnapokuwa safarini ukakufikeni msiba wa mauti. Muwazuie baada ya Swalaah, na waape kwa Allaah mkitilia shaka, (waseme): Hatutovibadilisha (viapo vyetu) kwa thamani yoyote ile japo akiwa ni jamaa yetu wa karibu. Na wala hatutoficha ushuhuda wa Allaah, kwani hakika hapo tutakuwa miongoni mwa wenye kutenda dhambi. 

 

 

 

فَإِنْ عُثِرَ عَلَىٰ أَنَّهُمَا اسْتَحَقَّا إِثْمًا فَآخَرَانِ يَقُومَانِ مَقَامَهُمَا مِنَ الَّذِينَ اسْتَحَقَّ عَلَيْهِمُ الْأَوْلَيَانِ فَيُقْسِمَانِ بِاللَّـهِ لَشَهَادَتُنَا أَحَقُّ مِن شَهَادَتِهِمَا وَمَا اعْتَدَيْنَا إِنَّا إِذًا لَّمِنَ الظَّالِمِينَ ﴿١٠٧﴾

107. Ikigundulikana kwamba hao wawili wana hatia ya kukhini, basi wawili wengine wanaostahiki kudai haki kisharia, na walio karibu zaidi (na mrithiwa) wasimame mahala pao, kisha waape kwa Allaah: Bila shaka ushahidi wetu ni wa kweli zaidi kuliko ushahidi wa wawili wao, nasi hatukufanya taksiri, kwani bila shaka hapo sisi tutakuwa miongoni mwa madhalimu.

 

 

 

 

ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يَأْتُوا بِالشَّهَادَةِ عَلَىٰ وَجْهِهَا أَوْ يَخَافُوا أَن تُرَدَّ أَيْمَانٌ بَعْدَ أَيْمَانِهِمْ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاسْمَعُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ ﴿١٠٨﴾

108. Hivyo inaelekea zaidi ya kwamba watatoa ushahidi kama ipasavyo au watakhofu visije vikaletwa viapo (vingine) baada ya viapo vyao. Na mcheni Allaah na sikizeni! Na Allaah Haongoi watu mafasiki.

 

 

 

 

يَوْمَ يَجْمَعُ اللَّـهُ الرُّسُلَ فَيَقُولُ مَاذَا أُجِبْتُمْ ۖ قَالُوا لَا عِلْمَ لَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ ﴿١٠٩﴾

109. Siku Allaah Atakayowakusanya Rusuli na Kuwaambia: Mlijibiwa nini? Watasema: Hatujui lolote, hakika Wewe Ndiye Mjuzi wa Ghaibu.

 

 

 

 

إِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ اذْكُرْ نِعْمَتِي عَلَيْكَ وَعَلَىٰ وَالِدَتِكَ إِذْ أَيَّدتُّكَ بِرُوحِ الْقُدُسِ تُكَلِّمُ النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلًا ۖ وَإِذْ عَلَّمْتُكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَالتَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ۖ وَإِذْ تَخْلُقُ مِنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ بِإِذْنِي فَتَنفُخُ فِيهَا فَتَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِي ۖ وَتُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ بِإِذْنِي ۖ وَإِذْ تُخْرِجُ الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِي ۖ وَإِذْ كَفَفْتُ بَنِي إِسْرَائِيلَ عَنكَ إِذْ جِئْتَهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿١١٠﴾

110. (Siku) Allaah Ataposema: Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Kumbuka Neema Yangu juu yako na juu ya mama yako, pale Nilipokutia nguvu kupitia kwa Ruwhil-Qudus (Jibriyl (عليه السلام, unasemesha watu katika utoto na utu uzimani, na Nilipokufunza kuandika na hikmah (ilimu na ufahamu wa kina), na Tawraat na Injiyl, na ulipounda kutokana na udongo kama umbo la ndege kwa Idhini Yangu, ukapulizia likawa ndege kwa Idhini Yangu,  na ulipomponyesha aliyezaliwa na upofu na mwenye barasi kwa Idhini Yangu, na ulipowafufua wafu kwa Idhini Yangu, na Nilipowazuia wana wa Israaiyl dhidi yako ulipowajia kwa hoja bayana, wakasema wale waliokufuru miongoni mwao: Haya si chochote ila ni sihiri bayana.

 

 

 

 

وَإِذْ أَوْحَيْتُ إِلَى الْحَوَارِيِّينَ أَنْ آمِنُوا بِي وَبِرَسُولِي قَالُوا آمَنَّا وَاشْهَدْ بِأَنَّنَا مُسْلِمُونَ ﴿١١١﴾

111. Na Nilipowatia ilhamu wafuasi watiifu kwamba: Niaminini Mimi na Rasuli Wangu. Wakasema: Tumeamini na shuhudia kwamba sisi ni Waislamu.

 

 

 

 

إِذْ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ هَلْ يَسْتَطِيعُ رَبُّكَ أَن يُنَزِّلَ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِّنَ السَّمَاءِ ۖ قَالَ اتَّقُوا اللَّـهَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١١٢﴾

112. Pindi waliposema wafuasi watiifu: Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Je, Anaweza Rabb wako Kututeremshia meza ya chakula kutoka mbinguni? Akasema: Mcheni Allaah, kama nyinyi ni Waumini.

 

 

 

 

قَالُوا نُرِيدُ أَن نَّأْكُلَ مِنْهَا وَتَطْمَئِنَّ قُلُوبُنَا وَنَعْلَمَ أَن قَدْ صَدَقْتَنَا وَنَكُونَ عَلَيْهَا مِنَ الشَّاهِدِينَ ﴿١١٣﴾

113. Wakasema: Tunataka kula kwenye meza hiyo ili nyoyo zetu zitulie, na tujue kwamba umetuambia kweli, na tuwe katika wenye kulishuhudia hilo.

 

 

 

 

قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ اللَّـهُمَّ رَبَّنَا أَنزِلْ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِّنَ السَّمَاءِ تَكُونُ لَنَا عِيدًا لِّأَوَّلِنَا وَآخِرِنَا وَآيَةً مِّنكَ ۖ وَارْزُقْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿١١٤﴾

114. Akasema ‘Iysaa mwana wa Maryam: Ee Allaah, Rabb wetu!   Tuteremshie meza ya chakula kutoka mbinguni ili iwe kwetu ni sikukuu kwa wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na iwe Aayah (Ishara, Hoja, Dalili) itokayo Kwako, basi Turuzuku, kwani Wewe Ni Mbora wa wenye kuruzuku.

 

 

 

قَالَ اللَّـهُ إِنِّي مُنَزِّلُهَا عَلَيْكُمْ ۖ فَمَن يَكْفُرْ بَعْدُ مِنكُمْ فَإِنِّي أُعَذِّبُهُ عَذَابًا لَّا أُعَذِّبُهُ أَحَدًا مِّنَ الْعَالَمِينَ ﴿١١٥﴾

115. Akasema Allaah: Hakika Mimi Nitaiteremsha kwenu. Lakini atakayekufuru miongoni mwenu baada ya hapo, basi hakika Nitamuadhibu adhabu ambayo Sitomuadhibu mmoja yeyote katika walimwengu.

 

 

 

 

وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنتَ قُلْتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَـٰهَيْنِ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ قَالَ سُبْحَانَكَ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أَقُولَ مَا لَيْسَ لِي بِحَقٍّ ۚ إِن كُنتُ قُلْتُهُ فَقَدْ عَلِمْتَهُ ۚ تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ ۚ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ ﴿١١٦﴾

116. Na pindi Allaah Atakaposema: Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Je, wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni waabudiwa wawili badala ya Allaah? (‘Iysaa) atasema: Subhaanak! (Utakasifu ni Wako). Hainipasi mimi kusema yasiyo kuwa haki kwangu. Ikiwa nimesema hayo basi kwa yakini Ungeliyajua. (Kwani) Unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yangu, na wala mimi sijui yale yaliyomo katika Nafsi Yako, hakika Wewe Ni Mjuzi wa Ghaibu.

 

 

 

 

مَا قُلْتُ لَهُمْ إِلَّا مَا أَمَرْتَنِي بِهِ أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۚ وَكُنتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَّا دُمْتُ فِيهِمْ ۖ فَلَمَّا تَوَفَّيْتَنِي كُنتَ أَنتَ الرَّقِيبَ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿١١٧﴾

117. Sijawaambia (lolote) ila yale tu Uliyoniamrisha kwamba: Mwabuduni Allaah Rabb wangu na Rabb wenu. Na nilikuwa juu yao shahidi wakati nilipokuwa nao. Uliponikamilishia muda Ukanichukua juu, Ulikuwa Wewe Ndiye Mwangalizi juu yao. Na Wewe Ni Mwenye Kushuhudia kila kitu.

 

 

 

 

إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١١٨﴾

118. Ukiwaadhibu, basi bila shaka hao ni Waja Wako, na Ukiwaghufuria basi hakika Wewe Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.[29]

 

 

 

 

قَالَ اللَّـهُ هَـٰذَا يَوْمُ يَنفَعُ الصَّادِقِينَ صِدْقُهُمْ ۚ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١١٩﴾

119. Allaah Atasema: Hii ndiyo Siku ambayo Asw-Swaadiqiyna utawafaa ukweli wao, watapata Jannaat zipitazo chini yake mito wadumu humo milele. Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Huko ni kufuzu kukubwa mno.

 

 

 

لِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا فِيهِنَّ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٢٠﴾

120. Ni wa Allaah ufalme wa mbingu na ardhi na yote yaliyomo humo. Naye juu ya kila kitu Ni Muweza.

 

 

 

 

 

[1] Ihraam: Rejea Aayah namba (95) Suwrah hii.

 

[2] Tofauti Ya Ikabu Na Adhabu: Rejea Al-Hashr (59:4).

 

[3] Aayah Ambayo Ingeliteremshwa Kwa Mayahudi, Wangelisherehekea Siku Iliyoteremshwa:

 

‘Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Myahudi mmoja alimwambia: Ee Amiri wa Waumini, lau ingeliteremka kwetu sisi Aayah hii:

 

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ

“Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni Neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislamu uwe Dini yenu.”  [Al-Maaidah (5:3)] Basi tungeliifanya kuwa ni siku ya kusherehekea. ‘Umar akasema: Wa-Allaahi, naijua siku gani imeteremka Aayah hii. Imeteremka Siku ya ‘Arafah, siku ya Ijumaa. [Al-Bukhaariy]

 

[4] Sababu Ya Kuteremshwa Hukmu Ya Tayammum (Kuikusudia Ardhi Safi Ya Mchanga Kwa Ajili Ya Wudhuu):

 

Mama wa ‘Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) amehadithia: “Tulikwenda katika moja ya safari tukafika Al-Baydaa au Dhaatul-Jaysh ambako kidani changu kilivunjika (na kikapotea). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawa anakitafuta, kisha pia watu wengineo wakainuka kukitafuta. Hapakuweko na maji sehemu hiyo, basi watu wakamwendea Abuu Bakr Asw-Swiddiyq na kusema: Huoni alivyofanya ‘Aaishah? Kamfanya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na watu wakae sehemu ambayo hakuna maji! Abuu Bakr akaja wakati Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa amelala akiwa amelaza kichwa chake mapajani mwangu. Akaniambia: Umemzuia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na watu sehemu ambako hakuna maji na wala hawana (akiba ya) maji. Basi akanigombesha na akasema Aliyomjaalia (Allaah) kusema kuhusu mimi, na akanipiga ubavuni kwa mkono wake. Hakuna kilichonizuia kusogea (kutokana na maumivu) isipokuwa kwa vile Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa amelala mapajani mwangu. Hapo Allaah Akateremsha Aayah ya tayammum (kutia Wudhuu kwa mchanga), basi wakatayammam. ‘Usayd bin Al-Hudhwayr akasema: Ee ahli wa Abuu Bakr! Hii si baraka ya kwanza kwenu. Kisha akaendeshwa ngamia ambaye nilikuwa nimempanda na tukakipata kidani kilichokuwa (kimejificha) chini yake.” [Al-Bukhaariy]

 

Rejea pia An-Nisaa Aayah (4:43) ambayo pia ni sababu ya kuteremshwa hukmu ya Tayammum.

 

[5]  Al-Masiyh (Nabiy ‘Iysaa) Sio Allaah Bali Ni Mwana Wa Maryam Na Ni Rasuli Wa Allaah:

 

☞ Ukurasa wa Tatu



Report Page